Ni rahisi sana kukelwa na jambo ambalo hulitaki kwenye dunia hii ya matokeo.
Mambo ni mengi haswa yanayotokea, kelele nyingi, usumbufu mwingi na mambo ni huku na huko.
Ni lahisi sana kulaumu wakati unapotatizwa na hali kama hizi lakini je ni kweli kulaumu kwako kwafaa?
Vipi dunia ingekuwa kimya kabisa hamna sauti yoyote ambayo tunaisikia tungekuwa katika hali gani? Mambo yangekuwaje?
Je tungelaumu au tungeshukuru? Kama kila kitu kwako ni uchovu basi anza kuchunguzachunguza ili uone.
Sauti za ndege kwetu ni faraja, sauti za watu kwetu ni faraja, popote pale tulipo kwetu ni faraja.
Kuwa na moyo wa shukrani, yote ni sawa.
Ukawe na siku bora na yenye mafanikio.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment