JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Friday, November 30, 2018

Katika Wiki Ya Kukua, Wewe Umeachwa.

 Sadick Kilasi     November 30, 2018     NJOZI     No comments   



Jambo la kwanza kabisa ambalo ni muhimu zaidi katika maisha pale ambapo umepitia katika wakati mgumu ama unaona upo katika wakati mgumu ni kumshukuru Mungu kwa sababu ya ugumu huo ambao umekuacha salama. Kama kwa sasa unajihisi kutokuwa sawa na mambo yako, ni wazi kwamba wewe ni mzima na endelea kufanya maamuzi ya kukupa uzima zaidi.

Wakati fulani nilikuwa naangalia filamu ya King Kong, nilijifunza kwamba, hata kama upo katika wakati mgumu kiasi gani bado unapaswa kufanya maamuzi ya kuendelea kuwa mzima zaidi licha  ya mazingira kutokuruhusu kuwa hivo. Unajua nini? Kile ambacho kinatokea kwetu sisi ni tofauti kabisa na sisi, yale ambayo tunatenda, yale ambayo tunatendewa, huwa yanakosa nguvu kabisa endapo hatutaruhusu yaingilie maisha yetu.

Nilipokuwa naangalia filamu ya King Kong, mhusika kunawakati alikuwa katika hali ngumu sana, wakati anasogea mbele alimwona mnyama mbaya ambaye ni hatari katika maisha yake lakini wakati anageuka nyuma, kumbe alikuwa anaviziwa kwa nyuma. Lakini bado hakujikunyata alifanya maamuzi ya kuendelea kuwa mzima zaidi. Kila hatua ambayo alikuwa anapiga ilikuwa ni hatari kwake lakini bado aliendelea kufanya maamuzi ya kuwa mzima zaidi. Maamuzi ambayo alikuwa anafanya yalikuwa ni ya kijasiri. Leo hii naweza kujifunza kutokana na maamuzi yake.

Kunawakati unaweza ukawa haupo sawa, usimuumize mwingine kwa sababu wewe haupo sawa. Usijiumize mwenyewe eti kwa sababu haupo sawa. Kila wakati ni sawa kufanya maamuzi sahihi.

Ukigundua umefanya jambo lisilofaa, usiendelee kufanya jambo lisilofaa. Tubu anza kufanya jambo linalofaa.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 28, 2018

Katika Wiki Ya Kukua, Kama Hatua Unazopiga Unapoelekea Mahali.

 Sadick Kilasi     November 28, 2018     NJOZI     No comments   



Kama ilivyo katika maisha ya kila siku, maisha ni utayari wa kuishi matuini sasa kwa Imani. Kilicho cha thamani zaidi ni utayari wa kuchukua hatua sasa maana hicho ndicho kitakupeleka katika matumaini yako.

Wakati wa kutembea, mguu mmoja ukiusindilia chini mwingine unakupa uafadhali kwa kuwa unakupa unafuu katika tembea, unakupa hamasa ya kuendelea mbele. Kwa hiyo, hatua moja moja ambazo tunapiga ni kama, kufa na kufufuka, unakanyaga hatua ya kwanza unaipa thamani, unendelea mbele, ya pili nayo unaipa thamani, unaendelea mbele.

Kila hatua utakayopiga inathamani kubwa sana katika maisha yako. Mshukuru Mungu kwa hatua ndogo ndogo unazopiga kwani hizi ndizi zinakupeleka katika kusudi na shabaha yako.

Mungu alipikuwa anaumba, alikuwa anathamini kila alichokuwa anakifanya, nasi lazima tumwige Mungu.

Ukawe na hatua nzuri, kila hatua kwako ni ya thamani sana, thamani kila hatua.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 26, 2018

Katika Wiki Ya Kukua, Washa Njiti Yako.

 Sadick Kilasi     November 26, 2018     NJOZI     No comments   

Katika Wiki Ya Kukua, Washa Njiti Yako.


Kwa mtu ambaye bado hajaanza kuishi tabia za ndoto yake huyo ni njiti ambayo bado haijawashwa na siku zote haina nguvu yotote kwa sababu haifanyi kazi yoyote. Kila mtu ndani yake ana nguvu ambayo inasubiri kuchochewa.

Kwa mtu ambaye anajua nguvu yake ama ndoto yake harafu haifanyii kazi huyu ni sawa na mtu ambaye kapata jiti ya kiberiti na ganda lake Na yupo msituni harafu hataki kuwasha kwa sababu labda anafikiri kwamba kuna cha ziada ambacho anahitajika kufanya zaidi.

Kwa mtu ambaye anaishi ndoto yake, huyu sasa ni sawa na mtu ambaye kawasha moto ndani ya msitu wa paini ambao moto wake huwa unakuwa hatari sana.

Kama bado hujawasha moto wako, tafuta ganda lako ambalo ni Mungu, Mungu wa enzi yote mtumainie yeye pekee. Hakuna jambo ambalo linashindikana.

Kama tayari unakila kitu, washa moto wako, huna cha kusubiri kwani duniani hakuna ukamirifu ila tunaishi tabia za ukamirifu.

Kama tayari unewasha moto wako, hongera. Jambo la kujua zaidi ni kwamba moto unavichocheo vyake, usiweke maji kwenye moto.

Jiweke chini ya haki ya Mungu ili usiwe na lawama yoyote katika safari yako ya kuyaendea matumaini yako yeye ni tuzo lako.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, November 25, 2018

Katika Wiki Ya Kukua.

 Sadick Kilasi     November 25, 2018     NJOZI     No comments   



Tumekuwa na wiki mbili, wiki moja ilikuwa ya shukrani na wiki ya pili ilikuwa wiki ya kutawala. Wiki hizi zote mbili zimekuwa wiki ambazi zimejenga misingi ya sisi kuendelea kuishi maisha yenye maana.

Kama umekuwa unachukua hatua kwa kile ambacho unajifunza, natumaini kwamba umeona mabadiliko kwa kiasi fulani katika maisha yako. Lengo letu kubaki na kuishi maisha ya kawaida, sisi kama washindi tulioushinda Ulimwengu tunaendeleza kile ambacho tumekianza na kuzidi kukua katika msingi huo.

Tumeingia katika wiki ya KUKUA, wiki ambayo inataka tuende hatua ya ziada kwenye vile ambavyo tunavifanya. Katika maisha kitu kizuri zaidi ni maamuzi bora ambayo yanaamuliwa kutoka katika msingi bora maana mbegu bora zimepandwa ndani mwetu zinahitaji kumwagiliwa ili kukua zaidi.

Unachiweza kufanya sasa ni kufikiri sahihi sasa na kufanya maamuzi ambayo yapo sahihi zaidi. Tunapaswa kukua kwenye kila kitu, tabia zetu binafsi, katika mahusiano, katika vile tunafanya na mengine zaidi.

Ninachoamini ni kwamba, si kile ambacho  umekifanya katika ubora mkubwa ndicho kilicho bora zaidi na wala si kile ambacho hujakifanya na unategemea kufanya ndicho kitu bora zaidi bali  kitu bora zaidi ambacho mimi naamini ni kile ambacho unakifanya kutokana na maamuzi yaliyo bora zaidi. Thamani ya maisha ni sasa, sasa inaweza kuharibu kabisa mambo yote mazuri uliyofanya nyuma na yale ambayo unatumai kufanya.

Biblia inatutaka wakati wote tuwashe taa, nuru iwe inang'aa.

Lengo letu si kuisha kawaida na kuishi kuwa wa kawaida bali kwa chochote kile ambacho kipo mbele yetu ama kinapita mbele yetu ama kufanywa nasi, kinatakiwa kipewe ubora wa kipekee ili kiwe bora zaidi. Boresha mahusiano yako, boresha shughuli zako, boresha ufikiri wako zaidi.

Kuwa zaidi, nenda viwango vya juu zaidi. Wiki ya kukua ndo imeanza leo, twende tukiwa tunataka kuwa na njizi kubwa zaidi. Natumai kwamba tayari una mbegu ya matumaini yako, mbegu ambayo inapaswa kuwa mti mkubwa.
 Asante sana

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Je! Ndege Hutegemea Tawi Alilotua?

 Sadick Kilasi     November 25, 2018     NJOZI     No comments   

Katika Wiki Ya Kutawala, Je! Ndege Hutegemea Tawi Ambalo Amesimamia.

Ni ndege huyu, ndegu huyu kiumbe, ambaye hupaa katika miti, je! hutegemea tawi ambalo ametua?

Ndege hategemei sana tawi ambalo ametua lakini hutegemea zaidi mbawa zake lakini pia ni lazima atue kwani hawezi kupaa wakati wote.

Mpendwa somaji, je! umekuwa unaweka matarajio makubwa kwa watu? Tangu sasa usiweke matarajio mengi kwa watu bali uwe na kiasi ili usiumie. Lakini pia lazima uwe na matarajio kwa watu, ni lazima utue maana hupaswi kutokuwaamini watu kabisa, utashindwa kuishi mahusiano na watu.

Yote na yote, mtumainie Mwenyezi Mungu, tia nanga kwake ili tumaini lako lisiwe la kugonjagonja. Kumbuka maisha ni furaha, maisha yakikosa harufu yatakosa ladha. Usikate tamaa mwamini Mungu.


Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Katika Wiki Ya Kutawala, Mungu Ndiye Mfalme Wa Kila Kitu.

 Sadick Kilasi     November 25, 2018     NJOZI     No comments   



Kuna wakati ambao sisi kama wanadamu huwa hatuwezi kuwa na uhakika wa mambo yajayo. Yawezekana yawezekana ni ugonjwa ambao unatusumbua, ama matatizo fulani ya kiafya, ulemavu na mambo mengine. Hapa tunahitaji Mungu mwenyewe ajidhihirishe. Wakati mgumu ndio wakati mzuri zaidi wa Mungu kujidhihirisha na kuonyesha nguvu zake.


Badala ya kujitabilia mambo maovu, tunahitaji kumpa Mungu na kumwachia ugumu wa nyakati ngumu kwetu. Ni vema kuishi maisha ya furaha kuliko kubaki katika hema ya kuugulia huku ukiwa huna tumaini lolote.

Sara alijua kwamba hana uwezo wa kuzaa kwa jinsi alivyojitabiria yeye kwa macho ya uanadamu lakini Mungu alikuwa na mpango wake juu yake.

Waweza kujikuta unabaki katika wakati mgumu wa kuugulia na jambo fulani labda umeambiwa haiwezekani kupona, lakini kumbe Mungu anampango juu yako. Miaka mingi unaugulia, unajikuta umetumia miaka mingi kuugulia kwa hicho, wakati mwingine hata maamuzi ambayo unafanya yanakuwa katika hali ya kukata tamaa, yaani kwa sababu huoni tumaini unafanya maamuzi ambayo si yako. Sara alifikiri kwamba  hawezi kuzaa tena akafanya maamuzi ya kumruhu mmewe Ibrahim azae na mfanyakazi wake, kumbe Mungu alikuwa hawazi kwa namna hiyo, mwisho Mungu anampa mtoto lakini maamuzi ambayo amefanya nyuma yanakywa kikwazo kwake na yanamnyima furaha kwa sasa.

Mtumainie Mwenyezi Mungu, uwe na moyo, usikate tamaa. Usifanye maamuzi ya hovyo eti kwa sababu ya kipindi cha mpito. Mungu ndiye anajua fungu lako, anajua wapi sahihi kwa wewe kusimama. Usikate tamaa.

Siku zote kinachotuumiza kwenye maisha ni kile ambacho hatutaki kukiamini na tunakiamini kidogo kidogo. Tumaini la kugonjagonja huumiza moyo.

Tumembiwa tuitawale dunia na tumaini letu litie nanga katika patakatifu pa huko mbinguni kwa yeye aliye mkuu, Mfalme wa mbingu na dunia, yeye anatawala kila kitu.

Usifanye maamuzi kwa sababu ya wakati wa mpito fanya maamuzi kwa sababu ya tumaini lako la mwisho. Matarajio madogomadogo yasikuumize kichwa kwani mtu akipotea njia anaweza kurudi ulikotoka na kuanza upya safari yako na kufanya mambo bora zaidi. Kujikwaa sio kudondoka, kudondoka sio kulala wala kulala sio kuamka. Bado unahitaji kukaza viungo vyako kwani viungo vyako hulegea ili vikazwe.

Jiweke chini ya haki ya Mungu, yeye ndiye mwanzo wako, ngao yako na tuzo lako. Yeye ndiye aliyekuumba.

Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 23, 2018

Katika Wiki Ya Kutawala, Jiweke Nafasi Ya Wengine.

 Sadick Kilasi     November 23, 2018     NJOZI     No comments   



Mlango mojawapo wa kuingia katika Ufalme wa Mungu ni kujiweka nafasi ya wengine.  Licha ya mlango huu, mlango mwingine ni mlango wa shukrani. Kwa hiyo kuna milango miwili, shukrani na kujiweka nafasi ya wengine.

Wakati kuhani alipokuwa anafanya ibada ya upatanisho ili kuondoa dhambi za wana wa Israeli, ilimbidi kwanza ajitakase yeye mwenyewe kwanza pamoja na jamaa zake yaani familia harafu baada ya yeye kuwa safi atafanya ibada kwaajili ya jumuiya yote ya wana wa Israeli. Ikisha ataingia mahali watakatifu na makaa ya moto na ubani na kuvukizia moshi ilikufunika kifuniko cha Sanduku la Agano.  Kumbuka, katika wiki ya shukrani tumejifunza kuwa, shukrani ni bayana ya mambo yasiyoonekana kwa macho, tukasema harufu. Lengo la kufunika kifuniko cha Sanduku la Agano, inamaanisha kutokujiangalia kimwili, yaani Sanduku ni miili yetu, sisi ni hekalu la Mungu.

Ndugu yangu, kujiweka nafasi ya wengine ndicho kitu ambacho kuhani alikuwa anafanya. Amri zetu kuu ni mbili tu, Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote na mpende jilani yako kama nafsi yako.

Nini kilichopo hapa, sisi sote tunamadhaifu, kuhani alikuwa anajitakasa yeye kwanza ikisha anawatakasa wengine. Je! wewe ukisamehewa huwezi kusamehe wengine? Ni rahisi kuwasamehe wengine kama hata wewe unajitambua na kujiona wewe ni mtu mwenye makosa, ulishakosa sana.


Ndugu yangu, watu hujiuliza ni kwa namna hani wanaweza kuachilia uchungu ambao unawaumiza, njia ni moja, ubongo wako unafanya kazi, je! wewe hujawahi kumuumiza mtu? Je! wewe hujawahi kumdanganya mtu? Usiseme huyu ameniumiza sana, Ndugu, chochote kile ambacho umemfanyia mtu mwingine kama hakifai huwezi kujua ni kwa kiasi gani kinaweza kuharibu maisha yake. Donge dogo la chachu huharibu chachu nzima.

Kama unaomizwa na uchungu ambao watu wamekufanyia, achilia kwa kukumbuka namna hata wewe ulivyowafanyia wengine, hii itakufanya ujione hata wewe hufai kitu na itakuwa rahisi kwako kusamehe. Kumbuka, ajikwezaye, hushushwa.

Kama mtu amefanya kosa usikimbilie kuhukumu bali angalia kwa jicho la upendo, hurumia, angalia mazingira ambayo yamesababisha kuwa katika hali hiyo. Hakuna jambo ambalo hutukia pasipokuwa na mbegu ya jambo hilo. Mara nyingi kila jambo ambalo kila jambo huwa linakuwa na nguvu hasi, nguvu hasi hii ndio husababisha ajali.

 Kwa hiyo mpendwa, siku hii ya leo, jiweke katika nafasi ya wengine na kuwa na shukrani bayana na mambo ambayo huwezi kuona kwa macho yako. Siku zote huwa kunakuwaga na dalili na dalili ndiyo inakupa furaha. Shukrani huleta furaha na kujiweka nafasi kwa wengine huleta raha. Raha ya kuwa pamoja ambayo husabishwa na upendo. Upendo ni kuwa tayari kuchukua madhaifu ya wengine.

Katika maisha yako, vipe vipaumbele zaidi vitu hivi viwili. Kujiweka nafasi ya wengine na shukrani.

Kajifunze kutoka;
Walawi 16.
1Yohana 5.

Tunaendela na tabia ya zetu nne za kutoongoza kuishi maisha yenye maana. Ikiwa ni wiki ya Kutawala, leo tunaongozwa na kujiweka nafasi ya wengine. Jipe thamani, wape thamani wale ambao  wamefanya makosa, warutubishe kwa sababu wewe umesharijua hili. Kuhani aliingia patakatifu wakati anajipatanisha mwenyewe akitoka anawapatanisha wenzake. Sisi sote ni kitu kimoja, haijarishi mtu amefanya kosa kubwa kiasi gani, kosa ni kosa yeye si kosa.

Kilicho ndani ya mwili huwa kinahitaji kutoka, kinatoka kwaajili ya wengine.

Kitu ambacho napenda katika maisha yangu, ni kuona wewe unatabasamu na tabasamu huja kwa kujitambua, madhaifu yako na maeneo ambayo upo bora. Na hapo marumaini ya kujiboresha huwa yanaanza ili kuhakikisha unafika katika viwango fulani baada ya kujiona. Wengi tunajitazama lakini hatujioni kwa sababu tupo bize kuwahukumu wengine, luwashabikia wengine na kujisahau kwa ajili yetu. Anza kujisoma.

Karibu kwa maswali juu ya hii program ya mwezi, nitumie ujumbe 0687000768. Tupo pamoja.


Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 22, 2018

Katika Wiki Ya Kutawala, Moyo Huwa Unakubali.

 Sadick Kilasi     November 22, 2018     NJOZI     No comments   



Ushawahi kuwa unafanya kitu harafu ukajikuta umeangukia katika kupenda zaidi kile ambacho unakifanya? Ni moyo, moyo huwa unakubali. Kwa kadili ambavyo akili yako unaipa jambo fulani kuwaza zaidi, moyo unakubali na hauoni namna nyingine unaona hicho ndicho kitu pekee cha kufanya.

Kipindi cha nyuma nikikumbuka, nilikuwa nakwenda mahala fulani kukaa na kupiga stori kila siku, nisipokwenda naona kana kwamba siku haijakwenda vizuri lakini hii yote ni kwa sababu ya moyo.

Sasa kwa hili ni muhimu zaidi kutambua, ni maeneo yapi na tabia zipi ambazo unapaswa kuwekeza zaidi ili moyo wako ukubali, sehemu ambayo unapaswa kuwekeza zaidi ni sehemu ambayo inakujenga ama inawajenga wengine.

Chagua tabia ambazo unataka kufanya na moyo uzikubali, rudia zaidi na zaidi ili moyo ukubali. Moyo ukishakubali utakuwa umefika kiwango cha uraibu ama uteja.  Ukifika kiwango hichi utajisikia kwenye kila ambacho unakifanya ni burudani kwako yaani utamu, haijatishi kwa wengine hiyo kazi watu wanaichukuliaje? Kwako wewe kwa sababu umekuwa mteja wa hilo, kwako ni utamu tu.

Kitu kigumu katika maisha, ni kukifanya kile ambacho kinanukia kuwa kitamu, mchakato, moyo unapokubali tunasema mwili umekubali.

Yesu alisema, ingieni kwa mlango mwembamba, maana huo ndio mlango wa uzima. Ikiwa kuna mlango basi ndani yake kuna uwazi, ikiwa kuna uwazi basi kuna sehemu ngumu ya kutokea.  Mambo ya kujenga huanza kwa ugumu lakini mambo ya kubomoa huanza kwa raha. Yesu anatuasa tuingie kwa mlango mwembamba maana huo ndio wenye uzima.

Ndugu yangu, kila mtu anauwezo wa kujenga tabia ambayo unapaswa kujenga ikiwa tu tayari umelijua hili. Na tabia njema za kujenga ni luangalia matunda ya Roho Mtakatifu ni yapi ili kuishi kwa hayo, uvumilivu, upendo, haki, huruma, shukrani na mengine. Ni muhimu zaidi kukuza tabia njema ambayo unahitaji kuwa nayo, unapaswa kuitawala tabia ambayo unataka kwa kukusudia kabisa.

Ili kujenga kitu chochote ambacho unahitaji ni wewe kuvaa viatu, utayari. Mungu atakusaidia kwenye hilo unalofanya ukimwomba msaada na kumpa moyo wako. Patanisha kile unachofanya na Mungu, patanisha meno yako ya chini na ya juu. Siku zote Mungu anasubiri wewe uchukue hatua ili kupatanisha. Kama yalivyo meno ya juu yanasubili ya chini ili kupatanisha.

Jitoe hapo ulipo, jitoe katika hema yako ambayo umejizungushia kwa muda mrefu, chagua hema mpya ambayo inakujenga na kukufanya kuwa bora zaidi ya leo. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 21, 2018

Katika Wiki Ya Kutawala, Inahitaji Utambuzi Na Akili Kumkichwa.

 Sadick Kilasi     November 21, 2018     NJOZI     No comments   



Njaa kubwa ya watu wa Ulimwengu huu ni kukosa utayari wa kutambua utofauti. Ili utambue utofauti inahitaji utulivu na akili kumkichwa.

Mtawala yeyote ambaye hawezi kutambua utofauti wa viwango mbalimbali vya watu anaowatawala, atafeli kutawala. Lazima atambue kwamba kuna maskini, watu wa kati na matajiri wakubwa. Ni muhimu kuyatambua madaraja haya kwa mtawala yeyote ambaye anatawala nchi. Si hali za kiuchumi tu, bali hata tabia za watu wa asili fulani (makabila) na dini kwa ujumla.

Siku zote ili uweze kutawala inapaswa angalau uwe na utambuzi wa taarifa fulani hata kama hujui kwa undani kuhusu watu hao.  Unapokuwa na utambuzi, unakuwa na malengo ni kipi cha kupaki na ni kipi cha kutanguliza katika maamuzi yako. Kwa mtawala kujua makundi ya watu ni muhimu zaidi, kwa mfano, utambua kwamba kabila la watu wa aina fulani wanapaswa kufanyiwa kitu fulani mapema zaidi kuliko makabila mengine, hii ni kutokana na tabia zao zilivyo, ama ni watu wa kuongeo na wenye ushawishi mkubwa. Nyerere alitumia mfumo huu kuongoza nchi lakini pia wakati Mungu anawaondoa wana wa Israeli Misri ilibidi aangamize uzao wa kwanza wa watoto wa Misri ili kuondoa utawala.

Katika maisha yetu tunatawala, kila mmoja ni mtawala. Kwanza kabisa tunaanza kujitawala wenyewe mpaka kuwatawala wengine. Ukifeli kujitawala mwenyewe utatawaliwa na hisia zako na ukifeli kuwatawala watu, utatawaliwa na watu.

Sasa unaweza kujiuliza, yaaani mimi niwe mtawala wa kila mtu? Niwe juu ya kila mtu? Huwi juu ya kila mtu lakini unakuwa na utambuzi wa kutambua tofauti. Kama tulivyosema hapo mwanzo, ukifeli kujitawala mwenyewe utatawaliwa na hisia zako na kama ukiweza kujitawala mwenyewe unaweza kuwatawala wengine pia.

Watu wengi tunaumizwa katika maisha yetu kwa kufeli kutawala (kutambua tofauti). Tunaumizwa na wengine kwa sababu tumefeli kutawala, tunaumizwa na mapito yetu kwa sababu tumefeli kutawala.

Utambuzi wa kuelewa kuwa mimi na mwingine tunawaza tofauti, tunafikiri tofauti na hisia zetu ni tofauti. Kila mmoja wakati wote huwa anakuwa yupo katika hema yake ya kipekee uliyojizungushia. Unapomwendea mtu usishangae anakuona kama wewe ni adui kwani hafikiri namna yako. Na mara nyingi watu huwa tunakazana kujilinda kwa ubinafsi bila kutambua utofauti.

Ndugu yangu, anza kuwa mtawala sahihi kwa kutofautisha utofauti. Usiangalie na kung'ang'ania mapito yako bali angalia ni namna gani ambavyo unaweza kuboresha kila kitu, unaweza kuboresha maneno mabaya uliyoambiwa na mwingine kuwa kama Mwalimu kwako badala ya kuumia, jielewe kwamba wewe ni tofauti na yeye na hata maneno yake anayosema wewe hayakuhusu kama hayaendani na wewe. Ushawahi kujiuliza kwanini mwanzilishi wetu Yesu Kristo alipoambiwa maneno yasiyomhusu alisema, WEWE WASEMA? Kuna maneno ambayo hayapaswi kuingia ndani mwako na mengine yanapaswa kuingia ndani mwako.

Mapito yako ni zawadi yako, usiumizwe na mapito yako, kama ulishawahi kumkosea mtu basi sasa fanya vizuri kwani hapo mwanzo ulikuwa huna utambuzi na kama ulikosewa sana basi sasa ishi kwa kutambua utofauti wa tabia za watu.

Basi, hii ndio thamani ya leo, fikira zetu zinapaswa kuvaa utayari wa kujenga na amani, usiwe kama watu wa kimwili ambao hutafsiri maneno kimwili na kuishi kuumizwa. Unapaswa kuwa mtu wa kiroho, ambaye unatawala kiroho.

Tawala, tawala kishukrani, tawala kiutambuzi, uona wema kwenye kila jambo. Kitu ambacho unapaswa kuishi ndugu yangu ni hiki, kuona wema kwenye kila jambo, ndani ya ubaya uzuri hauwezi kukosekana. Chakula kilichotumika kujenga mwili kinyesi chake hutumika kuritubisha ardhi. Nikupe siri nyingine,  watu wote waliozaliwa upya, miili yao ni zawadi kwa wale ambao hawajazaliwa upya, ni kinyesi kinachorutubisha kwa sababu wao si watu wa mwilini. Unapokuwa unaruhusu kuumizwa na mwingine  unajiweka katika viwango vya chini vya kutawaliwa na hisia zako, yaani kipande kidogo cha wewe badala ya wewe kutawala hisia zako.

Ukawe na siku ya kutawala, anza kujitafakari mwenyewe, anza kuishi na wewe ndani yako, jihimili ili uweze kuhimili mazingira yako. Ishi maisha yenye maana zaidi kwa kuboresha maisha yako.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 19, 2018

Katika Wiki Ya Kutawala, Toka Nje Ya Hema Yako.

 Sadick Kilasi     November 19, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Ulishawahi kukutana na mtu ambaye hashauriki kwa lolote like? Ulishawahi kukutana na mtu ambaye anamwambia hivi na hivi harafu akakwambia kwamba mimi ndivyo nilivyo maana hata ukoo wetu ndivyo tulivyo.

Hizi ni hema ambazo watu huwa wanajizungushia katika maisha yao. Itikadi kali ambazo watu wanakuwanazo. Mara nyingi watu wa namna hii huona kwa njia moja tu bila kufikiri nje ya boksi, kufikiri zaidi ya kufikiri.

Naam, siku ujikijizubgushia hema yako huwezi kutawala mazingira yanayokuzunguka ni lazima utoke nje ya hema yako. Toka nje ya hema hiyo uone utofauti wa mambo.

Kama upo ndani ya hema ya kuwalaumu wengine na umezoea kufanya hivyo, kuanzia leo, toka nje ya hema yako na kufikiri tofauti kwa njia tofauti.

Kama unapitia wakati mgumu katika maisha yako, hata kama unaona kwamba hamna njia ya tofauti, giza limetanda katika mazingira yako, toka nje ya hema yako na kufikiri zaidi ya unavyofikiri siku zote.

Wakati Wana wa Israeli walipokuwa wanakombelewa kutoka Misri, waliokuwa wamejizungushia hema yao ambayo walifikiri kana kwamba haiwezekani kutoka katika hali hiyo ya mateso, lakini Mungu alisema, nataka niondoe kwanza nira za Wamisri walizo lishwa. Bila kuondoa nira hizo hawezi kuona kitu ama unafuu mwingine zaidi ya kuona mateso yao pekee.

Toka nje ya hema uliyojizungushia, usiangalie kambi inayokuzunguka, mwangalie Mungu aliyekuumba, yeye anaweza kufanya lolote ambalo utamwomba.

Ili uweze kutawala unatakiwa uwe mtu ambaye huna itikadi yoyote, unatakiwa kuwa wazi katika akili yako. Unatakiwa kuwa msikilizaji unayesikia, ukisikia unabainisha kati ya wema na ubaya, unauchukua wema na ubaya unauacha kama ulivyo. Unapaswa kuishi kama mtoto ila uwe na utambuzi wa kutambua tofauti.

Toka nje ya hema uliyojizungushia kwa chochote kile, usifanye kwa mazoea, fikiri kwa utofauti. Boresha zaidi ulichonacho.

Ukawe na siku njema ya kuishi maisha yenye maana na kuchagua fungu sahihi kwenye kila jambo. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, November 18, 2018

Ndani Ya Wiki Ya Kujitawala, Jitambue Wewe Mwenyewe.

 Sadick Kilasi     November 18, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Ili uwe na uwezo wa kutawala vingine ama wengine kwanza wewe mwenyewe lazima uwe na uwezo wa kujitawala kwanza.

Kujitambua, nguvu yako iko maeneo gani yaani kitu ambacho unaweza kufanya kwa ubora wa hali ya juu, ama wakati mwingine inaweza ikawa kiafya, ni maeneo gani upo bora zaidi lakini pia kimadhaifu lazima utambue kwamba ni maeneo yapi wewe ni dhaifu, huwezi kufanya vizuri na ni maeneo yapi wewe ni dhaifu kiafya.

Eneo la kutawala linahitaji utambuzi na uelewa mzuri. Hii inasaidia kujijua wewe ni nani na unahitaji kufanya nini na mipaka yako ni ipi. Lakini yote hii ni kuhakikisha kwamba tunaishi maisha yenye weledi, furaha na amani.

Unapokuwa na uwezo wa kujitambua mwenyewe unauwezo pia wa kuwatambua wengine pia. Lengo pia ni wewe uweze kujihimili ili uwahimili wengine pia. Kila mtu anaubora wake na udhaifu wake. Vyote hivi viwili kwa mtu mwenye uwezo wa kujihimili havimtii tatizo kwani hatari kubwa katika maisha kwenye udhaifu ni kutanguliza woga badala ya shukrani.

Paulo pamoja na kuwa alikuwa ni msomi mkubwa na Mungu alimmiminia hekima nyingi na kuhubiri injili kwa kiasi kikubwa, inasemekana alikuwa na madhaifu yake ndani ya mwili wake, alikuwa anatembea huku ameinama kidogo mgongo wake. Lakini Paulo hajawahi kulalamika, kuna mahala kwenye vitabu Paulo alikiri kuhusu hili lakini hakuchukulia kama tatizo. Ukweli ni kwamba, udhaifu wetu ukiunganisha na maeneo ambayo ni bora ndiyo nguvu yetu.

Kwahiyo jichunguze ni maeneo yapi upo bora ili uyabireshe zaidi na ni maeneo yapi wewe ni dhaifu ili ubadilishe kuwa nguvu yako. Pale ambapo huwa tunapatanisha sehemu dhaifu na zenye uimara na ndipo huwa tunapata nguvu na ndiomaana maneno matakatifu yatwambia, kaza viungo vyako usilegee.

Uwezo wa kutajitawala mwenyewe ni jambo la muhimu zaidi. Ukiweza kujihendo mwenyewe, unaweza kuwahendo wengine. Mungu  hutaka nibadilike mimi kwanza ili niwabadilishe wengine lakini na wewe pia hilo linakuhusu. Badilika wewe ili uwabadilishe wengine pia. Kwa chochote kile unachofanya lazima iwe hivyo.

Nikukalibishe katika wiki hii ya kutawala, mwanzo wetu ndio huu na kitu cha kuangalia leo ni kuangalia wewe mwenyewe ni wapi upo bora na ni wapi dhaifu. Dunia ilianza katika hali hiyo, Mungu aliona ukiwa na utupu, giza likiwa juu ya vilindi vya maji lakini Roho alikuwa juu ya uso wa maji. Mungu akasema na iwe Nuru, ikawa nuru, uwepo wa Roho wake  ndio ulisababisha Mungu atamke nuru ndani ya giza.  Mungu akasema nuru ni njema kwenye giza. Kwahiyo wema wa nuru ni ulitokana na giza. Huku ndiko kutawala kutambua  tofauti.

Karibu sana, yapo mengi ya kujifunza na kubadili mitazamo juu ya mambo mengi ambayo wewe huchukulia kama mzigo lakini kumbe kwa sababu ya mtazamo wako tu.

Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, November 17, 2018

Katika Wiki Ya Shukrani, Itazame Wiki Yako Imekwendaje.

 Sadick Kilasi     November 17, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Kila jambo huwa linakuwa na ufunuo wake. Katika kumalizia wiki ya shukrani leo hii tangu tuanze jumatatu ya wiki hii, itazame wiki yako ili uone wapi ambapo umekwenda hatua ya zaidi na ni wapi umefeli.

Leo ifunue wiki yako, kwa kuitazama jicho la kujifunza zaidi. Ukweli ni kwamba, wakati umejizungushia hema kwenye mambo unayofanya huwezi kuona vizuri lakini pale utakapita ndipo utaona vizuri, na ndiomaana utakuta wengi tukitazama na kuzifunua historia za maisha tunajikuta kama tulikuwa bora sana, maisha ya zamani ni afadhari kuliko leo. Ushawahi kukaa na mtu ukawa unamchukulia kawaida lakini akiondoka ukajisikia kuwa kunautofauti kubwa na pengo lake laonekana sasa. Hivi ndivyo ambavyo kila kitu kilivyo. Unapopitia ile hali unayopitia inaweza kuchukuliwa ni kawaida lakini si kawaida kiroho. Na kwa kuishi maisha ya shukrani na kukipa thamani kila kitu, tunakuwa tunapandisha thamani ya kila kitu na ubora unakuwa mkubwa zaidi.

Leo ifunue wiki yako, kwa kutumia kanuni ya ndani, nje, kuwa mchezaji na mtazamaji, leo kuwa mtazamaji wa mechi uliyocheza wiki hii. Angalia ni maeneo yapi ulikuwa bora ili uboreshe zaidi na ni maeneo gani umefali ili uyarekebishe na kubaresha tena.

Haijarishi unaona umepiga hatua chache lakini ukweli unabaki kwamba umepiga hatua, endelea kuendelea tabia hiii ya shukrani ili kuwa bora zaidi kwa uvumilivu. Yape thamani maisha yako na kila kitu ulichonacho.

Asante kwa kuwa pamoja na mwanzo wetu wa kuishi maisha yenye maana na yenye weledi. Tuendelee kuwa pamoja ili kusonga mbele zaidi.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 16, 2018

Katika Wiki Ya Shukrani, Ni Nani Aliyempanzi Wa Tumaini Lako?

 Sadick Kilasi     November 16, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   




Siku zote mfumo wa maisha ni ule ule, IMANI, UTAYARI NA MATUMAINI.

Japokuwa wengi hufikiri kwamba watu ambao hawajihusishi na mambo ya kiroho ( dini) hawana imani, lakini ukweli ni kwamba wote tunaishi kwa mfumo huo huo. Utofauti ni kwamba, wengine hutumainia kifo na wengine hutumainia uhai wa milele.

Wale ambao hawasimamii chochote huongozwa na mwili, na wale ambao husimamia ukweli na upendo hawaongozwi na mwili bali na Roho.

Swali langu kwako wewe rafiki yangu? Ni nani aliyempanzi wa mbegu ya matumaini yako? Ni nani anayekuoza na kukutia nguvu kuendelea mbele? Wapi umetia nanga ili kuhakikisha meli yako haiendi mahali?

Ndugu Yangu, umtumainie Mwenyezi Mungu, wote ambao humwani Yesu, mpanzi wa tumaini lao ni Mwenyezi Mungu mwenyewe. Hufanya mambo yao kwa imani, kwani yeye ndiye aliye ngao yao.

Mungu alimwambia Abraham;
Mwanzo 15:1,Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likanena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na dhawabu yako kubwa sana.

 Kwa imani Abramu alitimiza maneno ya Mungu kwani Mungu alijitokeza kwake, akambia kwamba yeye ni ngao yako lakini pia akamwambia kwamba yeye ni tuzo lake. Mbegu ya matumaini ilipandwa ndani ya Abramu, alinza kuishi kama mtu mwenye matumaini, nanga yake ikiwa imetiwa kwa Mungu.

Ndugu, kuwa na matumaini yasiyo na shaka, mtumainie Mwenyezi Mungu, kuwa katika njia zake na pokea tuzo lake.

Mbegu ya matumaini yako lazima iwe Mungu mwenyewe, ikiwa ukitia malighafi kwenye kiwanda, bidhaa itakayotoka lazima iwe sawa na malighafi japokuwa hazita kuwa na sura sawa.

Ndugu yangu, Mtupe Paulo anasema, msijidanganye, marafiki wabaya huhatibu tabia njema, nasi twasema, kiwanda kibovu hakitoi bidhaa njema. Umtumainie Mwenyezi Mungu, ukitia juhudi na kujua kwa Mungu ndiye ngao yako. Usiogope, ukidondoka amka, maana umepewa udhaifu ili viungo vyako vikilegea uvikaze.

Mwamini Mungu, mpokee Kristo Yesu, tumaini lako litie nanga patakatifu huko mbinguni, Kristo Yesu amefanyika kuhani wetu akituombea mambo  mema kwa mfano wa ukuhani wa Melkizedeki ambaye alikuwa mfalme wa amani na hali.

Litie nanga tumaini lako huko, ili lisiteteleke, naam, meli ikitia nanga mahali pasipofaa itayumbayumba na haiwezi kutulia. Usijiamini peke yako. Watu husema, mtu asiyesimamia kwa lolote hudondoka kwa lolote.

Aliye kuumba umtumainie huyo. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 15, 2018

Mshukuru Mungu Kwa Kila Kitu.

 Sadick Kilasi     November 15, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Habari Ndugu yangu? Katika wiki ya shukrani, tunaendelea kuyapa thamani kubwa maisha yetu.

Leo hii tunaiendea siku yetu kwa kumshukuru Mungu kwa kila kitu. Unaposhukuru kwa kila kitu, unashukuru kwa sababu unaelewa ni kitu gani unashukuru.

Mpendwa Ndugu yangu, tunasema mapito ni zawadi yetu, kilichopo ni jibu ya changamoto yetu, naam, tumaini ni nguvu yetu. Ukweli ni kwamba hatuna cha kupoteza katika maisha yetu.


Sisi ambao tumechagua kuishi Nuru, neno ningeli halitutawali. Kama tulifanya makosa hapo mwanzo iliikuwa ni sababu ya kufanya maamuzi bora hivi sasa.

Tunapo mshukuru Mungu kwa kila kitu, hii inafanya tuthamini kile ambacho Mungu amekupa. Nenda leo kwa shukrani, mshukuru Mungu kwa chochote ambacho inakiona mbele yako, mshukuru Mungu kwa historia unazopata lakini pia tumaini letu linapenya patakatifu pa mbinguni, tumetia nanga huko ili tumaini letu liwe lenye nguvu.

Mshukuru Mungu kwa neno lake ambalo umekuwa unalisoma, mshukuru Mungu kwa watu waliokufa kwenye historia zao kwa kuingia katika hatari kubwa ili wewe upate kuishi maisha mema. Wapo wengi waliokufa katika biblia, ili wewe uwasome na uishi maisha yenye maana sasa.

Mshukuru Mungu kwa watu watumishi ambao wanakufundisha na unasoma vitabu vyao, usije ukafikiri huwa unasoma kwa nguvu zako.

Mshukuru Mungu kwa hali ya hewa hivi sasa ili ikichafuka usije ukajutia. Japokuwa itaonekana mjinga ama utajiona wewe mwenyewe mjinga ukimshukuru Mungu kwa ndege, wadudu na wanyama unaowaona, lakini nikwambie ukweli kila kitu cha asili ni zawadi kwa wenye mwili.

Angalia ndege, sauti zao zinakufariji, angalia wanyama pambo la ulimwengu, angalia miti huleta harufu nzuri na kusababisha mvua kunyesha, angalia watu wako wa karibu, ni zawadi yako hao. Usijali kama sasa wapo bize lakini ukweli ni kwamba ukisukwa na jambo zito hapo ndio wa kwanza kukuinua. Mshukuru Mungu kwa kila kitu, usiache chochote.

Unapomshukuru Mungu kwa kila kitu, ni sawa na kupokea kila kitu ambacho Mungu amekupa. Na zaidi ya yote, Mungu ataendelea kukupa zaidi kwa sababu akikupa unapokea.

Je! Ushawahi kumshukuru Mungu kwa ardhi uliyoikanyaga, thamani ya maisha yetu ni pale tulipo. Angalia kwa macho yako jinsi ulivyo hai, gusa mkono wako kwenye moyo uone moyo wako unavodunda, cheki macho yako yanavoona mengi, sikiliza ndugu yangu, akili yako ipo vizuri na ndiomaana unasoma hapa, masikio yako yapo sawa na ndiomaana unasikia, kinywa chako kipo sawa na ndiomaana unasema. Wapo wengi wenye mapungufu ya hivyo vitu, ijapokuwa ni kimoja tu kati ya hivyo, lakini vinawanyima furaha kwa sababu hawana.

Mpendwa Ndugu yangu, inawezekana maisha yako ni magumu, ni magumu kwa sababu hutimizi ndoto zako na huna furaha kwa hilo. Lakini nataka nikwambie kitu kimoja, kuna watu wanapigania maisha ya familia zao, hawajawahi kufikiria juu ya familia zao. Watoto wao kila siku wanahitaji ada na chakula. Kuna wengine wamekosa furaha kwa sababu hata mtoto wa kumlipia ada hana.

Ninachotaka ni nini Ndugu yangu, ni wewe kuangalia ulichonacho na ukione kwa macho yako ikisha mshukuru Mungu. Mungu ametupa kila kitu, lakini hatutaki kukubali kile Mungu ametupa,  Mungu hatupi kile ambacho tunataka bali anatupa kile ambacho tunahitaji.

Siku hii ya leo, ipe thamani kubwa sana, ukiipa leo thamani kubwa itafanya vizuri sana kwenye kile unachofanya, zaidi kesho itakuwa siku ya thamani zaidi ya leo. Ipe leo thamani kubwa tumia kila kitu ambacho umepewa na Mungu  ulichonacho kuhakikisha, maisha yako na ya wengine pia yanakuwa bora zaidi ya ulivyofikiri.

Usiangalie udogo wa jambo, bali tumia vizuri kama zawadi yako. Ndugu yangu, miili yetu ni mikubwa, na ipo kwa sababu ya cell za mwili ambazo ni ndogo ndogo sana kiasi kwamba hata kwa macho huzioni. Usiangalie ni kitu gani huna, bali angalia ni namna gani unavyoweza kubooresha maisha yako zaidi kwa vile vidogo ulivyonavyo ili vifanye kikubwa kiwe hai.

Siku ya leo na vyote unavyoviona ni zawadi yako. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 14, 2018

Katika Wiki Ya Shukrani, Tambua Kitu Kikuongoze Katika Maisha Yako.

 Sadick Kilasi     November 14, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Ukipita nje ya nyumba ambayo wanapika chakula kizuri, utasikia harufu nzuri ya chakula hicho ambacho kinapikwa ndani. Lakini pia kama chakula kinachopikwa si vizuri, utasikia harufu ya ubaya wa chakula.

Katika maisha ndivyo ilivyo, kila jambo huwa lina dalili ya kujiliwa yaani harufu ya kujiliwa na jambo jipya. Kama ndio harufu hiyo unaisikia maeneo ya nyumbani, basis utasema, leo inaonekana kuna chakula kizuri kinapikwa, lakini kutoka na harufu pia waweza kusema leo kuna chakula kibaya kinaandaliwa. Harufu hii haihitaji ukione chakula, bali ni manukato tu yanatosha wewe kukutambulisha.

Unajua mara nyingi kwa sababu ya kukosa umakini, huwa hatuwezi kuona jambo hili la kujiliwa na jambo jipya, dalili.  Kama upo makini unaweza kujiandaa na jambo lolote ambalo linatokea ikiwa upo makini na dalili hata kama linakuja kukuumiza lakini dalili itakulinda. Ukweli ni kwamba, mambo mengi ambayo hutuumiza si ugumu wa mambo hayo ila matarajio ambayo tulikuwa yumejiwekea yakienda tofauti na jinsi tulivyokuwa tunataka ndiyo hufanya tuumie. Moyo wetu unauwezo wa kukubali jambo lolote lile kama tayari tumelifanyia maandalizi kabla halijatokea, hata kama ni maumivu makali, kama uliuandaa moyo wako kupokea maumivu, maumivu hayo hayatakuwa sawa ukilinganisha kama hukujiandaa.

Itambue dalili, itambue harufu ya kujiliwa na jambo jipya, ili kama jambo linalokujilia ni baya ucheze mchezo wa ndani, nje, kujitoa katika mchezo ama kujiingiza katika mchezo.

Wakati mwingine unaweza ukawa unazungumza na mtu, lakini jinsi maongezi yetu yanavyokwenda wakati mwingine huanza harufu ya kumsengenya mtu, cheza mchezo wa kutoka nje ya mazungumzo, wakati mwingine unaweza ukawa unabishana na mtu kiutani tu, ila ukaisikia harufu ya ugomvi, toka nje ya mchezo. Usitake jambo baya likufikie, lakini pia hata kama hamuna uwezekano wa kuyafanya mazungumzo yenu yawe mazuri, usiruhusu matokeo ya dalili yakuumize wewe kihisia.

Yesu alifundisha juu ya jambo hili;  Mathayo 16:1-3, Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. Akajibu, akawambia, (kukiwa jiona, mwasema, kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu. Na asubuhi mwasema, leo kitakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kutambua uso mbingu; lakini je! ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?

Ndugu yangu, Yesu hakuishia tu katika hilo, bali alifundisha juu ya kupana na adui kabla hajakupeleka mahakamani. Lakini yote hii alikuwa anazungumzia harufu ya kujiliwa na jambo jipya na mtu aweze kupatana na jambo jipya.

Hakuna kitu ambacho hakina dalili, hakuna kitu ambacho hakina harufu ya jambo jipya. Dalili ama harufu ni kiungo ambacho kinakuunganisha kutoka jambo ulilokuwa na unalokwenda.

Mpendwa msomaji, katika wiki ya shukrani, mshukuru Mungu kwa kila jambo, naam, dunia huendeshwa kwa majira na wakati wake, lakini tunayozawadi ya pekee ambayo ni harufu, harufu ambayo inatuandaa kuishi jambo jipya.

Mshukuru Mungu leo kwa hali uliyopo, mshukuru Mungu leo kwa yale ambayo unayopia, kwamaana kama unapitia magumu sana hiyo ishara kwamba kunaunafuu unakuja katika maisha yako. Usiku menene sana katika maisha, husababisha pambazuko, ikifika saa nane usiku majira huanza kupambazuka.

Harufu ya maisha yako ni pale ulipo wewe, kila saa, kila wakati tunaingia jambo jipya lakini kila jambo jipya huwa na dalili, harufu. Kwa jinsi maisha yetu yalivyo ni kama mifupa yetu ilivyojipanga. Kwa wale ambao humwamini Yesu hawana usiku wala giza, Paulo anasema, ndani ya nyumba kubwa huwa kunakuwa na vyombo vya aina mbalimbali, vya thamani na visivyo vya thamani, Lakini sisi tunathamini vya thamani pekee. Ndiyo, sisi watu wa nuru, hatuangalii magumu, tunaangalia ni nini tutajifunza kupitia ugumu ule.

Endelea kusoma biblia kwa bidii ufikie uhuru wako wa kimazingira. Hamna namna, lazima tufurahie maisha wakati. Ishi maisha yenye maana na weledi.

Ukawe na shukrani juu yako na wakati wako, na mazingira unayopitia, kubali mazingira, chagua jambo jema kwenye mazingira yako, songa mbele.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, November 13, 2018

Katika Wiki Ya Shukrani; Anza Na Chochote.

 Sadick Kilasi     November 13, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Habari Ndugu yangu?

Katika kuendelea na wiki yetu ya shukrani, ndani ya program yetu ya tabia nne za kuishi kwa mwezi, ili kuishi maisha yenye maana, leo tuangalie, anza na kidogo ulichonacho.

Badala ya kuendelea kulalamika kwamba maisha ni magumu, angalia kwanza, je! hakuna namna ambayo unaweza kuanza na chochote? Mara nyingi ukiendelea kulalamika mika bila ya kuwa na jicho la shukrani huwezi kuona vile ambayo Mungu amekupa.


Badala ya kujiona kwamba wewe ni mtu thaifu na huwezi kufanya lolote na ni mtu ambaye usiye na kipawa chochote, jikubali na kwa kumtumainia Mungu aliyekuumba. Mungu alimwambia Musa, mimi ndiye niliyekuumba nitatia maneno yangu kinywani mwako.

Jikubali, chunguza chochote kile, ili mradi upo hai una chochote kile cha kuanza nacho. Mungu anasema katika kitabu cha ufunuo, wewe unayekiita upo hai kumbe imekufa, tafuta chochote kile ambacho kimebaki kwako na kua kwa hicho ukikesha usiku na mchana.

Mungu anachotaka ni wewe kujikubalia, jikibali pokea vyote ambavyo Mungu kakupa. Lugha ya Mungu ni moja, una nini mkononi mwako? Una nini pembeni yako? Anachotaka ni sisi kukua kwenye vyote ambavyo ametupa. Hakuna kitu amnacho Mungu kakiuumba ambacho huwezi kuanza nacho kuwa fursa kwenye maisha, kila kitu ni jibu la matatizo yetu.

Jikubali, kubali mazingira yanayokuzunguka kwa kupokea kwa shukrani kila ambacho Mungu amekupa. Chochote ambacho unaweza kukibooresha, hata kama kinaonekana ni takataka kwa wengine ukiboresha huwa na thamani kubwa sana. Hakuna kitu ambacho si jibu la changamoto zetu, hakuna kitu ambacho si kiungo kwenye maisha yetu. Kuwa na moyo wa shukrani, yathamini mazingira kwa kuona ni zawadi yako na kiungo cha maisha yako. Kama yalivyo macho yako na ndivyo kila unachokiona ni kiungo mwako, kuna wakati unatumia, kuna wakati hutumii, kila kiungo hufanya kazi kulingana na mazingira.

Anza na chochote, kua Na hicho. Thamani ya chochote kile inategemea mtazamo wako, kuwa na mtazamo chanya wa kugeuza mazingira hasi kuwa chanya. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 12, 2018

Ndani Ya Wiki Ya Shukrani, Mtazamo Wa Kudumisha Ili Kuwa Na Furaha Zaidi.

 Sadick Kilasi     November 12, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Ndani Ya Wiki Ya Shukrani, Mtazamo Wa Kudumisha  Ili Uweze Kuwa Na Furaha Zaidi.

Ni wiki ya shukrani, ambayo imeanza leo. Binafsi ninafuraha kubwa sana ninapokuqndia makala haya,  jambo ninaloweza kushukuru zaidi ni wewe kuendelea kuwa pamoja nasi.

Wiki ya shukrani katika program ya kuishi maisha ya maana kwa mwezi, binafsi ninafuraha sana na naendelea kufurahia maisha.

Katika wiki hii ya shukrani kuna mitazamo ambayo unapaswa kudumisha ili kuendelea kufurahia maisha. Mitazamo hiyo ni yale mafundisho ambayo yalifundishwa na Yesu maarufu kama mafundisho ya mlimani.


Mathayo 5:3-4, Heri walio maskini wa roho;  Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.

Mpendwa wangu ili kuendelea kudumisha furaha yako ni kwamba lazima uishi mtazamo chanya.

Usiangalie tatizo lako bali angalia ni kitu gani kitatokea baada ya kudumisha mtazamo wako chanya. Unajua mara nyingi sana watu tumekuwa tunafanya makosa, tunahuzunika tukitegemea kupata furaha, ni jambo ambalo haliwezekani kabisa.


Endelea kudumisha mtazamo wako chanya hata kwa wakati mgumu. Mambo mabaya hayana budi kuwepo lakini wewe kwa sababu ni mtu wa shukrani angalia tumaini lako la baadae. Haijarishi upo katika hali gani, zingatia kile kizuri wakati wote kwa sababu wakati unakuja utapokea tuzo lako. Ugumu unapita baada ya ugumu ulaini.


Usiangalie tatizo lako angalia tuzo lako. Endelea kufanya unachopaswa kufanya kwa sababu kila japo humtukia kwa wakati wake.

Una heri wewe ambaye ni maskini kwa sababu unaenda kuwa tajiri ukichukua hatua na kudumisha mtazamo wako chanya. Unaheri wewe ambaye unajisikia kuumwa kwa sababu kuumwa sio kifo bali ni mapito. Una heri wewe ambaye umeachwa kwa sababu huna lawama na mtu. Una heri wewe ambaye unasoma hapa na kufanya kazi lile ambalo unalisoma hapa kwa sababu harufu nzuri ya matumaini inanukia ya kuendelea kufurahia maisha.

Chochote kile ambacho ni kidogo, andelea kukipa thamani kitakupa majibu makubwa zaidi ya hayo.

Ishi kwa shukrani, usisahau ulikotoka ambako Mungu kakutoa, thamani kile ulichonacho sasa, furahia kile ambacho unatarajia kupokea.

Yape maisha yako thamani zaidi kwa shukrani, boresha zaidi maisha yako.

Sadick Kilasi wa
jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, November 11, 2018

Wiki Ya Shukrani.

 Sadick Kilasi     November 11, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Ni jumatatu ya tarehe 12/11/2018 siku ambayo tunaenda kuipa thamani kubwa sana. Siku ambayo tunaenda kuishi maisha ya maana zaidi yenye weledi, tukiongozwa na wiki ya shukrani. Tunakwenda kuyapa thamani maisha yetu kwa kuishi maisha yenye maana.

Unaanzaje kuishi shukrani pamoja na misukosuko mingi ambayo inakuzunguka?

 Kwanza kabisa, jambo la kwanza la kuiendea siku hii ya leo ni kuyakubali mazingira ambayo upo. Kama ndo unaamka basi mshukuru Mungu kwanza kwa uwepo wako, lakini pia angalia ni nani ambaye yupo jilani na wewe, mshukuru Mungu kwaajili ya huyo uwepo wake ni faraja kubwa sana kwako hata kama hajakufanyia lolote. Angalia kila kitu ambacho unakiona mshukuru Mungu. Hii unafanya kabla hujatoka nje. Unapofanya hivi unaanza kuishi matumaini kwa kuipa siku yako thamani yake na pia unakuwa unaipokea siku ambayo Mungu kakujalia na vyote ambavyo Mungu kakupa kwa siku hii ya leo. Tuliza mawazo yako hakikisha unafili mazingira na kila kinachokuzunguka. Ikubali siku kwa kuamka kiakili badala ya kuamka kimwili.

Baada ya kutoka nje, kubali kila kitu unacho kutana nacho kwa kusema, asante. Kila kitu kipo chini yako kitimie kama zawadi yako kwa wakati huo. Usikubali mambo ambayo ni ya tamaa yako yaiingilie siku ya leo.

Katika kuhusiana na wengine, mkubali kila mmoja. Tanguliza mapatano badala ya kuhukumu. Mwambie Mungu asante kwaajili huyu ayepo mbele yangu. Mpe thamani kubwa, mwangalie jinsi alivyo kwa jicho la wema. Mtazame harafu mwambie uvohisi juu yake. Kama kunautofauti, ufanye uso wako, uwe kioo kwake chenye kumfanya ajihi kwamba anahitaji kuendelea kuishi. Tumia maneno asante, nashukuru, samahani, kwa wingi usio na mipaka. Msifie pale anapofanya vizuri, mwombe samahani pale unapotia ushauri. Shauri kwa kiasi, ili thamani ya Ushauri wako iwe kubwa zaidi. Aliyeko mbele yako ni zawadi yako. Kila unachofanya tanguliza shukrani. Neno la lawama lisitoke kwako wala hukumu.

Leo ni siku yako ya kipekee, itumie leo kama ni siku yako ya mwisho kuishi leo. Kila jambo unalofanya, fanya kama hutapata nafasi tena ya kufanya.

Mungu atakuti nguvu, anachotaka kwako ni maandalizi ya moyo wako ili nguvu yake itawale moyo wako na akili zako. Shukrani ndiyo nguvu ya kuingia patakatifu yaani amani na furaha isiyoelezeka.

Siku njema yenye thamani zaidi.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tabia Nne Za Kuishi.

 Sadick Kilasi     November 11, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   


Kama tukiishi kawaida katika maisha tutabaki kuwa watu wa kawaida. Lakini kama tupo tayari kubadilika na kwenda mbali zaidi ya kawaida tutakuwa watu ambao si wa kawaida.

Hakuna mtu ambaye anapenda kuishi maisha ya kawaida, kila mtu anapenda kuwa mtu wa utofauti, zaidi ya pale alipo. Kila mmoja anapenda kuwa mtu wa thamani katika jamii, jamii imzungumzie kwa mazuri yake ambayo anafanya. Kila mmoja anapenda kuwa na furaha katika maisha lakini zaidi ya hayo kila mtu hupenda kuona namna gani ambavyo anakuwa na furaha katika maisha.

Japo wengi tunatamani kufikia kiwango kikubwa cha maisha ya furaha lakini wengi wetu hatupo tayari kuchukua hatua na kujizamisha kwenye kile ambacho tunataka kufanya. Wengi tunaishia ukingoni mwa mto japokuwa tunatamani kuvuka, kutoka pale tulipo  na kwenda kwenye iafadhari zaidi.

Wengine tunafeli katika maeneo fulani kwa sababu hatuna maarifa na huwa tunafikiri kwamba kama tukiwa na maarifa fulani tunaweza kuwa katika hali ya furaha.

 Lakini haijarishi kwamba unamaarifa ama la, kitu cha maana ni kwamba pale unapopata maarifa ni uchukue hatua.

Tuangalie tabia nne za kuishi.


1. Shukrani. Pale ambapo unakubali kile ulichopewa na Mungu hats kama ni kidogo, hiyo ndio Shukrani.  Katika kuhakikisha tunaishi maisha yenye maana tutaishi kwa shukrani katika program hii. Wiki ya shukrani itaanza kushukuru kwenye kila kitu ambacho tunakiona na hii itatufanya tukipe thamani kila kitu na kuona fursa sehemu ambayo ni ngumu.

2. Kutawala. Hii ni maana sana katika maisha. Ili uweze kutawala mambo unahitaji kuwa na uwezo wa kutofautisha. Ni kipi kipo nje ya uwezo wako na ni kipi kipo nje ya uwezo wako. Lakini hii itakusaidia kutokuumizwa na hisia mbalimbali zinazosababishwa na wewe mwenyewe na wengine pia. Yapo mengi yakujifunza kwenye kutawala na somo hili tutajifunza na kuishi wiki ya pili ya mwezi.

3. Kukua. Baada ya kutambua nini cha kufanya huhitaji kubaki kama ulivyo, unachohitaji ni kukua zaidi kwenye kile ambacho unakifanya. Chochote kile ambacho unakifanya ili kukipa thamani zaidi tunahitaji kubooresha zaidi na kukua zaidi. Somo hili nalo ni pana. Tutajifunza na kuishi wiki ya tatu.


4. Hamasa. Hamasa ni nguvu ya kukufanya undelee mbele pale unapolegea. Kwa tutakuwa tunajihamasisha kwa njia mbali mbali na njia ya kwanza kabisa ni shukrani kwa hatua ndogo ndogo ambazo unapiga.  Hamasa ni kitu cha muhimu zaidi ili kuendelea kufanya jambo ambalo unafanya.
Tabia hii tutaiishi wiki ya mwisho ya mwezi, itakuwa wiki ya hamasa ili kuendelea kuchukua hatua zaidi.

Hizi ndizo tabia ambazo tutaishi katika program yetu ya mwezi. Itakuwa ni program endelevu. Kila siku asubuhi tutakuwa na  jambo ambalo litakuwa focus zaidi, na kwa kadili ambavyo tutakuwa focus kwenye jambo hilo ndivyo tutakuwa na uelewa zaidi wa jambo hilo. Asubuhi tutakuwa na maelezo mafupi ya hatua za kuchukua kwa kutwa ili tuwe Na jambo la kutanguliza. Kuna mambo mengi sana ya kunyaka katika maisha, usipokuwa makini unaweza kujikuta inabaki njia panda hakuna unakifanya na hakuna kwako ambalo wewe ni mtaalamu wa jambo hilo. Ni muhimu kuwa na shina la jambo, matawi na majani.

Hakuna kinachotikea kama hakuna mtu ambaye hayupo  tayari kuchukua hatua. Kama tutabaki katika ukingo wa mto wa maji bila kujizamisha na hatuwezi kuvuka ng'ambo. Hata kama unamaarifa kama huchukui hatua huwezi kushiriki utamu wa jambo. Bahari kila siku matumaini yake ni kuvuka ukingo lakini haivuki na ndio maana maji yake hayafai kitu. Tumaini la kugonja gonja huumiza moyo.

Karibu tukue kwa pamoja. Lengo la program ni sisi kuwa bora na wengine kuwa bora kupitia sisi. Unaju kwa mtu ambaye anaweza kujihimili mwenyewe basi anauwezo wa kuwahimili wengine. Tunahitaji kuanzia hapa tulipo ili kuifanya dunia kuwa sehemu salama, na kama umebahatika kusoma makala haya ni muda wako wa kuchukua hatua. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, November 10, 2018

Kuwa Na Jicho La Tai, Ishi Matumaini.

 Sadick Kilasi     November 10, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Kuwa Kama Tai.

Tai ni ndege wa kipekee sana. Huishi kwa imani kubwa anapofanya mawindo.  Ukimwangali tai anapofanya mawindo unaweza kujifunza kitu kikubwa sana.

Tai anapotaka kufanya mawindo yake huenda juu sana (juu ya anga), ikisha hujitengeneza katika upande fulani wa pembe na kuangalia chini akiwa mbali kutoka juu. Huitazama dunia kwa lengo la kutaka kupata kitu huku akiwa amejitayarisha kupata anachotaka.

Hupata kile anachotaka kupata akiwa mbali sana juu ya anga, huangalia chini wakati mwingine humwona panya, nyoka na wanyama wengine wanaofaa kuliwa na yeye. Jicho lake hutazama akiwa mbali sana, huchagua anachotaka na kukiendea kile anachotaka kwa kasi ya ajabu. Bila kufanya kosa katika mkao ule ule ambao amekaa, hujiachilia na kukifuatia kile ambacho anakitumainia kukipata. Jambo la kushangaza ni kwamba hata chini kukiwa na wanyama wengi hufuata yule ambaye alikuwa amemtagenti katika pembe aliyokuwa amempimia. Jicho lake huona kutoka mbali sana, hata kama samaki akiwa amejificha chini ya maji jicho lake humwona na kumkamata kwa kujifanyia mawindo yake. Na huwa na maeneo maalumu ambayo atamshika,(shingoni) na kwa jinsi alivyokuwa amejiwekea shabaha yake hushika maeneo yale yale.

Mpendwa msomaji, ikiwa tunaweza kujifunza kutoka kwa tai basi tunaweza kuishi maisha ya maana sana.

Kitu kikubwa ambacho kinafanya maisha yetu yanakosa maana ni kukosa shukrani. Kama jicho letu lingekuwa kama la tai mambo yote yangekuwa na maana sana.

Watu wengi tumekosa matumaini kwa sababu hatuna shukrani. Hatutaki kuamini kile ambacho tayari tunacho, hatutaki kufanya chaguo la muhimu, hatutaki kupokea kile ambacho tayari tunacho. Siku zote tumekuwa tunaishi maisha ya kutamainia vile ambavyo tayari hatunavyo. Lakini licha ya kuwa tunatamania vile ambavyo hatuna bado vile ambavyo tunavyo hatuvikubali. Katika mfumo wa kutembea, huwezi kukandamiza ardhi inayofuata kwa unyayo wako kabla ya kukandamiza ardhi uliyokanyaga kwanza. Kandamiza ulipokanyaga ikisha uendelee mbele. Siku hizi watu wamepotoka kabisa, eti umaskini ni laana, laana maanake nini? Chukua hatua anza kukua ili kwenda unakoelekea.

Maisha yanacheza katika nyanja tatu; imani, utayari na matumaini. Imani huja kwa kusikia, kama huwezi kuamini kile ambacho umekiona, utaaminije kile ambacho hujakiona? Utayari ni kuishi kile ambacho tayari unacho. Matumaini ni maono ya mbali zaidi. Sasa huwezi kuwa na imani ya mbali kama hakuna kidogo cha jilani ambacho tayari unacho. Unapokubari kile ambacho ni kidogo inamaana tayari unaweza kukubali kwamba kuna vikubwa vinakuja.

Shukrani ni uwezo wa kukubali kidogo ambacho tayari unacho ili kupata kikubwa zaidi ambacho hicho sasa tunaita matumaini yako, ama maono yako.

Sasa rafiki yangu, kuwa na jicho la tai, kaa katika makao wa jicho la kuona chema kinachoweza kukupa nguvu ya kuishi tena. Ichunguze harufu ya maisha yako na kitumainie chakula hicho.

Kubali vile ambavyo Mungu kakupa tayari na uache kulalamika na songa mbele. Wakati nabii Elisha alipoletewa lalamiko na mke wa mwanafunzi wake ambaye tayari alikuwa amekufa, na mwanamke huyo alimletea mararamiko kwamba anadaiwa, nabii Elisha alimwuliza kwanza nikusaidie nini? Una nini nyumbani kwako? Akamwambia nina chupa ya mafuta, akamwambia akusanye vyombo vingi ili apate kumimina mafuta, alimimina mafuta vyombo vyote vikajaa mpaka akaenda kuazima vyombo kwa majilani, pale aliposema vyombo vimeisha na ndipo mafuta yaliisha ndani ya chupa. Akaenda kuuza mafuta na kupata fedha na kulipa madeni yake.

Ndugu yangu, popote pale tulipo kipo ambacho tunaweza kufanya, popote pale tulipo kipo ambacho kinaweza kuwa harufu nzuri ya maisha yetu, chukua hatua ili uishi utamu wa harufu. Ingia kwa shukrani wakati unapikea vitu vitakatifu. Acha kulalamika.

Makuhani katika Agano la kale walikuwa wanaingia patakatifu huku wamefumba macho. Ikiwa inamaanisha shukrani kwa kile ambacho tayari umepewa.

Acha kuwa mchoyo, uchoyo ni pale ambapo unasema huna kitu kumbe umeficha mengi ndani yako. Hakuna mtu ambaye hana kitu, mtu yeyote ana kitu cha kumpa mwingine. Neno linasema katika Zaburi, nyingi ni miungu lakini msipowasaidia wengine mtakufa maskini. Ikiwa tutakuwa wachoyo wa vile ambavyo tayari tunavyo  itakuwa kama watu waliokufa. Bwawa lenye maji ambapo haliingizi wala kutoa maji ni lazima maji yake yanuke tu. Hivyo hivyo uliyo unaweza kuirutibisha ardhi yaani watu. Wakati Mungu anatuumba hakutuumba tuwategemee wengine na kama unasoma hapa basi tayari wewe unapaswa kutegemewa na wengine.

Umefungia uwezo wako ndani yako, harafu unasema huna kitu, Mungu katuita sisi Miungu sasa unaposema huna kitu ni kufuru. Hatupati kile tuomba kwa sababu hatukubali kile ambacho tunapewa.

Sasa nataka tuanze kuishi kwa shukrani, nataka mimi na wewe rafiki yangu unayesoma hapa tuishi maisha badala ya kuigiza kuishi maisha.

Nimeanda mfumo wa kuishi maisha yenye maana kwa mwezi mzima; wiki ya kwanza itakuwa wiki ya shukrani, wiki ya pili itakuwa wiki ya kutawala, wiki ya tatu itakuwa wiki ya hamasa na wiki  ya nne ni wiki ya kukua.

Hivi ndivyo ambavyo tutaishi ndani ya mwezi mzima. Na vitu vipo ndani ya mwanadamu, ukisoma katika kitabu cha ufunuo utaona.
Ni lazima tuishi maisha yenye maana ili dunia iwe sehemu sahihi ya kuishi.

Katika maeneo yote manne tutakuwa tunaiendea siku kwa mfumo maalamu. Kama ni wiki ya shukrani basi jambo la kwanza kulitanguliza litakuwa ni shukrani na huku mengine yanafuata kwa nyuma, kama ni wiki ya hamasa basi mwogozo wetu kwa wiki hiyo ni hamasa, mengine yatafuata kwa nyuma.

Ni nani atashiriki? Tutatengeneza group ambalo kila siku asubuhi tutakuwa tunapata kianzio cha mwongozo wetu. WhatsApp group inatosha. Hii haina gharama yoyote. Kama upo tayari nitumie ujumbe  0687000768. Ni mengi ambayo tutajifunza na kufanya maisha yetu yawe na ladha na kwa wengine pia.

Watu wanao hitajika kuanzia kumi na tano, kushuka, ama kumi, ama watano ama pake yangu. Wowote wale ambao wapo tayari kufanya hivyo basi ndio hao.

Lengo ni kuanza na sisi wenyewe harafu baadae kutoka nje zaidi na kuwafanya wengine kuwa na matumaini zaidi kwa kutumia vipawa vya uwezo wetu.

Karibu sana, tuna ujumbe 0687000768 au sadikila65@gmail.com. Kwa pamoja zaidi tunakwenda mbali zaidi. Dunia imekosa kitu kinachoitwa umoja, badala yake kila mtu anaishi na kuhitaji kufalijiwa. ASANTE.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 8, 2018

Elewa Kinachofuata.

 Sadick Kilasi     November 08, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   


Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo humtukia mwanadamu na kufanya awe na uafadhari zaidi wakati anapitia katika hali fulani, msongo wa mawazo, uchovu na mengineyo yanayomfadhaisha.

Kupiga miayo, kukohoa, kujikwaa, kupiga chafya na mengineyo, Mungu huwa anakukumbusha na kutaka ukae katika hali inayofuata lakini kwa sababu umekosa shukrani ya kutambua kusudi la Mungu, huwezi kuona kwamba Mungu anatoa kile kilicho ndani yako ambacho kinakupa uchovu, unabaki kulalamika tu na kukumbatia ule uchungu. Unakosa uelewa kwamba, kujikwaa kunakutamburisha tu kuwa makini. Wajinga hulani wanapojikwaa, welevu hushukuru wanapojikwaa.

Sasa rafiki yangu, kuwa makini vitu hivyo vidogo vidogo. Ukijikwaa mara moja kama ukiwa na shukrani badala ya kulala mika huwezi kujikwaa tena.

Chochote ambacho kinatoka ndani yako, ni kiashiria cha kuashiria kwamba, sasa unapaswa kutoka katika hali fulani kwenda hali fulani. Mshukuru Mungu kwa kila jambo, kwani kwa kutambua huku hutakuwa na cha kupoteza.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 7, 2018

Asiye Na Maarifa Hali Vya Babaye.

 Sadick Kilasi     November 07, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   


Asiye Na Maarifa Hali Vya Babaye.

Baba hutunga sheria,  Mama hutunza sheria.

Ili kuhakikisha nafaidi kila kitu ambacho Mungu ameweka mbele yangu mimi mwanaye, alivyonipa kama zawadi, nimedhamilia kujifunza asili, mifumo, sheria na kanuni zote za dunia.

Dhamira yangu ni kuendelea kuichunguza asili ili nifaidi sheria ambayo imetungwa na Baba na napokea kile ambacho dunia imekitunza, kwani dunia ni Mama yetu ambaye ametunza vilivyotungwa na Mungu.

Ni vingi mno ambavyo vipo duniani ambavyo naweza kutumia kama zana katika shughuli zangu za maisha kwa ujumla.

Chochote ambacho najifunza huwa nakushirikisha, japo siwezi kukushirikisha kila kitu lakini kile ambacho kinauwezekano huwa nakushirikisha katika makala zangu za jikolaushauri.blogspot.com.  Lakini pia huwa sikupi kwa undani na ndiomaana nimeamua kuandika kitabu cha Dunia Mama Haimtupi Mwanaye, na yote ni kuhakikisha na wewe ndugu yangu unakipokea kile ambacho Mungu wetu ametupatia ili tuishi maisha yenye maana bila kulalamika.

Mara nyingi watu tunalalamika katika kila kitu kwa sababu hatuoni vile ambavyo Mungu anatupa ili viwe zana za kutatulia natatizo, kama mkono ulivyo katika kutatua matatizo yako. Unakusaidia kutatua matatizo yako.

Kwa hiyo ndugu yangu jiandae kwa kitabu hichi. Kitakufunza mambo ambayo unaishi kila siku na kila kitu kwako itakuwa ni zawadi yako ikiwa tu utakuwa na jicho la tai yaani kuona jema ndani ya ubaya. Kutokusubiri fursa zigonge mlango badala yake kufungua mlango ili fursa ziingie.

Hakuna maana ya kulalamika wakati unakula. Usipokuwa makini kusikiliza sauti Mungu hutakiona kile Mungu anakupa. Ukikosa maarifa huwezi kula mali za baba yako.

Andaa mate ila usifungue mdomo kwanza, chakula kipo jikoni kinaandaliwa, sijaweka mezani bado. Kikiwa tayari basi😃 utaachama.


Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, November 6, 2018

Mchakato Upo Kinywani Na Ladha Ipo Kinywani.

 Sadick Kilasi     November 06, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Furaha ndio kitu pekee ambacho hutafutwa kwa gharama kubwa na kila mtu, awe tajiri ama maskini.

Kosa kubwa ambalo watu wengi kufanya ni kushindwa kutambua ni wapi ambapo kitengo cha furaha hupatikana. Wengi hufikiri kwamba labda baada ya kutafuta kitu fulani na kukipata ndipo watapata furaha, lakini cha kushangaza ni kwamba hakuna kitu ambacho wanaambulia.

Na kosa kubwa ni kwamba, wengi hatujui ni nini hasa kinachosababisha furaha, ni kitengo kipi ambacho husababisha furaha.

Sasa ili kuhakikisha kwamba nataka uelewe, ni kipi hasa ni kitengo cha furaha, nimekuandalia dhana ya kula chakula na jinsi mfumo unavofanya kazi. Hamna namna usipofuata mfumo ambao ndio kanuni huwezi kufikia malengo yako kwa sababu ni kama unatoka nje ya mstari.

Wakati wa kula chakula, huwa kuna vitengo vitatu ambavyo mtu hushiriki katika utamu wa kula chakula. Simaanishi kwamba anakula sehemu tatu bali namaanisha kwamba, chakula cha aina moja anashiriki kula mara tatu.

Watu wengi huwa tunafikiri kwamba ni ulimi pakee ndio huonyesha ladha ya chakula, na tunasahau maeneno mawili ambayo humlidhisha mtu wakati wa kula chakula.

Eneo la kwanza ni kula chakula bila kukiona, ama kukitia mdomoni. Hapa mtu anaweza kufurahia harufu peke yake bila hata kugusa chakula na kutia mdomoni. Hakuna harufu nzuri ya chakula kama harufu ya chakula ambacho hukili, yaani unatamania tu. Kwa harufu na kuhisi bila kushiriki kimwili mtu anaweza kujiburudisha. Eneo hili ili ulidhike vizuri ni lazima uwe na shukrani kubwa sana.

Eneo la pili ni kinywani, hiki ni kitengo ambacho kila mtu anakifahamu kwa sababu hapa kila mtu huwa anajiona kila kitu anachofanya.  Ladha ya chakula hapa kila mtu anaitambua kwa ulimi, kuonja. Eneo hili unaweza kula chakula na kufurahia bila wasi, haijarishi ni kingi ama kidogo. Mwenye shukrani atafurahia.

Eneo la tatu ni tumboni. Sasa eneo hili halina tabu kwa sababu ndio mwisho wa chakula. Hili ni eneo ambalo chakula kinajaa tumboni, tumbo linakuwa limejaa lakini huwezi kuhisi harufu wala utamu bali kwenye tumbo usawa wa ujazo tu pekee. Kiasi kinaongoza. Mwenye shukrani atafurahia.

Leo napenda niongelee eneo la pili, eneo mchakato, eneo ambalo lazima kinywa kicheze. Ili uone ladha ya chakula kwa ulimi lazima uvunjevunje kile unakula. Ndipo ulimi wako utaona ladha ya chakula unachokula.

Na katika maisha ndivyo mambo yalivyo lazima uvunjevunje kile unafanya. Kama hutovunjavunja  huwezi kuona chochote.  Angalia jinsi kinywa chako kilivo, ulimi ni laini na hauna mifupa, meno ni magumu. Na kinachofanya chakula kiwe kitamu ni ushirikiano kati ya sehemu ngumu na laini.

Magumu yote unayopitia ndio ladha ya maisha. Utamu unakuwepo pale chakula kinamegwa megwa. Chakula kikifika tumboni hakina ladha na ndio maisha jinsi yalivyo, ukifikia ukamirifu huwezi kufurahia maisha. Na ndio maana Mungu alificha hekima, ili watu wawe wanatia juhudi katika kuifichua na kwa sababu inapatikana kwa gharama kabla haijafichuka na ikifichuka inakuwa na gharama kubwa kwa wasioijua kwani kwao ni giza tu.

Furaha kubwa katika maisha ni kugundua jambo jipya, (harufu), nguvu ya kuishi katika maisha ni kuliendea jambo jipya, (mchakato kinywani). Ushindi mkubwa katika maisha ni kufichua jambo jipya.( tumboni). Hizi ndizo zana tatu katika maisha, unazoweza kuishi kwa kutumia mfumo wa chakula.

Jambo moja ambalo unapaswa kujua ni kwamba, ushindi haupagi mtu furaha, bali mashindano ndiyo humpa mtu furaha. Kusinzia ni kutamu kuliko kulala. Ukifikia Mafanikio utakuwa unatamani kupata kingine kwahiyo kama unategemea matokeo ya jambo huwezi kufurahia maisha. Linda sana eneo la harufu na ladha. Harufu inakupa matumaini mapya, ladha inakupa nguvu ya kuyaendea matumaini.

Angalia kinywa chako kina meno ambayo ni magumu, na ulimi ambao ni laini. Bila ushirikiano wa vitu hivyo viwili chakula hakina ladha.

Usiogope mapito uliyopitia, usiangalie mabaya pekee bali angalia na mazuti uliyonayo. Hata kama wewe ni nani, tafuta jambo la kufanya, lifanye kwa moyo na hekima ya kujifunza kutoka katika mapito yako.

Ukipitia maisha magumu hapo nyuma, kupambambanua hekima ni rahisi kwa sasa kwa sababu tayari ulikuwa ndani ya mchezo. Ukipitia maisha laini, kupambanua maisha sasa inahitaji kutia juhudi kwa sababu huna mapito. Kwa hiyo mapito ni zawadi kwa wenye shukrani ili kuishi maisha ya furaha.

Ukawe na tafakari njema.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 5, 2018

Adhibu Matendo Yako.

 Sadick Kilasi     November 05, 2018     NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI, NJOZI     No comments   



Kuna utofauti mkubwa sana kati yako wewe na matendo yako. Chochote ambacho unakifanya sio wewe.

Sasa, ili kutokujutia na kuumizwa na kile ambacho umefanya, jitambue wewe ni nani. Wewe ni tofauti kabisa na chochote ambacho umekiona, unakiona na ambacho utarajia kukiona.

Mara nyingi maisha yetu, hayaumizwi na sisi bali kile ambacho kipo nje ya sisi, kile ambacho umeshuhudia, kile ambacho umefanya, kile ambacho unakiona, ndicho ambacho kinakuumiza.

Njia rahisi ya kutokuumizwa na chochote ni kuadhibu kile umefanya. Adhibu kwa kubooresha na kukua kwenye kile ambacho umefanya.

Adhibu kinywa chako kwa kuboresha maneno yako.

Adhibu mapito yako na makosa yako kwa kujifunza kutokana na makosa.

Wewe ni tofauti kabisa na mwili wako, wewe ni tofauti kabisa na mavazi yako. Kile ambacho kinakukela kiadhibu kwa kukiboresha.

Tafakari njema.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, November 3, 2018

Kama Ndege Arukaye Angani.

 Sadick Kilasi     November 03, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   



Maisha yetu kama ndege, ndege  viumbe warukao angani, na ndivyo safari ya maisha yetu jinsi.

Akiwa angani haachi alama yoyote, na popote alipopita amepitia hapo. Ndivyo yalivyo maisha yetu, tunajitambua pale tulipo. Yale tuliyopitia, tuliyotenda, tuliyo tamka yapo na sisi, yanatembea nasi.

Ndege huyu huenda kutua katika tawi alipendalo, na kutulia hapo. Ndivyo maisha yetu yalivyo. Popote ambapo utaweka kambi leo, ulipopita umepita, maamuzi uliyofanya nyuma yapo na wewe, mwelekeo wako ndio umekufikisha hapo ulipo. Utakayo wawazia leo ni kutokana na huko nyuma.

Ndege hatagemei tawi alituwa sana, bali hutegemea mbawa zake. Nasi vivyo hivyo, wapo wengi ambao wanatuzunguka, wazazi, ndugu marafiki, kile tulicho nacho lakini hatuwezi kuwekeza utegemezi kwa asilimia zote hapo, lazima tujitegemee wenyewe kwa kiasi kikubwa kama ndege atuavyo kwenye tawi lolote na hutegemea mbawa zake. Ukimtemea mwanadamu utafadhaika sana, ukitegemea kitu ipo siku kitu hicho kitaondoka, ukijitegemea mwenyewe ipo siku utakata tamaa, sasa mtegemee Mungu aliyekuumba na akaumba dunia na vyote yeye anaweza kuhimili kila kitu kilichopo duniani. Tia nanga ya matumaini kwake.

Kama ndege afanyavyo maamuzi ya kutua katika tawi la mti na ndivyo sisi tufanyavyo maamuzi. Jiangalie sasa, ni maamuzi gani unayafanya? ni wapi unaelekeza hema? mwelekeo wa kutua maamuzi ni wapi unaelekeza? Maadamu unayo sasa, unaweza kubadili mwelekeo na kufanya maamuzi yakufaa, kama ndege afanyavyo mchezo wa kumyenda juu angani wakati anabadili mwelekeo.

Chochote utaka kuamua, kitakuwa na wewe maisha yako yote. Na chochote itaamua kitaitwa leo, kama in kukuumiza kitakuumiza leo ya hiyo leo, kama ni cha kufurahisha kitakufurahisha hiyo leo. Lakini maadamu unayo sasa unaweza kufanya kila kitu kwenda sawasawa na ukawa unafanya ujazo wa maamuzi sahihi kila leo.

Kama ndege anavoonekana na ndivyo tulivyo, thamani ya kila kitu ni pale tulipo, basi, sisi ni uwepo tu. Ni kama umeme vile.

Ukawe na tafakari njema leo juu ya wewe.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ▼  November (25)
      • Katika Wiki Ya Kukua, Wewe Umeachwa.
      • Katika Wiki Ya Kukua, Kama Hatua Unazopiga Unapoel...
      • Katika Wiki Ya Kukua, Washa Njiti Yako.
      • Katika Wiki Ya Kukua.
      • Je! Ndege Hutegemea Tawi Alilotua?
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Mungu Ndiye Mfalme Wa Kil...
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Jiweke Nafasi Ya Wengine.
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Moyo Huwa Unakubali.
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Inahitaji Utambuzi Na Aki...
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Toka Nje Ya Hema Yako.
      • Ndani Ya Wiki Ya Kujitawala, Jitambue Wewe Mwenyewe.
      • Katika Wiki Ya Shukrani, Itazame Wiki Yako Imekwen...
      • Katika Wiki Ya Shukrani, Ni Nani Aliyempanzi Wa Tu...
      • Mshukuru Mungu Kwa Kila Kitu.
      • Katika Wiki Ya Shukrani, Tambua Kitu Kikuongoze Ka...
      • Katika Wiki Ya Shukrani; Anza Na Chochote.
      • Ndani Ya Wiki Ya Shukrani, Mtazamo Wa Kudumisha Il...
      • Wiki Ya Shukrani.
      • Tabia Nne Za Kuishi.
      • Kuwa Na Jicho La Tai, Ishi Matumaini.
      • Elewa Kinachofuata.
      • Asiye Na Maarifa Hali Vya Babaye.
      • Mchakato Upo Kinywani Na Ladha Ipo Kinywani.
      • Adhibu Matendo Yako.
      • Kama Ndege Arukaye Angani.
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates