JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, June 26, 2018

Jiandae Kutegua Chochote Kwa Wakati Wowote.

 Sadick Kilasi     June 26, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Maisha ni kama movie ndani ya wakati. Yapo mengi ambayo yanayojitokeza ndani ya movie hii ya maisha. Kwetu sisi movie hii inaanza baada tu ya kuzaliwa na mwisho wake ni kifo.

Kwa bahati mbaya au nzuri mhusika na sterling wa maisha ni muhusika mwenyewe anayeishi maisha.

Maisha ni movie ya ukweli na watazamaji wa hii movie ni ndugu na marafiki. Watazamaji hawa hupendelea kuitazama movie wakati imeisha yaani wakati hatupo duniani.

Tunaishi ndani ya wakati na hakuna anayejua siri ya zaidi yapale alipo zaidi ya Mungu wetu aliyetuumba. Zaidi ya hapo ulipo ni siri licha ya kwamba unamipango na malengo ambayo umejiwekea.

Kuna mengi yanatokea kwenye maisha yetu ni madogo sana ambayo wewe kama starling huwezi kuyaona lakini yanaweza kuharibu kabisa ladha ya movies hii ikawa haina ladha kabisa, hii ndio historian ya maisha yako. Mambo haya ni madogo kwa sababu yanadumu kwa muda madogo lakini ni mambo makubwa kwa sababu ndiyo mambo ambayo huwa yanaharibu maisha yetu.

Yapo yale ambayo yanajulikana kana kwamba ni makubwa kwa sababu huwa yanadumu kwa muda mrefu na kwa bahati nzuri tatizo lolote likijulikana si tatizo tena.

SOMA:Ishi Ndani Ya Wakati Usipoteze Chochote.

Habari ipo kwenye mambo madogo kabisa, kwa kweli haya yanahitaji umakini mkubwa sana ili kuyaona. Na mara nyingi huwa yanatokea na kufutika, yanatokea na kufutika na kama huishi kwa kanuni ya nje ndani huwezi kuona Bambi kama kama unaishi kwa mazoea. Mambo haya ndiyo huleta ladha ya maisha japo ni madogo. Haya ndiyo huamua mtu kuishi kwa kuraha au la.

Kila wakati tunategua kitendawili. Kwa sababu, sisi huishi katika hali tatu, mapito, tulipo na tunakokwenda. Mapito yetu tayari tumepita, tulipo tupo na kitendawili ni tunapokwenda.

Ulipo palinde sana rafiki yangu, haijarishi kiasi gani kila kitu kinategemea japo kwa bahati nzuri tunapokwenda ni fumbo kwa kila mtu. Tegua kitendawili kwa makini kwa sababu ulipo ndipo panaweza kujenga maisha yako au kuharibu kabisa maisha yako.

Hakikisha unatumia kanuni ya nje ndani wakati wote, hasa kwenye mahusiano. Mtu akikuudhi hakikisha unaacha naye salama. Linda sana uwepo wako kila mahara, tegeua kitendawili chako kwa makini maana kuharibu ni rahisi sana lakini kujenga ni kazi kweli.

Wakati wote ukiwa ndani ya mwili jiandae kwa lolote ili usistukie matokeo. Kila mahala ni vitendawili tu. Nafikiri ushawahi kukutana na mtu ambaye analalamika kwa kusem, huyu naye sijui matokeo wapi, kaharibu kila kitu. Hivi ndivyo mambo yanavyokwenda, punguza kulalamika, tafakari kila kitu, aise haijarishi upo katika hali gani, usijionee huruma mwenyewe wakati beba lawama na majukumu ya kila wakati.

Mungu akuongoze sawasawa na mapenzi yake.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, June 25, 2018

Kutumia Sheria Ya 'Ndani Nje' Kutatua Matatizo.

 Sadick Kilasi     June 25, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, MAHUSIANO, NJOZI     No comments   



Kila sehemu katika dunia tunayoishi ni kama muujiza, chochote ambacho unakiona kwa macho ni muujiza kwako. Ninaposema muujiza simaanishi ya kwamba ni kitu cha kutisha au ni kitu ambacho hujawahi kukiona, hapana, japo ni kile kitu ambacho unakiona nje lakini ndani huwezi kuona wala kuadhiri.

Kwa mfano, mchezo wa mpira, kwa kawaida mtu anayecheza ndani anakuwa ndani ya mchezo lakini kuna watu ambao wapo kama watazamaji, hawa huwa wanaangalia vizuri zaidi ya mchazaji mwenyewe lakini hawajisikii kama vile wachezaji wanavojisikia ndani, umeona. Kanuni hii nimeipa jina nje, ndani.

Kanuni hii inagusa katika kila eneo la maisha yetu. Na kama utakuwa makini utatatua kila jambo kwa kanuni hii.

Katika eneo la maisha. Tunaamka asubuhi na kuelekea kwenye shughuli zetu, na Mara nyingi tunakuwa ndani ya wakati, tunakuwa kama wachezaji ambao wanacheza, mara nyingi hatuwezi kutazama kila kitu ambacho tunakifanya. Kumbuka tunaishi ndani ya wakati na ndipo ambapo tutafanya vizuri mambo yetu, lakini si kila kitu tutafanya vizuri, kwahiyo ni vema wakati jioni tukashiriki maisha yetu kama watazamaji na si wachezaji tu.

Katika eneo la mazungumzo, kwanza kabisa kama tunavotambua lugha nini? Ni sauti ambazo zimekubaliwa na jamii fulani ili kuwasilisha ujumbe. Sasa changamoto nini, maneno yanatungwa si kitu ambacho kimejiunganisha na hali ya mtu anavojisikia. Kwahiyo maneno nje lakini kuna  mchezo ambao unaendelea ndani, kitu kinachoitwa hali ya mtu, namna anavojisikia. Kwahiyo kama unazungumza na unapaswa kuwa makini ili uone zile lugha za mwili kwa sababu maneno hayatoshi kuwasilisha ukweli.

Eneo la kusoma, unapokuwa unasoma kitabu unapaswa kuwa makini sana, unaposoma tunakuwa tunakalili, tunakuwa nje ya mchezo lakini ili ukweli uwe wako unapaswa uwe ndani ya huo ukweli. Kwahiyo ni vema ukisha soma kitabu ukatafakari yale ambayo umeyasoma yawe hali yako na si mshuhudiaji.

Katika ugomvi, ni vema ukawa nje ya ugomvi kuliko kuwa ndani ya ugomvi. Kuwa mtazamaji wa ugomvi na si mchezaji wa ugomvi.

Kanuni hii inatumika kila mahala, jambo la msingi ni hili unapotumia kanuni ya ndani, nje, kwa mambo ya muhimu hakikisha unakuwa ni mchezaji na ni mtazamaji. Na kwenye mambo ya hovyo wapaswa kuwa mtazamaji kwani hayana budi kuwapo, wewe shiriki kama mtazamaji.

Ukawe na tafakari njema, ukiwa nje ya mchezo wa uliyosoma hapa ili uwe ndani ya mchezo.

Karibu katika group letu la SURA YA UKWELI kujifunza zaidi.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, June 23, 2018

Viashilia Viwili Ambayo Vitaonyesha Kwamba Umefikia Katika Ukweli.

 Sadick Kilasi     June 23, 2018     NJOZI     No comments   



Katika maisha kuna mengi huwa tunajifunza na kuyatafuta huku na kuko. Hekima ndicho kitu ambacho watu wengi wanatamani kuifikia lakini mafanikio ya pesa na mahusiano ni maeneo ambayo watu wengi wanataka kuwa bora.

Mafanikio yote ya maisha yanapaswa kwenda sambamba. Kwanza linaanza swala la hekima harafu yanakuja mambo mengine. Lakini si kwamba unaanza kumiliki kwanza hekima ndipo mafanikio mengine yanafuata, hapana, bali ni wewe pale ambapo unaanza kuona mambo fulani ndipo sasa tunaweza kusema nimekuwa mkomavu sasa.

Mapito yako na hekima ni vitu ambavyo vinaushilikiano mkubwa sana na ndio maana huwezi kuachanisha kati ya mapito yako na hekima.

SOMA:Kaa Na Ujiulize Mwenyewe Unasemaje?

Vipo vitu viwili ambavyo ni vya muhimu sana ambavyo utaanza kuviona kuifikia ukomavu.

Kitu cha kwanza, siku ambayo utagundua hujui chochote basi ndio siku ambayo utakuwa umefikia hekima na ukuu wa ukweli. Sasa waweza kujiuliza sasa wewe unasema nitakapokuwa sijui chochote ndipo nitakapokuwa nimeiifikia hekima ya kweli kivipi? Wakati kuwa na hekima ni kuwa na welevu na mambo mengi, wewe unamaanisha nini?

Ipo tofauti ndogo sana ya mjinga na mwelevu. Mjinga anaamini mwenyewe yeye ni mwelavu na kwenye hekima anaamini yeye hajui chochote na hana chochote.

Kiachilia cha pili ni kuanza kutambua kanuni ya nje ndani, ndani nje. Hii ni kanuni ambayo inatumika kila mahala lakini huwezi kutambua kama huoni. Mfano ni pale mtu anapoongea kanuni hutumika, michezo mbalimbali ipo ndani ya kanuni hii, mapito ya maisha yako, yapo ndani ya kanuni hii.

Ukiaanza kutambua na kuona viashilia hivi basi wewe unaanza kuufikia ukuu wa ukweli. Kwa bahati mbaya watu huanza kuona hivi mpaka wakiwa na miaka arobaini na zaidi huko. Lakini wewe unapaswa kuanza kuishi sasa na siyo ukifikia miaka arobaini.

Unaweza ukawa unatembea huku umekufa, nakuambia ukweli. Ukisoma katika ufunuo kwenye kitabu cha Biblia, Ufunuo 3:1,  matendo yako yanakuonyesha kwamba u hai kumbe umekufa. Mbele anakwambi katafute chochote ambacho umebaki nacho, ukapambane usiku na mchana.

Kwahiyo ni vema tukajitaidi kuishi badala ya kutembea huku umekufa.

Ukawe na tafakari njema. Karibu ujiunge na group letu la SURA YA UKWELI ujifunze zaidi.

Mungu awe nawe.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Jifunze Kufanya Kitu Hiki Siku Zote Za Maisha Yako.

 Sadick Kilasi     June 23, 2018     MAHUSIANO     No comments   



Kuna kitu kimoja ambacho watu huwa hawapendi kujifunza kufanya na ndicho ambacho huleta mafanikio katika maisha.

Kitu hicho ni kujifunza kujishusha siku zote za maisha. Mtu ambaye anatabia ya kujishusha ni rahisi kupokea anachotaka, kwa sababu anayepokea siku zote ni yule ambaye hana. Mtu ambaye anacho hawezi kupokea chochote kwa sababu anacho. Kwa hiyo ili kupokea unachotaka ni vema ukawa mtu wa kukubali kwamba huna.

SOMA:Anayetunga Siye Anayeamua, Anayeamua Siye Anayetunga.

Mtu ambaye atabia ya kujishusha siku zote ni wa shukrani. Kwa hiyo ni vema tukawa watu wa shukrani ili tuendelee kupokea zaidi na zaidi. Huwezi kupata mafanikio yoyote katika maisha kama shukrani, na ambayo naizungumzia hapa ni ili shukrani ya kushukuru wakati wa hali ngumu, sio ile ya kinafki ambayo umepokea tayari ndiyo unashukuru, hapana, jishushe kabla hujapewa ili upate.

Ukawe na siku bora na kutawaliwa na shukrani ya kweli kutoka kwa Mungu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Ishi Ndani Ya Wakati Usipoteze Chochote.

 Sadick Kilasi     June 23, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Kama ilivyo kawaida kwenye hii dunia ambayo inaendeshwa kwa hisia na mitazamo, tunapaswa kuishi ndani ya Wakati.

Kuna mengi ambayo yanatokea ndani ya wakati yanahitaji kusuluhishwa ndani ya wakati. Kwa kweli hakuna wakati sahihi wa kufanya jambo sahihi, kila wakati ni sahihi kufanya jambo sahihi.

Tatizo kubwa kwenye ulimwengu huu wa matokeo ni kwamba watu wanatumia hisia zaidi, kama unahitaji kutatua jambo fulani ambalo ni la muhimu na wewe hisia zako ziko chini huwezi kuuona umuhimu wa kufanya jambo hilo, mpaka hisia zako zipande ndipo unapaswa kutatua jambo lilikuwa litatiliwe ndani ya wakati.

Mtu anayeishi ndani ya wakati, wakati wote kwake ni sahihi kufanya jambo sahihi. Fikiria mtu ambaye anauhitaji muhimu wa kutatua shida yake ndani ya wakati maalumu harafu ghalama yake ni ndogo tu, harafu ikatokea kwamba akashindwa kufanya lile jambo kwa muda kwa sababu ameshindwa kumudu ile ghalama na wewe ulikuwepo hapo, harafu baada ya muda kidogo ukamwendea wakati wa kutatua lile jambo umekwisha ukawa ndo unampa msaada wa pesa, tens zaidi ya pesa ambazo alikuwa unahitaji kwa kweli hata uona umuhimu wa zile pesa.

SOMA:Tiba Kwa Ajili Ya Mawazo Na Stress.

Ni sawa na kumpa maiti mamilioni wakati hawezi kufanya chochote.
Kwa hiyo tunapaswa kuishi ndani ya wakati ili tusipitwe na wakati.

Kufanya jambo sahihi hakuhitaji wakati bali kila wakati ni sahihi wa kufanya jambo sahihi. Ni vema, tumuuachie Mungu fikra zetu kwa sababu yeye ni Mungu wa haki siku zote kuliko kusubili kuanza kupandisha hisia zako kwa nguvu zako.

Fanya kwa wakati,
Kwa kuwa una wakati,
Utafika wakati,
Hutakuwa na wakati,
Wa kufanya kwa wakati.

Ishi ndani ya wakati.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, June 21, 2018

Acha Ushabiki Kuwa Mwanafunzi Kwenye Kila La Maisha Yako.

 Sadick Kilasi     June 21, 2018     MAHUSIANO     No comments   



Kama kuna kitu kikubwa ambacho kinaharibu maisha ya watu hasa kwa vijana basi ushabiki. Ushabiki umekuwa kila eneo la maisha yetu.

Katika kitabu cha Yeremia 12:5-6, Ikiwa umepiga mbio pamoja na hao waendao kwa miguu, nao wamekuchosha, basi wawezaje kushindana na farasi? Na ujapokuwa nchi ya amani u salama, lakini utafanyaje hapo katika kiburi cha Yordani? Kwa maana hata ndugu zako, na nyumba ya baba yako, wamekutenda mambo ya hila, naam, wamepiga kelele nyuma yako, usiwasadiki, wajapokwambia maneno mazuri.

Acha ushabiki kwenye kila eneo la maisha yako, ninapozungumzia ushabiki simaanishi ule ushabiki wa mpira na michezo mingine hapana, namanisha kwenye kila kitu, katika familia, kwenye kazi, popote ulipo kuwa na Ukweli, jifunze kwenye kila hali.

SOMA:Kaa Na Ujisikilize Mwenyewe Unasemaje.

Mungu alikuwa anamwambia Yeremia kwamba wewe unalalamika kwamba mimi nimewaacha watu wabaya wanapiga mbio lakini wewe huoni hapo hapo unapoishi nao wapo hivo hivo lakini huoni kabisa unawaona wale wa mbali. Umewashindwa watembea kwa miguu, je utawaweza farasi?

Hata sisi mambo yapo hivo hivo, tunatumia hisia zetu na mitazamo yetu kuhukumu watu walio mbali wakati mambo hayo hayo sisi wenyewe tunayafanya.

Kwenye kila eneo la maisha yako usichukulie kama kawaida, kila siku ni siku mpya. Mambo hayawi kama yalivo, jiandae kujifunza ili usistukie kitakacho tokea.

Usimwamini mtu yeyote kwenye kila eneo la maisha yako, usiwe shabiki kwa yeyote bali kuwa mwanafunzi kwa kila mtu, jifunze kwenye kila eneo la maisha yako hutakuwa na mtu wakumlaumu.

Duniani hamna ukamilifu kwahiyo ukiwa shabiki kwa watu utabeba na visivyo bebeka. Punguza kunoti mambo bali jifunze kumegamega na kufinyangafinyanga kila neno ili upate msingi wako ambao ndio ukweli ambao hauhitaji ukalili.

Usishabikie mtu yeyote, bali jifunze tu, hata kama unaangalia mpira ni vema ukawa unaangalia bila ushabiki ili ujifunze. Unaweza kujifunza namna ya kuwa jasiri na mambo mengi.

Kuna vitu viwili ambavyo dunia inatumia kufanya maamuzi, ni hisia na mitazamo. Hisia na mitazamo sio ukweli wenyewe.

Kwahiyo rafiki yangu kuwa makini na kila mtu.

Karibu kwenye group letu la SURA YA UKWELI tupate kujifunza kwa pamoja.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tiba Kwa Ajili Ya Mawazo Na Stress.

 Sadick Kilasi     June 21, 2018     NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI, NJOZI     No comments   



Tress za mawazo ni ugonjwa ambao unasumbua sana watu wengi hasa kwa zama hizi.

Wengi wanalalamika kwa maisha yamekuwa magumu, hali ni ngumu katika kila mahali. Lakini kwa bahati mbaya mambo hayajawahi kuwa rahisi hata kama unapesa mambo ya tress yanabaki pale pale kama furaha yako inategemea vitu.

Changamoto haiwakumbi watu kwenye kipato pekee bali katika mahusiano, kazi zetu, urembo wetu, imani yetu na kila sehemu ya maisha yetu.

Watu wengi wamejikuta wakifanya vitu vitu vingi ili kuondoa hali hii lakini wapi. Wengine huishia kutumia madawa ya kulevya, pombe, pombe Kali, mazoezi, kufanya mapenzi na mengine mengi lakini hali imebaki palepale kwa sababu ubongo umesha beba kitu hicho kipo ndani yako.

Kuna kitu kimoja ambacho unapaswa kutambua ili kutotawaliwa na tress na mawazo. ISHI NDANI YA WaKATI. Ndiyo, yapaswa kuishi ndani ya Wakati, haijarishi vipi unapaswa kuishi ndani ya wakati.

SOMA:Kuondoa Matatizo Yako Yote Fanya Kitu Hiki.

Nini maana ya kuishi ndani ya wakati?

Kuishi ndani ya wakati ni KUWA.  Mahali popote ambapo upo unapaswa kuwepo. Japo kuna mengi unahitaji kufanya lakini usiishie kusema tu kwamba nataka kufanya hiki na hiki, Hapana, unapaswa kujiunganisha na ndoto ili usitawaliwe na mfadhaiko.

Hivi ndivyo tunapaswa kuwa siku zote, yaani hakikisha kumiliki chochote fanya unachopaswa kufanya kwa wakati.

Ishi ndani ya wakati, usimiliki chochote, angusha mitazamo yako, ishi kwa usawa, kuwa wewe wakati wote, usiige wala kuiguza kwa yeyote, kuwa, fanya, pokea, Hizi ni tiba za mfadhaiko na mawazo.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, June 20, 2018

Anayetunga Siye Anayeamua Wala Anayeamua Siye Anayetunga.

 Sadick Kilasi     June 20, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, MAHUSIANO, NJOZI     No comments   



Siku zote katika familia baba ndiye anayetawala na kutunga mambo mbalimbali, mama kazi yake ni kutunza sheria ambazo zimetungwa na baba. Mama kazi yake ni kuhifadhi yale ambayo baba anayasema.

Lakini pamoja na kwamba baba ndiye anayetunga lakini siye anayetoa amri, lakini pamoja na kwamba mama ndiye ayetunza sheria siye ambaye anatoa amri katika familia.

Je ni nani ambaye huwa anatoa amri katika familia?

Ukipanda mbegu ardhi ndiye inayootesha ile mbegu lakini ardhi inakutegemea wewe mpanzi kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu wewe ndiye upandaye. Lakini baba kama mpanzi hawezi kujisifia bila mama muoteshaji ambaye ndiye mpanzi mwenyewe.

Mpendwa msomaji, watu hawa wawili baba na mama lazima waafikiane kwa pamoja ili wafanye Maamuzi yaliyo sahihi. Baba akifanya Maamuzi peke yake hayawezi kuwa maamuzi bora na sahihi katika familia mpaka mama ahakiki.
Mbegu huwa haioti mpaka ife lazima wote wawili wakubaliane kwa pamoja na wafanye maamuzi kwa pamoja.  Kuna msemo unasema wawili wakiungana nao wanakuwa mwili mmoja na kuwa kitu kimoja. Neno hili linapatikana katika Biblia.

Kanuni hii haifanyi kazi katika mazingira ya nje pekee, kanuni hii inafanya kazi mpaka kwenye saikolojia.

Kuna Maamuzi mawili ambayo ni hatari sana ambayo mhusika akiwa anatumia katika maisha yake.
😳Mtazamo
😭Na hisia zako.

Vitu hivi viwili usipo vipatanisha katika kufanya maamuzi ni hatari sana katika maisha yako. Maisha yako yatawaliwa na huzuni na kujisikia hovyohovyo kila wakati.  Na kama ni furaha utapata furaha ya muda na siyo ya kudumu siku zote. Wakati unaanza kufanya jambo utaanza kwa hisia na hamasa kwa sababu tu ni mwanzo.

Vitu viwili hivi vinapaswa kupatana kila eneo lako la maisha. Ukitaka kufanikiwa katika kila eneo lazima ulifie lile  jambo ndipo utapata mafanikio.

Kumbuka kitu kimoja rafiki yangu ambacho nimekuwa nazungumzia kila wakati, dunia haipo sawa lakini wewe kwa sababu si wa dunia hii lazima uishi kwa usawa. Usawa ndiyo maisha ya furaha na amani.

Tumia kanuni hii katika kila eneo la maisha yako ili uanze kufurahia maisha.

Kama bado hujajiunga na group letu la SURA YA UKWELI, tafadhari tuwasiliane ili kwa pamoja tupate kujifunza mengi zaidi.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, June 17, 2018

Kaa Na Ujisikilize Mwenyewe Unasemaje.

 Sadick Kilasi     June 17, 2018     No comments   



Katika ulimwengu huu wa matokeo mambo tote yanafanywa kwa hisia na mtazamo.

Lakini baada ya kuona watu wanatumia hisia zaidi na mtazamo yao ilibidi sheria ziwekwe. Je nini kilichokosekana kwenye ulimwengu huu? Kwa kweli ulimwengu huu umekosa kitu kinachoitwa usawa, uswa haupo ndiomaana tunaishi kwa sheria yaani komandi.

Je tunaweza kuishi kwa usawa katika ulimwengu huu? Ndio tunaweza, licha ya kwamba sheria ni nyingi kuliko kawaida lakini tunaweza kuishi kwa usawa pale tu tutakapoanza kujisikiliza wenyewe ndani mwetu.

Tatizo kubwa ni kwamba pale changamoto inapotokea tunatafuta majibu nje ya sisi na hilo ni tatizo kubwa mno.

Popote ulipo kukiwa na tatizo tambua umevunja sheria ya watu japo wewe ni mtu wa usawa ndani mwako, hii itakusaidia kuvumilia ile hali hata kama wewe sio mkosaji.

Kwa hiyo ukitumia akili yako mwenyewe kufanya maamuzi hakuna kitakacho kuumiza hata kama ni kigumu kiasi gani kwa sababu unatambua ya kwamba hii ni hali ambayo nimechagua mwenyewe bila kulazimishwa na yeyote.

Jifunze kujisikiliza mwenyewe kabla ya kutafuta majibu nje yako, utaishi kwa usawa na upendo.

Karibu katika group letu kujifunza zaidi.

Mungu awe nawe.

Jikolaushauri.blogspot.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, June 15, 2018

Usiamini Ukweli Namna Unavotaka Wewe Bali Amini Kwa Sababu Ndivyo Ukweli Unavotaka Uwe.

 Sadick Kilasi     June 15, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Kosa kubwa ambalo watu wamekuwa wakilifanya ni kuamini jambo kama wao wanavotaka lile na kuaminisha jambo hilo liwe hivo.

Wengi wamejikuta wapo kwenye vivuli vya ukweli kwa sababu ya kunoti mambo badala ya kujiingiza moja kwa moja kwenye hilo jambo na mwisho wamebaki wakimiliki mtazamo yao badala ya kumiliki ukweli wenyewe.

Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Usijiaminishe jambo kama wewe unavotaka hakikisha unatafuta ukweli halisi badala ya kumiliki kivuli cha ukweli.

Ukisoma kitabu hakikisha utafakari ulishosoma kwa kuvunjavunja neno moja baada neno ili uishi ndani ya ukweli.

Acha kunoti mambo kama yalivo bali hakikisha kila jambo unalosoma linakuwa lako wewe pekee.

Neno la Mungu ndilo kweli yenyewe. Vitabu vingi vya kawaida vinaandikwa kwa hisia zao na kuaminisha watu kwamba huo ndo ukweli yenyewe.

Duniani hakuna ukweli, hapa tupo bustanini kuwa ta tahadhari na jambo lolote lile lililo mbele yako. Maua na mbogamboga ni vya muda. Bustani sio shamba.

Kama bado hujajiunga na group letu la SURA YA UKWELI basi hakikisha kwamba unajiunga ili kujifunza zaidi.

Mungu awe nawe.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, June 14, 2018

Kuuondoa Matatizo Yako Yote Fanya Kitu Hiki.

 Sadick Kilasi     June 14, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, NJOZI, TAFAKARI YA ROHO     No comments   

.

Siku zote mimi huwa naamini hakuna matatizo duniani. Ninapoamini hivi simaanishi ya kwamba na wewe uamini ya hivi kwamba hakuna matatizo duniani, kwa kweli hilo sasa ndilo litakolokuwa tatizo lako sasa.

Tatizo lolote lile ambalo unalo kwa kawaida hilo si tatizo lako tatizo lako ni mtazamo wako.

Chochote kile ambacho unakimiliki ndicho tatizo lako. Hakuna mtu anayemiliki kitu na yeyote atakayemiliki basi hilo ndilo litakuwa tatizo lake.

Ninaposema kumiliki kitu ninamaanisha ya kwamba kumili kutoka ndani mwako mpaka nje yaani kwenye vitu unavyoviona.

SOMA:Mzazi Usimwadhibu Mtoto Kibinafsi.

Umiliki wa jambo au kitu unaanzia ndani yako kwenye fikra zako ndipo unatoka nje unapodhamini vitu. Nimekwambia siku zote tatizo lako tatizo lako si tatizo lako tatizo lako ni mtazamo wako.

Ukimiliki mtazamo wako kaa na utambue hilo ndo tatizo lako na ndiomaana hapo juu nimekwambia ya kwamba usiamini tu kwamba hakuna matatizo duniani, usiwe na mtazamo huu kabisa lisije kuwa tatizo kwako.

Leo nataka nikwambie kitu kimoja, kama kuna tatizo lolote ambalo unalo basi yakupasa uondoe huo mtazamo wako na usimiliki chochote ndani ya akili yako ubaki mtupu.

Tunamshukuru Mungu kwaajili ya upendo wake ambao ametupa, anatupa,  maisha ni sasa na siyo baadae.

Tatizo lako unahofu na hicho ulichonacho usije kukipoteza wakati jibu la mambo yote ni wakati (muda).

Usimiliki chochote kwenye maisha yako kisije kuwa hicho ndicho kitakuwa tatizo lako.

Ukawe na siku bora na tafakari njema. Karibu katika group letu la SURA YA UKWELI ili upate kujifunza mengi zaidi, nafasi zimebaki nne kati ya watu watano. Group ni bure kabisa, Ila ni watu watano tu ambao wanakiu ya kutomiliki chochote.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, June 13, 2018

Mzazi Usimwadhibu Mtoto Kibinafsi.

 Sadick Kilasi     June 13, 2018     MAHUSIANO     No comments   



Siyo vibaya mtoto kupewa adhabu kutoka kwa mzazi wake. Mtoto lazima aonywe kwa sababu anapaswa kuonywa.

Katika dunia hii ya wema na ubaya adhabu kwa mtoto ni ya muhimu sana ili kumpa tahadhari mtoto.

Lakini kuna kitu kimoja ambacho wazazi huwa wanafanya bila kutambua wanapompa adhabu mtoto ni kwamba wanampa adhabu mtoto kibinafsi yaani mzazi anamwadhibu mtoto kama anavotaka yeye. Wengi wanawadhibu watoto kuvutia kwao haijarishi inafaida au la. Wengine huadhibu watoto wao kwa sababu huogopa aibu kutoka kwa watu wengine.

Wengine huwaadhibu watoto wao lakini wao huendelea kufanya yaleyale makosa ambayo watoto wanefanya ama la wanafanya makosa mengi tu ambayo wao wenyewe huyafunika makosa yao.

Katika dunia hii ya matokeo, dunia ambayo ambayo inaendeshwa kwa mtazamo ni vema mzazi ukawa unamwadhibu mtoto huku ukitambua kabisa namuonya au nampa tahadhari ya kwamba dunia hii ni ya kuwa na tahadhari na kila kitu. Lakini ikiwa utamwadhibu mtoto wako kwa kuona kwamba unachofanya ni sahihi, utamwonya bila kujua unachofanya. Dunia hii hakuna aliyekamilika. Mwoonye mtoto kwa upendo si kwa mapenzi. Mpe tahadhari mtoto si kumwambia usifanye kabisa. Dunia hii ni ya hisia na mtazamo. Katika mazingira yoyote unayoyaona tambua kwamba ni mtazamo wako lakini sio wewe. Ushawahi kuona jambo kwa kipindi fulani ulikuwa unaamini ni sahihi lakini ikafika wakati lile jambo kumbe ulikuwa unakosea yaani halipo hivo tofauti na ulivokuwa  unaona, kwahiyo kuwa makini na kila kitu kwenye hii dunia.

Je ni ipi adhabu nzuri?

Ni Mungu pekee ambaye hutoa adhabu nzuri ya upendo na yenye faida. Wana yaani wakomavu hufurahia sana adhabu ya Mungu kwa sababu inafaida kubwa sana baadae.

Mungu hutoa adhabu kwa watoto wake kwa muda maalumu kwa umri maalumu na hali maalumu.

Kwahiyo ni vema mzazi kuwa na utambuzi wa adhabu ambayo unampa mwanao, je imejiunganisha na upendo wa Mungu? Adhabu kwa mtoto ni muhimu.

Ukawe na siku bora kabisa na kutafakari hili. Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp basi tuwasiliane ili uungwe kwenye kundi. Kuna mengi yakujifunza karibu sana ujiunge nasi. Tuwasiliane kwa 0687000768 au sadikila65@gmail.com. Tuma ujumbe.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, June 12, 2018

Upendo Na Haki Vikifanya Kazi Kwa Pamoja Huleta Usawa.

 Sadick Kilasi     June 12, 2018     MAHUSIANO, TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai unaendelea vizuri. Karibu katika makala hii ili tuweze kujifunza haya niliyokuandalia.

Upendo ni neno ambalo dunia imekuwa ikilizungumzia sana, lakini kwa bahati mbaya wengi wamekuwa wanapiga kelele kuhusu upendo wasitambue nini hasa maana ya upendo.

Tabia ya watu kutopenda kujifunza kwenye mambo madogomadogo imepelekea kutotambua nini hasa kinachoelezewa. Mara nyingi watu wamemekuwa wakikumbatia kivuli cha upendo wakifikiri huo ndo upendo wenyewe. Tabia ya watu kuamsha hisia zao wenyewe wanavotaka ndizo zimepelekea kupoteza ladha ya ukweli.

Tujue nini hasa maana ya upendo,

Upendo ni hali ya kuvutia mtu au kitu kwenye moyo. Mtu anapoona kitu au mtu akivuta kwenye moyo, ndipo mwenyewe anakili kwamba nimependa kitu hiki au mtu huyu. Upendo kama upendo hufanya kazi kwa mfumo binafsi, mhusika binafsi anavutiwa na kitu ikisha anasema nimekipenda.

Watu wengi, hasa vijana wamejikuta wakitumbukia kwenye hali hii wakijua ya kwamba wamependa kumbe wanajidanganya. Unapokuwa unatumia hisia zako binafsi kupenda kitu unakuwa na mapenzi na kitu na huo sio upendo halisi bali ni kivuli chake. Siku zote upendo wa dunia au wa mwanadamu ni wa kibinafsi tu na wengi wamejikuta wakitumbukia kwenye mtego huu ambao mwisho hujikuta ile hali ambayo walikuwa nayo mwanzo inaanza kupotea kidogo kidogo kwa sababu hisia  au hamasa hii huwa haidumu.

Je upendo wa kweli ni upi?

Upendo wa sababu.
Upendo uliounganishwa na haki.

Nini maana ya haki?
Haki ni umiliki wa jambo. Mtu anapokuwa anatambua jambo basi anamiliki haki yake ya utambuzi na hiki ndicho kinampa amani na furaha ya kweli ambayo huleta upendo wa kweli.

Je upendo wa kweli ni upi?
Kumpenda asiyekupenda huo ndo upendo wa kweli. Hichi ndicho kitu ambacho Mungu anahitaji kutoka kwetu na sio kuwa na upendo wa kibinafsi ambao ni kumpenda unayetaka kumpenda, kwa kweli huo si upendo wa kweli. Tunajidanganya tu mwisho maisha yanakuwa maisha ya kujilazimisha na kuvumiliana kitu ambacho Mungu hatarajii kutoka kwetu.Upendo wa kweli haubagui bali unadondoka popote palipokosa upendo.

Ni hayo tu rafiki yangu kwa leo ambayo nimekuandalia, japo yapi mengi sana ya kujifunza juu ya upendo na haki, kama unaswali lolote tafadhari usiache kuuliza lakini pia kwa muda mrefu nilikuwa bado nilikuwa sina group ya kujifunza zaidi sasa napenda kutangaza nafasi za watu watano pekee ambao wanapenda kujifunza zaidi. Group hili litaendeshwa kwa njia ya mtandao wa WhatsApp.

Kwa sasa napenda kutoa nafasi hii ya watu watano kwanza harafu baadae tutaangalia uzito wa mambo utakavokuwa. Na kwa nafasi hii tano za kwanza group litakuwa bure kabisa. Japokuwa kutakuwa kunasheria kwenye group ambazo zitatakiwa kufwatwa.

Mpendwa rafiki yangu kuna mengi sana ambayo nimekuandalia na nitakuandalia wakati, tutashirikisha mengi. Tafadhari kujiunga na group tuma ujumbe kwenye namba hii 0687000768 au email yangu ni sadikila65@gmail.com, tuma namba yako ya WhatsApp na majina yako. Nafasi tano tu, tafadhari uwe na nia ya kujifunza, umiliki ukweli nao ukweli ukuweke huru. Asante sana.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, June 9, 2018

Ukweli Haupambwi.

 Sadick Kilasi     June 09, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   



Kitu kikubwa ambacho ulimwengu umekosa kwa asilimia kubwa basi ni ukweli. Ukweli umekuwa adimu kama madini ya thamani kubwa. Watu wakikutana na ukweli huwa wanachoka haraka sana na kuukimbia kwa sababu ukweli sura ni mbaya sana.

Najua kila mtu anakitabu cha dini kwao lakini kwa sababu vitabu vya dini huzungumza na kueleza mambo ya ukweli wengi huwa hawapendi kabisa kusoma vitabu hivi.  Ukweli una sura mbaya, ukweli haupambwi ndivyo vitabu vya dini vilivyo.

Watu wanakimbia ukweli na kukimbilia mambo ya udakuudaku, mambo ya hovyo hovyo watu ndiyo wanayapenda. Watu wanapenda giza kwa sababu ya tamaa zao. Kuna jambo la ajabu ambalo dunia inayo, ni maajabu kweli kweli, mtu akifanya jambo sawa huwa halizungumzwi kabisa lakini mtu akifanya jambo ovu linasambaa kama upepo.

Hii dunia imejaa maajabu kweli kweli hata kama ukizungumza ukweli usipoupamba kiasi cha kuuharibu watu ndo wanaitikia, watu hawataki kabisa kujifunza bali wanataka kushabikia mambo.

Rafiki yangu wewe ni moja kati ya hao, badilika dunia hii inaendeshwa kwa hisia, jifunze kupitia maabdiko matakatifu, jifunze kwenye kila mazingira unayopitia, jifunze kwa  Watu ambao wamefikia ukomavu mkubwa, jifunze kwenye kila hali unayopitia, hali yoyote unayopitia ni hali lakini sio uhalisia wenyewe.

Vitabu vitakatifu hufundisha kweli yenyewe, vitabu hivi huweka mambo yote wazi wazi yaliyojificha yanafunuliwa kwa kila adumuye katika kusoma, Binafsi naiamini Biblia takatifu na hiyo ndo kweli yangu.

Kwenye huu ulimwengu wa miujiza ni bora kuwa na wasiwasi na kila kitu kwa sababu mambo yanaendeshwa kwa hisia za watu fulani ambayo wanapambapamba mambo ili kivutia zaidi.

Ukawe na tafakari njema.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, June 7, 2018

Chochote Kinachofanyika Kwenye Ulimwengu Huu Ni Cha Kibinafsi.

 Sadick Kilasi     June 07, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Kama unaishi kwenye dunia hii ya matokeo ukweli ni kwamba utakuwa umeona mengi na kufanya mengi sana. Wakati mwingine unafanya unalofanya ukiwa hujui nani unamfanyia kwa vile labda hujajiuliza maswali kwanini unafanya.

Ukweli ni kwamba chochote kinachofanyika chini ya jua ni cha kibinafsi ni Mungu pekee ambaye anafanya kwa upendo wake yeye mwenyewe kwetu sisi bila kujali kivipi sisi tulivyo. Lakini sisi tunayowafanyia wengine yote ni ya kibinafsi.

Ndoa ni ya kibinafsi, lugha tunayozungumza ni ya kibinafsi, pesa tunazotumia ni za kibinafsi, hewa unayovuta ni ya kibinafsi, malezi ya watoto ni ya kibinafsi. Chochote kinachofanyika ni cha kibinafsi.

Rafiki yangu, nakwambia chochote kinachofanyika ni kibinafsi ili uwe makini na kila kitu ili usije ukajikuta unajistukia pale ulipofika.

Kuwa makini na chochote unachofanya usije ukaumiza wengine au ukajikuta unaumia mwenyewe.

Ukawe na tafakari njema katika hili.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, June 3, 2018

Kama Dunia Ingekuwa Hivi..

 Sadick Kilasi     June 03, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Ni rahisi sana kukelwa na jambo ambalo hulitaki kwenye dunia hii ya matokeo.

Mambo ni mengi haswa yanayotokea, kelele nyingi, usumbufu mwingi na mambo ni huku na huko.

Ni lahisi sana kulaumu wakati unapotatizwa na hali kama hizi lakini je ni kweli kulaumu kwako kwafaa?

Vipi dunia ingekuwa kimya kabisa hamna sauti yoyote ambayo tunaisikia tungekuwa katika hali gani? Mambo yangekuwaje?

Je tungelaumu au tungeshukuru? Kama kila kitu  kwako ni uchovu basi anza kuchunguzachunguza ili uone.

Sauti za ndege kwetu ni faraja, sauti za watu kwetu ni faraja, popote pale tulipo kwetu ni faraja.

Kuwa na moyo wa shukrani, yote ni sawa.

Ukawe na siku bora na yenye mafanikio.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, June 1, 2018

Kuwa Na Matumizi Mazuri Na Hali Yako.

 Sadick Kilasi     June 01, 2018     NJOZI     No comments   



Yapo mambo mengi yanayotokea katika maisha yetu, nayo tumepewa na Mungu ili tuyatawale.

Kila kilichopo mbele yako ni cha  kukitawala lakini si kikutawale.

Itawale hofu yako na siyo kuruhusu hofu ikutawale wewe.

Itawale furaha yako na si kurusu furaha yako ikutawale wewe.

Itawale hasira yako na si kuruhusu hasira yako ikutawale wewe.

Itawale vitu vyako na si kurusu vitu vyako vikutawale wewe.

Yatawale maumivu yako na si kuruhusu maumivu yako yakutawale wewe.

Chochote mile ambacho unakiruhusu kikutawale wewe basi hayo ni matumizi mabaya ya kitu hicho.

Vitu vyote vipo kwa sababu, ikiwa vitatumika vibaya basi vitakuwa ni tatizo kwenye maisha yetu.

Usiruhusu chochote kikutawale katika maisha yako bali unachopaswa kufanya ni kukitumia vema.

Ukawe na siku bora kabisa.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ▼  June (17)
      • Jiandae Kutegua Chochote Kwa Wakati Wowote.
      • Kutumia Sheria Ya 'Ndani Nje' Kutatua Matatizo.
      • Viashilia Viwili Ambayo Vitaonyesha Kwamba Umefiki...
      • Jifunze Kufanya Kitu Hiki Siku Zote Za Maisha Yako.
      • Ishi Ndani Ya Wakati Usipoteze Chochote.
      • Acha Ushabiki Kuwa Mwanafunzi Kwenye Kila La Maish...
      • Tiba Kwa Ajili Ya Mawazo Na Stress.
      • Anayetunga Siye Anayeamua Wala Anayeamua Siye Anay...
      • Kaa Na Ujisikilize Mwenyewe Unasemaje.
      • Usiamini Ukweli Namna Unavotaka Wewe Bali Amini Kw...
      • Kuuondoa Matatizo Yako Yote Fanya Kitu Hiki.
      • Mzazi Usimwadhibu Mtoto Kibinafsi.
      • Upendo Na Haki Vikifanya Kazi Kwa Pamoja Huleta Us...
      • Ukweli Haupambwi.
      • Chochote Kinachofanyika Kwenye Ulimwengu Huu Ni Ch...
      • Kama Dunia Ingekuwa Hivi..
      • Kuwa Na Matumizi Mazuri Na Hali Yako.
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates