Tress za mawazo ni ugonjwa ambao unasumbua sana watu wengi hasa kwa zama hizi.
Wengi wanalalamika kwa maisha yamekuwa magumu, hali ni ngumu katika kila mahali. Lakini kwa bahati mbaya mambo hayajawahi kuwa rahisi hata kama unapesa mambo ya tress yanabaki pale pale kama furaha yako inategemea vitu.
Changamoto haiwakumbi watu kwenye kipato pekee bali katika mahusiano, kazi zetu, urembo wetu, imani yetu na kila sehemu ya maisha yetu.
Watu wengi wamejikuta wakifanya vitu vitu vingi ili kuondoa hali hii lakini wapi. Wengine huishia kutumia madawa ya kulevya, pombe, pombe Kali, mazoezi, kufanya mapenzi na mengine mengi lakini hali imebaki palepale kwa sababu ubongo umesha beba kitu hicho kipo ndani yako.
Kuna kitu kimoja ambacho unapaswa kutambua ili kutotawaliwa na tress na mawazo. ISHI NDANI YA WaKATI. Ndiyo, yapaswa kuishi ndani ya Wakati, haijarishi vipi unapaswa kuishi ndani ya wakati.
SOMA:Kuondoa Matatizo Yako Yote Fanya Kitu Hiki.
Nini maana ya kuishi ndani ya wakati?
Kuishi ndani ya wakati ni KUWA. Mahali popote ambapo upo unapaswa kuwepo. Japo kuna mengi unahitaji kufanya lakini usiishie kusema tu kwamba nataka kufanya hiki na hiki, Hapana, unapaswa kujiunganisha na ndoto ili usitawaliwe na mfadhaiko.
Hivi ndivyo tunapaswa kuwa siku zote, yaani hakikisha kumiliki chochote fanya unachopaswa kufanya kwa wakati.
Ishi ndani ya wakati, usimiliki chochote, angusha mitazamo yako, ishi kwa usawa, kuwa wewe wakati wote, usiige wala kuiguza kwa yeyote, kuwa, fanya, pokea, Hizi ni tiba za mfadhaiko na mawazo.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment