Sheria ni taratibu ambazo zimewekwa baada ya watu kushindwa kuishi kwa nidhamu yao binabsi.
Sheria inamipaka katika kufanya jambo lolote lile, sheria haina usawa.
Maisha yoyote ambayo hayana usawa ni vigumu sana maisha hayo kuwa na furaha kwa sababu ya mipaka ambayo sheria imeiweka.
Watu wanapenda sana kuwa na kiongozi japokuwa hawapendi kuongozwa. Kuongozwa na mtu ni kuwa chini ya sheria ambayo mara nyingi watu wameshindwa kuishi chini ya sheria.
Watu hawepindi kuongozwa kabisa japokuwa wanapenda kuwa na kiongozi. Watu wanapenda kuwa na kiongozi ili mambo yanapokwenda vibaya wamjue mtu wa kumtupia lawama. Si kwamba watu wanapenda kuwa na kiongozi awaongoze raha sha! Wanapenda kuwa na kiongozi ili atupiwe lawama.
Unapomwambia mtu fulani fanya hivi na hivi ni sawa na kuwa sheria kwake haijarishi jambo unalomwambia ni zuri au la kwake sheria ni tatizo na ndiomaana kuishi na mtu na kumwambia usifanye hiki na hiki huwezi kubadilisha mtu, labda aige kutoka kwako au apate pigo ambalo litakuwa funzo kwake.
Kila mtu anapenda kuwa katika hali kujiachia mwenyewe kuwa huru, haya ndiyo maisha ambayo watu wanataka, kuwa huru kwa kila jambo.
Unapokuwa unahusiana na mtu harafu mwisho kukawa na migogoro wewe ni kama sheria kwake, unapizuia mtu asifanye jambo mtu analotaka kufanya ni sawa na kuwa sheria kwake na wewe ni chanzo cha migogoro.
Usiwawekee watu mipaka. Kocha Makirita anasema, njia nzuri ya kumbadirisha mtu ni wewe kubadilika. Badilika wewe na kisha wao wataona tunda kutoka kwako.
Ukawe na siku bora.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment