Mfumo wa watoto wa kuelewa mambo ni kukalili. Wanatumia zaidi ubongo uliojificha kuelezea mambo japokuwa wanakuwa hawana mambo mengi sana ambayo wameyaficha nyuma ya ubongo wao.
Japo kuwa wanatumia zaidi akili hii iliyojificha lakini kunawakati wanashangaza kidogo hasa wakiwa wadogo miaka mitatu mpaka sita hivi, wanamaswali magumu sana, sasa hapa ndipo wanajaribu kutumia akili isiyo fikika.
SOMA:Hiki Hapa Ndo Chanzo Kikuu Cha Msongo Wa Mawazo.
Labda Mpendwa msomaji nikufafanulie kidogo juu ya aina za akili kwa mjibu wa wanathiolojia na kwa uchunguzi wangu mwenyewe. Kuna akili za aina tatu, akili ya ubunifu, akili iliyojificha na akili isiyofikika.
Watoto wanapokuwa wanauliza maswali wanakuwa wanatumia akili isiyofikika na unapowapa jibu, wanaweka jibu hilo kwenye akili iliyojificha.
Watoto wanapokuwa wanaliza haya maswali wanakuwa wanachezea akili yao japokuwa wengi tunajua watoto wanapenda kuchea vitu pia.
Watoto wanapenda kujua kila kitu kwa sababu ubongo wao unaruhusu kufanya hivo. Watoto hawatumii zaidi ubongo wa ubunifu kwa sababu bado akili yao iliyojificha haijakusanya mambo mengi ambayo yatafanyika kama mawazo. Akili zetu zinafanya kazi kama mawingu, sasa mawingu ya mbele, yanayotembea tembea ndiyo akili ya ubunifu au mawazo.
Watu wazima wanatumia zaidi akili hii ya ubunifu na akili iliyojificha lakini hawapendi zaidi kutumia akili isiyofikika ambayo ukitumia mara zote unakuwa na furaha.
Kutumia akili isiyofikika ni pale ambapo unakuwa na usawa na ndiomaana unapotumia akili hii unakuwa na furaha. Akili hii inataka wakati wote uwe mjinga yaani uwe tayari kufundishika.
Akili hii itakupa Haki, amani na furaha. Ni vema zaidi watu wazima tutumie akili hii tuwe tayari kufundishika kama watoto na mwisho akili nyingine zitakuwa zinajiendesha zenyewe bila shuruti ya mawazo hasa kwenye akili ya ubunifu na akili iliyojificha.
Ni vema kuchezea akili, kujiuliza maswali kama, kwanini, imekuajekuaje, hapa utakuwa umetambua haki yako ni kutafuta sababu na ukipata sababu utapata amani ni mwisho ni furaha kwa sababu umepata ukweli. Kweli humweka mtu huru.
Chezea akili kama mtoto kwa akili isiyo fikika, usishikilie jambo kwa kuaminishwa na mtu utakosa haki ya kumiliki jambo.
Ukawe na siku bora katika kuchezea akili.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 068700768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment