Kumekuwa na tabia za watu kushindwa kabisa kuheshimu sheria na misingi ambazo wazee watu walipigania mpaka kuutoa uhai wao. Wazee wetu na mababu zetu walipigana vikali ili watoto wao tupate kuishi vema.
Tunaishi kwenye nchi kama Tanzania lakini hatujali na hatutambui ya kwamba wazazi wetu walipigania kwa nguvu hadi kutoa uhai wao kwa ajili ya amani ya Tanzania. Lugha hii nzuri ya kiswahili unayoisoma hapa watu walitumia ghalama kubwa sana kuhakikisha inakuwa lugha inayozungumzwa na watu. Lakini sasa hivi wapo watu ambao wanatumia lugha hiihii kuwaumiza wengine.
Dini tunazoenda kuabudu wapo watu ambao walikufa kwaajiri ya dini hiyohiyo ambayo wewe leo unaifanyia mzaha na kuikejeri. Mpendwa msomaji, hivi wazee wetu wanapotuona tunachezea dini ambayo wao walijitoa uhai kwaajili yetu sisi unafikiri wanajisikiaje? Hii mbaya sana hii.
Leo hii kijana unalewa na kutukana matusi ovyo wakati mzazi wako alikulea akitegemea utakuwa nguzo ya 👪 familia lakini wewe unaishia kuvuta bange na kulewa mapombe. Mpendwa msomaji tubadirike na tusimame imara kuenzi na kuendeleza misingi ya wazee wetu.
Leo hii tunawazungumzia akina Mwalimu Nyerere, Yesu, Mtume Muhammad, Kinjitikire Ngwale, Mkwawa, Martin Luther na mengine wengi walipigania ukweli ulio kuwa unapingwa vikali hadi kutoa uhai wao ili sisi tusimame kwenye msingi wa ukweli na usio yumbishwa na chochete, walipigana kwaajili yetu.
Mpendwa msomaji, tulichoachiwa kinamaana kubwa sana na tunapaswa kukilinda, kukiheshimu na kukiendeleza kwaajiri ya watoto wetu na wajikuu na vitukuu. Tunapoanza kuharibu na kuweka misingi yetu mibovu ya uongo tunakuwa tunaangamiza kizazi chetu kijacho. Lugha za matusi, kutokuwa na uumini wa dini za kiroho, ubinafsi ni vitu visivyo faa kwenye jamii, ni hatari kwa watoto wetu.
Mpendwa msomaji, tambua maisha ya mwili yana ukomo, watoto, wajukuu na vizazi vya baadae vinatutegemea sana sisi. Kuishi maisha ya hovyo saizi na ubinafsi ni kuangamiza watoto wetu. Unategemewa badirika.
Endelea kijifunza na kutembelea blogu hii, kuna mengi sana ya kujifunza.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment