Jinsi Ya Kutoka Katika Msongo Wa Mawazo Kwa Kwa Kutumia Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji.
Ninamshukuru Mungu ambaye ameniwezesha kupata wakati mzuri wa kuchunguza mazingira mbalimbali na kuniwezesha kupata dhana mbalimbali ambazo zitanisaidia na kuwasaidia wengine katika kufikia lengo la kila mmoja la kuishi maisha yenye maana na furaha. Ninamshukuru Mungu ambaye anahusika katika kila jambo ili kuhakikisha tunafikia lengo hilo la kuchunguza na kupata maana halisi kwa kutumia misingi ya neno la Mungu na mazingira ambayo tunaishi.
Maisha yetu yamekuwa kama bahati hivi, hisia zetu zimekuwa zinapanda na kushuka, mawazo yamekuwa yanakuja na kuondoka, kitu ambacho kimesababisha sisi kukosa furaha na kushindwa kuwa na matumaini yenye nguvu.
Kwa sabubu tumedhamiria kufanya kitu na tumekusudia kufikia lengo tukijiweka chini ya neema ya Mungu tunategemea tutafikia viwango vikubwa vya kuijua asili na kueletea maana kwenye mawazo na Ubongo wa mwanadamu.
Tuliahidi kwamba mwaka 2019 kwa kadili ambavyo Mungu atajalia utakuwa mwaka wa falsafa, ambayo ambapo ni kuchunguza na kuleta kitu kipya ambacho kinaleta mantiki na kueleweka.
Falsafa ya kilimo na ufugaji, na jinsi ya kutumia mfumo wa kilimo na ufugaji ili kuyaondoa mawazo mabovu ambayo yanakugandamiza na kukuchelewesha kuwa na fikira chana ni falsafa ambayo ni bora zaidi, na namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuelewa hili.
Watu wengi sana wanateswa na fikira ambazo hawazitaki, ni fikira ambazo kwao ni mzigo lakini jinsi ya kutua hizi fikira mgandamizo linakuwa ni jambo gumu kwa kwani kwa kadili ambavyo wanajitaidi kujiachilia kutoka kwenye fikira hizo mgandamizo ndivyo wanajikuta katika hali mbaya zaidi. Na hapo ndipo utawakuta watu hawa wanajiingiza kwenye pombe, wengine wanaumia tu na kuvumilia na kusubili mawazo hayo yaondoke yenyewe. Wengine hali hii ikiendelea wanakata tamaa kabisa na kushuka kabisa kihisia na kukosa hamasa ya kuishi maisha yenye maana na furaha.
Ili kujiondoa katika hili tunapaswa kutumia dhana ya ukulima na ufugaji, na ili kuielewa vizuri unapaswa kuelewa nini maana ya ukulima na nini maana ya ufugaji. Kutokana na sisi wenyewe kutokufanya lolote ardhi yetu yaani Ubongo hujilima na kusababisha miiba kumea na kusababisha sisi kufuga mawazo ambayo sisi wenyewe hatuyahitaji.
Dhana hii ni ngumu kidogo kuifanyia kazi ijapokuwa ni rahisi kuelewa. Ila hakuna jambo ambalo haliwezekani kama ukijiweka chini ya haki ya Mungu, kwani Mungu ni mweza wa kila jambo.
Kwa wale ambao wangependa kujifunza dhana hii ambayo ni highest level thinking, (najisifu mbele za Mungu), hakikisha unakuja inbox, tutajifunza pole pole na kufikia viwango vikubwa zaidi na zaidi kwani hakuna lisiliwezekana chini ya uwepo wa Mungu, na tutatumia neno la Mungu ili iwe rahisi kwa kila mmoja kuelewa na kujifunza zaidi.
Karibu sana, na asante.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment