Mwaka 2018 kwetu sisi mimi na wewe rafiki yangu mpendwa ni mwaka wa tofauti kabisa na ndiomaana nimeamua nikushirikishe maneno ambayo tutakwenda mwaka mzima na siyo kwa mwaka 2018 pekee bali maisha yetu yote. Maneno ambayo tunatakiwa kwenda nayo mwaka mzima ni KUWA, FANYA, POKEA.
Unaotumia maneno haya matatu katika jambo ambalo unalifanya au umelipeda, mafanikio ya ukweli kwako inakuwa sio kitu cha ajabu wala bahati.
KUWA, ni wewe mwenyewe kuhusika na hapa ndipo mchakato unapo anzia badala ya kutaka matokeo ambayo huna uelewa nayo kivipi yamefikia pale. Unapokuwa wewe mwenyewe, unaweza ukawa umependa kitu fulani sasa unachofanya ni kurudi kwenye mchakato ambao utakupeleka kwenye matokeo unayotaka. Mfano; wewe unapenda ulipwe mshahala wa milioni moja, badala ya kutaka ile milioni moja wewe unachatakiwa kujiuliza ni kwamba kivipi sasa naweza kuongeza au kutoa dhamani ili nilipwe milioni moja, huu ni mchakato kufikilia.
FANYA, sasa huu ndio mchakaato wa kuchukua hatua, ambao utakupeleka kwenye matokeo unayo taka, yale mambo unayofanya, juhudi unazoweka hapa ndipo unapohusika, unafanya wewe mwenyewe. Tukurudi kwenye mfani uleule wa milioni moja sasa baada ya kufikilia sasa wewe unachukua hatua, kama ni kuweka dhamani zadi katika maeneo yako ya kazi basi unaanza kuongeza dhamani, kwa njia yoyote unaofikilia.
POKEA, hii ndio hatua ambayo kila mtu anaipenda, au ni kwamba hili ndilo gori la kila mtu analopenda kufika , kwahiyo unapokea ulicho kifanya.
Rafiki yangu michakato hiyo mitatu ni ya muhimu sana katika kuyafikia malengo yetu mwaka huu 2018, unachotakiwa ni kutenda kazi yale unayojifunza.
Maisha ni KUWA+FANYA=POKEA
Endelea kujifunza kupitia blogu hii, ombi langu kwangu ni unisaidie kuwashirikisha wengine ili ujumbe huu uwafikie wengi zaidi, na kama unaswali lolote basi tuwasiliane kwa 0687000768, tuma ujumbe nitakujibu, au kwa bara pepe ni sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment