Ni kweli hawana cha kufanya kwa sababu hawajaona cha kufanya lakini kipo cha kufanya. Watu wengi huwa wanafikiri chochote unachofanya unapaswa kulipwa hela, lakini hiyo si kweli.
Kama huna chochote kile cha kufanya yaani hujasimama kwa chochote tafuta kitu cha kufanya ambacho kitakusimamisha.
SOMA:Kipi Kinakusukuma Kukua?
Biblia inasema wewe ni hai kwa macho ya watu lakini umekufa. Inakwambia tafuta jambo lililo salia, jambo jema, tena inakwambia uwe mwenye kukesha katika hilo jema ulilolichagua kufanya. Ufunuo 3:1-3 kasome ujifunze.
Tafuta kitu ambacho unaweza kusimama nacho kikakupa jina lako wewe ili mladi kiwe msaada kwa wengine.
Sio lazima jambo hilo likupe pesa, hapana, lazima ujijenge wewe mwenyewe kwanza.
Ni vema kutumia falsafa ya mti ili kukua vema.
Ukawe na siku bora rafiki yangu.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment