Katika maisha kuna mengi huwa tunajifunza na kuyatafuta huku na kuko. Hekima ndicho kitu ambacho watu wengi wanatamani kuifikia lakini mafanikio ya pesa na mahusiano ni maeneo ambayo watu wengi wanataka kuwa bora.
Mafanikio yote ya maisha yanapaswa kwenda sambamba. Kwanza linaanza swala la hekima harafu yanakuja mambo mengine. Lakini si kwamba unaanza kumiliki kwanza hekima ndipo mafanikio mengine yanafuata, hapana, bali ni wewe pale ambapo unaanza kuona mambo fulani ndipo sasa tunaweza kusema nimekuwa mkomavu sasa.
Mapito yako na hekima ni vitu ambavyo vinaushilikiano mkubwa sana na ndio maana huwezi kuachanisha kati ya mapito yako na hekima.
SOMA:Kaa Na Ujiulize Mwenyewe Unasemaje?
Vipo vitu viwili ambavyo ni vya muhimu sana ambavyo utaanza kuviona kuifikia ukomavu.
Kitu cha kwanza, siku ambayo utagundua hujui chochote basi ndio siku ambayo utakuwa umefikia hekima na ukuu wa ukweli. Sasa waweza kujiuliza sasa wewe unasema nitakapokuwa sijui chochote ndipo nitakapokuwa nimeiifikia hekima ya kweli kivipi? Wakati kuwa na hekima ni kuwa na welevu na mambo mengi, wewe unamaanisha nini?
Ipo tofauti ndogo sana ya mjinga na mwelevu. Mjinga anaamini mwenyewe yeye ni mwelavu na kwenye hekima anaamini yeye hajui chochote na hana chochote.
Kiachilia cha pili ni kuanza kutambua kanuni ya nje ndani, ndani nje. Hii ni kanuni ambayo inatumika kila mahala lakini huwezi kutambua kama huoni. Mfano ni pale mtu anapoongea kanuni hutumika, michezo mbalimbali ipo ndani ya kanuni hii, mapito ya maisha yako, yapo ndani ya kanuni hii.
Ukiaanza kutambua na kuona viashilia hivi basi wewe unaanza kuufikia ukuu wa ukweli. Kwa bahati mbaya watu huanza kuona hivi mpaka wakiwa na miaka arobaini na zaidi huko. Lakini wewe unapaswa kuanza kuishi sasa na siyo ukifikia miaka arobaini.
Unaweza ukawa unatembea huku umekufa, nakuambia ukweli. Ukisoma katika ufunuo kwenye kitabu cha Biblia, Ufunuo 3:1, matendo yako yanakuonyesha kwamba u hai kumbe umekufa. Mbele anakwambi katafute chochote ambacho umebaki nacho, ukapambane usiku na mchana.
Kwahiyo ni vema tukajitaidi kuishi badala ya kutembea huku umekufa.
Ukawe na tafakari njema. Karibu ujiunge na group letu la SURA YA UKWELI ujifunze zaidi.
Mungu awe nawe.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment