Siku zote katika familia baba ndiye anayetawala na kutunga mambo mbalimbali, mama kazi yake ni kutunza sheria ambazo zimetungwa na baba. Mama kazi yake ni kuhifadhi yale ambayo baba anayasema.
Lakini pamoja na kwamba baba ndiye anayetunga lakini siye anayetoa amri, lakini pamoja na kwamba mama ndiye ayetunza sheria siye ambaye anatoa amri katika familia.
Je ni nani ambaye huwa anatoa amri katika familia?
Ukipanda mbegu ardhi ndiye inayootesha ile mbegu lakini ardhi inakutegemea wewe mpanzi kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu wewe ndiye upandaye. Lakini baba kama mpanzi hawezi kujisifia bila mama muoteshaji ambaye ndiye mpanzi mwenyewe.
Mpendwa msomaji, watu hawa wawili baba na mama lazima waafikiane kwa pamoja ili wafanye Maamuzi yaliyo sahihi. Baba akifanya Maamuzi peke yake hayawezi kuwa maamuzi bora na sahihi katika familia mpaka mama ahakiki.
Mbegu huwa haioti mpaka ife lazima wote wawili wakubaliane kwa pamoja na wafanye maamuzi kwa pamoja. Kuna msemo unasema wawili wakiungana nao wanakuwa mwili mmoja na kuwa kitu kimoja. Neno hili linapatikana katika Biblia.
Kanuni hii haifanyi kazi katika mazingira ya nje pekee, kanuni hii inafanya kazi mpaka kwenye saikolojia.
Kuna Maamuzi mawili ambayo ni hatari sana ambayo mhusika akiwa anatumia katika maisha yake.
😳Mtazamo
😭Na hisia zako.
Vitu hivi viwili usipo vipatanisha katika kufanya maamuzi ni hatari sana katika maisha yako. Maisha yako yatawaliwa na huzuni na kujisikia hovyohovyo kila wakati. Na kama ni furaha utapata furaha ya muda na siyo ya kudumu siku zote. Wakati unaanza kufanya jambo utaanza kwa hisia na hamasa kwa sababu tu ni mwanzo.
Vitu viwili hivi vinapaswa kupatana kila eneo lako la maisha. Ukitaka kufanikiwa katika kila eneo lazima ulifie lile jambo ndipo utapata mafanikio.
Kumbuka kitu kimoja rafiki yangu ambacho nimekuwa nazungumzia kila wakati, dunia haipo sawa lakini wewe kwa sababu si wa dunia hii lazima uishi kwa usawa. Usawa ndiyo maisha ya furaha na amani.
Tumia kanuni hii katika kila eneo la maisha yako ili uanze kufurahia maisha.
Kama bado hujajiunga na group letu la SURA YA UKWELI, tafadhari tuwasiliane ili kwa pamoja tupate kujifunza mengi zaidi.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment