Lazima Mbegu Itoe Mazao.
Inawezekana una ndoto ambayo umeibeba ndani yako lakini kwa kipindi hichi huoni dalili ambayo inaonyesha kwamba utatimiza ndoto yako, tambua kitu kimoja, usipokata tamaa mbegu lazima itoe matunda yake. Simama imara kuwa na ushujaa mwingi mbele za Mungu, kwani yeye ndiye Mungu wa kila kitu.
Kuna wakati mazingira huwa hayaonyeshi uwepo na kukua kwa ndoto zetu lakini ukweli ni kwamba ikiwa tunatembea katika njia za ndoto zetu bado ndoto zetu zinaendelea kukua zaidi na zaidi. Bila kutegemea kuona muujiza fulani ambo Mungu kaleta mbele yetu bado tunamatumaini ya kuendelea mbele kwa sababu ile mbegu ipo ndani mwetu na inafanya kazi na kuendelea kukua.
Haijarishi mazingira ya nje yanakataa kabisa kuwa uwezekano na dalili zimepotea lakini ndani kabisa Mungu anatimiza kusudi aliloliweka ndani mwetu.
Mwanzo 21:1. BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema.
Hilo neno, akamjia, linaonyesha kwamba mchakato ulikuwa unaendelea pole pole, kumbuka BWANA alimuahidi Sara kwamba anatazaa mtoto.
Mwanzo 18:10 Akamwambia, hakika nitakurudia wakati huuhuu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwako nyuma yake.
Mbegu iliyopandwa ndani ya Sara ilikuwa inakua polepole na mwisho matunda yake yanaonekana nje baada ya Mungu kumfanyia kama alivyokuwa amemwahidi.
Kuwa na matumaini, usipoteze uelekeo wako wakati wa mchakato. Mtumainie Mungu, mbegu yako itatoa matunda, aliyeanzisha lazima atamaliza.
Asante.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment