JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, March 12, 2019

Vita Vya Akili

 Sadick Kilasi     March 12, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Vita Vya Akili Na Jinsi Ambavyo Tunapaswa Kuvaa Utayari Unaofaa.


Akili zetu hupitia vita vikali sana, ukizingatia kwa hivi sasa jinsi dunia inavyokwenda kasi na mambo jinsi yanavyokwenda.


Kukua kwa maendeleo ya teknolojia kumetufanya watu tuwe karibu sana kiasi kwamba tumekuwa tunajisahau sisi wenyewe na kuchukuliwa na mafuriko ya internet ambamo ndani yake kuna mikondo mikali sana ya mitandao ya kijamii na google yenyewe kwa ujumla.


Lakini pia hilo linapelekea mashindano ya kimaisha ambayo yanasababisha watu kukosa kuishi maisha yao halisi ambayo Mungu pekee ndie anajua timanzi ya kila mmoja.


Mara nyingi tunapowatazama watu waliofanikiwa mafanikio ya nje akili zetu moja kwa moja zitwambia hayo ndiyo maisha sahihi ya kuishi na si pale tulipo. Kwa kweli maendeleo ya internet yanatuchua bila sisi wenyewe kujua.  Dunia inatulaghai hasa, kweli kweli na huo ndo ukweli wa maisha.

Kila mtu anataka kufanikiwa, mafanikio ya kimwili zaidi, kuwa na gari nzuri, nyumba nzuri, kuvaa vizuri lakini hakuna mtu ambaye yupo tayari kuinamisha mgongo ili awe daraja la mwingine. Kuna pumbazo ambalo akili zetu zimepumbazwa badala ya vitu kutusaidia bali sisi tunekuwa watumwa wa vitu.

Hivi ndivyo vita ya akili, akili zetu zinahitaji utulivu mkubwa sana ili kuepuka kuchukuliwa na hisia za mazingira ambayo tunaishi na kuamini kwamba bila kitu hiki mambo hayawezekani. Akili zetu zinahitaji kukazwa na sisi wenyewe ili kutokusumbuliwa na hisia kama mti unavyosumbuliwa na upepo kupelekwa huku na huku.

Kanuni ya NDANI/NJE ama kwa jina lingine kukusanyika na kutawanyika inapaswa kutumika vizuri sana ili tukae katika mkao wa UFALME na si kupelekwa huku na huko kwa tamaa za dunia hii.

Kuna mkao mmoja ambao Mungu anataka tukae wakati wote naam, mkao huu ni wa UTUPU na UKIWA.

Mathayo 5:3 Heri walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.

Utayari huu ni uwezo wa kuishi Leo bila kujali matatizo ya jana na bila wasi wasi wa kesho. Huu ni uwezo wa kuvuta mafanikio ya baadae na kuishi leo na ndio maana twasema hakuna mafanikio duniani ila kuna kuishi mafanikio.

Ikiwa unaishi na kuona umepungukiwa na kitu wahitaji kutambua kwamba Mungu hunyeshea mvua sehemu iliyo kame kwa wakati na majira sahihi, kwahiyo utulivu ni muhimu zaidi kwani kwa mtazamo huo unafikia utoshelevu wa maisha yako.

Dunia isigulaghai ndugu yangu, hisia zozote ambazo zinakuja ili kujaribu kukuondoa nje ya kuishi yaani uwepo wako unapaswa kujiuliza mbona hivi sasa ni mzima? Kwanini wanilaghai kwamba hapa hapafai? Chochote ambacho kinatokea mbele ya hivi sasa kinahitaji kukuboresha tu. Pale ulipo ndipo pa muhimu sana kuliko baadae yako kwani hakuna atambuaye jibu la baada ya dakika moja.

Tulicho na uhakika sana katika maisha ni pale tulipo na mitazamo tuliyonayo juu ya baadae ndio hutupa uzima hivi sasa. Kwahiyo jali sana uwepo wako, ishi leo, ongoza sehemu yako kwa usahihi.


Hali ya ukiwa na utupu inaweza kukufanya ukafanya maamuzi mazuri, yaani huyo Roho Mtakatifu aliyepo ndani yako kuliko kupelekwa huku na huku bila wewe mwenyewe kujua.

Ukiwa katika hali ya ukiwa na utupu ni kwamba, uamuzi wowote utakaoufanya utakuwa ni mpya kwako, kwani utakuwa sawa sawa na mtu ambaye anacheza draft, anafikiri kabla ya kutenda.

Jitunzie uhalisi wako wewe mwenyewe ili uishi maisha yako wewe mwenyewe.

Mhubiri 6:9 Heri kuona kwa macho, kuliko kutanga-tanga kwa tamaa. Hayo nayo ni ubatiri na kujirisha upepo.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ▼  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ▼  March (14)
      • Jihadhari Sana Na Kitu Hiki.
      • Hata Kama Unayhakika Kiasi Gani.
      • Ukweli Wa Maisha Na Mafanikio
      • Kura Yako Ina Nguvu Kuliko Hata Risasi.
      • Rangi Nne Unazopaswa Kujivisha.
      • Jiweke Nafasi Ya Wengine.
      • Kuwa Na Utulivu
      • Mbegu Lazima Itoe Matunda Yake.
      • Usipokuwa Makini Utakuwa Mtumwa Hata Wa Ukucha Wako
      • Vita Vya Akili
      • Mazingira
      • Huu Ndio Utajiri Ambao Unapaswa Kuutafuta Kwa Bidii.
      • Jinsi Ya Kutumia Falsafa Ya Mfanyabiashara Na Msom...
      • Umuhimu Wa Kuwa Na Ndoto
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates