Tai ni ndege wa kipekee sana. Huishi kwa imani kubwa anapofanya mawindo. Ukimwangali tai anapofanya mawindo unaweza kujifunza kitu kikubwa sana.
Tai anapotaka kufanya mawindo yake huenda juu sana (juu ya anga), ikisha hujitengeneza katika upande fulani wa pembe na kuangalia chini akiwa mbali kutoka juu. Huitazama dunia kwa lengo la kutaka kupata kitu huku akiwa amejitayarisha kupata anachotaka.
Hupata kile anachotaka kupata akiwa mbali sana juu ya anga, huangalia chini wakati mwingine humwona panya, nyoka na wanyama wengine wanaofaa kuliwa na yeye. Jicho lake hutazama akiwa mbali sana, huchagua anachotaka na kukiendea kile anachotaka kwa kasi ya ajabu. Bila kufanya kosa katika mkao ule ule ambao amekaa, hujiachilia na kukifuatia kile ambacho anakitumainia kukipata. Jambo la kushangaza ni kwamba hata chini kukiwa na wanyama wengi hufuata yule ambaye alikuwa amemtagenti katika pembe aliyokuwa amempimia. Jicho lake huona kutoka mbali sana, hata kama samaki akiwa amejificha chini ya maji jicho lake humwona na kumkamata kwa kujifanyia mawindo yake. Na huwa na maeneo maalumu ambayo atamshika,(shingoni) na kwa jinsi alivyokuwa amejiwekea shabaha yake hushika maeneo yale yale.
Mpendwa msomaji, ikiwa tunaweza kujifunza kutoka kwa tai basi tunaweza kuishi maisha ya maana sana.
Kitu kikubwa ambacho kinafanya maisha yetu yanakosa maana ni kukosa shukrani. Kama jicho letu lingekuwa kama la tai mambo yote yangekuwa na maana sana.
Watu wengi tumekosa matumaini kwa sababu hatuna shukrani. Hatutaki kuamini kile ambacho tayari tunacho, hatutaki kufanya chaguo la muhimu, hatutaki kupokea kile ambacho tayari tunacho. Siku zote tumekuwa tunaishi maisha ya kutamainia vile ambavyo tayari hatunavyo. Lakini licha ya kuwa tunatamania vile ambavyo hatuna bado vile ambavyo tunavyo hatuvikubali. Katika mfumo wa kutembea, huwezi kukandamiza ardhi inayofuata kwa unyayo wako kabla ya kukandamiza ardhi uliyokanyaga kwanza. Kandamiza ulipokanyaga ikisha uendelee mbele. Siku hizi watu wamepotoka kabisa, eti umaskini ni laana, laana maanake nini? Chukua hatua anza kukua ili kwenda unakoelekea.
Maisha yanacheza katika nyanja tatu; imani, utayari na matumaini. Imani huja kwa kusikia, kama huwezi kuamini kile ambacho umekiona, utaaminije kile ambacho hujakiona? Utayari ni kuishi kile ambacho tayari unacho. Matumaini ni maono ya mbali zaidi. Sasa huwezi kuwa na imani ya mbali kama hakuna kidogo cha jilani ambacho tayari unacho. Unapokubari kile ambacho ni kidogo inamaana tayari unaweza kukubali kwamba kuna vikubwa vinakuja.
Shukrani ni uwezo wa kukubali kidogo ambacho tayari unacho ili kupata kikubwa zaidi ambacho hicho sasa tunaita matumaini yako, ama maono yako.
Sasa rafiki yangu, kuwa na jicho la tai, kaa katika makao wa jicho la kuona chema kinachoweza kukupa nguvu ya kuishi tena. Ichunguze harufu ya maisha yako na kitumainie chakula hicho.
Kubali vile ambavyo Mungu kakupa tayari na uache kulalamika na songa mbele. Wakati nabii Elisha alipoletewa lalamiko na mke wa mwanafunzi wake ambaye tayari alikuwa amekufa, na mwanamke huyo alimletea mararamiko kwamba anadaiwa, nabii Elisha alimwuliza kwanza nikusaidie nini? Una nini nyumbani kwako? Akamwambia nina chupa ya mafuta, akamwambia akusanye vyombo vingi ili apate kumimina mafuta, alimimina mafuta vyombo vyote vikajaa mpaka akaenda kuazima vyombo kwa majilani, pale aliposema vyombo vimeisha na ndipo mafuta yaliisha ndani ya chupa. Akaenda kuuza mafuta na kupata fedha na kulipa madeni yake.
Ndugu yangu, popote pale tulipo kipo ambacho tunaweza kufanya, popote pale tulipo kipo ambacho kinaweza kuwa harufu nzuri ya maisha yetu, chukua hatua ili uishi utamu wa harufu. Ingia kwa shukrani wakati unapikea vitu vitakatifu. Acha kulalamika.
Makuhani katika Agano la kale walikuwa wanaingia patakatifu huku wamefumba macho. Ikiwa inamaanisha shukrani kwa kile ambacho tayari umepewa.
Acha kuwa mchoyo, uchoyo ni pale ambapo unasema huna kitu kumbe umeficha mengi ndani yako. Hakuna mtu ambaye hana kitu, mtu yeyote ana kitu cha kumpa mwingine. Neno linasema katika Zaburi, nyingi ni miungu lakini msipowasaidia wengine mtakufa maskini. Ikiwa tutakuwa wachoyo wa vile ambavyo tayari tunavyo itakuwa kama watu waliokufa. Bwawa lenye maji ambapo haliingizi wala kutoa maji ni lazima maji yake yanuke tu. Hivyo hivyo uliyo unaweza kuirutibisha ardhi yaani watu. Wakati Mungu anatuumba hakutuumba tuwategemee wengine na kama unasoma hapa basi tayari wewe unapaswa kutegemewa na wengine.
Umefungia uwezo wako ndani yako, harafu unasema huna kitu, Mungu katuita sisi Miungu sasa unaposema huna kitu ni kufuru. Hatupati kile tuomba kwa sababu hatukubali kile ambacho tunapewa.
Sasa nataka tuanze kuishi kwa shukrani, nataka mimi na wewe rafiki yangu unayesoma hapa tuishi maisha badala ya kuigiza kuishi maisha.
Nimeanda mfumo wa kuishi maisha yenye maana kwa mwezi mzima; wiki ya kwanza itakuwa wiki ya shukrani, wiki ya pili itakuwa wiki ya kutawala, wiki ya tatu itakuwa wiki ya hamasa na wiki ya nne ni wiki ya kukua.
Hivi ndivyo ambavyo tutaishi ndani ya mwezi mzima. Na vitu vipo ndani ya mwanadamu, ukisoma katika kitabu cha ufunuo utaona.
Ni lazima tuishi maisha yenye maana ili dunia iwe sehemu sahihi ya kuishi.
Katika maeneo yote manne tutakuwa tunaiendea siku kwa mfumo maalamu. Kama ni wiki ya shukrani basi jambo la kwanza kulitanguliza litakuwa ni shukrani na huku mengine yanafuata kwa nyuma, kama ni wiki ya hamasa basi mwogozo wetu kwa wiki hiyo ni hamasa, mengine yatafuata kwa nyuma.
Ni nani atashiriki? Tutatengeneza group ambalo kila siku asubuhi tutakuwa tunapata kianzio cha mwongozo wetu. WhatsApp group inatosha. Hii haina gharama yoyote. Kama upo tayari nitumie ujumbe 0687000768. Ni mengi ambayo tutajifunza na kufanya maisha yetu yawe na ladha na kwa wengine pia.
Watu wanao hitajika kuanzia kumi na tano, kushuka, ama kumi, ama watano ama pake yangu. Wowote wale ambao wapo tayari kufanya hivyo basi ndio hao.
Lengo ni kuanza na sisi wenyewe harafu baadae kutoka nje zaidi na kuwafanya wengine kuwa na matumaini zaidi kwa kutumia vipawa vya uwezo wetu.
Karibu sana, tuna ujumbe 0687000768 au sadikila65@gmail.com. Kwa pamoja zaidi tunakwenda mbali zaidi. Dunia imekosa kitu kinachoitwa umoja, badala yake kila mtu anaishi na kuhitaji kufalijiwa. ASANTE.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment