JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Saturday, March 30, 2019

Jihadhari Sana Na Kitu Hiki.

 Sadick Kilasi     March 30, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Jihadhari Sana Na Kitu Hiki Rafiki Yangu.

Tangu zamani, zama za hapo mwanzo kabisa za kuwepo mwanadamu, mwanadamu alikuwa anasogea mbele kwa sababu ya mahitaji na thamani ya yale mahitaji.

Mwanadamu alikuwa anapata taarifa na hiyo taarifa ndiyo ilikuwa inamwendesha mtu huku na huko ili kujihakikishia anajipatia uhalisi Wa kweli wa ile taarifa. Kilichokuwa kina msukuma zaidi mwanadamu ni thamani ya ile taarifa na thamani ya ile taarifa ilitegemea uadimu wa ile taarifa.

Mpaka leo hii, bado tunaendeshwa na vitu hivi viwili, yaani taarifa na thamani ya ile taarifa. Japokuwa maendeleo ya ulimwengu yamekuwa makubwa zaidi lakini, hivi sasa ndicho kipindi ambacho tunaweza kusema ni ufunuo wa taarifa. Tunapata taarifa nyingi sana tukiwa pekee yetu kuliko hata tukiwa kwenye mahusiano na wengine.

Zamani hizo watu walikuwa wanapokea taarifa kwa kuhisi, wakati mwingine mtu mpaka mnyama mkali anamsogelea ndipo anaisoma taarifa na kuanza kukimbia. Lakini pia link ya kupokea taarifa wakati mwingine ilikuwa ni mtu na mtu, ambayo mchakato wake ulikuwa ni mrefu sana.

Watu wenye taarifa za motomoto walikuwa na thamani kubwa sana. Mtu mwenye taarifa za motomoto alichotegemea ni kutengeneza utajiri katika maisha yake.

Sasa hizi sasa ni zama za ufunuo wa taarifa. Ni kipindi ambacho tunapaswa kuwa makini sana, kwani kila mmoja anakazana kutafuta taarifa na kuuza kwa bei ghali sana. Dunia ya sasa imejaa wanyama wakali ambao hawang'ati lakini wanakufanya kuwa zezeta.

Unaweza kujikuta unaaminishwa vitu ambavyo havipo na kila siku ukawa unakazana kutafuta hiyo taarifa na mwisho ukaifikia lakini uhalisi wake haupo jinsi ambavyo ulikuwa unategemea.  Mfano, michezo ya betting ni taarifa ambazo hazina maana na hazina utu ndani yake. Vitu kama hivi hutucheleweshea kuishi maisha yetu na kushindwa kukamirisha vile vitu vya muhimu zaidi katika maisha yetu.

Betting ni mchezo wa kijinga na kila hatua unayopiga kwenye betting ni ujinga  na ili kuondoa ujinga wa betting ni kuacha kubeti na kuwa kama zamani.

Lakini pia zipo taarifa kutenda miujiza, taarifa hizi nazo ni hatari kwa sababu zinatufanya tunakimbizana huku na huko na kuona kana kwamba labda sehemu tuliyopo si sehemu sahihi. Ni kweli miiujiza ipo lakini si kitu ambacho kinatawala wakati wote, kwa hiyo si taarifa za muhimu kiasi kikubwa hivyo. Kama kwa mamiaka na mamiaka dunia imeishi bila miujiza, kwanini sasa hivi miujiza kiwe kitu cha muhimu sana?

Mpendwa msomaji, chunga sana usije ukajikimbia katika maisha yako. Kuwa tayari kukataa taarifa ya vitu ambavyo huvihitaji, simamimia misingi ambayo wewe mwenyewe unahitaji kuishi nayo.

Usipoteze hata dakika moja kukimbizana na kitu ambacho hakipo katika msingi wa maisha yako. Kama unamsingi katika maisha yako, kitu ambacho kitahitajika utahitaji na si uhitaji kwa sababu kinatuita.

Kama huna kitu cha kufanya angalia katika maisha yako umepungukiwa nini ikisha tafuta njia ya kujenga ulichopungukiwa.

Katika maisha, kwenye chochote kile unachofanya simamia misingi miwili mikubwa,  imani na upendo. Ishi maisha yako, ukweli wa maisha upo na wewe.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, March 25, 2019

Hata Kama Unayhakika Kiasi Gani.

 Sadick Kilasi     March 25, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Hata Kama Unauhakika Kiasi Gani Unapaswa Kuhoji Ukweli Halisi Wa Hilo Unalolifanya.

Kuna mambo mengi sana ambayo huwa tunaamini ni kweli kutokana na viwango ambavyo sisi wenyewe tumejiwekea. Akili zetu ndizo huweka viwango hivi vya ufikiri, na tunazivisha akili zetu vazi hilo na kuamini kwamba ndo usahihi huo.

Fikiri wewe ambaye huwa unaenda ofsini kila siku. Ukifika asubuhi unafanya usafi ofsini kwako mpaka jioni unaondoka kwenda nyumbani lakini akili yetu huzoea mazingira ya kazi, kwa kadili ambavyo mazingira yanachafuka ndivyo unavyojiwekea kiwango cha usafi kuwa ndio hicho. Yaani naweza kusema kwamba mazingira ya nje yanavyochafuka na ndivyo akili zetu huwa zinachafuka na kuendana na mazingira.

Mpaka jioni bado akili huwa zinaamini kwamba usafi wa asubuhi ambao ulifanywa bado upo. Naweza kusema hili ni pumbazo kubwa sana katika maisha.

Asubuhi tukifika ofsini ndipo hugundua kwamba ofisi ilikuwa chafu sana kwa sababu akili zetu zinakuwa zimetakasika usiku na tunaamuka tukiwa na akili mpya.

Sasa ni kitu gani ambacho nataka kukuonyesha hapa, UWE MTU WA KUSTUKASTUKA, na  hapo ndipo utayaona mazingira vizuri la sivyo utakuwa ndani ya pumbazo ambalo huwezi kulikona kwa macho.

Katika maisha huwa tuna viwango ambavyo huwa tunajiwekea, viwango ambavyo si kweli kabisa katika maisha yetu. Kila eneo la maisha lina makosa fulani ambolo tunapaswa kusahihisha kila wakati.

Popote pale ulipo unapswa kuelewa ni kitu gani kinaendelea katika maisha yako ili kuelewa mchakato kamili wa mwenendo wa kile ambacho unakifanya.

Usiwe unajua tu, unapaswa kuelewa pia kile unachojua.

Wakati Adamu na Hawa walipotenda dhambi kiwango ambacho walijiwekea ili kuficha aibu yao mbele za Mungu ilikuwa ni kuvaa majani ya mitini. Sasa hiki ni kiwango kidogo sana cha ufikiri ambacho walifanya na ndipo Mungu mwenyewe akawatengenezea vazi la ngozi.

Kuna wakati katika maisha ya viwango vyako unapaswa kumwambia Mungu akuvishe vazi yeye na si kutegemea akili yako ambayo wakati wote inakuweka kwenye pumbazo fulani.

Mungu pekee asipohusika katika viwango vyako, viwango vyako ni bure, bure kabisa.

Jipatie kitabu cha DUNIA MAMA HAIMTUPI MWANAE kwa 5000, soft copy.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, March 21, 2019

Ukweli Wa Maisha Na Mafanikio

 Sadick Kilasi     March 21, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Ukweli wa Maisha Juu Ya Mafanikio Na Mjini.

Unakumbuka wakati ambao wewe ambaye ulikuwa unatoka kijijini kwenda mjini ni hali gani ambayo ulikuwa unajisikia?

 Namshukuru Mungu kwamba mimi nimepitia kila mahala yaani kijijini huko kabisa, kwahiyo angalau naweza kuielewa asili kwa kiasi.

Sasa hapa simanishi ulipokuwa unatoka kijijini kwenda mjini, ni lazima utoke kijijini kwenda mjini ama kuja Dar es salam, hapana, kila sehemu inamjini mwake. Hata nikiwa pale katikati ya Posta inanihitaji niingie mjini zaidi ama ndani ya majengo mazuri. Lakini pia nikiwa kijijini ambako sisi tunakuita kijijini bado kuna mjini kwake. Kuna nyumba fulani utajikuta unatamani kulala ndani yake, (hivyo ndivyo tulivyokuwa tunapenda tulipokuwa watoto wadogo) unakuta nyumba zote ni za nyasi lakini kuna nyumba nyingine tunafili kulala humo.

Nimekutolea mifano hii ili ujue ni kitu gani nataka kulega. Najua ni kiasi gani huwa unajisikia pale unapotoka kijijini kwenda mjini ama unapobadili mazingira kwenda mazingira mengine ambayo unahisi ni mazuri zaidi.

Lakini mara nyingi ukibadili mazingira na kwenda ambayo ulikuwa unahisi ni mazuri zaidi, ukidumu hapo kwa muda mrefu utajikuta katika hali ya kawaida kabisa, ile hali ya uzuri inaondoka kabisa. Utajikuta unaona kawaida kabisa.

Siku zote huwa nawambia watu, hakuna mafanikio duniani ila kuna kuyaishi mafanikio. Usipoyaishi mafanikio huwezi kufanikiwa kamwe.

Neno Mjini, mimi mwenyewe, kwa kadili ambavyo naelewa, ni hali ya kujisikia, kujisikia utoshelevu wa uzuri fulani.

Ukiwa unapiga hatua, ama kuelekea mahali, hatua moja ya kwanza utajisikia utoshelevu. Mfano, ukiwa unapanda ngazi, mguu mmoja unapokuwa ngazi ya chini, mwingine ngazi ya juu, unaponyanyua mguu wa ngazi ya chini, huu mwingine unapata maumivu. Maumivu haya yakiambatanishwa na uafadhari huwa yanaleta raha fulani, kwa sababu mguu huu wa chini haukai sana kwa muda mrefu na kukufanya wewe usimamie mguu mmoja.
Hii ndio maana, dunia haikuumbwa siku sita pekee, bali iliumbwa siku sita na siku ya saba Mungu akamalizia na kupumzika.

Ukiwa katika ngazi ya kwanza, mguu mmoja, mguu mwingine unakuja kukanyaga ngazi inayofuata, naam, maumivu na raha humohumo. Kila hatua unayopiga unafili, Na hii ndio maana Mungu alisema, zaeni mkaongezeke na kuijaza dunia.

Furahia maisha pale pale ulipo, bila kujali uko wapi na tengeneza kusudi la kusonga mbele. Haijarishi upo kijijini ama Mjini, wewe songa mbele. Unaweza kuwa kijijini lakini saikolojia yako ikasomeka kuwa upo mjini lakini pia unaweza kuwa mjini lakini saikolojia yako ikasomeka kuwa upo kijijini. Lakini pia unaweza kuwa na fedha nyingi lakini saikolojia yako ikasomeka kuwa wewe ni maskini lakini pia unaweza kuwa maskini saikolojia yako ikasomeka kuwa ni tajiri.

Anza kuishi maisha yako, ipe dunia kile ambacho Mungu amefanya uipe dunia. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, March 20, 2019

Kura Yako Ina Nguvu Kuliko Hata Risasi.

 Sadick Kilasi     March 20, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Kura Yako Ina Nguvu Kuliko Risasi.

Ushawahi kujiuliza ni kiasi gani maamuzi yako ni jinsi gani yalivyo na nguvu katika maisha yako?

Kama ulikuwa hujui kila kitu ambacho unakiona ni uumbaji wako wewe mwenyewe uliouchagua.

Ikiwa umetazama na umejiridhisha kwenye kile ambacho umekitazama na kufanyia maamuzi, maamuzi yako ndio maisha yako.

Maamuzi yako yana nguvu kuliko hata risasi. Chochote kile ambacho utakifanyia maamuzi tayari utakuwa umefanya uumbaji.

Chochote kile ambacho utaamua leo basi kaa na utambue kuwa kitabaki kuwa kovu katika maisha yako yote.

Anza kufanya maamuzi kutokana na jinsi ulivyochagua kuishi. Jihakikishie maamuzi bora kabisa kabla hujafanya maamuzi bora kabisa.

Maamuzi yoyote ambayo huwa unafanya huwa yanakuwa na kura ndani yako na baada ya hapo unakaa katika njia ya maamuzi yako.

Usifanye maamuzi mabovu ukitegemea matokeo ya maamuzi hayo yatakuwa mazuri wala usiseme haya ni maamuzi mabovu na madogo, hakuna maamuzi madogo duniani wala hakuna maamuzi makubwa duniani bali uumbaji itakaojitengenezea wewe ndio utakaoamua.

Hatari ya maamuzi yako ni kwamba yanaweza kujenga ama kubomoa. Unaweza ukajengeka kwa maamuzi yako ama unaweza kubomoka kwa maamuzi yako.

Unaweza kuumiza wengine kwa maamuzi yako ama kuwajenga kwa maamuzi yako.

Hata risasi usipoifanyia maamuzi wewe, risasi haiwezi kufanya maamuzi.
Hiyo ndiyo nguvu ya maamuzi. Amua leo na sasa unaamua nini? Mimi, leo, nimeamua, nimeamua kuishi leo, kuishi kama siku yangu ya mwisho kuishi leo.

Unataka kujua ni namna gani nitaishi leo? Nimefanya maamuzi leo, nitaishi leo naam kila leo ni leo daima.



Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Rangi Nne Unazopaswa Kujivisha.

 Sadick Kilasi     March 20, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Rangi Nne Ambazo Kila Mmoja Anapaswa Kujivisha.

Kuna kipindi ambacho niliendesha program ya tabia nne ambazo kila mmoja anapaswa kuwa nazo. Wale waliohudhuria natumai walinufaika na ile program.

Makala hii ya leo inalenga kitu kile kile ambacho tulijifunza kwenye ile program lakini leo tunatumia mfumo wa rangi ili kufikisha ujumbe. Rangi hizi NNE ni Mungu ambaye anataka kila mmoja ajivishe ili kuishi maisha ya furaha na utumishi kwa ujumla.

Kama tulivyosema jana kwamba kila mmoja ambaye amezaliwa upya basi huyo ni kuhani wa Kristo Yesu.

Kuna rangi nne tu ambazo kila mmoja anapaswa kujivisha ili kuishi maisha ya furaha na tano si rangi bali ni mwonekano wa furaha yenyewe. Ukiwa utajivisha rangi hizi basi maisha ya furaha kwako si kitu cha kuuliza.

Kutoka 28:5, Nao wataitwaa dhahabu, na nguo ya rangi ya samawi, na rangi ya zambarau, na rangi nyekundu, nguo ya kitani nzuri.

Kila rangi hapo unapaswa kuwa na tabia fulani ambazo zinawakilisha tabia hiyo. Kwa ufupi ngoja nikuonyeshe hapo chini tabia hizo.


1.Dhahabu.
Rangi ya dhahabu ni rangi ambayo inawakilisha tabia ya sufuri. Huu ni mkao wa ukiwa na utupu. Mara nyingi mkao huu ni mkao wa maombi na kutunza uhalisi. Hali hii ni hali ambayo mtu anakuwa zero. Lakini huu pia ni mkao wa ubatizo.

Kutoka 14:14, BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

Kumbukumbu La Torati 31:2, Akawaambia, Mimi leo ni mwenye miaka mia na ishirini; siwezi tena kutoka na kuingia, na BWANA ameniambia, Hutovuka mto Yordani.

 Matendo ya Mitume 22:1, Enyi wanaume, ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea mbele yenu sasa.

Kwahiyo rangi ya dhahabu inawakilisha kuishi leo na sasa.


2. Samawi/Buluu.
Hii ni rangi ya muhimu sana ambayo kila mmoja anapaswa kujivisha. Rangi hii ni mwondoko kutoka kwenye dhahabu kuja kwenye buluu ama samawi. Mwondoko wa tai ndio hutawala hana, ambapo ni shukrani kwa hali yoyote ile uliyonayo.
Na pia hii huwakilisha Roho wa Mungu. Hapa ndipo Yesu alisema, mtu asipozaliwa kwa Maji  na Roho hawezi kuingia Ufalme wa Mungu.

Yohana 3:5, Yesu akajibu, Amino, amini, nakuambia Mtu asipozaliwa kwa  maji na kwa Roho, hawezi kuingia Ufalme wa Mungu.

Mpendwa msomaji, kwenye rangi hii ni vema nikaelezea zaidi kwa sababu watu wengi tumefeli na ghadhabu ya Mungu ni kwa sababu ya rangi ya samawi. Wengi tumejivisha rangi karibia zote lakini wengi rangi hii tumeshindwa kujivisha. Watu waliokuwa wanajenga mnara wa babeli walikosa rangi hii, lakini pia watu walipomwasi Mungu kule jangwani baada ya Musa kupanda juu ya mlima wa Mungu, wenyewe wakajitengenezea ndama wa dhahabu walikosa rangi hii. Lakini pia ufunuo wa Yohana juu ya mwanamke kahaba alikosa rangi ya buluu.

Rangi hii nayo inatabia zake, ikitanguliwa na shukrani na kuondoa unafiki. Nimeandika kitabu cha UKRISTO NA MAISHA, nimeelezea juu ya injili ya maji na Roho, kwahiyo unaweza kujipatia bure kabisa soft copy yako mapema kabisa. Kwa hiyo pata kitabu hichi kujua zaidi juu ya injili hii.

Katika harati za hivi sasa ni muhimu sana kuishi rangi hii ya buluu, watu wamekuwa bize sana na mambo ya dunia na uwepo wa Mungu umekuwa mdogo sana. Angalieni tusije tukatengenezewa mijeredi na Kristo Yesu tukachapwa mijeredi. Ni wakati wa kulitia jina la Kristo wakati wote.

3. Zambarau.
Hii ni rangi ambayo inawakirisha kiasi na Ufalme. Kila mmoja anapaswa kuishi kutokana upekee kutokana na jinsi Mungu alivyomwandaa bila kuingilia maisha ya wengine. Lakini rangi hii inaongozwa na kutawala pamoja na mwisho wa mipaka yako. Na tabia nyingine huongozwa na rangi hii.

4.Nyekundu.
Rangi nyekundu inawakilisha upendo na ukiweza kuishi tabia hizo nyingine za rangi hizo tatu hapa huhitaji kufanyia kazi. Kila kitu kitakuwa kinajiendesha chenyewe baada ya kuishi tabia za rangi hizo za mwanzo.

5.MWISHO✊. Ni mwonekano wa vazi la furaha ambalo umejivisha la kitani nzuri sana.
Nitaandika kitabu juu ya rangi hizi, na nitakuwa nachambua kila rangi na tabia zake kwa undani sana. Nitakuwa naandika makala ambazo ndizo baadae kitakuwa kitabu, kwahiyo jiandae. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, March 19, 2019

Jiweke Nafasi Ya Wengine.

 Sadick Kilasi     March 19, 2019     No comments   


Kuna wakati ambao huwa tunahisi kukosewa sana na wale watu wa karibu yetu, na hivyo akili zetu haraka kabisa hutufanya tuone wale wengine hawastahili na sisi ndio tubastahili.  Kwa maana hiyo huwa tunawafunga hao watu gerezani, na gereza ambalo huwa tunawafunga ni katika  Ubongo wetu. Baada ya kuwafunga shughuli inayofuata huwa ni ulinzi. Ubongo wetu huwa unang'ang'ania kwamba lazima mfungwa wetu tusimwachilie kirahisi lazima aonekane mwovu na lazima tumchunge ili asitoke kabisa.

Bila kujua kwamba tunajiumiza wenyewe kwa kung'ang'ania kuwaona wengine hawastahili. Haina maana kwamba mtu akikosea asiambiwe lakini kuna njia namna ya kumwambia mtu. Na njia hii itatusaidia sisi tusimtie mtu gerezani.

Njia yenyewe ni; mtu akikukosea mwonye lakini kumbuka na wewe wale uliowakosea, kwa kufanya hivi unajaribu kuona mwingine hastahili na wewe pia hustahili na mwisho mnatengeneza usawa.

Paulo anasema, Wagalatia 6:1-5, Ndugu zangu, mtu akighafirika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho  mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake yeye mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.

Kila mtu aliyepo duniani ni mdhamini wa makosa yake na ndiomaana tunajitaidi kuonyesha kwamba sisi si watenda makosa wakati wote.
Anza kuwa na huruma badala ya kuhukumu.

Kujiweka nafasi ya wengine ni moja ya mlango wa utumishi wa kikuhani, na kila mmoja aliyezaliwa upya huyo ni kuhani wa Kristo.

Ufunuo Wa Yohana 5:10, ukawafanya kuwa ufalme wa makuhani kwa Mungu wetu; nao qanamiliki juu ya nchi.

Mambo Ya Walawi 16:21, Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama uovu wote wa wana wa Israeli, makosa yao, naam, dhambi zao zote; ataziweka juu ya kichwa chake, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.

Kuhani alikuwa anawakilisha jumuiya yote ya wana wa Israeli ili kumtwisha dhambi mbuzi na dhambi za watu zilitakasika kupitia tendo moja la kuhani wao.

Ikiwa tupo tayari kujiweka nafasi ya wengine na kuwaombea wale wanatukusea na kuwapenda zaidi hapo tunaonyesha tendo la ukomavu wa kiroho.

1Petro 2:5, Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

Kuwa tayari kujiweka nafasi ya wengine ili uingie patakatifu pa BWANA. Kujiweka nafasi ya wengine ni moja ya milango ya kuingia patakatifu.

Sasa, anza kujiweka nafasi ya wengine na waombee wanaokukosea, waweke watu hao mbele za Mungu.
Ukiwa tayari leo, kuwaombea hao kwa Mungu, na kuteseka kwaajili yao kwa muda mwingi ukiwaombea, hakika utaona utofauti.

Waefeso 6:18, kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.

Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Kuwa Na Utulivu

 Sadick Kilasi     March 19, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Kuwa Na Utulivu Ili Uelewe Mchakato.

Hapo nyuma nilishawahi kuandika makala juu ya HUKUMU ambayo ni sawa na KANUNI na HAKI ambayo ni sawa TIMAZI. Tukajifunza juu ya namna fundi kujenga anavyo tumia kanuni hii kuunyosha ukuta wake na tukasema kanuni hii ni kanuni ambayo kila mmoja anapaswa kuishi ili kuepukana kuishi kwa kuumizwa na wengine. Na ni kanuni ambayo inamfanya mtu aishi maisha anayotaka.


Sasa leo nitaandika kitu ambacho kinafanana na hicho lakini hiki hakielezeki vizuri kimanti kwa sababu ni hali ya undani sana.

Hakuna kitu ambacho katika maisha yetu ambacho hutokea kama muujiza, ila sisi ndo huwa tunachukulia kama muujiza. Kila kitu huwa na mbegu ambayo mwisho huleta matunda nje ambayo kila mmoja anaona na anatambua. Mara nyingi mbegu ile huwa ni molecular ndogo sana ambayo kwa kawaida huwa ni ngumu kuchambuliwa kwa lugha ya kawaida na ndio maana wataalamu wanasema kwamba hakuna lugha ambayo ilisha wahi kutafsiri kwa usahihi mhemuko ambao tunajisikia. Mfano ; Ukimkuta mtu ambaye ana furaha ya kiwango cha juu anaweza kufurahi mpaka akaanza kulia ama kufanya mambo ambayo mtu huwezi kutegemea.


Utulivu katika maisha ni jambo la muhimu sana, yaani wewe mwenyewe kuwa mtulivu wa kujisikiliza kwa sababu kuna mambo mengine huwa hayawezi kuelezeka ama kufundishika, yanakutegemea wewe mwenyewe.

Mfano; Shetani anapoanza kupanda mbegu mbaya ndani mwako ambayo tunaweza kusema anapoanza kuweka timazi ndani mwako huwa ni ngumu kutambua lakini tunastukia tayari tunaung'ang'ania ubaya ambao shetani kaweka ndani mwetu.

Yesu alifundisha juu ya jambo hilo pale alipoulilia mji wa Yerusalemu na wakati ambao alifundisha juu ya ishara.

Lakini pia imeandikwa kwamba, usemapo ni salama hapo ndipo mabaya huwa yanakuwa nawe karibu sana. Kwa sababu kila mtu lazima ajaribiwe lakini jaribu si la kuendekeza na ndiomaana imeandikwa kwamba tupanie mambo ya juu.

Ukitengeneza utulivu wa hali ya juu sana kila hali ambayo ipo ndani mwako utaisikia inapoanza na hili hawezi kukufundisha mtu ila wewe mwenyewe kuwa na utulivu katika maisha Na kujivisha utayari wa kutaka kujifunza kutoka kwako wewe mwenyewe.

Mara nyingi tumekuwa tunasoma vitabu sana ambavyo vinatuelezea sisi lakini ukweli ni kwamba sisi wenyewe ni kitabu ambacho kinaweza kusomwa na sisi wenyewe. Na uzuri wa sisi wenyewe kujifunza ni kwamba tunakuwa katika hali ile ile.

Ni moja ya mbili yaani 1/2 huwa tunaambulia wakati tunajifunza kupitia yale ambayo tumeyafanya kupitia sisi wenyewe. Kwa hiyo kujifunza na kutafakari sana yale ambayo umefanya ni muhimu sana kuliko hata kusoma kitabu.


Kaa na uanze kujisikiliza ili utengeneze timazi yako wewe binafsi ili uwe wa kipekee. Kila kitu ambacho unakiona nje huwa kinaanzia ndani mwako na ukiwa tayari utasikia kwa sauti kubwa tu.

Tunapaswa kuishi maisha ya furaha lakini tunapoendeshwa na hali linakuwa ni jambo ambalo halina maana kabisa. Sisi tunapaswa kuendesha kila kitu ambacho kinajaribu kuja kwetu.

Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, March 17, 2019

Mbegu Lazima Itoe Matunda Yake.

 Sadick Kilasi     March 17, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Lazima Mbegu Itoe Mazao.

Inawezekana una ndoto ambayo umeibeba ndani yako lakini kwa kipindi hichi huoni dalili ambayo inaonyesha kwamba utatimiza ndoto yako, tambua kitu kimoja, usipokata tamaa mbegu lazima itoe matunda yake. Simama imara kuwa na ushujaa mwingi mbele za Mungu, kwani yeye ndiye Mungu wa kila kitu.


Kuna wakati mazingira huwa hayaonyeshi uwepo na kukua kwa ndoto zetu lakini ukweli ni kwamba ikiwa tunatembea katika njia za ndoto zetu bado ndoto zetu zinaendelea kukua zaidi na zaidi. Bila kutegemea kuona muujiza fulani ambo Mungu kaleta mbele yetu bado tunamatumaini ya kuendelea mbele kwa sababu ile mbegu ipo ndani mwetu na inafanya kazi na kuendelea kukua.

Haijarishi mazingira ya nje yanakataa kabisa kuwa uwezekano na dalili zimepotea lakini ndani kabisa Mungu anatimiza kusudi aliloliweka ndani mwetu.

Mwanzo 21:1. BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema.

Hilo neno, akamjia, linaonyesha kwamba mchakato ulikuwa unaendelea pole pole, kumbuka BWANA alimuahidi Sara kwamba anatazaa mtoto.

Mwanzo 18:10 Akamwambia, hakika nitakurudia wakati huuhuu mwakani, na tazama,  Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni  pa hema iliyokuwako nyuma yake.


Mbegu iliyopandwa ndani ya Sara ilikuwa inakua polepole na mwisho matunda yake yanaonekana nje baada ya Mungu kumfanyia kama alivyokuwa amemwahidi.

Kuwa na matumaini, usipoteze uelekeo wako wakati wa mchakato. Mtumainie Mungu, mbegu yako itatoa matunda, aliyeanzisha lazima atamaliza.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, March 14, 2019

Usipokuwa Makini Utakuwa Mtumwa Hata Wa Ukucha Wako

 Sadick Kilasi     March 14, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Usipokuwa Makini Utakuwa Mtumwa Hata Wa Ukucha Wako.


Tulipata uhuru kutoka kwa wakoloni wakati Babu zetu walipokuwa wanalipigania hili taifa, tumezaliwa na kupokea historia hiyo ambayo inaonyesha kwamba Wazee wetu waliteseka sana wakati huo.

Ijapokuwa inaonyesha kwamba Babu zetu pekee walikuwa watumwa lakini dhana ya Falsafa inaonyesha kwamba hata wale ambao walikuwa wanawatumikisha walikuwa watumwa maana iliwalazimu kujikosa wao na kuwachunga wale ambao wao waliowaona kuwa ni watumwa.

Marko 10:43-44. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu nayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote.


Kwahiyo tulipopata Uhuru  sisi Waafrika hata wakoloni nao walipata uhuru wao, maana muda wote wao walikuwa bize namna ya kutuchunga sisi na sisi tulikuwa bize namna ya kujitoa kwao. Utofauti wetu ulikuwa ni mwonekano wa kimavazi lakini kila kitu tulikuwa sawa.


Fikira za wakoloni zilikuwa zinawaambia kwamba sisi ni watu na fikira za Waafrika zilikuwa zinakubali kwamba wao ni watumwa kwa sababu dhamiri zilikuwa zinayasoma matendo ya mwili lakini dhamiri zenyewe zilikuwa  zinashindwa kujisoma zenyewe. Ili kupata uhuru inapaswa dhamiri fikira ziwe na uwezo wa kusoma dhamiri na dhamiri isome matendo.

Sasa usipokuwa makini katika maisha yako utakuwa mtumwa wa ukucha wako, naam, utaanza kukazana kuufuga ukucha na kukazana kuurinda ili usivunjike. Kuna watu ambao wana kucha ndefu kiasi kwamba hata kushika kitu kwa uhuru linakuwa ni jambo gumu kwani wanarinda ukucha usije ukavunjika. Kuna watu ambao bila kujiangalia kwenye kioo hawezi kutoka ndani, kuna watu ambao bila kunyoa denge hawezi kuona mambo kuwa yataenda sawa, na yapo mengi ambayo wengi tumefungwa kwa hayo na tunaamini kwamba haiwezekani kuishi bila kwa hayo.

Ndugu, usiwe mtumwa kwenye mambo ambayo hayana maana kabisa. Usipoteze hata dakika moja ya kukosa kuishi kwa sababu ya vitu ambavyo wewe mwenyewe umevifuga. Ni bora kujifunga kwa mambo ambayo hukuelewa lakini si jambo ambalo wewe mwenyewe umefuga.

Naam, anza kuishi maisha yako, kuwa makini na maisha yako, usikubali vitu vidogo viendeshe maisha yako na kukufanya kuwa mtumwa bila sababu eti kwa sababu ya ukucha ulioufuga.

Usifanye kosa ambalo alilifanya Yona la kuanza kuthamini Mtango badala ya watu, eti kwa sababu mtango huwa unampa kivuli.
Wewe ni zaidi ya ukucha, wewe ni zaidi ya matendo yako, wewe ni zaidi ya mali ulizonazo na kila kitu ambacho huwa unafikiria ambacho kipo nje ya wewe.

Tunza Uwepo wako na uishi maisha ya furaha wakati wote, tumia fikira zako kiusahihi.

Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, March 12, 2019

Vita Vya Akili

 Sadick Kilasi     March 12, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Vita Vya Akili Na Jinsi Ambavyo Tunapaswa Kuvaa Utayari Unaofaa.


Akili zetu hupitia vita vikali sana, ukizingatia kwa hivi sasa jinsi dunia inavyokwenda kasi na mambo jinsi yanavyokwenda.


Kukua kwa maendeleo ya teknolojia kumetufanya watu tuwe karibu sana kiasi kwamba tumekuwa tunajisahau sisi wenyewe na kuchukuliwa na mafuriko ya internet ambamo ndani yake kuna mikondo mikali sana ya mitandao ya kijamii na google yenyewe kwa ujumla.


Lakini pia hilo linapelekea mashindano ya kimaisha ambayo yanasababisha watu kukosa kuishi maisha yao halisi ambayo Mungu pekee ndie anajua timanzi ya kila mmoja.


Mara nyingi tunapowatazama watu waliofanikiwa mafanikio ya nje akili zetu moja kwa moja zitwambia hayo ndiyo maisha sahihi ya kuishi na si pale tulipo. Kwa kweli maendeleo ya internet yanatuchua bila sisi wenyewe kujua.  Dunia inatulaghai hasa, kweli kweli na huo ndo ukweli wa maisha.

Kila mtu anataka kufanikiwa, mafanikio ya kimwili zaidi, kuwa na gari nzuri, nyumba nzuri, kuvaa vizuri lakini hakuna mtu ambaye yupo tayari kuinamisha mgongo ili awe daraja la mwingine. Kuna pumbazo ambalo akili zetu zimepumbazwa badala ya vitu kutusaidia bali sisi tunekuwa watumwa wa vitu.

Hivi ndivyo vita ya akili, akili zetu zinahitaji utulivu mkubwa sana ili kuepuka kuchukuliwa na hisia za mazingira ambayo tunaishi na kuamini kwamba bila kitu hiki mambo hayawezekani. Akili zetu zinahitaji kukazwa na sisi wenyewe ili kutokusumbuliwa na hisia kama mti unavyosumbuliwa na upepo kupelekwa huku na huku.

Kanuni ya NDANI/NJE ama kwa jina lingine kukusanyika na kutawanyika inapaswa kutumika vizuri sana ili tukae katika mkao wa UFALME na si kupelekwa huku na huko kwa tamaa za dunia hii.

Kuna mkao mmoja ambao Mungu anataka tukae wakati wote naam, mkao huu ni wa UTUPU na UKIWA.

Mathayo 5:3 Heri walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.

Utayari huu ni uwezo wa kuishi Leo bila kujali matatizo ya jana na bila wasi wasi wa kesho. Huu ni uwezo wa kuvuta mafanikio ya baadae na kuishi leo na ndio maana twasema hakuna mafanikio duniani ila kuna kuishi mafanikio.

Ikiwa unaishi na kuona umepungukiwa na kitu wahitaji kutambua kwamba Mungu hunyeshea mvua sehemu iliyo kame kwa wakati na majira sahihi, kwahiyo utulivu ni muhimu zaidi kwani kwa mtazamo huo unafikia utoshelevu wa maisha yako.

Dunia isigulaghai ndugu yangu, hisia zozote ambazo zinakuja ili kujaribu kukuondoa nje ya kuishi yaani uwepo wako unapaswa kujiuliza mbona hivi sasa ni mzima? Kwanini wanilaghai kwamba hapa hapafai? Chochote ambacho kinatokea mbele ya hivi sasa kinahitaji kukuboresha tu. Pale ulipo ndipo pa muhimu sana kuliko baadae yako kwani hakuna atambuaye jibu la baada ya dakika moja.

Tulicho na uhakika sana katika maisha ni pale tulipo na mitazamo tuliyonayo juu ya baadae ndio hutupa uzima hivi sasa. Kwahiyo jali sana uwepo wako, ishi leo, ongoza sehemu yako kwa usahihi.


Hali ya ukiwa na utupu inaweza kukufanya ukafanya maamuzi mazuri, yaani huyo Roho Mtakatifu aliyepo ndani yako kuliko kupelekwa huku na huku bila wewe mwenyewe kujua.

Ukiwa katika hali ya ukiwa na utupu ni kwamba, uamuzi wowote utakaoufanya utakuwa ni mpya kwako, kwani utakuwa sawa sawa na mtu ambaye anacheza draft, anafikiri kabla ya kutenda.

Jitunzie uhalisi wako wewe mwenyewe ili uishi maisha yako wewe mwenyewe.

Mhubiri 6:9 Heri kuona kwa macho, kuliko kutanga-tanga kwa tamaa. Hayo nayo ni ubatiri na kujirisha upepo.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, March 7, 2019

Mazingira

 Sadick Kilasi     March 07, 2019     No comments   


Kuna mazingira mawili ambayo yanaweza kukusukuma kwa kiasi kikubwa ukajisaidia. Moja ni msukumo unaotoka ndani na mbili ni mazingira ya nje. Kama chakula kilichopo ndani hakitakiwi, kitasukumwa kutolewa nje kwa nguvu kwa haraka. Yuda alipoingiliwa tayari na shetani, Yesu alimwambia uyatendayo yatende upesi. Lakini pia tamaa ya Yuda kutaka kutokea vipande vya fedha  ilimvuta zaidi kumsaliti Yesu. Mazingira ya nje, yanamvuto mkubwa sana wa kufanya mtu ajisaidie. Wewe unajua, kuna wakati huwa unaweza kujizuia ukiwa kwenye mazingira ambayo yanabada na uwezekano wa kujisisaidia unapokuwa haupo unaweza kuvumili lakini unapokutana na mazingira ambayo yanaruhusu na akili yako inakubali utakuta unaachilia mwenyewe.

Katika maisha, uliposimama panaweza pakasababisha ukachukua hatua fulani lakini pia ndoto uliyonayo inauwezo mkubwa sana wa kukuvuta na kujikuta unafanya mambo yanayoendana na akili yako. Kama ulipo hapana siafu naam kusogeza miguu na kustuka ni ngumu. Lakini kama ulipo pana siafu taratibu mwenyewe sehemu ambayo haina siafu itakuvuta uindee hiyo.

Ili kuwa na ndoto anza kuangalia mapungufu ya pale ulipo  na ona ukamirifu ambao unataka uwe. Ndoto ni muhimu katika maisha yako.

Mungu akubariki katika safari ya maisha.
🕴🚶🏃✊
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Huu Ndio Utajiri Ambao Unapaswa Kuutafuta Kwa Bidii.

 Sadick Kilasi     March 07, 2019     No comments   


Huu Ndio Utajiri Ambao Unapaswa Kuutafuta Kwa Bidii Sana.

Inasemekana kiswahili kilizaliwa Unguja kikakulia Tanganyika ambako ni Tanzania bara. Kiswahili ni moja ya lugha bora zaidi yenye utajiri mkubwa wa misamiati na lugha bora ya kifalsafa kutokana na jinsi muundo wake ulivyo.

Kilichofanya kiswahili kukulia Tanganyika na si Unguja ni uwepo vitu vingi Tanzania bara na jinsi asili ilivyokaa. Falsafa ni muundo maalumu ambao unaeleweka ambao ukiufuata lazima utapata matokeo unayotaka.


Ukiutazama ufagio ambao unatumika kufanyia usafi utagundua kwamba ni muunganiko wa vijiti vidogo vidogo sana ambavyo kwa pamoja hufanya usafi. Neno la Mungu ambalo asili yake ni maji hututakasa siku baada ya siku baada ya siku. Paulo alisema, Neno la Mungu ambalo hututakasa hivi sasa.

Mwanzo  ufagio ni kajiti kamoja tu, baada ya kuunganika vijiti vingi sana hufanya ufagio na kutumika kufanya usafi. Mitazamo ni dhana ndogo ndogo sana ambao hukufanya ubadilike wakati ukikutana na ukuta mbele yako.


Moja ya utajiri mkubwa sana ambao unapaswa kuutafuta basi ni utajiri wa mitazamo. Huu ni utajiri ambao kila mmoja anapaswa kuwa nao.

Mitazamo ndio inaendesha maisha, mitazamo ni uzima wa mtu. Tunaweza kusema kwamba mitazamo ni umeme unaosafiri kwenye waya wake ambao ni waya huo ni wewe.

Kuumizwa na wengine husabishwa na umaskini wa mitazamo. Kama huna utajiri wa mitazamo bado maisha kwako yatakuwa kama mzigo mzito kwa sababu umeme utafeli kwenda sawasawa na inavyotakiwa.

Tabia ambazo unapaswa kukuza ili kuwa tajiri wa mitazamo.

1. Kwanza kabisa kuweka kusudi la kumjua Mungu zaidi ya ulivyo sasa.

2. Unyenyekevu. Lazima uwe na tabia ya kuwa mnyenyekevu wa kujishusha na kupokea kila kitu kwa shukrani na kujifunza. Unyenyekevu ni siri ya kupokea uwingi wa kuishi.

3. Kuwa tayari kubadilika. Kuna wakati utakutana na mambo tofauti na jinsi ambavyo ulikuwa unaamini lazima uwe tayari kubadilika na kuchukua hatua. Lazima usiwe mtu wa king'ang'anizi kwenye mambo mbalimbali.

4. Punguza tabia ya kuwaridhisha watu. Mara nyingi watu huwa tunataka watu waamini kama sisi tunavyoamini, ukweli ni kwamba ni jambo ambalo haliwezekani kabisa. Lazima uwe tayari kusimamia ukweli unapotokea na si kuwaridhisha watu na kutegemea sana watu.

5. Usomaji wa Vitabu. Hili ni jambo la muhimu sana katika maishi kwa kila mmoja. Kusoma vitabu linapaswa kuwa ni jambo ambalo kila mmoja yupo tayari nalo wakati wote.

Katika hizo tano mbili ni za muhimu. Moja unyenyekevu. Unyenyekevu unaweza kukusababisha ukajifunza mengi sana hata bila kusoma vitabu. Kila kitu ambacho kinapita mbele yako unapaswa kukielewa. Mbili ni usomaji wa vitabu. Haya mawili ni muhimu sana. Yote haya yanaongozwa na utayari wa kutaka kujifunza.

Kuwa tajiri wa mitazamo. Kuwa tayari kujifunza.

Pata soft copy yako kwa shilingi 5000 ya kitabu cha DUNIA MAMA ili kukuza mitazamo yako. Kitabu hichi utasomea kwenye simu yako, kwahiyo litakuwa ni jambo rahisi kuendelea kujifunza na kujipatia oksijeni ya mitazamo. Unaponunua kitabu hichi unakuwa tayari unaisapoti huduma hii kwa ujumla.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, March 5, 2019

Jinsi Ya Kutumia Falsafa Ya Mfanyabiashara Na Msomi Kukwepa Mbinu Za Shetani.

 Sadick Kilasi     March 05, 2019     No comments   


Jinsi Ya Kutumia Falsafa Ya Mfanyabiashara Na Msomi Kukwepa Mbinu Za Shetani.

Biashara ni mchakato ambao unaendelea na Msomi ni mtu ambaye huona vitu ambavyo havionekani kwa macho na kuleta dhana ambayo italeta suruhisho kwenye changamoto ambayo anataka kutatua.

Sasa falsafa ya mfanyabiashara na msomi ni mchakato ambao unaenda kwa pamoja kwa wakati mmoja.


Msomi hutumia jicho la tai na kuona wema ama kitu ambacho anakihitaji kutoka kwenye vitu vingi vya mfanya biashara.

Sasa katika maisha kila kitu ni biashara, yani naweza kusema hata macho yako yanafanya biashara, kwa sababu macho yako usipoyatumia yanakosa soko yaani yanadoda kwa sababu hayana kazi ya kufanya.

Nataka nikuonyeshe mfano huu ili unielewe vizuri, siku moja nilikuwa nimekaa na rafiki yangu kwenye benchi, akipita chinga, anayeuza heleni, chanuo na vikolokolo vingi vya ulembo. Sasa kwa sababu rafiki yangu alihitaji chanuo, akosoma vitu vya mfanya biashara ikisha akaiona chanuo na kuinunua,  akachana nywele zake. Sasa alipochana nywele mimi nikajiuliza swali, kwanini huyu jamaa amechana nywele? Mbona hata angeacha ingekuwa haina shida? Nikapata jibu kwamba, anauza nywele zake. Kama asingechana nywele, kuna watu fulani angeendana nao lakini pia baada ya kuchana nywele kuna watu wa aina fulani angeendana nao.
Inamaana kwa vyovyote vile na kwa mkao wowote ule bado kuna watu wa kuendana nao ambao wanakusoma na wanaona unafaa kuendana nao.  Ndege wafananao huruka kwa pamoja.



Sasa dhana hii ya kuibua kitu kimoja na kuishi na kuamini hicho, mara nyingi shetani hutumia dhana hii kumfanya mtu kuwa mtumwa wa mazingira. Mtu anakuwa anaamini kwamba hakuna zaidi ya hili. Kumbuka kwamba, Mungu alipomwumba mwanadamu aliagiza kwamba, Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akamwambia, Zaeni, mkaongezeke, na kuijaza nchi, na kuitisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kitu kiendacho katika nchi.


Sasa kuna kitu ambacho nataka nikwambie ndugu yangu, hakuna kitu ambacho ni sahihi wakati wote. Ni wewe tu ndiye sahihi wakati wote na Mungu unayemtumainia. Matendo unayofanya si sahihi wakati na ndiomana imeandikwa usitende haki sana.

Werevu ndio sifa kubwa ya shetani. Kuna wakati fulani unaweza ukaona kana kwamba umemweza shetani lakini kumbe kakuweza.

Moja ya jambo la muhimu katika maisha ni kulihimili ombwe kati yako na kile ambacho unatazamia kufanya. Sio kila kitu ni sahihi wakati wote, na  huo ndo ukweli wa maisha. Siku ambapo utasema hiki ndicho sahihi zaidi kuliko vingine utakosa uhuru wa kuishi na utashindwa kutawala vingine kwa sababu unamiliki kimoja.

Mwenyezi Mungu pekee ndiye ndiye wa kumtumainia na si matendo yako. Kuna vitu vya kupigania katika maisha, naam, kupigania kuishi kwa upendo ni jambo la heri. Basi, kuna mambo mawili ya muhimu katika maisha, imani na upendo.

Pata Kitabu cha DUNIA MAMA HAIMTUPI MWANAE kwa shilingi 5000. Lipa kwa 0687000768 au 0755783228. Jina litakuja Sadick. Ikisha nitumie ujumbe WhatsApp ili nikutumie.

Mithali 6:9, Heri anayeona kwa macho, kuliko kutanga tanga kwa tamaa. Hayo nayo ni ubatili mtupu.

Hekima ni taa safi mbele ya uso wa  mwenye hakima.

Sadick Kilasi wa jikolaushari.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, March 3, 2019

Umuhimu Wa Kuwa Na Ndoto

 Sadick Kilasi     March 03, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Umuhimu Wa Kuwa Na Ndoto.

Inasemekana kwamba Areksander Mkuu ndiye mtu mashuhuri kwa makamanda kuwahi kutokea duniani. Mtu huyu historia yake imeandikwa katika kitabu cha nabii Daniel. Areksander Mkuu alipiga vita nchi nyingi sana na kuzishinda. Siraha yake kuu inasemekana alikuwa anatumia hofu kuwashinda maadui zake. Hii ndio siraha yake ambayo ilimfanya ashinde kwa kiasi kikubwa. Alijijengea jina kubwa ili kila mmoja atakaye msikia apate kuogopa. Mtu huyu alikuwa na Mwalimu wake aitwaye Aristoteli, moja ya wanafalsafa wakubwa zaidi duniani. Kumbuka kwamba hawa wana Falsafa wa Ugiriki ndio wameleta mapinduzi makubwa katika Elimu hii ambayo tunatumia mpaka leo kwahiyo wana Elimu kubwa sana. Kwahiyo Mwalimu wake alimfunza mbinu zote za kimafumbo ili kuwa mshindi.

Sasa leo hatuchambui habari za Areksander bali tunatazama umuhimu wa kuwa na ndoto. Habari hii tunatumia kama kielelezo ambacho kitatusaidia kujua kwanini kuwa na ndoto au matazamio.


Kila mmoja anapaswa kuwa na matumaini. Sababu kubwa ambayo mimi nataka kwanini uwe na matumaini kwa sababu matumaini ni siraha kubwa sana dhidi ya maadui zako waliopo mbele.

Ndoto au matumaini ama matazamio ni mjumbe ambaye husafisha njia ya wewe kupitia. Mtu mwenye matumaini lazima anakuwa na afya bora kwa sababu ya mitazamo aliyonayo. Kwa mtu yeyote yule ni muhimu kuwa na matumaini.
Wakati Zakaria, baba yake, Yohana Mbatizaji alipozaliwa kama ishara ya ujio wa Kristo Yesu, alitabiri,  Luka 1:79, Kuwaangaza wakaao katika Giza na uvuli wa mauti, na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.
Wakati mtu anakuwa na matumaini anakuwa na ujasiri wa kuendelea mbele kwani tayari amemtuma mpelelezi ambaye ameandaa njia yake na kumfanya akanyage kwenye njia sahihi.

Wakati wana wa Israeli hawajavuka katika mto wa Yordani tayari mataifa ambayo yalikuwa ng'ambo ya Yordani yalilegea kabisa.

Yoshua 2:9-11.
akawambia wale wanaume, Mimi najua kwamba Bwana amewapa nyinyi nchi hii, na ya kuwa hofu imetuangukia  mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa nchi wameyeyuka mbele yenu. Maana tumesikia jinsi Bwana alivyokausha maji bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliowatendea wawili wa Waamori waliokuwa huko ng'ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa. Na mara tuliposikia hayo mioyo yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wowote katika mtu awaye yote, kwa sababu yenu; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na katika nchi chini.


Ukitamka maneno yenye mwelekeo chanya yanakuwa ni chakula bora mbele ya mwili wako na afya kwa ujumla. Na hata mazingira ya nje litakuwa ni jambo rahisi kuendana nayo kwani fikira zako ni chanya.

Unapokuwa na matumaini ni sawa na kutuma mpelelezi ambaye anakwenda kuwatia hofu maadui zako ambao wanakuzua mbele yako. Kwa sababu ya umbali ulipo na wewe linakuwa ni jambo rahisi kwa maadui zako kuwa na hofu kwa sababu hawajui nini wewe unafikiria.

Kuwa na matumaini ndugu yangu. Mjue Mungu naye Mungu atakuonyesha kusudi la kufanya.

Nimeandika kitabu cha Ukristo Na Maisha, kitabu ambacho ni msingi wa injili na mwanzo wa kumjua Mungu. Kitabu hichi kinapatikana kwa njia ya soft copy na hard copy, lakini kwa sasa kitabu hichi kinapatikana bure kabisa kwa njia ya soft copy, hard copy ni ngumu kipatika kwa urahisi. Unaweza kuchukua hii soft copy na kwenda kufanya hard copy na kutoa nyingi uwezavyo.
Hicho ni bure kabisa.

Lakini pia kuna kitabu ambacho nimekiandika kinaitwa Dunia Mama Haimtupi Mwanae, hiki kinapatikana kwa njia ya soft copy pekee na gharama yake 5000 tu.

Lipia kwa 0687000768 au 0755783228, majina yatakuja Sadick Lazaro Kilasi. Ikisha nitumie ujumbe kwenye namba yangu ya WhatsApp ili nikutumie kitabu. Tafadhari narudia tena hakikisha ukisha lipa nitumie ujumbe WhatsApp ili nikutumie kitabu baada ya kuona namba yako, ukituma pesa pekee namba yako sita iona na itakuwa changamoto.

Asante. Mungu akubariki. Kuwa na matumaini.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ▼  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ▼  March (14)
      • Jihadhari Sana Na Kitu Hiki.
      • Hata Kama Unayhakika Kiasi Gani.
      • Ukweli Wa Maisha Na Mafanikio
      • Kura Yako Ina Nguvu Kuliko Hata Risasi.
      • Rangi Nne Unazopaswa Kujivisha.
      • Jiweke Nafasi Ya Wengine.
      • Kuwa Na Utulivu
      • Mbegu Lazima Itoe Matunda Yake.
      • Usipokuwa Makini Utakuwa Mtumwa Hata Wa Ukucha Wako
      • Vita Vya Akili
      • Mazingira
      • Huu Ndio Utajiri Ambao Unapaswa Kuutafuta Kwa Bidii.
      • Jinsi Ya Kutumia Falsafa Ya Mfanyabiashara Na Msom...
      • Umuhimu Wa Kuwa Na Ndoto
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates