Mara nyingi kunawakati huwa tunajutia mambo yetu, utasikia mtu akisema ningelijua, ningelifanya kitu fulani, ningelijua ningelisoma, ningelijua ngingeliokoka mapema.
Ni kweli tunajutia kwa mambo ambayo hatujafanya huko nyuma, lakini yameshapita, haijarishi yana nafasi kwa saizi au hayana nafasi, Ukianza kujutia sana lazima yatakuletea matatizo makubwa.
Ningelijua ningeli....Swali langu kwako wewe msomaji, Je ungefanya nini? Inaonekana kabisa ulikuwa hujui sasa kitu gani kinakufanya ujutie hivvo? Inawezekana ulikuwa unajua lakini hukufanya kwa sababu fulanifulani unazozijua wewe, lakini bado ulikuwa mjinga ulikuwa huna taarifa za kutosha kuhusu jambo hilo unalojutia.
Unajutia kwanini? Kuna mambo mengine huwezi hata kuyabadilisha kwenye hii dunia. Pia yapo mengine ambayo unaweza kufanya hata sasa, je kwanini unajutia? Mpendwa msomaji, usije ukajuta kwanini ulizaliwa kwani sio sababu yako wewe kuzaliwa na huwezi kubadilisha. Mpendwa msomaji ujutupo kwanini hukulea familia, basi acha kabisa kujuta chukua hatua sasa hivi kalee familia hata kwa neno tu inatosha na kama huna pesa acha kujuta tafuta pesa, unashindwa kuishi kwa sababu ya majuto yako.
Mpendwa msomaji ili kuondoa hofu inayotokana na woga ulionao juu mambo ya nyuma, kama huwezi kubadilisha acha liende na nishawahi kuandika makala kama hii istagramu, nilieleza kabisa muda mwingine ni kama tamaa kwa sababu unataka vyotevyote na haiwezi kuleta maana kabisa. Lakini kama hilo jambo unaweza kulibadili basi badili na lifanye kabisa.
Woga ni kwasababu ya yaliyopita na hofu ni kuhofia ya mbele kwa sababu ya woga, woga wako ndio umaskini wako Rose alisema kwenye nyimbo yake. Vijana hatuna cha kuhofia, lazima tuishi sasa na tutambue thamani ya muda.
Katika yale maneno matatu ya mwaka 2018 ya kusafirinayo, neno KUWA, bayana ya maneno mengine mawili ya FANYA na POKEA, Neno hili kuwa lina muhimu sana katika kuondoa woga na hofu, kwahiyo lazima tuishi sasa bila kukumbuka mabaya ya nyuma na tutasonga mbele.
Nikukumbushe pia falsafa ya mti, lazima mizizi iende chini, china lako liwe kubwa na matawi na majani na maua na matunda kwa wingi sana. OMBI; Niombe unisaidie kuwashirikisha wenngine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi, usiache kutoa maoni au pendekezo juu ya makala hii na blogu kwa ujumla, pia kuna mfumo wa kujiunga nasi ili upokee makala kwa njia ya barua pepe.
Wako Sadick kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment