JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, November 28, 2017

Huu ndio wakati ambao unaweza kujenga fikra zako na ukajengeka na baadae kuyafikia mafanikio makubwa

 Sadick Kilasi     November 28, 2017     UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu yetu ya JIKO LA USHAURI? Natumai umeshinda vizuri upo salama kabisa. Bila shaka siku yako imekuwa bora sana. Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye katufikisha wakati huu wa usiku na hatuna budi kumshukuru, Mungu wetu muumba mbingu na nchi tunakushukuru kwaajiri ya siku hii ya leo asante kuturinda siku nzima, tazama sasa ni wakati wa usiku huu na tunenda kulala, wakati huu nyama zetu zinaenda kufa, ehe Mungu wetu ukawe pamoja nasi na ukatuamshe salama katika siku ya kesho, tunaomba utusamehe dhambi zetu tulizofanya leo na hata sasa.

Mpendwa rafiki yangu kuna wakati ambao ni mzuri kwetu sisi kujifunza na kujenga fikra zetu kwa usahihi. Wakati huu mtu huwa anajengeka kwa ubora sana na hasa unapokuwa unajirudiarudia akili huwa inafanya kazi kubwa sana. Wakati wenyewe ni wakati wa changamoto. Changamoto ndizo huwa zinamjenga mtu nakuwa bora sana.

Mpendwa rafiki yangu kama unataka kujengeka kiakili na hekima basi huu ndio wakati wake hakuna sehemu nyingine ambayo unaweza kujengeka kiakili kama wakati huu. Watu wengi wenye mafanikio makubwa duniani hao ndio wametatua changamoto nyingi sana na ndozo zili waweka pale walipo.

Ukweli ni kwamba maisha bila ya changamoto si maisha, fikiria ya kwamba tungekuwa tunaishi bila ya changamoto vipi ingekuwaje? maisha yangekuwa wapi? vipi tungekuwa hapa tulipo au tungekuwa huko tulikokuwa zama za mawe?  Ukweli ni kwamba maisha bila changamoto tungekuwa tumekufa kabisa maana vitu ambavyo vimekufa havina changamoto.

Mpendwa rafiki yangu wakati changamoto inapotokea hakikisha unaiangalia kwa jicho la upana, ipe wakati wakufikiria wewe mwenyewe bila ya kukimbilia kwa watu kuomba msaada na hapa ndipo mantiki yako itakapo kuwa kubwa. Unaweza ukapata jibu la kukosea lakini ukishajua ya kwamba hapa nimekosea na ukarudia tena ukafanya vizuri ni wazi kabisa ya kwamba hutokosea tena.

Sisi binadamu tunapenda mambo yetu yawe laini na wakati tunakutana na changamoto tunaona kuwa pale ndio ukomo wa mambo lakini kumbe haipo hivo. Changamoto yako ni yako huna haja ya kumpa mtu mwingi lakini ukishindwa mwambie akupe maelwkezo sio maelezo. Maelekezo yatakujenga inamaana kwa hali hiyo huwezi kufanya makosa tena.

Mpendwa rafiki yangu jambo la kufanya saizi ni kuepuka zile hamasa sizo na maana, mtu unachangamoto unaambiwa tulia tu mambo yatakaa sawa, ukweli ni kwamba unatakiwa kufikiria siyo kusema utafanikiwa pasipo njia. Chukua hatua saizi jiulize uliambiwa ya kwamba utafanikiwa tu leo uko wapi? Hamasa inatakiwa ukipe wewe mwenyewe sio mtu mwingine kwani maisha ni wewe, hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuchukua jukumu la maisha yako.

Kama wewe huwa unakuwaga na mawazo yale ya kusaidiwa na mtu mwingine yaani kuwa tegemezi basi umepotea sana kwa sababu huwezi ukajijenga wewe mwenyewe binafsi. Changamoto ni ladha ya maisha na utamu wake anujua muhusika.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi lakini pia unaweza kujiunga nami kwa kujaza fomu ambayo inamaelezo ya kwamba jiunge nami. 

Utatu wa maisha ni KUWA+FANYA=SUBIRI MATOKEO.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
WWWW
W
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 27, 2017

Hivi ndivyo unavyotakiwa kuishi kwenye jamii inayokuzunguka ili kupata mafanikio makubwa

 Sadick Kilasi     November 27, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa rafiki yangu, natumai umeamka salama na upo na mwenye nguvu tele. Kitu pekee ambacho ni cha dhamani sana ni wewe kuwa na pumzi hiyo uliyo nayo haijarishi upo katika hali gani, ukuwa na pumzi na unaweza kusoma tayari wewe unaweza kufanya kitu chochote na kikawagusa wengine na kuleta matokeo ulio talajia. Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu katika hili kwasababu bila yeye tusingeweza kufanya kitu chochote maana kwa usiku ambao tulikuwa tumelala ni sawa mtu mfu. Kwa hili tumshukuru mwenyezi Mungu, tunakushukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii mpya na uzima huu tulio nao, tunakuomba katika siku hii ya leo kila tutakapo kwenda kukanyaga ukatubariki na uwepo wako ukadhihirike, tunakuomba utusamehe hdambi zetu.

Mpendwa rafiuki yangu katika maisha hasa ya sasa kumekuwa na changamoto nyingi sana. Ajira na mahusiano vimekuwa vitu vinavo wapa watu wakati mgumu katika maisha yao. Rafiki yangu tukizungumzia kwenye swala la ajira kwa sasa limekuwamni tatizo kubwa sana, watu ambao walikuwa na uhakika wa ajira lakini lakini sasa   hawana uhakika tena katika ajira zao. Ukweli ni kwamba mambo yamebadirika haswa katika nyanza hizi za ajira.

Tukizungumzia kwenye swala la mahusiano nalo pia limeadhirika sana katika zama hizi za mawasiliano. Ukweli ni kwamba mawasiliano yamekuja kuleta tofauti kubwa sana kwenye uhusiano wetu na watu wetu wa karibu. Zamani mtu wa mbali akitaka kuwasiliana na wewe alikuwa anaandika barua na inakufikia wewe kwa hali hiyo barua zilikua zinatugusa sana wakati tunasoma unajisikia muhemuko fulani. Lakini sasa haipo kabisa.

Kwenye swala zima la kazi na mahusiano zamani mtu ukipata kibarua unaenda kumfuata mtuwako wa karibu na kumwambia bwana e kuna kibarua sehemu flanitwende tukafanye tupate ridhiki lakini kwa sasa haipo hiyo. Watu ambao walikuwa na uhakika na ajira na kazi zao kwenye makampuni na katika sehemu mbalimbali  lakini kwa saizi unaweza ukaamka asubuhi na ukaambiwa tumempata mtu wa nafasi yako kwa sababu ana uwezo zaidi yako.

Ndoa zimekuwa zikivunjika kwa sababu watu wanaoana kwa sababu wanategemea matarajio fulani kutoka kwa wenza wao wanapokosa hivo vitu basi ndoa imeisha.

Hvi ndivyo unavyotakiwa kujiweka na kuishi kwenye jamii yako, kuwa MUHIMU na sio kuwa wa dhamani. Unapokuwa wamuhimu katika jamii yako kamwe hakuna mtu ambaye atachukua nafasi yako inamaana pasipo wewe hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika. Mpendwa wangu mambo yanabadirika unaweza ukaamka asubuhi unaenda kazini unafika kazini unaambiwa hamna kazi hapa na kazi hauna. Rafiki yangu unaweza ukaamka asubuhi akaambiawa na mwenza wako wewe hunifai huna pesa na sababu zingine mbalimbali.

Unapokuwa wa dhamani kumbuka wewe unapanda na kushuka na kwa zama hizi za mabadiriko mbona kesho dhamano yako inaisha, hapo ndipo unapoanza kujiuliza nimelogwa nini? Hujalogwa tatizo ni wewe umejiweka katika dhamani na kwa hali hio watu wamepanda dhamani na hapo ndipo unaanza kukimbizana na ajira.

Wewe ni mtu wa muhimu sana kwenye jamii na ni wakipekee sana, ipo njia ya wewe kuwa mtuwa muhimu katika jamii inayokuzunguka, jiulize swali hili darasani bila mwalimu inawezekana? Na hapo utajua kwanini unatakiwa kuwa wa muhimu.

Endelea kutembelea JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi.
Fomula ya maisha ni kuwa+fanya=matokeo
Wako SADICK KILASI.
Mawasiliano 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 24, 2017

Hii ndio sheria ya dunia

 Sadick Kilasi     November 24, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena,  natumai umeamka salama kabisa na Mungu ni mwema aliyetuamsha kutoka kwenye kifo cha mwili maana mwili wetu ukiwa umelala ni sawasawa  na mtu aliyekufa, hata mtu akija kukufanyia lolote wewe huwezi kujua kwahiyo Mungu mweyewe ndio anajua. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya hili, Mungu tunakushukuru kwa ajiri ya kutuamsha salama, unatupenda zaidi ya kawaida kwa hili tunakushukuru siku zote upo na sisi kwaajili ya kuturinda na sisi hatuna kitu cha kukulipa wewe asante sana, tunaomba katika siku hii ukawe nasi pioa tunaomba utusamehe makosa yetu.


Mpendwa rafiki yangu leo sitaandika lolote zaidi ya haya kukwambia ya kwamba sheria ya dunia ni kwamba toa kwanza harafu suburi matokeo yatakayo toka.

Naomba uende ukatafakari juu ya hili je watu wanaotoa wapoje? Kumbuka ya kwamba kwa neema yake sisi tulipona kwahiyo uzima tulionao hatukupata bure.

Uwe wewe kama wewe.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 23, 2017

Kama bado unasubiri kitu hiki kutoka kwa wengine huwezi kukipata kamwe

 Sadick Kilasi     November 23, 2017     MAHUSIANO, NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, hongera kwa kuamshwa salama natumai umuzima kwa sababu aliye kuasha kakuamsha akiwa anatambua ya kwamba wewe ni mazima. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye katuamsha kutoka kwenye hali ambayo kimwili tunakuwa tumekufa baki nafsi zetu tu ndo zinakuwa zinaishi, hongera sana rafiki yangu mpendwa ni jambo zuri kutoka kwenye hali hiyo ya kifo cha mda.


Sasa rafiki yangu mpendwa leo nimekutayarishia maada hii ambayo inasema 'kama bado unasubiri kitu hiki kutoka kwa wengine huwezi kukipata kamwe' je ni kitu gani hichi? Basi kuwa na mimi mpaka mwisho na tutiririke wote kwa pamoja utajua maana chochote kwa taratibu kinakujengea utaratibu.

HESHIMA ni jambo la muhimu sana katika maisha yetu, kama bado wewe unasubiri heshima kutoka kwa wengine ili na wewe uweze kuwaheshimu wao utasubiri sana na huwezi kupata hiyo heshima kamwe. 

Unajua kwanini? kwa sababu wote mnasubiri kitu kimoja mwenzako anasubiri wewe umuheshimu na wewe unasubiri heshima kutoka kwake. Mpendwa rafiki yangu hebu fikiria kitu kimoja ukichukua sumaku mbili halafu ukazielekezea ule upande unao fanana vipi huwa zinagusana? Nafikiri huwa hazigusani  na ndivyo ilivyo kwenye mmoja asipokuwa tofauti hanuwezi kutengeneza kitu kipya.

Mpendwa rafiki yangu hii ni asili ya dunia hebu fikiria kwanini kusingekuwa na matajiri tu dunia nzima, labda niseme vipi dunia ingekuwa ya matajiri pekee? au ya masikini pekee? Nafikiri kitu hicho haakiwezekani lazima kuwe na tajiri na maskini, jumulisha na kutoa, positive and nagative haya sasa mambo ya umeme.

Mpendwa rafiki yangu anza sasa kuwahaimu watu, wewe uwe wa kwanza kuwaheshimu wao na mambo yataenda sawa kama wewe ulivokuwa unataka. Heshima sio kuwa fedha au kuwa na kitu fulani hapana huo  ni woga wala sio heshima. Watu wanawaogopa wenye pesa sio wanawahesimu. Hebu fikiria jambo hili yule mtu aliyekuwa anamuheshimu boss wake kwa sababu anapesa na yeye akipata pesa unafikiri atamuheshimu tena?

Neno langu kwako mpendwa rafiki yangu ni wape heshima wengine nao watakuheshimu kumbuka wao wanasubiri kutoka kwako.

Yote juu yako.
Makala hii imeandikwa na Sadick Kilasi
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 22, 2017

Ijenge tabia ikisha nayo itakujenga wewe

 Sadick Kilasi     November 22, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa rafiki yangu natumai umeamka salama na upo tayari kwaajili ya siku hii ya leo. Ni jambo la jema na kufurahisha kuiona siku hii ukiwa na pumzi  njema kwa sababu hicho ndicho kiashiria  pekee kinacho kutamburisha ya kwamba bado unanafasi ya kufanya jambo fulani ambalo litakupeleka katika hatua fulani na mwisho kuifikia ndoto yako. Mwili ambao hauna pumzi haufanyi jambo lolote ni kama gogo tu kwahiyo weweambaye una hekalu lenye pumzi huna budi kumshukuru mwenyezi Mungu; Mungu tunashukuru kwa ajili ya siku hii ya leo ambayo umetuamsha salama tunaomba utubariki siku hii ikawe siku ya ukuu kwetu yenye furaha na mafanikio katika mambo tutakayoenda kuyafanya uwepo wako ukadhihirike, tunaomba urtusamehe makosa yetu.

Mpendwa wangu rafiki hinyo sasa ulivyo unavo jiona, unavo jitafsiri, hayo mafanikio uliyo nayo, hizo tabia unazozipenda au kuzichukia vyote hinyo vimesababishwa na wewe mwenyewe, wewe ndiye uliyejifikisha hapo ulipo sasa unaweza ukawa unapachukia hapo ulipo au unapapenda lakini wewe ndiye mhusika mkuu unaweza ukasema sasa nitoke hapa nilipo niende katika hatua nyingine nzuri zaidi au nzuri kutokana hapa ambapo sipapendi.

Mpendwa wangu kujenga tabia nzuri si jambo rahisi, kujenga tabia ya kukupereka kwenye mafanikio sio jambo rahisi. Kujenga tabia mbaya ni rahisi sana lakini ni vigumu kuacha ila kujenga tabia nzuri ni ngumu kujenga lakini ni rahisi kuacha. Kwa maana hiyo ili uwe na tabia nzuri ni lazima sasa ufanye maamuzi ni magumu na uanze kuyafanya na uyaendeleze. Na hii huwa inaanza pole pole sio kwa papala tabia murudio wa mambo kwahiyo jinsi unavorudiarudia baadae inakuwa ndo tabia yako.

Kama unataka kujenga tabia ambayo ni nzuri inabidi uanze kujenga vichocheo vya tabia yako ambayo unataka kuijenga  mfano; wewe unataka kuamka kila siku asubuhi na mapama ila wewe huwa huwezi kuamka asubuhi na mapema kichocheo cha kwanza unaweka alamu, alamu ikipiga tu unaamka kwahiyo kupitia alamu umeaka asubuhi na mapema kinachofuata ni labda wewe unataka kuanza tabia ya kufanya mazoezi asubuhi kwahiyo kichocheo cha kufanya mazoezi kuamka mapema.

Sasa tayari baada ya hapo umemaliza mazoezi labda unasali au tahajudi baada hapo unaenda kuoga kwahiyo mazoezi ni kichocheo cha kusali ni kichocheo cha kwenda kuoga baaada ya kwenda kuoga labda unasoma au kuandika kwahiyo unajijengea hivo na inaendelea ratiba ya namna hiyo mpaka jioni kwa hiyo tayari unakuwa umeijenga siku katika hali ya ratiba labda kwa wakati mwingine unaweza kujiwekea vipaumbele vyako wakati wa kazi za mchana. Sasa mrudio wakila siku baadae inabadirika na kuwa tabia yako.

Ili kuwa karibu nami na kupata makala mpya na huduma nyingine hakikisha unajiunga nami kwa kujaza fomu ipo hapo palipo andikwa jingenasi tayari unakuwa unapokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, November 21, 2017

Mbinu mbalimbali za kujifunza ili kuongeza maarifa kwenye maisha

 Sadick Kilasi     November 21, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamuka salama kabisa na upo tayari kwenda kuongeza dhamani katika shughuli zako. Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii maana bila yeye tusingeweza sisi peke yetu. Wapo watu ambao wameshindwa kuiona siku hii ya leo kwahiyo sisi tulio iona hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kusema asante Mungu kwa ajili ya siku hii ya leo, ambayo ni siku ya kipee kwetu na tunakushukuru kwa kutusaidia kuiona siku hii ya leo tunaomba ukawe pamoja nasi katika siku hii yote na ikalete matokeo mazuri na tunaomba utusamehe makosa yetu.

Mpendwa wangu rafiki yangu karibu sana kwenye makala hii ya leo ambayo mimi rafiki yako nimekuandalia ambapo nitakuonyesha mbinu mbalimbali za kujifunza ili kuongeza maarifa kwenye maisha yako.

Kwanza naomba nikutaarifu ya kwamba sisi watu wa ngozi nyeusi hatupendi kujifunza kabisa yaani mtu kujifunza anaona ni kitu cha ajabu sana yaani tunapenda kila kitu kwetu kiwe rahisi tu kama kuangalia TV maana kuangalia sio kazi ila kazi ipo kwenye kulichukulia lile jambo ambalo umeliangalia yaani wewe binafsi unamutazamo gani juu ya kitu ambacho umekiangalia.

Wakati tulipo hitimu ngazi mbalimbali, tujua tumesha maliza kila kitu lakini ukweli ni kwamba hujamaliza na huwezi maliza kwa  sababu mambo yanabadilika sasa kama mambo yanabadilika wewe usipo jifunza si utaachwa pale na mawazo yako ya zamani unaweza ukasema mbona mimi naona poa tu mambo yanaenda, kiuhalisia yanaenda lakini lazima ujue wewe unaendeshwa mara huku mara huku kwa sababu huna upekee uliopo ndani yako. Kwahiyo kujifunza kunakupa wewe upekee wako binafsi.

Sasa nisikuchoshe sana mpendwa wangu ngoja tuende mojakwamoja katika mbinu mbalimbali za kujifunza kwenye maisha.

Mbinu ya kwanza ni kujifunza kupitia mazungumzo yako na mtu mwingine au kikundi fulani. Sasa hapo kila neno linalozungumzwa lazima ulichukulie kwa uzito kiasi na uliangalie kwa mtazamo wako binafsi na ili kujifunza zaidi lazima uwape nafasi zaidi kuriko wewe kuwa mzungumzaji zaidi na wewe unakuwa msikilizaji sana kuriko kuzungumza. Haijarishi yuho mtu anazungumza kitu gani hata kama ni pumba anaongea lazima usikilize itakusaidia kitu fulani. Kama wewe unataka mambo mazuri kila siku sasa mabaya utayajuaje? Kuwa msikilizaji.

Penda sana kujisomea vitabu mbalimbali. Hii mbinu kwangu mimi naichulia kama mbinu kuu katika kujifunza, usomaji wa vitabu una raha yake bwana na hapa ndipo kwenye maarifa ya watu chanya, kwa sababu mtu anayeandika kitabu huwa anatoa kitu kilichopo ndani yake kwahiyo kama wewe ukikisoma kile kitabu tayari unachukua upekee wa mtu mwingine. Sasa ukisoma vitabu vingi utatengeneza kitu kipya kutoka kwenye vitu mbalimbali. Mpiganaji BLUES LEE alijifunza style mbalimbali za mapigano halafu akaja kutengeneza kitu ambacho kipya kabisa na ndicho kilicho mpa jina kubwa.

Jifunze kupitia internet. Saizi mambo yamerahizishwa yaani mda wote unaweza kujifunza yaani kila kitu kipo poa tu unacho taka unakipata.

Jifunze kupitia mikanda mbalimbali ya cd. Ndio unaweza kujifunza kupitia mbinu hii kwa kuangali tv ukajifunza.

Zipo mbinu mbalimbali za kujifunza ni nyingi sana kama luenda kwenye semina  kwahiyo ni nyingi sana lakini kujifunza ni jukumu lako wewe lazima uongeze maarifa kwa namna yoyote ile na kujifunza ndiko kunawapa watu mafanikio pia kunawapa watu uhuru wa maisha.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 20, 2017

Kila kitu kipo tayari unasubiri nini rafiki yangu kupuliza kipyenga?

 Sadick Kilasi     November 20, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu, karibu katika makala hii ya leo ili uweze kujifunza na kuongeza maarifa. Natumai unaendelea vizuri na upo tayari kwa ajiri ya siku hii ya leo katika shuguli zako za maendeleo au kuongeza dhamani katika maeneo mbalimbali. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii ya leo, huwezi kusema ni kwaajiri ya uwezo wangu utakuwa unaongopa sana. Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii.

Mpendwa rafiki yangu kati ya kipindi ambacho mambo yote yapo sawa basi zama hizi mambo yote yapo tayari, ni kila nyanja mambo yapo sawa na tunainjoi sana kuishi zama hizi ambazo ni zama za mawasiliano. Chochote unachotaka kipo tayari ni wewe kukamirisha tu ratiba yako, kitu gani unataka? puliza kipyenga sasa.

Je unataka kuanza biashara na hauna mtaji? Huwezi kusema siwezi kuanza biashara kwa sabababu sina mtaji wa kuanzia utakua unakosea sana japo hukosei kwa namna moja au nyingine unakosea, zipo biashara ambazo unaweza kuanza hivyohivyo ulivyo na ukaendelea mbele. Biashara kama network marketing[biashara ya mtandao] ni biashara ambazo unawza kuanza bila ha mtaji.

Je unataka kuanza mazoezi na unashindwa namna ya kunza? Tayari kila kitu kipo cha kukuongoza ni wewe tu sasa kusema sasa nataka kuanza mazoezi download alamu aplication ambazo zitakuamsha asubuhina jifunze namna kuanza mazoezi, zipo aplication ambazo zina sound ambazo zitakupa hamasa ya kuendelea kufanya mazoezi.

Unataka kuandika na kuacha alama kwenye maisha yako kila kitu kipo sawa, blogu ni jukwaa zuri sana la kuandika na unakuwa unaandika mafunzo au habari yoyote ile unayotaka kutoa cha msingi uwe unatoa kitu cha dhamani kwenye jamii na inafaidika kutoka kwako na hapa ndipo unapoweza kuanza kutengeneza kipato chako kwa kutumia tu simu hiyohiyo uliyo nayo, kwahiyo tayari biashara bila mtaji.

Je wewe unataka marafiki wa ukweli wa kusafiri nao katika ndoto yako unaona kama huna watu sahihi? Mpendwa wangu kama wewe upo tayari basi wapo wengine nao wapo hivohivo  sasa wewe anza kuwaonesha watu hao ya kwamba wewe ni mtu sahihi sasa kama hivi kama wewe unataka kwa rafiki yangu au mtu wangu wa nguvu basi jaza form hapo chini tayari unakuwa rafiki yangu tutakuwa wote.

Kila kitu kipo sawa ila wewe haupo sawa na wewe ndio refa wa maisha yako, na kila kitu kina mda wake kama ulivyo mpira wa miguu  ni dakika tisini tu kwahiyo ndio maana tuliwekewa masaa, kama huchukui hatua shauri yako. Mchezo dakika tisini tu unaweza ukaishi kwa mfumo huo tu kwa kuchukulia maisha yapo ndani ya dakika tisini, ukipoteza dakika moja inakula kwako.

Puliza kipyenga sasa wakati ni sasa hili ndilo jambo la msingi kwenye maisha yako na chukua hatua.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com


Subscribe to our mailing list

* indicates required
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 17, 2017

Hii ndio silaha pekee uliyonayo wewe ukiitumia vizuri lazima itakupa mafanikio makubwa

 Sadick Kilasi     November 17, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Wakati mwingine unaweza ukawa unajiuliza nitafanya nini kwenye hii dunia mbona kila kitu ambacho nataka kufanya kinafanywa na wengine? Wakati bado hujaingia kwenye hilo jambo ulikuwa unaona kama wafanyaji ni wachache lakini baada ya kuingia unaona wanaofanya ni wengi na tayari unaanza kukata tamaa nakuona ya kwamba huwezi kushinda nao.

Ni kweli kama unataka kushindana nao hutoweza utashindwa lakini nikutie moyo ya kwamba wewe unayo silaha pekee ambayo silaha yenyewe ni wewe kama wewe. Ikiwa kwenye shughuli hiyo utasimama wewe kama wewe lazima utapenya kwenye kundi kubwa  ambalo linawashindani wengi.

Utasimamama wewe kama wewe kwa kutoa kile kitu ambacho kipo ndani yako. Unajua binadamu kabla hujatoa hiyo sauti ya nje huwa unajiongelesha ndani kwanza yaani unaweza ukajiuliza swali harafu ukajijibu mwenyewe halafu ndipo unamuuliza mtu mwingine sasa ile sauti yako ya ndani ndiyo uitumie kama silaha ya mafanikio yako.

Kitu ambacho unatakiwa kukitambua mpendwa wangu ni kwamba binadamu hatufanani kwa kila kitu hata muwe mapacha wa kufanana bado kuna vitu vinatofautiana. Ukisimama wewe kama wewe lazima uoneshe uhalisia wako watu watakupenda wewe kama Sadick Kilasi hiyo kopi watu hawata ipenda.

Ukijitofautisha na washindani wako kwa jia hii ni lazima utafanikiwa tu haijarishi mnafanya kitu kimoja mpo wangapi kumbuka unatakiwa kufanya sauti yako ya ndani, mawazo yako ya ndani na ikisha fanya kwa ubunifu mkubwa tayari wewe utatengeneza chako.

Kitu cha kukumbuka hapa lazima utambue ya kwamba sio kila mtu ni wakwako bado kuna watu wengine sio wa kwako, watu wanao mpenda Sadick sio wote watakao mpenda Juma na huo ndio upekee wenyewe na ukitaka watu wasio kukubali wakukubali basi ongeza ubunifu lakini sio wote watakukubali.

Kama wewe ni mwimbaji anza kuimba wape watu ujumbe mzuri na wakipekee  na watu waseme ladha kama hizi nitazipata wapi. Kama wewe unapenda kuandika andika kwa ubunifu mkubwa.

Fanya kazi kwa ugmu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 16, 2017

Woga wako ndio umaskini wako

 Sadick Kilasi     November 16, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama na upo tayari kwaajiri ya siku hii ya leo na kupambana ili kuzifikia ndoto zako. Nikupe hongera mpendwa wangu na nikutie moyo ya kwamba kuiona siku hii ya leo ni ushindi mkubwa sana, wewe waweza ukawa umekata tamaa ya kwamba mimi siwezi kwasababu nipo kitandani miaka kumi sijaamka naumwa kwahiyo mimi ni wa kusubili kufa tu lakini ukweli haupo hivo kuumwa ni hali tu na bado hivyo ulivyo kuna jambo kubwa unaweza ukalifanya  na hata yule mzima wa afya bado naye hana galanti ya maisha yake lolote linaweza kutokea kwa hapo ulio kuanzia sasa hebu fanya kitu ukiamini maisha bado yanaendelea.

Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii, Mungu tunakushukuru kwaajili ya siku hii, tunaomba utujalie wakati wote wa siku nzima na utusamehe makosa yetu.

Hapo ulipo sasa hivi ni kwaajili ya maamuzi uliyo kuwa umeyafanya huko nyuma, kama ulikuwa unafanya maamzi ambayo ni mabovu najua hali yako sio nzuri kutokana maamuzi yako lakini kama maamuzi yako yalikuwa mazuri sasahivi unakula dodo. Siku zote maamuzi ndio hutupa matokeo ya uamuzi wako.

Binadamu sisi tunakitu kinachoitwa woga,ni kitu kibaya sana hichi japo wakati mwingine ni kitu kizuri sana lakini mimi naona kwa woga ni mbaya zaidi maana unaogopa jambo ambalo huna uhakika nalo yaani unaogopa kwa sababu hutaki kuingia kwenye hatari, hutaki kuingia kwenye hatari kwa sababu unataka vitu ambavyo tayari vimefanywa na wengine.

Unaogopa kuingia kwenye biashara kwa sababu unahofia kushindwa. Sasa hofu ya kushindwa inatoka wapi wakati kunaneno 'shindwa' hapo inamaana kushindwa kupo huwezi kushinda wakati wote, wewe ni nani ushinde wakati wote chukua hatua ukisndwa leo anza tena.

Unaogopa kuacha kazi yenye kipato kidogo na hulidhiki nayo kwa sababu hujui wapi pa kuanzia. Ni woga wako tu kwani hapo ulipo ulianzaje chukua hatua na jifunze juu yakujikwamua na kipato chako kidogo.

Kwanini unaogopa kwa sababu huna uhakika na matokeo yajayo na njia rahisi ya kuushinda woga wako ni kufanya lile jambo unnaloogopa. Na hata kama ukishindwa wewe ni wa kwanza kushindwa? Hivi unajua woga unaumiza zaidi kuliko matokeo hayohayo ya kushindwa. Wewe unafikiria nini kichwani mwako endapo utashindwa? Unaogopa kuchekwa? Je ukibaki hapo ulipo hutochekwa? Nani atajali zaidi unachofanya nafikiri ni wewe mwenyewe zaidi utajicheka mwenyewe, Je unafikiri watu wajari sana unachofanya wala hawana mpango na wewe na hata akiongea kitu sawasawa na kutoa maoni au like kwenye post ya facebook. Wacha woga kwa sababu ya watu wewe ndio wa muhimu zaidi.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com

M
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 15, 2017

Jiulize, mimi nipo bize na nini?

 Sadick Kilasi     November 15, 2017     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama na unaendelea vizuri. Najua upotari kwa mapambano ya wajibu wetu wa kutafuta mafanikio ali kuzifikia ndoto ni jambo zuri. Kitu cha muhimu siku mpya unapoianza na lazima kujitafakari wewe umetoka wapi, uko wapi, na unaenda wapi? Siku hazigandi huwezi kuifidia ikitoka imetoka hata uew vipi mda hauzuiriki.

Ni jambo la kumushukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii, Mungu tunakushuru kwaajiri ya siku hii asante kwa ktujalia, tunaomba siku hii ikawe siku ya mazuri kwetu kila tutakachofanya kikalete matokeo chanya, tusamehe makosa yetu.

Leo mpendwa rafiki yangu nimeona nikuulize swali wewe upo bize kitu gani? kitu gani kinakuchukulia mda wako kwa kiasi kikubwa? Nimi hasa unafanya  wewe mpaka unakuwa bize? Usinijibu mimi wewe ndio ujijibu mwenyewe.

Imekuwa ni kawaida mtu akiulizwa vipi wewe mbona hupatikani? Mimi nipo bize na kazi. Je ni kweli upo bize na kazi au ndo unatuzuga? Ni kweli upo kazini lakini vipi mda wote unafanya kazi au mda mwingi unatumia kuchati tu kwenye mitandao ya kijamii. Vipi hupi stori maeneo ya kazi wewe na marafiki zako na kumasema bosi? Jijibu mwenyewe wewe ndio unaya jua.

Vipi masaa yako ishilini na nne unayapangiliaje? Mda wa kuingiza kipato chako unakuwa au mda wote unakuwa kanisani tu, umesahau kabisa mda huu wa kipato?

Vipi wewe sio mzee wa huku na huko unazulula tu, mara nipo Mbezi mara nipo Mbagara huna jambo la muhimu unalofanya, upo bize na mabo ambayo hayana umuhimu.

Rafiki yangu mpendwa mda ni mali sana na unapokuwa bize na kitu kifanye kwa uhakika na kikupe matokeo unayotaka ubize usio na maana hauna maana  ni sawa na kusukuma ukuta harafu hausogei. Pangilia mda wako unapokuwa bize uwe bize kwelikweli usijidanganye mwenyewe na ukweli hauficha jambo mwisho sisi nje tutaona tu ulichokuwa unafanya.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, November 14, 2017

Hata kama umekata tamaa bado kuna vitu vipo ndani yako ambavo vinaweza kukupa mafanikio makubwa sana

 Sadick Kilasi     November 14, 2017     NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, ambayo ni siku mpya natumai umeamka salama na upo tayari kwaajiri ya mapambano. Ukitaka kujua hali yangu mimi nip fiti nina afya njema na nipo tayari kwa ajiri ya siku hii kujiongeazea dhamani na kuwapa dhamani wengine na hili ndilo kusudi la kila mtu ni kuhakikisha unajipa dhamani na ikisha unawapa dhamani wengine.

Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa huu uzima na kwaajiri ya siku hii mpya mbayo tayari umeshaiona. Mungu tunakushuru kwaajiri ya siku hii ya leo siku ambayo wapo wengi walitamani kuifikia lakini wameshindwa, hii ni siku ya dhamani sana kwaajiri yetu ni siku ambayo wapo wengine wanaolewa, ni siku ambayo wapo wengine wanaenda kufanya makuu na makubwa na siku ambayo wapo wenginewanazaliwa na kwa hilo tunakushukuru sana, tunakuomba utujalie katika kazi zetu zikawe na baraka kubwa tukafanye kwa ubora mkubwa na mafanikio makubwa, tunaomba utusamehe makosa yetu maana wewe ni Mungu wa huruma utusamehe.

Inawezekana na umekata tamaa kabisa katika swala zima la kuyafikia mafanikio, unaona hakuna njia  yoyote ambayo inaweza kukupeleka moja kwa moja katika mlima wako wa mafanikio, unaona kiza kizito mbele.

Lakini ukweli ni kwamba bado ipo mjia ambayo unaweza kuitumia, hebu wewe mwenyewe fikilia kwa undani kuna kitu ndani yako ambacho kinaweza kutenda mambo makubwa sana, kkikubwa wewe ni kukisisimua na kukirihusu kianze kufanya kazi. Ndani ya miili yetu kuna vitu viwili ambavyo ni vya asili kuna vipawa na nguvu fulani ya ujasili ambayo imejificha sana. Ukijuwa kuvitumia vitu hivi viwili utapata mafanikio makubwa sana.

Talanta yako ambayo ni kipawa ni lahisi kuijua wakati wa utoto wako lakini kwenye utu uzima ni ngumu kidogo kuitambua kutokana na mambo mengi ambayo unakuwa unayafanya lakini bado uwezekano upo wa kutambua talanta yako. Lazima utafute kipawa chako kikupe nafasi ya mafanikio.

Nguvu iliyo jificha hii hutenda mambo kiautomatiki lakini wewe unatakiwa uifanye itende kazi wakati wote.Kama huijui nguvu hii hebu fikiria wakati fulani uapokuwa kwenye jambo la hatari unaweza ukajikuta umefanya kitu kikubwa bila wewe mwenyewe kujijua, ulikuwa huwezi kukimbia baada ya kukutana na hatari ukakimbia, ulikuwa huwezi kuruka baada ya kukutana na hatari ukaruka yenyewe hufanya kazi automatic.

Lakini kitu hiki pia hujitokeza wakati flani labda kuna aibu au mbele za watu unajikuta umefanya mambo makubwa bila wewe mwenyewe kutegemea mpaka baadae unajiuliza hivi ni mimi kweli na ukiambiwa ufanye tena huwezi. Hii ndio silaha yetu sisi ambayo unaweza ukaitumia na kupata mafanikio kwa sababu hii ipo kwaajiri ya kukulinda wewe usipatwe na mabaya lazima uitumie hii kama mambo yote yameshindikana.Nakupa siri hiyo sasa.

Utafanyaje ili ifanye kazi rudia tena kufanya lile jambo gumu kwa ujasiri mkubwa, rudia tena na tena jitoe kimasomaso, wewe ni mshindi.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 13, 2017

Mshinde kwanza huyu mpinzani wako ulienae kusafisha njia ya mafanikio

 Sadick Kilasi     November 13, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, natumai umeamka salama na unaendelea vizuri na ukitaka kujua hali myangu mimi nipo vema kabisa na nipo tayari katika mapambano ya kila siku ili nifikie kilele ninachotaka. Natumai na wewe mpendwa wangu upo tayari kuweka juhudi katika kuyafikia mafanikio na malengo ulio jiwekea na hii ndio taratibu za maisha ya mwanadamu. Weka malengo chukua hatua.

Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii mpya, tunakushukuru Mungu kwaajiri ya siku hii mpya ulio tujalia, hii ni hatua mojawapo kubwa na dhamani sana ambayo umetupeleka, tunajua wapo wengi walitamani kuifikia siku hii lakini washindwa na sisi kuifikia siku hii si kwasababu sisi ni wazuri sana bali ni upendo wako tu, tunakuomba siku ya leo ikawe siku ya furaha na mafanikio na kila tutakachokwenda kugusa wewe ukakibariki. Tunaomba utusamehe dhambi zetu.

Mpendwa wangu karibu ujifunze makala hii ya leo.Yupo mpinzani ambae huwa anatusumbua sana sisi binadamu na yeye huyu ndiye anaye tuendesha mara nyingi, ukimshinda huyu ni rahisi sana kukamirisha malengo yako madogomadogo na hata badae kuyafikia malengo makubwa.

Mpinzani huyu ni nani? hisia za mwili wako, mambo yote tunayofanya kama sio zuri basi tu ni hisia ndizo zinazo tuendesha wala sio kitu kingine. Mwili unaendeshwa kwa hisia zako ndio maana unashindwa kukamirisha malengo yako na hii ni mbaya sana.

Tunasema hisia zetu ni mpinzani mkubwa kwa sababu unaweza ukawa umeweka malengo yako madogamadogo kwa mfano; kuamka asubuhi na mapema na kufanya mazoezi lakini mwili wako ukakataa kabisa kuna kitu kinakujia,  wewe unasema ngoja nifanye lakini mwili unakukatalia  kabisa mwili unakwamba hapana wew rudi kulala kwanza wewe huna shida yoyote na wewe unakubali unarudi kitandani unalala tena. Mimi nakupa pole hayo sio maamuzi yako maamuzi yako ni malengo yako likini huyo ndo mpinzani wako inatakiwa umushinde.

Unatembea barabarani ukaona kanguo kazuri ukanunua bila malengo yako. Huyo ni mpinzani wako kanunua sio wewe ila anatumia pesa yako vibaya  inatakiwa umushinde asikuendeshe kabisa kabisakabisa ni mbaya huyo.

Huna sababu ya kuwatafuta wapinzani wako wa mbali wakati huyu wajilani yako ujamshinda, ni vigumu kuyafikia malengo yako. Sasa kivipi utashinda hili ni lazima ulazimishe kwa sababu ni kitu ambacho kipo ndani yako sema tu 'HAPANA SIWEZI KUFANYA HIVI HAYA SIYO MALENGO YANGU'. Huna sababu ya kwenda mbali huyu ndiye adui yako mkuu wa mafanikio yako.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0659639168, 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, November 12, 2017

Kama bado hujaanza biashara basi haya hapa ndio mawazo yangu ya biashara.

 Sadick Kilasi     November 12, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, UJASIRIAMALI     No comments   

Ni siku nyingine tena, ambayo ni siku mpya natumai umeamka vizuri na upo tayari kwaajiri ya mapambano ya siku hii. Na kama wewe unataka kujua hali yangu basi mimi ni mzima wa afya na nipo tayari kwaajiri ya siku hii ya leo katika kupambana na kufikia malengo yangu na kuwapa dhamani wengine.

Kama wewe unasoma hapa kaa na ujue ya kwamba wewe ni mzima tayari na huna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya pumzi uliyonayo, haijarishi upo katika hali gani upo kitandani unaumwa wewe bado unayo fursa ya kufanya chochote kwenye maisha, waweza kuongea kitu ambacho kinaweza kubadili maisha ya mtu mwingine kwahiyo kwa hali yoyote ile ambayo mpendwa wangu upo nayo basi siku hii ya leo unaweza kufanya kitu chochote kile na kuwapa dhamani wengine. Kwa yote tumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii ya leo, Mungu tunakushukuru kwaajili ya siku hii ya leo, hii ni siku mpya na  ni siku ambayo kuna watu waliiwekea malengo yao lakini wameshindwa kuifikia siku hii lakini sisi tumeifikia, sio kwamba sisi tuwazuri sana kwako bali tu ni upendo wako ulionao tunasema asante. Tunakuomba siku hii ya leo iakawe siku ya tofauti tukaijenge vizuri na kuwapa dhamani wengine na katika vyote tunavyoenda kugusa vikawe na baraka, tunakuomba utusamehe makosa yetu.

Mpendwa wangu karibu katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI uendelee kujifunza na kuulisha ubongo wako na mwisho uyaishi haya unayo jifunza na uyafikie mafanikio yako. Kama bado hujaanza biashara basi haya ndiyo mawazo yangu ya biashara kikubwa wewe tu kuchukua hatua.

Kama bado hujaanza biashari unaweza kuanza biashara ya kilimo na mbogamboga. Unaweza kuanza kilimo hapo maeneo ya nyumbani ukilima mbogamboga na mwisho ukatengeneza kipato chako.

Unaweza ukaanza ufugaji wa kuku wa kienyeji. Kijana unaweza kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji ambao hauna ghalama sana  na mwisho ukatengeneza kipato chako kwa kuuza mayai au kuku.

unaweza ukawa unauza vyakula vya nafaka. Kijana unaweza ukaanza biashara ya uuzaji wa vyakula vya nafaka.

Kijana unaweza kuanza ufugaji wa mbuzi wa maziwa. Unaweza kuanza ufugaji wa mbuzi wa maziwa na ukatengeneza pesa kwa kuuza maziwa.

Mwisho unaweza kufanya kitu chochote kile ambacho unahisi kitakuingizia kipato, kama huwa unafikiria biashara fulani inalipa na nyingine hailipi mimi huwa naona huo sio ukweli kikubwa ni uvumilivu tu kwenye hiyo biashara na aina ya wateja unao walenga kama biashara yako inawelenga wateja wachache basi na kipato chako kitakuwa kidogo au kama biashara yako inawalenga wateja ambao ni wakipato cha chini basi kipato chako kitakuwa kidogo ni mfumo wako tu wa biashara ndio ambao utakupa kipato unachokitaka. Kama unataka kipato kikubwa toa dhamani kubwa.

Biashara zote zinalipa anza sasa kufanya na kama huna mtaji jaribu kuangalia biashara ambazo hazina mtaji na uanze nazo kikubwa kuchukua hatua, kama huwezi kutembea tafadhari tambaa kikubwa unachatakiwa ni kusogea mbele sio kubaki hapo ulipo na kutafuta visingizio hilo sio suruhisho. Na mwisho lazima utambue hata kama ukiwalaimu wenine na kuwasingizia au ukajilaumu mwenyewe na kusingizia kitu flani bado haita leta maana yoyote na bado utaendelea kuishi sijui utafanya nini?

FANYA KAZI KWA UGUMU UTAFANIKIWA.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 10, 2017

Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.

 Sadick Kilasi     November 10, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikoni na kukupikia mambo mazuri kila siku, ni kitu ambacho huwa napenda kukushirikisha katika uwaja huu juu ya mambo yale ambayo najifunza na hii ndo njia pekee ambayo naitumia kukupa nilichonacho.

Naomba tumushukuru mwenyezi Mungu, e Mungu wetu muumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo ndani yake tunakushukuru kwa kutujalia siku hii ya leo, tunakushukuru kwa sababu unatupa tunachotaka  na si kwamba sisi ni wazuri sana bali ni upendo wako ulionao tunasema asante kwa hilo, tunakuomba siku hii ya leo  kila tutakacho gusa kikatupe neema na mafanikio na ndimi zetu zikatawaliwe na maneno ya kishujaa na hekima na hivi ndivyo tunaomba, tunakuomba utusamehe makosa yetu.

Mpendwa wangu karibu katika makala hii ya leo ambayo nimeamua nikuletee wewe inahusu juu ya mtu ambaye anaitwa Malcolm X. Unaweza kujinza kupitia historia ya huyu mtu ambaye alikuwa na akili sana mtukutu na baadae alikuja kubadirikana  kuwa mtu mzuri aliwaongoza watu kutetea haki za watu weusi huko Marekani. Hizi hapa nukuu zake ambazo aliwahi kutamkaaaa;

'Mtu asiyesimamia chochote basi ataanguka kwa chochote'.

'Hakuna atayekupa uhuru, hakuna atakaye kupa usawa wa haki, kama wewe ni mwanaume nenda ichukue'.

 'Hautakiwi uwe kipofu kwa uzalendo nchi yako mpaka unashindwa kujipigania ukweli. Baya ni baya tu haijarishi  limefanywa na nani au kusemwa na nani'.

'Shule yangu ilikuwavitabu na maktaba nzuri, nilitumia maisha yangu yote kule  nikiwa nasoma na kutimiza azma yangu ya udadisi'.

'Elimu ni paspot ya baadae kwani kesho kwani kesho ipo kwa wanayoitalisha nayo leo'.

Hizi ni baadhi za nukuu zake ambazo aliwahi kutamka na kupitia hizi mpendwa rafiki yangu unatakiwa kujifunza kitu. Yapo mengi aliyoyafanya mtu hebu fanya kuitafuta historia yake utajifunza mengi kupitia yeye. Kuwa mtu wa kujifunza siku zote rafiki ya ujiandae na kesho.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 9, 2017

Hapa ndipo ushindi wa mafanikio unapoanzia

 Sadick Kilasi     November 09, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu msomaji na mfuatiliaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, hongera kwa kuamka salama na jimbo zuri sana na linaleta faraja sana. Mpendwa wangu kuamka salama kwa siku ya leo huo ni ushindi mwingine ambao mwenyezi Mungu kakupatia siku hii ya leo kwa sababu wapo wengine ambao wameshindwa kabisa kuiona siku kama wewe ulivo iona, ni wajibu wako sasa mpendwa wangu kuitumia siku hii ya leo kuacha alama yako hapa duniani kwasababu upo hai tumia fursa hii sasa haijalishi upo na hali gani kikubwa tu uwe mzimana unapumua fanya chochote kile ambacho wewe unaona kitakuongezea dhamani. Tusisahau kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya uzima huu na kwa nafasi hii, Mungu wetu tunakushukuru kwaajiri ya siku hii mpya ambayo umetujali tumeweza kuifikia salama, tunakuomba ukatuongoze katika siku hii, katika hatua yoyote tutakayo ipiga uwepo wako ukatawale kazi zetu ziinuliwe, tunaomba utusamehe makosa yetu. Mpendwa rafiki yangu inawezekana umekuwa umejifunza sana juu ya kutafuta mafanikio lakini bado unao kuna hali fulani ni ngumu kwak, yawezekana upo na hamasa kubwa katika jambo hilo ambalo unategemea likupe mafanikio lakini bado unaona kuna kitu fulani kipo mbele yako kinakuzua kupata unachota na hamasa ni kubwa. Yawezekana unawazo kubwa sana la biashara na linakupa maumivi kwa sababu unawaza sana ukweli ni kwamba ushindi wako utaanzia pale tu utakapo THUBUTU yaani kuchukua hatua. Hata kama umesoma sana juu ya jambo fulani umejifunza kwa ugumu bila ya uthubutu ni sawa na mtu ambaye hajafanya jambo lolote na hajui kitu tena bola yeye maana wewe unakua na maumivi ambayo yatakutesa wakati wote. Uthubutu ni muunganiko wa matendo na njozi, kwahiyo ukiwa na njozi yako unataka kufanya jambo fulani jitaidi kuchukua hatua hata kama ni ndogo sana. Njozi ni dira yako na uthubutu ni matendo yako. Ngoja nikupe kisa hiki; siku moja fisi alikutana na binadamu akataka amdhuru lakini alishindwa kumkabili ila akajiwekea moyoni mwake ya kwamba atamfuata nyumanyuma ili siku moja mkono wa binadamu ukidondoka aule lakini miaka ilinda mpaka fisi yule mda wake wa kufa ulipo fikia mkono wa binadamu hakudondoka na yeye akafa. chukua hatu sasa hivi na kuwa na uthubutu katika jambo lolote unalowaza na hilo ndio wazo zuli na ushindi wako wa mafanikio unaanzia hapo. Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa. Wako SADICK KILASI Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com

Subscribe to our mailing list

* indicates required
Email Format
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 8, 2017

Ubongo wako ni karakana ambayo inayoshughulika kukufanikisha, fanya mambo haya ili utengeneze mafanikio

 Sadick Kilasi     November 08, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu, karibu tena katika masomo yetu ya JIKO LA USHAURI. Ni jambo zuri mimi na wewe kuwa wazima maana kama wewe natumai wewe ni mzima hata kama upo kitandani bado unayo nafasi ya kufanya kitu cha tofauti na kupata matokeo unayotaka kikubwa ni wewe kuanza mabadiliko na kuchukua hatua kama wewe unasubili mambo yakae sawa ili uchukue hatua basi unakosea sana mambo hayawezi kukaa sawa kama wewe hujachukua hatua, chukua hatua kwanza ili mambo yako yakae sawa. Kuna msemo mmoja unao sema kama huwezi kupaa basi kimbia na kama huwezi kukimbia basi tembea lakini pia kama huwezi kutembea basi tambaa. Kinachotakiwa wewe ni kutoka hapo ulipo na kuchukua hatua.

Mpendwa wangu ni vema tungemshukuru Mwenyezi Mungu, Mungu tunakushukuru kwaajiri ya uzimaa huu tulio nao, ni kwaajili ya upendo wako tu ndio maana tu wazima, tunakuomba siku hii ya leo ikawe siku ya mafanikio makubwa kwetu kila tutakacho gusa kikalete matokeo makubwa katika kazi na kutafuta kwetu, lakini pia tunaomba utusamehe makosa yetu.

Ubongo wako ni karakana ambayo inashughulika kukufanikisha wewe, sasa fanya mambo haya yafuatayo ili ufanikiwe;

Kwanza kuwa mbunifu, kama usingekuwa ubunifu wa Thomas Edson basi mpaka leo tungekuwa tunaishi kwenye kiza. Bwana huyu ndiye aliyegundua na kutengeneza balbu ambazo mpaka leo zinatusaidia ambapo yeye aligundua miaka ya 1880 huko.

Pili jifunze kuwa mvumilivu. Wakati umefanya ubunifu wako jifunze kuwa mvulivu katika jambo hilo ulilogundua, mambo huwa hayaendi kama vile unavotaka wewe lazima kunachangamoto. Thomas Edson wakati anatengeneza hiyo bulb alifanya majaribio 3000 na alitumia vifaa zaidi ya 6000 na ndipo alipopata anachotaka. Kwahiyo mambo si rahisi kama ile uonavyo kwenye ubongo wako lazima uwe mvumilivu.

Na tatu punguza kulisha ubongo wako vitu hasi. Kuna vitu kama kuangalia sana tv, kuwa na matazamo hazi, marafiki na watu wa karibu ni mambo yanayotuathiri mara nyingi kwahiyo kama wewe unataka mafanikio lazima uvikwepe vitu hivo.

Ubongo wa mwanadamu ni kama parachuti inafanya kazi pale inapokuwa imefunguliwa kwahiyo hatuna budi kuusisimua ubongo wetu.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, November 7, 2017

Huyu ndiye adui mkubwa wa mafanikio yako

 Sadick Kilasi     November 07, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Mpendwa wangu ni siku nyingine tena ambayo ni siku mpya kabisa na kama ulikuwa hujui zimebaki siku arobaini na tatu tumalize mwaka, anglia siku zinavokwenda juzi tu tulikuwa tunasherekea mwaka mpya leo mwaka umeisha na malengo yako uliyokuwa umejiwekea mwezi wa kwanza saizi ndo unajaziajazia, ni jambo zuri kama unaibuka mshindi wa malengo yako, hongera sana.

Kama unasoma hapa natumai umeamka salama na hauna budi kumshukuru mwenyezi Mungu katika hili, E mwenyezi Mungu tunasema asante kwaajili ya siku hii mpya tunajua usingekuwa wewe isinge wezekana, tunaomba utusamehe makosa yetu na katika kazi za mikono yetu tunaomba utubariki, mahala popote tutakapo enda kugusa siku hii ya leo uweza wako ukadhihirike.

Karibu mpendwa wangu msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI ili ujifunze maana mimi rafiki yako kila siku nimekuwa nikiingia jikoni na kukupikia vitu ili tufaidi mmi na wewe. Kujifunza ndo maisha ila kushukua hatua ndo maisha ya ukweli. Leo mpendwa wangu nataka nikuonyeshe adui yako mkubwa wa mafanikio yako.

Inawezekana umekuwa ukitafuta mafanikio kwa hali namali lakini unaona huyapati, unatafuta huku na kule kutafuta nani adui na mwishowe anona kama unamikosi na unakata tamaa kabisa na kuona haiwezekani kabisa lakini ukweli ni kwamba yupo adui ambae upo nae ambae anasababisha yote haya na adui ni kutokujipanga.

Kama wewe hujaweka malengo na mikakati katika jambo ambalo unalifanya na unataka kufanikiwa ni lazima utashindwa tu. Kila kitu kina ugumu wake na changamoto zake hakuna jambo lahisi dunia na kama lipo ujue haliwezi kukupa kitu chenye dhamani kubwa wasema lazima ulipie ghalama kutokana na dhamani ya kile kitu ili uweze kukipata.

Subscribe to our mailing list

* indicates required
Email Format
Ikiwa utakuwa umejipanga inamaana utakuwa umezijua changamoto zotena upo tayari kupambana nazo na ndiomaana umeanza kufanya jambo hilo. Jipange hakuna jambo rahisi kwenye maisha, wewe mwenyewe unaweza kujifunza hata kwenye vitabu vya dini uone jinsi manabi walivo pita hali ngumu katika kutangaza dini zao. Kaa na ujue hakuna jambo lahisi chini ya jua na kama lipo basi dhamani yake na ndogo na haliwezi kukupeluka unakotaka wewe.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0659639168 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 6, 2017

Nyenzo kumi za kukufanya ufanikiwe kimaisha

 Sadick Kilasi     November 06, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, tumeamka salama kabisa, na kama unasoma hapa natumai umuzima afya tele kabisa na upo tayari katika kupambana ili kufikia mafanikio ulio jiwekea. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu katika yote alio tutendea. E Mungu muumba mbingu na nchi tunakushukuru kwa ajiri ya siku hii na uzima tulio nao tunasema asante, tunaomba utusamehe makosa yetu tuliyo fanya kwa kutenda na kwa mawazo, tunaomba utubariki katika kazi zetu za mikono kila tutakacho gusa na kukanyaga leo uwepo wako ukadhihirike.

Mpendwa wangu msomaji karibu ujifunze katika makala hii ya leo yenye kichwa cha [ nyenzo kumi za kukufanya ufanikiwe kimaisha ]. Hizi ni nyenzo ambazo ukianza kuziishi lazima utafanikiwa.

Lazima uwe na afya bora. Ili upate mafanikio ya ukweli lazima uwe na afya bora lazima uujali mwili wako kwa kufanya mazoezi, kula mlo kamili na kupata mapumziko kwa wakati sahihi.

Kuwa na mahusiano na watu sahihi. Lazima uwe na mahusiano na watu sahihi na wenye mtazamo kama wako hawa watakusaidia kwenye mambo mbalimbali kama kujifunza.

Kuwa na malengo ambayo unataka kuyafikia. Lazima uweke malengo yako ambayo unataka kuyafikia na hayo ndiyo yanayo kupa chachu ya kutaka kufanikiwa.

Kuwa na imani ya kwamba utafanikiwa. Lazima uwe na imani ya kwamba utafanikiwa na huu ndio mtazamo wako juu ya mafanikio. Kama huamini huwezi fanikiwa lazima utaishia njiani.

Kuwa mtu wa kujifunza kila siku. Mambo mapya yanatokea kila siku kwahiyo lazima uwe mtu wa kujifunza na kutafuta habari juu mambo mbalimbali ya hicho unachofanya.

Tengeneza fikra nzuri juu ya watu wanao kuzunguka. Lazima uwe na fikra nzuri juu ya watu wanao kuzunguka kwa kuwapenda na kuwajali na sio kuwazalau.

Amini katika Mugu yote yanawezekana. Ndio usimsahau Mungu wako lazima uamini katika yeye yote yanawezekana na yeye ndiye muweza wa kila kitu kwa hiyo lazima uamini katika hilo.

Lazima uwe mtu wa matendo. Ndio imani bila matendo ni sawa sawa na hakuna kitu kwahiyo lazima uwe mtu wa vitendo sio kuamini na kujifunza tu.

Lazima uwe mtu wa kuchangamkia fursa mpya zinapojitokeza. Wanasema fursa ni matumizi mazuri ya bahati kwahiyo bahati nzuri inapojitokeza kwako lazima uitumie vizuri. Fursa huwa inakuja haraka na kupotea haraka kwahiyo lazima uwe mtu wakutambua  na kujifunza sana mambo mengi.

Hizo ndio nyenzo kumi za kukufanya ufanikiwe kimaisha, zifanyie kazi na zitakua matokeo makubwa sana.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, November 5, 2017

Dunia inavokuendesha bila wewe kujua

 Sadick Kilasi     November 05, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu yetu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai unaendelea vizuri na umuzima wa njema kabisa kabisa na upo tayari kuelekea kwenye mapambano yatakayo kufikisha kwenye kilele chako cha mafanikio. Kwa kuamka salama wote mimi na wewe sisi sote hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa yote haya alioyotufanyia kwa kutuamsha salama, wote huu ni upendo wa mwenyezi Mungu ambao anatuonyesha sisi na sisi hatuna budi kusema asante na tunaomba utuongoze katika siku hii ya leo akatutangulie kila chochote tunachoenda kukigusa.

Mpendwa wangu karibu kwenye makala hii ya leo ambayo dunia inavyokuendesha bila wewe kujua. Makala hii inamlenga kila mtu ambaye bado hajajua hili ya kwamba yeye anaendeshwa na dunia.

Ni ukweli usio pingika dinia kila siku inabadilika na dunia inavobadilika ndani yake kuna mambo mengi sana yanayo tokea. Mambo hayo hutokea kila siku yapo mambo mazuri na yapo mambo ambayo si mazuri, yote haya atokea kwenye hii dunia.

Mara nyingi yale mambo mabaya yanapo tokea huwa hayawi mabaya ila sisi ndo tunafanya yawe mabaya kwa siku hizi kila siku kuna fashion mpya za nguo zinatoka na wewe kila fashion unataka kuivaa unasema hutaki kupitwa na wakati tayari hapo unaendeshwa na hisia zako, tayari hapo jambo zuri linageuka kuwa baya maana wewe unaadhirika unataka kila kitu uwe nacho kitu ambacho hakiwezekani.

Tumeona wenyewe miaka kama minne huko nyma mambo yalivokuwa kwa vijana wakiume, suluali walikuwa wanavalia kwenye magoti milegezo ya kufa mtu wanajiita wahuni kwa kiga tabia za watu na kwa wenzetu wakina dada wao nao wanakangamoko sijui, sasa hivi wao wana mfumo mpya wa uvaji wa madela ambayo madela ni vazi la kuhemika wao sasa wamegeuza wanavaa wanavo jua wao.

Yote hii ni kuiga mambo ambayo hayana maana kabisa, na yanakuondolea heshima yako. Mambo haya yanapokuja ni vyema kujiuliza mara mbili hivi jambo hili ni zuri kweli kulifanya? Linanipa faida gani? Kwanini nafanya? Hapo utajua ufanye au usifanye ila ukumbuke usikubali kuendeshwa na dunia mambo mengine wacha yapi.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0659639168 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 3, 2017

Jiulize tena, tena na tena.

 Sadick Kilasi     November 03, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, karibu mpendwa tumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya haya yote aliyotutendea. E Mungu mwenyezi muumba mbingu na nchi tunakushukuru kwaajili ya siku hii mpya na uzima huu ambao mpaka sasa tunapumua, tunasema asante kwa kutujalia kuwa na uzima huu, si kwasasabu ya uwezo wetu bali upendo wako wewe, si kwasababu sisi ni wazuri sana bali ni upendo wako wewe, kwaajili hiyo tunakutukuza wewe Mungu wetu. Tunakuomba ukasimame mwenyrwe katika siku hii ya leo, kila mahala tutakapo kwenda kukanyaga na kushika nguvu na uweza wako ukatawale, katika kazi za mikono yetu ukasimame mwenyewe, tunaomba wakati wote utukumbushe kuwa watu wa uadilifu, heshima,nidhamu na kujituma ili tupate kujengeka katika misingi yetu ya mafanikio. Tunakuomba Mungu wetu utusamehe makosa yetu tuliyo fanya wakati wote.

Mpendwa wangu msomaji ipo haja ya wewe leo kukaa chini na kutafakali kwa makani sana, jiulize maswali wewe ni nani? kwanini upo duniani? kwanini Mungu kakuumba wewe? Nini kikubwa ambacho unatakiwa kukifanya hapa duniani?

Mpendwa wangu jiulize tena na tena bila kuchoka na hakikisha unapata majibu ambayo yatakufunulia yote hayo na mwisho wa siku utapata kujitambua. Hii ndiyo itakuwa tafakali ya leo na kwa maswali yote hayo usisahau kumtukuza mwenyezi Mungu.

Endelea kutembelea blogu hii ya JIKO LA USHAURI ili kujifunza zaidi na ukiacha maoni yako comment yako basi ni kitu kizuli sana na unaweza kujisajiri ili kupata makala jila inapotoka.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Makala hii imeandikwa na SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 2, 2017

Sababu kubwa kwanini wajasiriamali ni muhimu sana kwenye maisha yetu.

 Sadick Kilasi     November 02, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpya hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu, Mungu tunasema asante kwaajili ya siku hii mpya, tunashukuru kwa kutufanya tumeiona siku mpya maana tunaamini kuna watu wameshindwa kuiona siku hii, sio kwa sababu sisi tumefanya mambo mazuri sana hapana bali ni kwa upendo wako tu. Tuanaomba Baba akutubariki katika siku hii ya leo, katika mienendi yetu ukatutanguli wewe kila tunapo kanyaga na kufanya shughuli zetu, lakini pia tunaomba ubariki ndugu zetu, viongozi wetu, jamaa zetu na watu walio kata tamaa ukawabariki. Amina.

Mpendwa rafiki yangu karibu tena katka JIKO LA USHAURI ujifunze na kuongeza maarifa ili yakusaidie kwenye harakati zako za maisha na kujenga mafanikio makubwa. Leo mpendwa wangu nimekupikia makala yenye kichwa kisemacho [sababu  kubwa sana kwanini wajasiriamali ni muhimu sana kwenye maisha yetu].

Vitu vyote vizuri unavyoviona duniani hapa kama havijaumbwa na mwenyezi Mungu basi hiyo ni kazi ya mjasiriamali. Majumba makubwa, barabara nzuri, simu hiyo au kifaa hicho unachotumia kusomea haya makala hiyo yote ni kazi ya mjasiriamali. Watu hawa ni waajabu sana wanafanya kazi kubwa sana.

Wakati dunia inaumbwa ilikuwa haipo hivi, vitu vyote wao ndio wamefanya tufike hapa tulipo fika. Mwenyezi Mungu katuumba sisi, mawe milima na vitu vyote ikisha akamwambia mwanadamu hivi vyote virukao na vitembeavyo na vitu vyite vilivyo chini ya jua ni mali yako wewe, enenda katumie na kutawala. Lakini wajasiriamali pekee ndio wanao nufaika na kutawa vizuri vitu hivi.

Wao ndio hufanya kazi kubwa kutatua kero zinazo tukera duniani madaraja, barabara nzuri za kupitia magari, magari yenyewe ni kazi ya mikono yao. Wajasiriamali ni watu wa kujituma sana wanatumia bongo zao kuhakikiasha wanatatua kero zinazotukira. Ni wazi kabisa dunia imepitia vipindi tofautitofauti zama za mawe, zama za moto na zama za chuma  yote hii ni kazi yao. Jaribu kufikiria miaka kumi nyuma angalia dunia ilivyoenda mbali na kusonga mbele ambapo sasa hivi tunasema dunia ipo kwenye kiganja yote hii ni kazi ya mjasiriamali.

Mjasiriamali ni mtu wa namna gani? Yupoje na anaakili ya namna gani mpaka kutengeneza vitu vikubwa namna hii? Najua unaweza ukawa unajiuliza maswali kama hayo lakini majibu yake ni kwamba wajasiriamali ni watu wa kawaida tu. Ila wao wanapo kutana na changamoto huwa wanafikiria kwa kina sana na kusisimua bongo zao kitu ambacho sisi wengine hutufanyi jambo hilo. Wakikutana na changamoto wanaimeng'enyameng'enya  na kulichambua makini mkubwa sana na majibu yake ndo hapa tulipo fikia.

Kwahiyo ipo haja ya kusisimua ubongo wetu, kufikiri kwa kina ili kutatua kero zinazo tusumbua na hapo ndipo tutakapo kuwa wajasiriamali. Endelea kutembea mtandao huu ili kujifunza zaidi.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 1, 2017

Hii ndio siri kubwa ya woga

 Sadick Kilasi     November 01, 2017     UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena ambayo nisiku mpya, hatuna budi kusema asante Mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii mpya si kwa mapenzi yetu bali ni kwa mapenzi yako Mungu, tunaomba ututangulie katika siku hii yote, uwepo wako ukatubariki.

Mpendwa waangu karibu katika mafunzo haya ya makala ndani ya JIKO LA USHAURI upate kujifunza ili kujiongeza na kupata maarifa na hekima zaidi. Leo nimependa nikudokeze siri woga ulionao.

Leo sitaongea sana ila nitakuonyesha tu maana ya woga na jinsi ulivo na unavofanya kazi.

Woga ni utepe mwembamba sana ambao unaficha kitu kikubwa kilichopo mbele yako. Woga ni kutokuwa na uhakika na jambo linalofuata mbele yako. Kama wewe huna uhakika na jambo unalofanya woga ndio hutawala bila kujali kitu kile kipoje.

Woga huwa unaonyesha kufeli tu au matokeo hasi katika jambo hilo unalotaka kufanya. Woga huwa unafanya kazi haraka sana pale unapo kutana na jambo geni ambalo hujawahi kufanya kabisa. Hivi ndivyo woga unavyo fanya kazi.

Kwanini ni utepe mwembamba? Kwa sababu ni hali ndogo sana hata kama hujawahi kufanya jambo lile ukianza kufanya woga huondoka taratibu haijarishi ni matokeo gani utapata mazuri au mabaya. Kama wewe unajua kuendesha baiskeli basi kwa mara ya kwanza unajua jinsi ilivyokuwa na woga jinsi ulivyokuwa unakutawala. Tafakali hili mwenyewe ikisha unweza kukoment hapo chini.

Kuushinda woga inatakiwa kuanza kufanya kile kitu unachoogopa.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ▼  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ▼  November (22)
      • Huu ndio wakati ambao unaweza kujenga fikra zako n...
      • Hivi ndivyo unavyotakiwa kuishi kwenye jamii inayo...
      • Hii ndio sheria ya dunia
      • Kama bado unasubiri kitu hiki kutoka kwa wengine h...
      • Ijenge tabia ikisha nayo itakujenga wewe
      • Mbinu mbalimbali za kujifunza ili kuongeza maarifa...
      • Kila kitu kipo tayari unasubiri nini rafiki yangu ...
      • Hii ndio silaha pekee uliyonayo wewe ukiitumia viz...
      • Woga wako ndio umaskini wako
      • Jiulize, mimi nipo bize na nini?
      • Hata kama umekata tamaa bado kuna vitu vipo ndani ...
      • Mshinde kwanza huyu mpinzani wako ulienae kusafish...
      • Kama bado hujaanza biashara basi haya hapa ndio ma...
      • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye ana...
      • Hapa ndipo ushindi wa mafanikio unapoanzia
      • Ubongo wako ni karakana ambayo inayoshughulika kuk...
      • Huyu ndiye adui mkubwa wa mafanikio yako
      • Nyenzo kumi za kukufanya ufanikiwe kimaisha
      • Dunia inavokuendesha bila wewe kujua
      • Jiulize tena, tena na tena.
      • Sababu kubwa kwanini wajasiriamali ni muhimu sana...
      • Hii ndio siri kubwa ya woga
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates