Moja kati ya tatizo kubwa ambalo linatukumba ni migogoro mbalimbali. Na matatizo mengi ndio yanaanzia hapa, migogoro ndio inasababisha kuvunjika kwa ndoa, matatizo makazini, vita, hofu na migogoro mingine kwa ujumla.
Tinaposhindwa kukubali ya kwamba sisi ndio chanzo cha migogoro na kuanza kuwanyoshea vidole wengine, hapo ndipo tatizo linapoanza, unapokuwa unategemea mazuri kutoka kwa wengine hapo ndipo migogoro inapoanzia, unapokuwa umeshindwa kujishusha wakati umekosea hapo ndipo migogoro inapoanza, unaposhindwa kutambua ya kwamba uwepo wako umesababisha migogoro hapo ndipo migogoro inapozidi kuwa mikubwa. Mpendwa msomaji, si wewe lakini ni wewe maana bila wewe isingetokea na wala usingeshuhudia hilo, chanzo kikubwa ni wewe na si mwingine. Anayeshuhudia migogoro ni wewe, anayehusika ni wewe.
Mpendwa rafiki yangu msomaji, migogoro ipo na haiwezi kuisha, jambo la muhimu kutambua ni kuchukulia ya kwamba wewe ndiye mhusika wa migogoro na ukitambua hilo usimchukie mpinzani wako na wala usijichukie wewe, kwasababu sisi ni binadamu na wote tunamapungufu, ukianza kutambua hilo huwezi kumchukia mwenzio au kujichukia mwenyewe, wewe chukia hali iliopo pale. Hapo ndipo utaanza kutambua dhamani yako na wengine, kumbuka tumelelewa tofauti kila mmoja wetu, tunapoanza kuwasilisha kila mmoja tabia yake lazima migogoro iwepo.
Mpendwa msomaji siku zote fanya kile ambacho kinawajenga watu na sio kuwabomoa, usibishane na mtu kama akikukosea bali wewe jishushe tu kwa sababu unaelewa.
Endelea kujifunza kupitia blogu hii. Usisahau kutoa maoni yako.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com//.
0 comments:
Post a Comment