Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji, Karibu tena katika blogu yetu ya JIKO LA USHAURI ili tupate kujifunza kwa pamoja.
Katika maisha wakati unafanya jambo lolote linalohusu jamii liwe zuri au baya tegemea upinzani kutoka kwa wengine. Hata kama unafanya jambo zuri kiasi gani lakini bado upinzani lazima utakuwepo.
Upinzani sio jambo baya, upinzani ndio unaofanya jambo zuri kusimama na kuinuka. Huwezi kukubarika kabla ya kupingwa, lazima upingwe ndipo ukubarike. Kupingwa na kukubarika ni lazima kuwepo kwa sababu ndio asili ya dunia, kwani kweli asingesimama kama uongo asingekuwepo.
Mpendwa msomaji, furahia anayekupinga maana yeye anakufanya jina lako liwe kubwa lakini mwogope mbaya maana huyo hataki hata kukusikia, yeye anaua ulicho nacho hataki hata kukusikia. Na ndiomaana hutakiwi kumukosoa mpinzani wako hadharani, atajitetea na wewe utaonekana mjinga, mwite faragha.
Anaye kupinga sio adui yako, adui yako upo naye anakuua kimyakimya.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Ombi usiache kuwashirikisha wengine ujumbe huu, lakini pia usiache kutoa maoni yako juu ya blogu hii.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment