Hofu ni hali ya kuhofia kuchukua hatua dhidi ya matokeo utakayopa. Hofu husababishwa na woga, woga husababishwa na matokeo, matokeo husababishwa na matendo.
Woga ni kutokubali matokeo. Zao la woga ni hofu. Woga huleta mgando, ambaye anashindwa kuchukua hatua kwa sababu ya kumbukumbu ya matokeo mabaya ya nyuma.
Matokeo ni kufauru au kushindwa, unapokuwa na hofu unakuwa mnyonge kupita kiasi. Unapokuwa huna woga kabisa juu ya hatua unayochukua na ukashindwa kuleta matokeo uliyotarajia, huleta woga.
Mpendwa msomaji, woga na hofu, vyote vinahitajika katika maisha ya mwanadamu, lakini kinachotakiwa ni kuwa na kiasi. Ukishindwa kuchukua hatua kwa woga unakuwa kama jiwe ambalo lipo kwenye ukingo wa maji, linaogopa kulowa maji wakati maji yanazidi kuula msingi wake. Lazima litalowa tu.
Endelea kujifunza kupitia blogu hii. Usiache kutoa maoni yako juu makala hii na blogu kwa ujumla pia usiache kuwashirikisha wengine ujumbe huu.
Wako Sadick Kilasi
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment