Siyo vibaya mtoto kupewa adhabu kutoka kwa mzazi wake. Mtoto lazima aonywe kwa sababu anapaswa kuonywa.
Katika dunia hii ya wema na ubaya adhabu kwa mtoto ni ya muhimu sana ili kumpa tahadhari mtoto.
Lakini kuna kitu kimoja ambacho wazazi huwa wanafanya bila kutambua wanapompa adhabu mtoto ni kwamba wanampa adhabu mtoto kibinafsi yaani mzazi anamwadhibu mtoto kama anavotaka yeye. Wengi wanawadhibu watoto kuvutia kwao haijarishi inafaida au la. Wengine huadhibu watoto wao kwa sababu huogopa aibu kutoka kwa watu wengine.
Wengine huwaadhibu watoto wao lakini wao huendelea kufanya yaleyale makosa ambayo watoto wanefanya ama la wanafanya makosa mengi tu ambayo wao wenyewe huyafunika makosa yao.
Katika dunia hii ya matokeo, dunia ambayo ambayo inaendeshwa kwa mtazamo ni vema mzazi ukawa unamwadhibu mtoto huku ukitambua kabisa namuonya au nampa tahadhari ya kwamba dunia hii ni ya kuwa na tahadhari na kila kitu. Lakini ikiwa utamwadhibu mtoto wako kwa kuona kwamba unachofanya ni sahihi, utamwonya bila kujua unachofanya. Dunia hii hakuna aliyekamilika. Mwoonye mtoto kwa upendo si kwa mapenzi. Mpe tahadhari mtoto si kumwambia usifanye kabisa. Dunia hii ni ya hisia na mtazamo. Katika mazingira yoyote unayoyaona tambua kwamba ni mtazamo wako lakini sio wewe. Ushawahi kuona jambo kwa kipindi fulani ulikuwa unaamini ni sahihi lakini ikafika wakati lile jambo kumbe ulikuwa unakosea yaani halipo hivo tofauti na ulivokuwa unaona, kwahiyo kuwa makini na kila kitu kwenye hii dunia.
Je ni ipi adhabu nzuri?
Ni Mungu pekee ambaye hutoa adhabu nzuri ya upendo na yenye faida. Wana yaani wakomavu hufurahia sana adhabu ya Mungu kwa sababu inafaida kubwa sana baadae.
Mungu hutoa adhabu kwa watoto wake kwa muda maalumu kwa umri maalumu na hali maalumu.
Kwahiyo ni vema mzazi kuwa na utambuzi wa adhabu ambayo unampa mwanao, je imejiunganisha na upendo wa Mungu? Adhabu kwa mtoto ni muhimu.
Ukawe na siku bora kabisa na kutafakari hili. Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp basi tuwasiliane ili uungwe kwenye kundi. Kuna mengi yakujifunza karibu sana ujiunge nasi. Tuwasiliane kwa 0687000768 au sadikila65@gmail.com. Tuma ujumbe.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment