Kitu kikubwa ambacho ulimwengu umekosa kwa asilimia kubwa basi ni ukweli. Ukweli umekuwa adimu kama madini ya thamani kubwa. Watu wakikutana na ukweli huwa wanachoka haraka sana na kuukimbia kwa sababu ukweli sura ni mbaya sana.
Najua kila mtu anakitabu cha dini kwao lakini kwa sababu vitabu vya dini huzungumza na kueleza mambo ya ukweli wengi huwa hawapendi kabisa kusoma vitabu hivi. Ukweli una sura mbaya, ukweli haupambwi ndivyo vitabu vya dini vilivyo.
Watu wanakimbia ukweli na kukimbilia mambo ya udakuudaku, mambo ya hovyo hovyo watu ndiyo wanayapenda. Watu wanapenda giza kwa sababu ya tamaa zao. Kuna jambo la ajabu ambalo dunia inayo, ni maajabu kweli kweli, mtu akifanya jambo sawa huwa halizungumzwi kabisa lakini mtu akifanya jambo ovu linasambaa kama upepo.
Hii dunia imejaa maajabu kweli kweli hata kama ukizungumza ukweli usipoupamba kiasi cha kuuharibu watu ndo wanaitikia, watu hawataki kabisa kujifunza bali wanataka kushabikia mambo.
Rafiki yangu wewe ni moja kati ya hao, badilika dunia hii inaendeshwa kwa hisia, jifunze kupitia maabdiko matakatifu, jifunze kwenye kila mazingira unayopitia, jifunze kwa Watu ambao wamefikia ukomavu mkubwa, jifunze kwenye kila hali unayopitia, hali yoyote unayopitia ni hali lakini sio uhalisia wenyewe.
Vitabu vitakatifu hufundisha kweli yenyewe, vitabu hivi huweka mambo yote wazi wazi yaliyojificha yanafunuliwa kwa kila adumuye katika kusoma, Binafsi naiamini Biblia takatifu na hiyo ndo kweli yangu.
Kwenye huu ulimwengu wa miujiza ni bora kuwa na wasiwasi na kila kitu kwa sababu mambo yanaendeshwa kwa hisia za watu fulani ambayo wanapambapamba mambo ili kivutia zaidi.
Ukawe na tafakari njema.
0 comments:
Post a Comment