JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, February 19, 2019

Falsafa Ya Ufungaji Wa Mbuzi Na Uhuru.

 Sadick Kilasi     February 19, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Falsafa Ya Mbuzi Kufungwa Na Jinsi Ambavyo Unaweza Kuishi Maisha Yenye Maana.

Habari Ndugu yangu?
Jana niliandika makala juu ya mitazamo, nikasema kwamba mitazamo ni kama oksijeni ya pili ambayo kila mmoja anapaswa kuwanayo ili maisha yakae katika mstari unaofaa na yawe maisha yenye furaha na raha ikiwa inatawala. Kama hukusoma makala hiyo wapaswa kusoma.

Kuna dhana ya kifalsafa ya mbuzi kufungwa na jinsi ambavyo unaweza kuishi. Katika maisha yetu  wafugaji wengi wamekuwa wanawafunga mbuzi kwa kamba kitu ambacho kinamfanya yule mbuzi kutokuwa na uhuru wa kwenda kule anakokutaka baada ya kuzuuiliwa na mipaka ya kamba.

Katika maisha yetu hata sisi tunatawaliwa na mipaka lakini kwa kila mmoja mmoja tofautitofauti. Wengine kamba zao ni ndefu zaidi na wengine kamba zao ni fupi zaidi. Kama ilivyo kwa mbuzi ndivyo ilivyo hata kwetu, mfungaji wa kamba anapomfunga mbuzi, mbuzi hana mamlaka ya kulalamika, na sisi pia Mungu kamweka kila mmoja aanzie sehemu.

Ili kufurahia maisha inabidi uishi na ufurahie ile sehemu yako uliyopewa bila kujali wengine kamba zao zilivyo. Usije ukaanza kulalamika na kusema, mbona kamba yangu ni fupi na wengine kamba yao ni ndefu kwa hiyo siwezi kufurahia maisha kwa sababu hapa nilipo nimeonewa. Ndugu yangu, furahia maisha sehemu uliyopo, acha kulalamika na kusahau ulikotoka.

Watu wengi huwa tunasahau tulikotoka baada ya kujilinganisha na wengine. Katika hii dunia kila mmoja amekuja kuwasilisha upekee yaani kila mmoja sehemu yake kama hufurahii hatua ya uhuru ambayo Mungu kakupa basi mimi nitakuonyesha ulikotoka na ndipo utatambua hapo ulipo ni sehemu gani na uuone uhuru wako wa kufurahia maisha ulivyo mkubwa.

Wakati hujatungwa kwenye tumbo la Mama ulikuwa na uhuru mdogo sana kwani ulikuwa ni maji maji tu kwa wazazi wako.

Ukashinda kwa kupata uhuru mkubwa zaidi kwa kutungwa kwenye tumbo la Mama yako lakini hukuwa na uhuru wa kula mwenyewe na hukutembea ulivyokuwa unataka.

Ukazaliwa ukapata uhuru mkubwa zaidi lakini hukuwa na uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kubebwa huku na huku bila wewe mwenyewe kupenda.

Ukaanza kutembea na hapa ndipo ulipojipatia uhuru wa kuishi na kufurahia maisha. Ulikuwa una furaha kwenye kila kitu licha ya kwamba wazazi walikubana na kuweka mipaka juu yako lakini wewe hukujali sana ulichojali wewe ni kufurahia maisha tu.

Leo hii umekuwa mtu mzima, kijana mwenye nguvu, unauhuru wa kufanya mengi lakini kwa bahati mbaya umesahau hatua za uhuru wako na umejifunga mwenyewe kwa dhamiri za kwako kwa kujiloga mwenyewe na tamaa zako. Huwezi kufurahia maisha eti kwa sababu wengine wamepata uhuru zaidi yako na ukiwatazama unashindwa kabisa kulala.

Ukishindwa kupokea uhuru wa kwanza kwa shukrani huwezi kupokea uhuru mwingine zaidi.

Ishi rafiki yangu, furahia maisha popote ulipo haijarishi upo sehemu gani na wakati gani. Kama wakati wako wa kufa umefika utakufa tena utakufa ukiwa unaishi na hutakuwa na deni lolote katika maisha haya. Lakini pale  ambapo utakuwa unanung'unika utakufa ukiwa umebeba mizigo kwenye ubongo wako, yanini sasa hii yote, kwani ulikuja umebeba mizigo kwenye ubongo wako?

Hatujaja kukusanya vitu ulimwenguni bali tumekuja kutimiza yaliyotimia tayari ambayo Mungu aliandaa. Kumbuka ulikotoka na ukijali hapo ulipo utaenda mbele zaidi.

Furahia na ufanyie kazi uhuru ulionao na tambua uhuru mkubwa zaidi unaokuja mbeleni. Jifunze kwa uhuru uliopita. Mipaka yako Mungu ndiye kaweka usifisi mambo ambayo hayapo. Kumbuka kila mtu anaongoza sehemu yake.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ▼  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ▼  February (11)
      • Kutekeleza Na Kutafakuri Ulichotekeleza.
      • Jivishe Reflector Yako.
      • Falsafa Ya Ufungaji Wa Mbuzi Na Uhuru.
      • Mitazamo Ni Kama Oksijeni Ambayo Watu Hawaijui.
      • Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji
      • Kila Tendo Ni Kujisaidia
      • Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji 2
      • Link Yako
      • Jinsi Ya Kutoka Katika Msongo Wa Mawazo Kwa Kutumi...
      • Tumia Vizuri.
      • Tano Ambazo Zitakujaza Furaha, Visababishi Vya Fur...
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates