Kuna mazingira mawili ambayo yanaweza kukusukuma kwa kiasi kikubwa ukajisaidia. Moja ni msukumo unaotoka ndani na mbili ni mazingira ya nje. Kama chakula kilichopo ndani hakitakiwi, kitasukumwa kutolewa nje kwa nguvu kwa haraka. Yuda alipoingiliwa tayari na shetani, Yesu alimwambia uyatendayo yatende upesi. Lakini pia tamaa ya Yuda kutaka kutokea vipande vya fedha ilimvuta zaidi kumsaliti Yesu. Mazingira ya nje, yanamvuto mkubwa sana wa kufanya mtu ajisaidie. Wewe unajua, kuna wakati huwa unaweza kujizuia ukiwa kwenye mazingira ambayo yanabada na uwezekano wa kujisisaidia unapokuwa haupo unaweza kuvumili lakini unapokutana na mazingira ambayo yanaruhusu na akili yako inakubali utakuta unaachilia mwenyewe.
Katika maisha, uliposimama panaweza pakasababisha ukachukua hatua fulani lakini pia ndoto uliyonayo inauwezo mkubwa sana wa kukuvuta na kujikuta unafanya mambo yanayoendana na akili yako. Kama ulipo hapana siafu naam kusogeza miguu na kustuka ni ngumu. Lakini kama ulipo pana siafu taratibu mwenyewe sehemu ambayo haina siafu itakuvuta uindee hiyo.
Ili kuwa na ndoto anza kuangalia mapungufu ya pale ulipo na ona ukamirifu ambao unataka uwe. Ndoto ni muhimu katika maisha yako.
Mungu akubariki katika safari ya maisha.
π΄πΆπ✊
0 comments:
Post a Comment