JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, January 30, 2018

Mda wa maisha ni mfupi unapokuwa unakazana kufanya hivi.

 Sadick Kilasi     January 30, 2018     NJOZI     No comments   

Maisha ni mafupi sana, unapokazana kufanya kila kitu, Maisha ni mafupi sana, unapokazana kukusanya vitu vyote vya dunia.
Maisha ni mafupi sana, unapokuwa mbinafsi sana lakini pia maisha yanakuwa mafupi pale unapokuwa na tamaa sana.
Ni kweli kabisa maisha ni mafupi sana, kiwango cha kawaida ni miaka sabini, lakini ukijitaidi sana miaka themanini, mda ni mdogo sana.
Mpendwa msomaji, maisha ni marefu sana, unapokuwa umetambua kusudi la kuishi maisha na ukakamirisha kwa mda, maisha ni marefu sana.
Jambo la msingi ndugu msomaji,  kazana kufanya mambo ya muhimu achana kukazana kukimbizana na kila kitu, mda wa maisha ni mfupi sana, chagua ya muhimu kwako yafanyie kazi na kamieisha mambo mengine anachana nayo, dinia hii ya matokeo kila siku jambo jipya linaibuka na huwezi kwenda na kila kitu.
Endelea kutembelea blogu hii kijifunza zaidi. Tafadhari usiache kuwashirikisha wengine ujumbe huu.
Wako Sadick Kilasi
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Unapohofia kuchukua hatua .

 Sadick Kilasi     January 30, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Hofu ni hali ya kuhofia kuchukua hatua dhidi ya matokeo utakayopa. Hofu husababishwa na woga, woga husababishwa na matokeo, matokeo husababishwa na matendo.
Woga ni kutokubali matokeo. Zao la woga ni hofu. Woga huleta mgando, ambaye anashindwa kuchukua hatua kwa sababu ya kumbukumbu ya matokeo mabaya ya nyuma.
Matokeo ni kufauru au kushindwa, unapokuwa na hofu unakuwa mnyonge kupita kiasi. Unapokuwa huna woga kabisa juu ya hatua unayochukua na ukashindwa kuleta matokeo uliyotarajia, huleta woga.
Mpendwa msomaji, woga na hofu, vyote vinahitajika katika maisha ya mwanadamu, lakini kinachotakiwa ni kuwa na kiasi. Ukishindwa  kuchukua hatua kwa woga unakuwa kama jiwe ambalo lipo kwenye ukingo wa maji, linaogopa kulowa maji wakati maji yanazidi kuula msingi wake. Lazima litalowa tu.
Endelea kujifunza kupitia blogu hii. Usiache kutoa maoni yako juu makala hii na blogu kwa ujumla pia usiache kuwashirikisha wengine ujumbe huu.
Wako Sadick Kilasi
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, January 28, 2018

Wanao leta upinzani, wanatuinua.

 Sadick Kilasi     January 28, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji,  Karibu tena katika blogu yetu ya JIKO  LA USHAURI ili tupate kujifunza kwa pamoja.
Katika maisha wakati unafanya jambo lolote linalohusu jamii liwe zuri au baya tegemea upinzani kutoka kwa wengine. Hata kama unafanya jambo zuri kiasi gani lakini bado upinzani lazima utakuwepo.
Upinzani sio jambo baya, upinzani ndio unaofanya jambo zuri kusimama na kuinuka. Huwezi kukubarika kabla ya kupingwa, lazima upingwe ndipo ukubarike. Kupingwa na kukubarika ni lazima kuwepo kwa sababu ndio asili ya dunia, kwani kweli asingesimama kama uongo asingekuwepo.
Mpendwa msomaji, furahia anayekupinga maana yeye anakufanya jina lako liwe kubwa lakini mwogope mbaya maana huyo hataki hata kukusikia, yeye anaua ulicho nacho hataki hata kukusikia. Na ndiomaana hutakiwi kumukosoa mpinzani wako hadharani, atajitetea na wewe utaonekana mjinga, mwite faragha.
Anaye kupinga sio adui yako,  adui yako upo naye anakuua kimyakimya.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Ombi usiache kuwashirikisha wengine ujumbe huu, lakini pia usiache kutoa maoni yako juu ya blogu hii.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, January 27, 2018

Tunaposhindwa kuheshimu misingi ya mababu zetu.

 Sadick Kilasi     January 27, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Tunaposhindwa kuheshimu misingi ya mabuzetu wa zamani na kuanzisha misingi yetu mibovu,  tunakuwa tunakosea sana. Mababu na wazee wetu wa zamani walitutengenezea misingi imara ambayo mpaka sasa itatufanya tumesimama imara.

Kumekuwa na tabia za watu kushindwa kabisa kuheshimu sheria na misingi ambazo wazee watu walipigania mpaka kuutoa uhai wao. Wazee wetu na mababu zetu walipigana vikali ili watoto wao tupate kuishi vema.

Tunaishi kwenye nchi kama Tanzania lakini hatujali na hatutambui ya kwamba wazazi wetu walipigania kwa nguvu hadi kutoa uhai wao kwa ajili ya amani ya Tanzania. Lugha hii nzuri ya kiswahili unayoisoma hapa watu walitumia ghalama kubwa sana kuhakikisha inakuwa lugha inayozungumzwa na watu. Lakini sasa hivi wapo watu ambao wanatumia lugha hiihii kuwaumiza wengine.

Dini tunazoenda kuabudu wapo watu ambao walikufa kwaajiri ya dini hiyohiyo ambayo wewe leo unaifanyia mzaha na kuikejeri. Mpendwa msomaji, hivi wazee wetu wanapotuona tunachezea dini ambayo wao walijitoa uhai kwaajili yetu sisi unafikiri wanajisikiaje? Hii mbaya sana hii.

Leo hii kijana unalewa na kutukana matusi ovyo wakati mzazi wako alikulea akitegemea utakuwa nguzo ya 👪 familia lakini wewe unaishia kuvuta bange na kulewa mapombe. Mpendwa msomaji tubadirike na tusimame imara kuenzi na kuendeleza misingi ya wazee wetu.

Leo hii tunawazungumzia akina Mwalimu Nyerere, Yesu, Mtume Muhammad, Kinjitikire Ngwale, Mkwawa,  Martin Luther na mengine wengi walipigania ukweli ulio kuwa unapingwa vikali hadi kutoa uhai wao ili sisi tusimame kwenye msingi wa ukweli na usio yumbishwa na chochete, walipigana kwaajili yetu.

Mpendwa msomaji, tulichoachiwa kinamaana kubwa sana na tunapaswa kukilinda, kukiheshimu na kukiendeleza kwaajiri ya watoto wetu na wajikuu na vitukuu. Tunapoanza kuharibu na kuweka misingi yetu mibovu ya uongo tunakuwa tunaangamiza kizazi chetu kijacho. Lugha za matusi, kutokuwa na uumini wa dini za kiroho, ubinafsi ni vitu visivyo faa kwenye jamii, ni hatari kwa watoto wetu.

Mpendwa msomaji, tambua maisha ya mwili yana ukomo, watoto, wajukuu na vizazi vya baadae vinatutegemea sana sisi. Kuishi maisha ya hovyo saizi na ubinafsi ni kuangamiza watoto wetu. Unategemewa badirika.

Endelea kijifunza na kutembelea blogu hii, kuna mengi sana ya kujifunza.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Kama bado umekuwa unasubiri hali hizi mbili kutoka kwa wengine, hutopata.

 Sadick Kilasi     January 27, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, hongera mpendwa msomaji kwa ajili ya siku hii ambayo umefanikiwa kuingia. Mungu wetu ameandaa kila kitu na ndiomaana sisi tunaingia siku ambayo mwenyewe alisha iandaa. Mungu alitutengenezea mazingira ya kufurahia hapa duniani ila sisi tunaenenda tunavotaka sisi na kutengeneza mbinu za kwetu na hapo ndipo maisha yanapokuwa magumu.

Moja kati ya misemo au kauli ambazo hutumika mitaani kwenye suala la upendo ni nampenda anaye nipenda, anayenipenda bado hajazaliwa. Na kwenye furaha tumekuwa tukiitafuta furaha kwa gharama kubwa mno ambayo imekuwa ikishindwa kutupa matokeo tunayotaka, kutafuta pesa, kutibiwa unapoumwa, kuoa mwanamke mzuri na mengine mengi ya dunia hii, tunachohangaikia ni furaha tu.

Vitu hivi viwili Upendo na furaha tunavitafuta kwa nguvu sana. Tumekuwa tukitegemea kutoka kwa wengine na tukitambua ya kwamba wao ndio watakao tupa furaha.

Watu wa dunia hii ni waajabu sana wamejaa tumejaa ubinafsi wa kutosha, kila kitu tunataka kupewa kutoka kwa wengine. Watu wote wanao jaribu kuwapatia vitu watu wanachotaka ni kuona wengine wanafurahi na wao ndio wafurahi.

Tumekuwa tukisubiri upendo kutoka kwa wengine baada ya kuona wale tunao jaribu kuwapatia vitu wanafurahia kwa mda harafu furaha ile inakata kama mafuta ya taa na moto. Tukijaribu sana kuwapatia vitu wengine na mwisho tunaona tumeferi mwisho tunasema na kusingizia ya kwamba anaye nipenda bado hajazaliwa.

Hali hizi mbili zimekuwa zikitafutwa kama vitu kwenye hii dunia. Mpendwa msomaji anayekupenda na anaye kufurahia wewe humjui kwani hadi mzazi mwenyewe anategemea mtoto wake afurahie na ndipo na yeye afurahi. Kwa sababu unapotegemea unaweza kusaliti ukipata sehemu nyingine. Upendo wa mzazi huwa unapungua mtoto anapokuwa mkubwa kwa sababu mtoto anakuwa mbali na mzazi, mzazi anashindwa kutegemea furaha ya moto.

Firaha ya kweli na upendo wa kweli uko wapi? Tunaweza kujifunza kutoka kwa watoto wadogo vichanga, ambao bado hawajamezwa na ya dunia hii huwa wanakuwaje. Watoto wadogo hawa hufurahi pasipo kufurahishwa, hupenda pasipo kuchagua.

Mpendwa msomaji watoto hawa hawategemei furaha ya wazazi wao, ila wao ndio hugawa furaha kwa wengine, hata wewe ikunje uso vipi kenyewe kanakuchekea tu, ukicheka yeye anaongeza kicheko.

Mpendwa msomaji unamsubiri wa kukupenda, unamfurahia anayekufurahisha, wewe hutapata furaha na upendo kamwe kwa wengine, vyote hivyo unavyo, wewe ni kuashilia tu basi.

Endelea kukifunza kupitia blogu hii, yapo mengi ya kujifunza zaidi na zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com. Tuma ujumbe au maoni nitakujibu.
Jiko la ushauri 
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, January 25, 2018

Tatizo sio wao, tatizo ni wewe na migogoro ndipo inapoanzia

 Sadick Kilasi     January 25, 2018     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki, natumai umeamka salama na upo tayari kwa ajiri ya kwenda kuweka kazi na matokeo chanya katika majukumu yako. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kitujalia siku hii. Si kwasababu sisi tunafaa sana bali ni neema tu zinazotubeba. Wapo watu ambao walitamani kuiona siku hii lakini wameshindwa, sisi tulio pata fursa hii lazima tuitumie vizuri katika mambo yetu na mipango yetu na kuacha legacy kwa ajili ya wengine.

Moja kati ya tatizo kubwa ambalo linatukumba ni migogoro mbalimbali. Na matatizo mengi ndio yanaanzia hapa, migogoro ndio inasababisha kuvunjika kwa ndoa, matatizo makazini, vita, hofu na migogoro mingine kwa ujumla.

Tinaposhindwa kukubali ya kwamba sisi ndio chanzo cha migogoro na kuanza kuwanyoshea vidole wengine, hapo ndipo tatizo linapoanza, unapokuwa unategemea mazuri kutoka kwa wengine hapo ndipo migogoro inapoanzia, unapokuwa umeshindwa kujishusha wakati umekosea hapo ndipo migogoro inapoanza, unaposhindwa kutambua ya kwamba uwepo wako umesababisha migogoro hapo ndipo migogoro inapozidi kuwa mikubwa. Mpendwa msomaji, si wewe lakini ni wewe maana bila wewe isingetokea na wala usingeshuhudia hilo, chanzo kikubwa ni wewe na si mwingine. Anayeshuhudia migogoro ni wewe, anayehusika ni wewe.

Mpendwa rafiki yangu msomaji, migogoro ipo na haiwezi kuisha, jambo la muhimu kutambua ni kuchukulia ya kwamba wewe ndiye mhusika wa migogoro na ukitambua hilo usimchukie mpinzani wako na wala usijichukie wewe, kwasababu sisi ni binadamu na wote tunamapungufu, ukianza kutambua hilo huwezi kumchukia mwenzio au kujichukia mwenyewe, wewe chukia hali iliopo pale. Hapo ndipo utaanza kutambua dhamani yako na wengine, kumbuka tumelelewa tofauti kila mmoja wetu, tunapoanza kuwasilisha kila mmoja tabia yake lazima migogoro iwepo.

Mpendwa msomaji siku zote fanya kile ambacho kinawajenga watu na sio kuwabomoa, usibishane na mtu kama akikukosea bali wewe jishushe tu kwa sababu unaelewa.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii. Usisahau kutoa maoni yako.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com//.



Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, January 24, 2018

Wewe ni kuchagua tu, kila kitu kipo pande mbili.

 Sadick Kilasi     January 24, 2018     No comments   

Moja ya vitu vya kushangaza kwenye hii dunia kila kitu kipo tayari yaani wewe ni kuchagua tu, chagua upande mmoja kuwa nacho au kutokuwanacho, kukataa au kukubali. Dunia hii inamaajabu yake kila kitu ni chaguo, lazima ufanye chaguo kwenye kila jambo.

Mpendwa rafiki yangu, unazingatia kitu gani unapofanya chaguo kwenye mambo yoyote unayoyofanya? Maana kila kitu ni chaguo. Naomba tushirikishane ili tujifunze kwa pamoja namna ya kufanya chaguo kwa kutoa maoni yako.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii, usiache kutushirikisha wewe unazingatia nini unapofanya chaguo.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, January 23, 2018

Tabia hizi mbili, ndizo zinazokufanya kuwa mtu mwenye manufaa kwa watu na kupoteza utu wako.

 Sadick Kilasi     January 23, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, siku mpya ambayo mwenyezi Mungu katujalia kuiona, na sisi hatuna budi kuitambua siku hii ya kwamba ni siku ya muhimu kwetu. Siku muhimu lazima tuidhamini na gharama yake ni kubwa mno kwa sababu tumeifikia kwa neema tu za mwenyezi Mungu. Wapo ambao walitamani kuiona siku lakini wameshindwa, sisi ambao tumejaliwa kuiona lazima tuidhamini siku hii na kutoa matokeo chanya katika maeneo mbalimbali ya shughuli zetu.

Mpendwa msomaji karibu katika makala ya leo, makala hii ya leo inakichwa kinachosema, tabia hizi mbili, ndizo zinazokufanya kuwa mtu mwenye manufaa kwa watu na kupoteza utu wako. Tabia hizi mbili ndizo ambazo zinaweza kukupa mafanikio ya kweli au kuwa mtu mwenye manufaa kwa watu. Ninaposema mtu mwenye manufaa kwa watu ni yule mtu ambaye anatumika kama chombo tu yaani anakuwa ni usefully kwa mtu. Mtu ambaye anatumika kwa mtu huwa anakosa umuhimu, wakati wowote anaweza kupakiwa kama chombo fulani, mfano ghari, simu yaani vitu vyote huwa ni vya kupaki pale vinapokosa manufaa na haviwezi kutumika tena.

Hii ni changamoto ambayo inatukumba wengi sana, hasa tabaka la chini kabisa na la kati. Watu maskini na watu tabaka la kati huingia kwenye changamoto hii bila wao wenyewe kujua sababu zilizopelekea kuwa hivo. Watu wenye manufaa ni wale watu ambao kila siku wanapambana na kutetea nafasi zao za kazi na hata kwenye biashara hali hii ipo. Ukiona wewe kila siku unapambana kutokuachishwa kazi, basi tambua wewe ni mwenye manufaa, ukiona wewe unapambania cheo fulani tambua wewe ni mwenye manufaa. Rafiki yangu chenye manufaa kimekosa umuhimu, kwahiyo wakati wowote kinaweza kupakiwa pembeni.

Hizi ndizo tabia mbili ambazo zinakufanya uwe mtu wa manufaa kwa watu na kugeuzwa kitu na kupoteza utu wako.

1.Ubinafsi. Tabia ya ubinafsi ndio tabia ya kwanza ambayo hupelekea kuwa kitu kwa watu badala ya kuwa mtu. Ubinafsi hupelekea kuwa mtu mwenye manufaa kwa watu, huwezi kuona watu wanachangamoto gani, unachojali wewe ni tumbo lako tu. Kuna msemo mmoja ambao watu wa kipato cha chini hupenda kuutumia kwamba 'natafuta pesa ya kula tu', ni msemo mbaya sana. Walio fanikiwa ni watu ambao wametatua matatizo ya wengine yaani watu. Wanacho kazana wao ni kutatua changamoto za watu na hapo umuhimu wao kwenye jamii unaonekana. Unaposema natafuta pesa ya kula tu ni lazima utaendelea kupambania kakazi uliko nako kwa sababu unajijali wewe tu.

2.Kukosa mtazamo mwiingine juu ya kile unachafanya. Kuendelea kufanya kile unachofanya kwa sababu anaona ya kwamba hakuna namna basi lazima utaendelea kuwa mwenye manufaa, mtakuwa mnapabania kitu kimoja na yule mwajiri anaangalia na kuchagua ni yupi mwenye manufaa makubwa kwangu ndiye anaye nifaa, akisha kupata yule ataendelea kupambania cheo chake na zama hizi wapo wengi wasomi na mwisho na utapoteza utu kwa kupakiwa pembeni.

Mpendwa msomaji, tulikuja duniani kuziba mapengo penye pango na sio kupambania pengo.Tunakosa umuhimu kwa sababu ya ubinafsi wetu, tunakosa umuhimu kwenye jami kwa sababu ya mtazamo wetu mdogo, tumekuja kusababisha utu palipokosa utu, tunaalikwa kutatua changamoto za watu, na sio kuwa mtu mwenye manufaa kwa mtu mmoja yaani unageuzwa kuwa gari yaani natumia kwa mda harafu nitaacha, mbaya sana hii.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii, na OMBI; Naomba nisaidie kushirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi, usiache kutoa maoni yako juu ya makala hii na blogu kwa ujumla.

Wako SADICK KILASI wa jikolaushauri.blogspot.com
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmaili.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, January 22, 2018

Ningelijua ninge....Je ungefanya nini?

 Sadick Kilasi     January 22, 2018     MAHUSIANO, TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Ni siku nyingine tena siku mpya, ambayo mwenyezi Mungu katujalia kuiona, hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa ajiri ya hili. Ni neema na rehema za Mungu kuiona siku mpya kwani sisi hatukustahili hata kuiona siku hii. Mungu mkuu, Mungu wa upendo, katufanya kuwa wana na kutupa rehema na mimi na wewe tukaiona siku hii.

Mara nyingi kunawakati huwa tunajutia mambo yetu, utasikia mtu akisema ningelijua, ningelifanya kitu fulani, ningelijua ningelisoma, ningelijua ngingeliokoka mapema.

Ni kweli tunajutia kwa mambo ambayo hatujafanya huko nyuma, lakini yameshapita, haijarishi yana nafasi kwa saizi au hayana nafasi, Ukianza kujutia sana lazima yatakuletea matatizo makubwa.

Ningelijua ningeli....Swali langu kwako wewe msomaji, Je ungefanya nini? Inaonekana kabisa ulikuwa hujui sasa kitu gani kinakufanya ujutie hivvo? Inawezekana ulikuwa unajua lakini hukufanya kwa sababu fulanifulani unazozijua wewe, lakini bado ulikuwa mjinga ulikuwa huna taarifa za kutosha kuhusu jambo hilo unalojutia.

Unajutia kwanini? Kuna mambo mengine huwezi hata kuyabadilisha kwenye hii dunia. Pia yapo mengine ambayo unaweza kufanya hata sasa, je kwanini unajutia? Mpendwa msomaji, usije ukajuta kwanini ulizaliwa kwani sio sababu yako wewe kuzaliwa na huwezi kubadilisha. Mpendwa msomaji ujutupo kwanini hukulea familia, basi acha kabisa kujuta chukua hatua sasa hivi kalee familia hata kwa neno tu inatosha na kama huna pesa acha kujuta tafuta pesa, unashindwa kuishi kwa sababu ya majuto yako.

Mpendwa msomaji ili kuondoa hofu inayotokana na woga ulionao juu mambo ya nyuma, kama huwezi kubadilisha acha liende na nishawahi kuandika makala kama hii istagramu, nilieleza kabisa muda mwingine ni kama tamaa kwa sababu unataka vyotevyote na haiwezi kuleta maana kabisa. Lakini kama hilo jambo unaweza kulibadili basi badili na lifanye kabisa.

Woga ni kwasababu ya yaliyopita na hofu ni kuhofia ya mbele kwa sababu ya woga, woga wako ndio umaskini wako Rose alisema kwenye nyimbo yake. Vijana hatuna cha kuhofia, lazima tuishi sasa na tutambue thamani ya muda.

Katika yale maneno matatu ya mwaka 2018 ya kusafirinayo, neno KUWA, bayana ya maneno mengine mawili ya FANYA na POKEA, Neno hili kuwa lina muhimu sana katika kuondoa woga na hofu, kwahiyo lazima tuishi sasa bila kukumbuka mabaya ya nyuma na tutasonga mbele.

Nikukumbushe pia falsafa ya mti, lazima mizizi iende chini, china lako liwe kubwa  na matawi na majani na maua na matunda kwa wingi sana. OMBI; Niombe unisaidie kuwashirikisha wenngine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi, usiache kutoa maoni au pendekezo juu ya makala hii na blogu kwa ujumla, pia kuna mfumo wa kujiunga nasi ili upokee makala kwa njia ya barua pepe.

Wako Sadick kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Maajabu niliyokutana nayo nilipo jiangalia kwenye kioo.

 Sadick Kilasi     January 22, 2018     PATA BLOGU, TAFAKARI YA ROHO, USWAZI TRICK     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI,  hongera kwa kuiona siku hii mpya. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu aliyetuarika siku hii ya leo na tumeifikia. Ni kwa neema tu sisi kuiona siku hii ya leo, maana wapo ambao walitamani kuiona siku lakini haijawa hivo, ni upendo na rehema zake tu kwetu.

Leo mpendwa msomaji, nakwenda kukushirikisha maajabu niliyo kutananayo nilipo jiangalia kwenye kioo. Karibu tuwe pamija mpaka mwisho ili nawe uyaelewe vizuri maajabu hayo.

Nilikuwa najiangalia kwenye kioo, nilikuwa saluni, nikajiangaliaaaa nikaondoka, nilipofika nje nikaona kama nimesahau hivi, nikarudi tena, nikajiangalia vizuri kabisa na kujikagua, nikatoka, nilipofika nje, nikajisahau tena, nikarudi nikajiangalia tena, nikatoka nje, nikajisahau tena lakini hapo nikakumbuka kuna siku niliwahi kusoma mstari mmoja kwenye biblia unaosema 'imani bila matendo ni kma mtu kujiangalia kwenye kioo, akisha kujiangalia na kuondoka anajisahau'.

Mpendwa rafiki yangu msomaji unayesoma hapa, inawezekana kuna mipango mingi sana ambayo umepanga kuifikia mwaka 2018, kama mtu anayejiangalia kwenye kioo yaani utakuwa feki. Imani na matendo ni vitu ambavyo vinaenda sambamba, unafanya kile unacho amini. Imani ni hali lakini matendo ni kitendo kinaonekana. Ili cha ndani kipate kuonekana nje lazima kuwe na matendo si kuamini tu. Tuamini na tutende.

Endelea kutembea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI. Naomba unisaidie kuwashirikisha wengine ili ujumbe uwafikie wengi zaidi. Usisahau kutoa juu ya makala hizi na blogu kwa ujumla.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, January 20, 2018

Hii ndio sababu ambayo inafanya watu kupitia changamoto kwenye maisha.

 Sadick Kilasi     January 20, 2018     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, USHAURI     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai umeamka salama kabisa. Ni siku nyingine tena, kwa neema ya mwenyezi Mungu tumeifikia siku hii, basi hatuna budi wa kumshukuru yeye kwa sababu yeye ndiye ndiye mweza wa kila kitu. Pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya jambo lolote. Kwa neema zake na huruma basi anatuamsha kila siku, japo wapo ambao walitamani kuiona siku hii lakini wameshindwa, je? sisi ni akina nani mpaka sasa tu salama?

Karibu mpendwa msomaji tujifunze kwa pamoja somo nililo kuandalia leo, sababu ambayo inawafanya watu kupitia changamoto kwenye maisha.

Imekuwa ni tabia ya kawaida watu kulalamika wakati tunapitia kwenye changamoto, tumekuwa tukiona kama tumetengwa na wengine na kuona kama wengine hawatujali kabisa. Tumekuwa tukitaka kufurahia maisha wakati wote, bila kujiuliza ukifurahia maisha wakati wote kitu gani kitatokea? Tumesahau kabisa ya kwamba bila changamoto huwezi kuona furaha, lazima changamoto iwepo harafu ndipo furaha ifuate.

Maisha yangekosa hizi pande mbili basi yangekuwa hayana maana kabisa, je? tungepata furaha wapi bila kupitia ladha hii ya changamoto?

Sababu kubwa inayofanya sisi tupitie changamoto ni tupate ukomavu na wala si mateso, ni wakati ambao tunatengenezwa kuwa wastahimilivu, tunatengenezwa kuwa na subiri w, watu wagumu na wenye nguvu ya uvumilivu.Mungu anapo acha tupitie hali hii anataka kutupa nafasi nyingine zaidi sasa ili  aone ukomavu wetu lazima atuache kidogo tupitie changamoto na aone ustahimili wetu, akiona tu wakomavu anatupa cheo kinachofuata lakini kama tukishindwa hatupi kabisa.

Mpendwa msomaji cgangamoto ni ladha ya maisha, changamoto ni sehemu ya ukomavu wa kuifikia nafasi nyingine.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi, pia naomba unisaidie kuwashirisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi.

Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com. Toa maoni kuhusu blogu hii kupitia mawasiliano hayo.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, January 19, 2018

Hili ndilo neno ambalo ukitamka tu, lazima utafanikiwa katika jambo unalotaka kufanya

 Sadick Kilasi     January 19, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Habari rafiki? Karibu katika makala ya leo ambayo nimekuandalia leo ili tujifunze kwa pamoja mimi na wewe msomaji wangu.

Katika maisha kuna mengi sana tumekuwa tunayafanya, kuna mengi sana tumekuwa tunayatenda, kunamengi sana tumekuwa tunayanena. Tumekuwa tunayafanya mengi kwa kuwajenga wengine lakini wakati mwingine tumekuwa tunawabomoa na kuwaumiza wengine na wakati mwingine tumekuwa tunajiumiza wenyewe.

Lakini yote haya ambayo tumekuwa tunayafanya yamekuwa yakitegemea neno moja tu, 'sababu' Neno hili linaweza kutumika vizuri au linaweza kutumika vibaya. Neno hili linamtegemea mtumiaji mhusika mwenyewe, linaweza kutumika kubomoa au linaweza kutumika kujenga.

Wakati ambapo limekuwa likitumika kujenga, mfano; sababu iliyonifanya nifungue biashara ya duka la vyakula eneo hili ni uhaba wa maduka ya vyakula maeneo haya, sababu iliyo nifanya niweke usafiri maeneo haya ni uhaba wa daladala maeneo haya. Kwa hapa neno hili limetumika ili kuwasaidia wengine, na sababu zenyewe zinaleta maana kabisa.

Lakini pia hili neno linaweza likatumika kuwaumiza wengine, mfano; sababu iliyonifanya nifungue duka la vyakula maeneo haya nimeona nimeona huyu jamaa anauza sana kwahiyo hii biashara maeneo haya inalipa, sababu ya kutokufanya biashara kwa sababu nimekosa kampani ya watu. Rafiki yangu huku pia sababu zinaleta maana kabisa.

Neno hili linatakiwa kutumika vizuri sana. Jambo lolote lile ukilipa sababu linanguvu sana na ndio maana hata siku moja hutoweza ona watu wote wamekubali kitu kimoja hata kiwe kizuri kiasi gani wapo watakao pinga kwa sababu ya sababu. Watapinga jambo zuri na wataeleweka kwa wengine na upinzani utakuwa mkubwa na maana ya kupinga itaonekana, nimemwuua kwa sababu ni mwizi, inaleta maana lakini ni mbaya sana hii.

Mimi na wewe rafiki yangu neno sababu lipite pale tu, tunapotaka kuwajenga wengine na sio kubomoa wengine, kutatua matatizo ya wengine. Ukianza na wewe, utaishia na wewe. Usifanye kitu cha kibinafsi huwezi leta maana hata siku moja. Hivi rafiki yangu ushawahi kujiuliza kwa kwanini viongozi wa serikali huwa wanaanza kwa unyenyekevu halafu mwishoni wanakuwa mafisadi. Alianza kwa kuanza kutatua mataizo ya kwake binafsi, alikuwa hana hela ndio maana akagombea sasa hii ni sababu mbaya katika uongozi, anza kuangalia matatizo ya watu kabla ya wewe, hutokuwa fisadi.

Sababu iliyotufanya tuwepo si kwasababu tupo, ni kwasababu ya wengine kwani tulikuwepo kabla ya kuwepo. Sababisha kwa wengine.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii ya JIKO LA USHAURI, pia naomba unisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi, utakuwa umesababisha.
Katika yale maneno matatu ya mwaka 2018, neno la KUWA, linataka uwe unapenda kujiuliza wewe mwenyewe.

Wako SADICK KILASI wa jikolaushauri.blogspot.com
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com, leo usiache kutoa oni au dukuduku yako.
Asante.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, January 18, 2018

Sio kila jambo sawa, mambo mengine ni upuuzi tu.

 Sadick Kilasi     January 18, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu mpendwa, siku mpya, hongera kwaajiri ya siku hii mpya na hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii mpya. Ni kwa neema na rehema za upendo wake sisi kuina siku hii ya leo. Jambo moja ambalo unatakiwa kulitambua wewe msomaji ni kwamba wapo wengi sana ambao walitamani sana kuiona siku hii lakini wameshindwa, sasa wewe ni nani mpaka uione siku hii ya leo? Kwa maana hiyo lipo kusudi kubwa ambalo mwenyezi Mungu anataka utende si bure rafiki yangu.

Karibu katika somo la leo, ili kwa pamoja tupate kujifunza hili jambo ambalo mimi rafiki yako nimekuandalia wewe msomaji wangu.

Katika dunia hii ya sasa, dunia yenye mambo mengi ya kufanya, dunia iliyojaa wapimgaji wengi na wakatisha tamaa, dunia yenye kelele nyingi za vitu, dunia yenye ya walio feli wengi na walio fanikiwa, dunia ambayo wakati hauendi na mtu lakini binadamu wanaenda nao, dunia iliyojaa fursa nyingi sana mpaka zinakuwa utapeli, dunia iliyojaa kiza kinene kwa kutokuwa na taarifa sahihi, dunia iliyojaa matokeo mengi kuliko kawaida sio kila jambo ni sahihi, mambo mengine ni UPUUZI tu, ndio ni upuuzi tu.

Hatuwezi kwenda na kila kitu lazima mengine tuchukulie kama upuuzi tu. Akili zetu haziwe kupokea kila kitu, sasa sisi tutakuwa ni dampo la kutupia takataka, mambo mengine ni upuuzi na bora niwe mjinga kwenye mambo mengine maana kila mtu anaujinga wake. Bora niwe mshamba tu, mimi siendi na wakati, wacha wakati uende zake.

Istragram na kubishana na watu, mwaka 2018 kwangu mimi ni upuuzi tu, siwezi kuvipa mda vitu hivi, upuuzi huu.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii ili kupata maarifa zaidi na pia usiache kunishirikisha mambo ambayo kwako wee msomaji mwaka 2018 ni upuuzi tu yaani huwezi kuvipa mda hata kidogo. Nishirikishe kwa kunitumia meseji na kwa maoni na
ushauri.

Wako Sadick Kilasi,
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, January 17, 2018

Wazo lenye nguvu

 Sadick Kilasi     January 17, 2018     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu, siku mpya ambayo mwenyezi Mungu katujalia kuiona. Sisi tulio wazima wa afya hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya upendo wake wa kutujalia siku hii ya leo. Kwaajili ya neema na rehema za mwenyezi Mungu tumejaliwa kuiona siku hii mpya. Tunasema ni neeema na rehema za mwenyezi Mungu ni kwa sababu si kwa uweza wetu au si kwa sababu tumebarikiwa sana hapana ila ni kwa sababu ni neema ya bure ya mwenyezi Mungu.

Karibu tujifunze kupitia makala ya leo ambayo nimekuandalia wewe mpendwa wangu msomaji ili wote kwa pamoja tupate kujifunza na tunufaike kwa namna moja au nyingine kwa namna kila mmoja atakavo jaliwa kuelewa.

Moja kati ya sifa ya Mwalimu Nyerere ni kupenda watu wawe katika hali ya umoja, na hiki ndicho kitu ambacho Mwalimu alikipigania sana. Pamoja na yote aliyofanya yeye alitaka watu tuwe na umoja. Alijitaidi sana kutengeneza umoja na amani, yeye alipiga vita sana ukabila na udini, alipiga vita sana ubinafsi yaani umimi, alipiga vita sana udini. Mwalimu aliona mbali alitambua ya kwamba tukiwa na umoja amani itapatikana. Yeye alitamani Afrika nzima kiwe kitu kimoja, Mwalimu hakufanya yote haya kwaajili yake peke yake bali aliwatumikia watu bila ya kujali au kubagua watu wa aina fulani.

Wazo lenye nguvu ni lile wazo ambalo lipo kwaajiri ya kuwasaidia wengine, inawezekana unaona na unakelwa na mambo fulani ambayo jamii inakosa au inachangamoto fulani lakini wewe una wazo, waweza kuwasaidia kupitia wazo lako. Tumezaliwa ili tutoe nuru penye kiza, tumezaliwa kuwa nuru kwa wengine, tumezaliwa kukamirisha palipo kosa ukamirifu, hili ndilo kusudi kuu la maisha. Wazo lenye nguvu ni kwaajili ya kuwasaidia watu kama alivo kuwa Mwalimu anafanya, yeye alijitaidi kuwasaidia watu kuwa na umoja bila ya kuchagua huyu wa nchi fulani na huyu wa nchi fulani, alitenda sawa sawa na mapenzi yake bila kubagua , alijaa utu ndani yake.

Rafiki yangu msomaji usianze kukimbizana kutafuta vipawa, mara mimi nimezaliwa nifanye nini!  Tupo kwaajili ya wengine si kwaajili yetu, wazo lolote lile ambalo unahisi litasaidia watu wewe litoe kwa ajili ya wengine. Wazo lenye nguvu ni lile ambalo lipo wajili ya kuwasaidia wengine bila kujali kundi la watu fulani yani linasaidia bila mipaka.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii, na kumbuka kutumia vizuri falsafa ya mti ambayo ni mizizi inayoenda chini zadi huufanya mti usitikiswe na chochote.

Wako Sadick Kilasi
Mawasliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com, tuma ujumbe kwa maoni na ushauri.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, January 16, 2018

Huyu ndiye mtu adimu kupatikana zama hizi za taarifa

 Sadick Kilasi     January 16, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu mpendwa, siku mpya, hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii mpya. Ni neema tu ya mwenyezi Mungu ambayo imetufikisha siku hii ya leo, maana kuna watu walitamani kuiona siku hii ya leo lakini wameshindwa, Wewe rafiki yangu unayesoma hapa na mimi unafikiri tunakitu gani cha ajabu kama si neema na rehema za mwenyezi Mungu? Jana tumekufa leo tumefufuka.

Karibu tujifunze kupitia makala niliyo kuandalia leo, tutiririke kwa pamoja ili tujifinze kwa namna moja ama nyingine na kuelewa. Basi nikusihi rafiki yangu uwe makini sana na si kuwa makini bali umakini ulio makinika.

Moja ya sifa kubwa ya Watanzania ni kwamba ni watu wenye ukaribu na ukarimu sana. Hii ndio sifa kubwa tulionayo watanzania. Lakini mimi huwa naona kuna kitu kimoja ambacho watanzania pamoja na sifa hizo tuna kitu kimoja kinaitwa unafki. Unafiki kwangu mimi ndo naona ndo sifa kubwa tulionayo wtanzania. Watanzania wapo tayali kukupambapamba wakati wewe upo pale lakini ukiondoka nyuma watakusema vibaya. Watanzania hawana sura ya ukweli, hata kama umetenda jambo baya watakwambia umetenda jambo zuri, ukitenda jambo zuri watakusapoti wakati wewe upo pale lakini ukiondoka watakusema tu kwa mabaya.

Mtu adimu kupatikana katika zama hizi za internet ni mtu ambaye ukikosea atakufuata faragha na kukwambia bwana hapa umekosea, watu hao zama hizi za facebook, istragram na mitandao mingine ya kijamii ni adimu sana kupatikana, wapo ila ni wachache sana kupatikana. Wengi sana hasa sisi watanzania mtu akitukosea tunakimbilia kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kutangaza, fulani kafanya hivi, fulani kafanya hivi, tunasahau kitu kimoja hapana binadamu aliye kamirika.

 Watanzania tunakaribiana lakini si wamoja. Tupo kwaajili ya kufunika mapungufu ya wengine na si kuwa wanafiki kwao, mtu akikosea mwambie ukweli palepale yeye mwenyewe na sikutangaza, kumbuka mwenyezi Mungu alimpunguza Adamu sehemu ya ubavu wake na kumfanya Hawa kwahiyo watu wote tunamapungufu. Tusiwe wanafiki kwao bali tukamirishe utu palipo kosa utu.

 Endelea kujifunza kupitia blogu hii ya jikolaushauri.bloguspot.com kupata maarifa zaidi na falsafa ya mti ndipo itatenda kazi zaidi hasa kwenye mizizi nawe mizizi yako itazama chini sana na mti hauta kosa maji na utakuwa kama mti ulio pandwa kandokando ya mto ambao mda wote wastawi kama kitabu cha biblia kinavosema. Mpendwa rafiki kwa jambo lolote tuwasiliane kwa mawasiliano ya hapo chini.

Maisha ni kuwa, husika mwenyewe,  fanya mwenywe, pokea mwenyewe.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, January 15, 2018

Maneno matatu ya kusafiri nayo mwaka 2018 ili kujenga mafanikio ya kweli

 Sadick Kilasi     January 15, 2018     NJOZI     No comments   

Moja kati ya kosa kubwa ambalo watu wengi hufanya ni kudeal na matokeo, yaani anacho kiona kwa nje ndicho anacho kitaka. Sio mbaya kupenda kitu unacho kiona lakini mara nyingi huwa tunasahau mchakato ambao ulifikisha pale ambapo tunaona matokeo, na ndipo tamaa ya mtu inapo anzia na matatizo mengi yanapoanza.

Mwaka 2018 kwetu sisi mimi na wewe rafiki yangu mpendwa ni mwaka wa tofauti kabisa na ndiomaana nimeamua nikushirikishe maneno ambayo tutakwenda mwaka mzima na siyo kwa mwaka 2018 pekee bali maisha yetu yote. Maneno ambayo tunatakiwa kwenda nayo mwaka mzima ni KUWA, FANYA, POKEA.

Unaotumia maneno haya matatu katika jambo ambalo unalifanya au umelipeda, mafanikio ya ukweli kwako inakuwa sio kitu cha ajabu wala bahati.

KUWA, ni wewe mwenyewe kuhusika na hapa ndipo mchakato unapo anzia badala ya kutaka matokeo ambayo huna uelewa nayo  kivipi yamefikia pale. Unapokuwa wewe mwenyewe, unaweza ukawa umependa kitu fulani sasa unachofanya ni kurudi kwenye mchakato ambao utakupeleka kwenye matokeo unayotaka. Mfano; wewe unapenda ulipwe mshahala wa milioni moja, badala ya kutaka ile milioni moja wewe unachatakiwa kujiuliza ni kwamba kivipi sasa naweza kuongeza au kutoa dhamani ili nilipwe milioni moja, huu ni mchakato kufikilia.

FANYA, sasa huu ndio mchakaato wa kuchukua hatua, ambao utakupeleka kwenye matokeo unayo taka, yale mambo unayofanya, juhudi unazoweka hapa ndipo unapohusika, unafanya wewe mwenyewe. Tukurudi kwenye mfani uleule wa milioni moja sasa baada ya kufikilia sasa wewe unachukua hatua, kama ni kuweka dhamani zadi katika maeneo yako ya kazi basi unaanza kuongeza dhamani, kwa njia yoyote unaofikilia.

POKEA, hii ndio hatua ambayo kila mtu anaipenda, au ni kwamba hili ndilo gori la kila mtu analopenda kufika , kwahiyo unapokea ulicho kifanya.

Rafiki yangu michakato hiyo mitatu ni ya muhimu sana katika kuyafikia malengo yetu mwaka huu 2018, unachotakiwa ni kutenda kazi yale unayojifunza.

Maisha ni KUWA+FANYA=POKEA
Endelea kujifunza kupitia blogu hii, ombi langu kwangu ni unisaidie kuwashirikisha wengine ili ujumbe huu uwafikie wengi zaidi, na kama unaswali lolote basi tuwasiliane kwa 0687000768, tuma ujumbe nitakujibu, au kwa bara pepe ni sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, January 14, 2018

Heri ya mwaka mpya,hii ndio falsafa ya kuishi nayo mwaka 2018.

 Sadick Kilasi     January 14, 2018     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, USHAURI     No comments   

U hali gani rafiki msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Heri ya mwaka mpya. Kwanza nikupe hongera kwa kuufikia mwaka mpya 2018, ni ushindi mkubwa na wa kipekee sana, wapo wengi sana waliotamani wauonea mwaka 2018 lakini haikuwezekana, kwako wewe umeuona mwaka mpya.

Rafiki msomaji wa blogu hii, nimekuwa kimya kwa mda mrefu, kama wiki tatu hivi, kwanza kabisa naomba niombe radhi kwa kutokuandika na kutoa makala, kuna changamoto kidogo ili nikumba kwahiyo nikawa nafeli kwa hilo. Naomba tusizungumzie sana hilo lakini, kwa ujumla niombe samahini tu. watu wanasema ukizungumzia sana matatizo ni kama kupalilia matatizo.

Mwaka huu nimejipanga msomaji wangu nitakuwa naandika kila siku makala, kwahiyo rafiki yangu tegemea kupokea makala kila siku, kwahiyo rafiki yangu jiandae kujifunza zaidi na zadi.

Mwanzo wa mwaka kila mtu huwa anaweka malengo na mipango mikubwa sana, kama umefanya hivo hongera sana kwa sababu ndo mwanzo wenyewe, lakini bila kuchukua hatua bado itakuwa kwako ni changamoto na sawasawa na mchezo wa kujifurahisha mwenyewe. Ili kuona matokeeo ya malengo yako lazima uanze kuchukua hatua. Hatua hizo ndogondogo ndizo zitakazo kufikisha kule unakotaka kufika.

Mwaka 2018 tunapaswa kutumia falsafa ya mti, tukishi falsafa hii na kuifanyia kazi kila siku kufikia malengo yetu kitakuwa sio kitu cha ajabu kwetu na tutajengeka vizuri

Sehemu tatu kuu za mti.
Sehemu ya kwanza kabisa ya mti ni kule juu kabisa kule kwenye majani na matawi, ndiko kunako onekana kiurahisi, kila mtu anaona tufanye yale ni matokeo ya kile tunachofanya, ni ndoto ya kila mtu kufika pale.

Sehemu ya pili inayo onekana kiurahisi ni shina, sasa shina ni hatua zile unazopiga zitakazo kupeleka kwenye majani na matawi kule.

Sehemu ya tatu ambayo ndiyo kiini sasa na mwano wakila kitu ni mizizi, hapa ni mawzo yako, maarifa uliyo nayo kwenye kichwa chako. Kumbuka rafiki yangu mizizi ndio inayosimamisha mti na haionekani na wewe mawazo yako hakuna mtu anaye yaona.

Mti haukuwi bila ya maji, kukosa maarifa mizizi lazima iende chini, mti hausimami bila shina, kuchukua hatua katika malengo yetu na majani na matawi ni matokeo ya huku chini kabisa kwenye mizizi na shina, ndoto ulionayo ni itategemea mawazo yako na hatua utakazo chukua. Ishi falsafahii mwaka 2018 utasimama.

Maisha ni KUWA+FANYA=POKEA
Wako Sadick Kilasi
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com, blogu ni jikolaushauri.blogspot.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ▼  January (17)
      • Mda wa maisha ni mfupi unapokuwa unakazana kufanya...
      • Unapohofia kuchukua hatua .
      • Wanao leta upinzani, wanatuinua.
      • Tunaposhindwa kuheshimu misingi ya mababu zetu.
      • Kama bado umekuwa unasubiri hali hizi mbili kutoka...
      • Tatizo sio wao, tatizo ni wewe na migogoro ndipo i...
      • Wewe ni kuchagua tu, kila kitu kipo pande mbili.
      • Tabia hizi mbili, ndizo zinazokufanya kuwa mtu mwe...
      • Ningelijua ninge....Je ungefanya nini?
      • Maajabu niliyokutana nayo nilipo jiangalia kwenye ...
      • Hii ndio sababu ambayo inafanya watu kupitia chang...
      • Hili ndilo neno ambalo ukitamka tu, lazima utafani...
      • Sio kila jambo sawa, mambo mengine ni upuuzi tu.
      • Wazo lenye nguvu
      • Huyu ndiye mtu adimu kupatikana zama hizi za taarifa
      • Maneno matatu ya kusafiri nayo mwaka 2018 ili kuje...
      • Heri ya mwaka mpya,hii ndio falsafa ya kuishi nayo...
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates