JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Wednesday, February 27, 2019

Kutekeleza Na Kutafakuri Ulichotekeleza.

 Sadick Kilasi     February 27, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Kutekeleza Na Kutafakuri Ulichotekeleza.


Unaweza kujiuliza katika maisha, kwanini huwa tunafanya tunachokifanya? Ili iwaje?

Ukimtazama mtoto namna ambavyo anatekeleza mambo waweza kupata majibu ya mambo mengi sana katika maisha na ukatambua tofauti kati ya mtoto na mtu mzima.

Mtoto huwa anafanya anachotaka kufanya na mtu mzima pia huwa anafanya anachotaka kufanya. Mtoto atashika hiki ataacha na mtu mzima hivo hivo, anashika hichi harafu anaacha. Mtoto na mtu mzima, tunashika na kupeleka hapa na kuacha. Lakini kila kitu ambacho tunakifanya, kipo ndani ya dunia. Wengine wanakusanya na wengine wanatawanya. Sasa ni kipi cha muhimu zaidi katika maisha haya?

Unaweza ukawa unafanya jambo fulani ukajiona wewe ndo upo sahihi kuliko wengine, lakini je, ni kweli? Kwanini? Kwanini Mungu ambaye aliumba mbingu na nchi ameacha mambo mengine yaendelee kuwepo ambayo mimi aka wewe tunayatazama kwa jicho la ubaya?

Kwanini mzazi amwazibu mtoto pale anapohisi yeye kwamba mtoto amekosea? Na kuna uhakika gani kwamba mtoto amekisea na sehemu ambayo wewe mzazi umweka ndio sehemu salama zaidi wakati wewe mwenyewe jibu la dakika moja ijayo hujui kitu gani kitatukia?

Hakika maisha ni siri nzito ambayo Mungu pekee ambaye anaona kotekote anaweza kufasiri zaidi. Lakini mimi huwa naamini kwamba maisha ni kutenda na kutafakuri kile ambacho nimekitenda na kurahia, kama hakinifurahishi naboresha ikisha nafurahia kazi yangu niliyoifanya.

Kwahiyo kuna mambo mawili tu ambayo ndo maisha;
1.Kutenda na
2. Kutafakuri kile ambacho nimekitenda.

Utofauti wa mtoto na mtu mzima ni huu, mtoto anafanya harafu hatafakuri lakini mtu mzima anatenda lakini anatafakuri. Sasa ubaya unakuja hapa, mtu mzima anatafakuri lakini halidhiki lakini mtoto hatafakuri lakini analidhika.

Sasa katika  na kuchua zile tabia za kitoto huwezi kufurahia maisha. Lazima uchukue tabia za kitoto na uzitumie na kuchanganya na tabia za utu uzima na hapo ndipo utafikia kiwango kikubwa cha furaha.

Watu huwa tunafanya kosa hili moja, kupokea na kutokutunza ulichopokea. Naweza kusema, ulevi wa maisha, mtu mlevi ni yule ambaye anatamani ile pombe iliyopo mbele bila kuijali ambayo amekunywa tayari na mwisho pombe inapitiliza tu mwilini. Pombe hiyo haifanyi kazi kama pombe bali mtu huyu ataitwa mraibu wa pombe. Badala ya kuwa pombe unakuwa sasa utapia pombe. Paulo alimwambia Timotheo, tumia sasa kidogo mvinyo kama dawa. Ni muhimu kukitunza kila kitu ambacho kinapitia kwako ili kifanye kazi.

Kuna tabia tano ambazo huwa zinaleta furaha lakini zikiongozwa na mambo hayo mawili. Katika kitabu cha DUNIA MAMA, tumechanganua sana juu ya mambo hayo mawili, hakikisha unajipatia soft Copy yako kwa shilingi 5000 tunaposubiri hardcopy. Tuma pesa yako kwenda 0687000768 au 0755783228, na ni vizuri kunijurisha ili  nami nikutumie haraka.

Kuyaishi maisha unapaswa kuongozwa na mambo hayo mawili, kwa hiyo ni muhimu kuyajua zaidi hayo mambo. Nimekuwa nasoma neno la Mungu na nashukuru Yesu ananifundisha lakini pia nimekuwa natumia mazingira ya kawaida ambayo tunaishi ili kukusanya na kuelewa ni kitu gani kimekosekana watu hatuna furaha lakini nimegundua kuna mambo mawili ambayo yanaongoza maisha lakini pia kuna tabia tano ambazo husababisha furaha. Kwa kadili ambavyo tunakwenda tutashirikishana kwa wakati.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, February 25, 2019

Jivishe Reflector Yako.

 Sadick Kilasi     February 25, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Jivishe Reflector Yako.

Siku moja nikiwa kazini kwenye zangu za ujenzi niliambiwa lazima nivae reflector. Nikawauliza kwanini nivae reflector wakati  reflector yenyewe ni kinguo kilaini sana kiasi kwamba ni rahisi kuadhirika kwa jambo lolote kwa sababu hamna ugumu ambao utazuaia? Nikajibiwa kwamba unavaa ili upate kuonekana na wengine ili kupunguza ajali, kwa sababu hiyo reflector inapopigwa na jua inaakisi mwanga na ni rahisi mtu kuonekana.

Moja kati ya jambo muhimu zaidi ni kujivisha reflector yako yaani kuchagua upekee wako na kujizamisha kwenye upekee huo.
Watu wakivaa nguo za rangi fulani ni rahisi kuwatofautisha hata wakiwa mbali. Ni lazima uwe na upekee wako ambao ndio itakuwa zawadi yako ya pekee.

Moja ya sababu ya mtu kuishi maisha ya furaha ni kuwa na kitu cha kuwapa watu. Niamini mimi ukimpa mtu kitu unajihisi wewe unasababu ya kuendelea kuishi. Sasa watu wengi hatupendi vitu ambavyo tayari tunavyo, bali tunapenda vitu ambavyo hatuna. Na ndio maana imeandikwa, Madhabahu tunayoihudumia vyombo vyake hatuvitumii. Wewe unapaswa kuwapa wao na wewe uwe tayari kupokea kutoka kwako. Ushirikiano unajengwa kwa mapungufu. Mapungufu yanaleta mwingiliano na mwingiliano huleta kujengana.

Ili kuwa na upekee wako zipo tabia ambazo ubapaswa kuwa nazo na moja kati ya tabia hizo ni kukumbuka ni wapi ulikotoka. Mapito yako ya nyuma. Ukikumbuka ulikotoka mapito yako na asili ya wazazi wako lazima utajivisha rangi yako ya upekee. Hii ni moja ya njia ya kuvisha reflector yako ya upekee wako na itakuwa rahisi kuonekana kwa sababu wewe ni wa kipekee. Paulo alimwambia Timotheo, achunge sana Imani ambayo ilikuwa kwa Bibi yake, kwa Mama yake na anaamini kwamba hata kwake ipo. Na akamwonya kwamba asifuate namna ya dunia hii, ajisikilize zaidi ndani mwake.

Huwezi kutoa maji kwenye mafuriko na maji yako yakaeleweka. Huwezi kupiga kelele penye kelele ukasikika. Naam, uelewe mto wako na uuishi mto wako.

Jipatie soft copy ya Dunia Mama kwa shilingi 5000 tu ili ujengeke katika upekee wako.
Tuma malipo kwenye namba yangu 0687000768, nami nitakutumia kitabu. Asante, Mungu akubariki.

Sadick Kilasi wa jikilaushauri.blogspot.com.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, February 19, 2019

Falsafa Ya Ufungaji Wa Mbuzi Na Uhuru.

 Sadick Kilasi     February 19, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Falsafa Ya Mbuzi Kufungwa Na Jinsi Ambavyo Unaweza Kuishi Maisha Yenye Maana.

Habari Ndugu yangu?
Jana niliandika makala juu ya mitazamo, nikasema kwamba mitazamo ni kama oksijeni ya pili ambayo kila mmoja anapaswa kuwanayo ili maisha yakae katika mstari unaofaa na yawe maisha yenye furaha na raha ikiwa inatawala. Kama hukusoma makala hiyo wapaswa kusoma.

Kuna dhana ya kifalsafa ya mbuzi kufungwa na jinsi ambavyo unaweza kuishi. Katika maisha yetu  wafugaji wengi wamekuwa wanawafunga mbuzi kwa kamba kitu ambacho kinamfanya yule mbuzi kutokuwa na uhuru wa kwenda kule anakokutaka baada ya kuzuuiliwa na mipaka ya kamba.

Katika maisha yetu hata sisi tunatawaliwa na mipaka lakini kwa kila mmoja mmoja tofautitofauti. Wengine kamba zao ni ndefu zaidi na wengine kamba zao ni fupi zaidi. Kama ilivyo kwa mbuzi ndivyo ilivyo hata kwetu, mfungaji wa kamba anapomfunga mbuzi, mbuzi hana mamlaka ya kulalamika, na sisi pia Mungu kamweka kila mmoja aanzie sehemu.

Ili kufurahia maisha inabidi uishi na ufurahie ile sehemu yako uliyopewa bila kujali wengine kamba zao zilivyo. Usije ukaanza kulalamika na kusema, mbona kamba yangu ni fupi na wengine kamba yao ni ndefu kwa hiyo siwezi kufurahia maisha kwa sababu hapa nilipo nimeonewa. Ndugu yangu, furahia maisha sehemu uliyopo, acha kulalamika na kusahau ulikotoka.

Watu wengi huwa tunasahau tulikotoka baada ya kujilinganisha na wengine. Katika hii dunia kila mmoja amekuja kuwasilisha upekee yaani kila mmoja sehemu yake kama hufurahii hatua ya uhuru ambayo Mungu kakupa basi mimi nitakuonyesha ulikotoka na ndipo utatambua hapo ulipo ni sehemu gani na uuone uhuru wako wa kufurahia maisha ulivyo mkubwa.

Wakati hujatungwa kwenye tumbo la Mama ulikuwa na uhuru mdogo sana kwani ulikuwa ni maji maji tu kwa wazazi wako.

Ukashinda kwa kupata uhuru mkubwa zaidi kwa kutungwa kwenye tumbo la Mama yako lakini hukuwa na uhuru wa kula mwenyewe na hukutembea ulivyokuwa unataka.

Ukazaliwa ukapata uhuru mkubwa zaidi lakini hukuwa na uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kubebwa huku na huku bila wewe mwenyewe kupenda.

Ukaanza kutembea na hapa ndipo ulipojipatia uhuru wa kuishi na kufurahia maisha. Ulikuwa una furaha kwenye kila kitu licha ya kwamba wazazi walikubana na kuweka mipaka juu yako lakini wewe hukujali sana ulichojali wewe ni kufurahia maisha tu.

Leo hii umekuwa mtu mzima, kijana mwenye nguvu, unauhuru wa kufanya mengi lakini kwa bahati mbaya umesahau hatua za uhuru wako na umejifunga mwenyewe kwa dhamiri za kwako kwa kujiloga mwenyewe na tamaa zako. Huwezi kufurahia maisha eti kwa sababu wengine wamepata uhuru zaidi yako na ukiwatazama unashindwa kabisa kulala.

Ukishindwa kupokea uhuru wa kwanza kwa shukrani huwezi kupokea uhuru mwingine zaidi.

Ishi rafiki yangu, furahia maisha popote ulipo haijarishi upo sehemu gani na wakati gani. Kama wakati wako wa kufa umefika utakufa tena utakufa ukiwa unaishi na hutakuwa na deni lolote katika maisha haya. Lakini pale  ambapo utakuwa unanung'unika utakufa ukiwa umebeba mizigo kwenye ubongo wako, yanini sasa hii yote, kwani ulikuja umebeba mizigo kwenye ubongo wako?

Hatujaja kukusanya vitu ulimwenguni bali tumekuja kutimiza yaliyotimia tayari ambayo Mungu aliandaa. Kumbuka ulikotoka na ukijali hapo ulipo utaenda mbele zaidi.

Furahia na ufanyie kazi uhuru ulionao na tambua uhuru mkubwa zaidi unaokuja mbeleni. Jifunze kwa uhuru uliopita. Mipaka yako Mungu ndiye kaweka usifisi mambo ambayo hayapo. Kumbuka kila mtu anaongoza sehemu yake.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Mitazamo Ni Kama Oksijeni Ambayo Watu Hawaijui.

 Sadick Kilasi     February 19, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Hichi Ndicho Ambacho Dunia Inahitaji Sana Na Kimesahaurika Kwa Watu.


Ukiacha hewa ya oksijeni na ukiacha maji na kujumuisha na chakula kitu cha tatu ambacho dunia inakihitaji kwa kiasi kikubwa basi ni MTAZAMO. Hichi ndicho ambacho dunia inakihitaji sana na ndicho ambacho dunia imekusahau sana.

Nawezs kusema mitazamo ni kama oksijeni kwani ndiyo ambayo inasimamia uhai unaotuzwa kwenye mwili. Kama mtu akishindwa kuendesha mitazamo yake juu ya maisha yake ni sawa na fedha ambayo tayari kutu imengia, pole pole shilingi italiwa na mwisho itaisha kabisa.

Mitazamo ndicho ambacho kilimfanya Adamu ajione uchi na kukubali kutawaliwa na shetani lakini pia mitazamo ndio Yesu alileta ili kwa mitazamo tupate kupona. Anasema, Njoni kwangu nyinyi nyote mtesekao na mizigo, nanyi mtapumzishwa. Jivikeni nira yangu, kwani  NIRA yangu ni laini na nyepesi.

Gharama ya mitazamo ni kujifunza, na gharama ya kujifunza ni kuwa mtu wa kujishusha kwa kukubali kuwa mjinga na kujiuliza kwa kujifunza kwenye vitu vya kijinga kabisa. Gharama ya mitazamo ni kusoma sana, haijarishi wewe ni nani unapaswa kuwa mtu wa kujifunza na kuendana na mabadiliko.

Mitazamo ni oksijeni ya kipekee ambayo dunia haiitambui kwani haionekani kwa macho. Watu tunapenda kuendeshwa na vitu ambavyo vinaonekana na ndio maana Mungu aliifanya oksijeni ijiendeshe automatic la sivyo watu wote  tungeng'ang'ania vitu ambavyo vinaonekana kwa macho.

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Mitazamo inamtaka mtu ambaye yupo tayari kubadilika na si kung'ang'ania kile ambacho unakijua kwani kitakuangamiza.

Jiuleze, unachukua muda gani kusoma, unachukua muda gani kujitafakarisha? Maisha yetu yamekuwa maisha ya mkukumkuku kwa sababu ya mitazamo yaani kwa sababu ya kushindwa kujiendesha badala yake kuendeshwa na mazingira.

Badili fikira zako, chukua hatua ya kusoma hasa neno la Mungu na anza kuwa mtu wa kujitafakarisha.

Magonjwa mengi ya ajabu yanatuvamia kwa sababu ya mitazamo yetu. Tunaruhusu hali fulani na hiyo hali inaruhusu udhaifu na hofu nyingi katika maisha yetu Yaani mtu anaweza akaamka asubuhi akawa anasumbuliwa na ndoto yake ya usiku na ikaharibu kabisa siku yake na siku yake ikawa hovyo kabisa hii yote ni kwa sababu ya mitazamo. Utayari wa kupokea jambo.
Viatu ulivyo vaa vitakupeleka unakokwenda.

Anza kubadili mitazamo kwa kujifunza. Nimekuwa natumia muda mwingi kuandika ili kukuweka katika hali fulani ambayo ni barabara sahihi na si barabara ya mkukumkuku, kwa hiyo lazima utambue kuwa huu ni ulimwengu wa matokeo yaani kila kitu ambacho kinatokea tayari kimetokea katika ulimwengu ambao hauonekani kwa macho kwahiyo unaposhindwa kuelewa vizuri unajiangamiza mwenyewe bila kujua.

Asante na karibu katika magroup yetu ili uendelee kujifunza na kubadili mitazamo yako. Mungu akubariki. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, February 15, 2019

Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji

 Sadick Kilasi     February 15, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Jinsi Ya Kutoka Katika Msongo Wa Mawazo Kwa Kwa Kutumia Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji.

Ninamshukuru Mungu ambaye ameniwezesha kupata wakati mzuri wa kuchunguza mazingira mbalimbali na kuniwezesha kupata dhana mbalimbali ambazo zitanisaidia na kuwasaidia wengine katika kufikia lengo la kila mmoja la kuishi maisha yenye maana na furaha. Ninamshukuru Mungu ambaye anahusika katika kila jambo ili kuhakikisha tunafikia lengo hilo la kuchunguza na kupata maana halisi kwa kutumia misingi ya neno la Mungu na mazingira ambayo tunaishi.

Maisha yetu yamekuwa kama bahati hivi, hisia zetu zimekuwa zinapanda na kushuka, mawazo yamekuwa yanakuja na kuondoka, kitu ambacho kimesababisha sisi kukosa furaha na kushindwa kuwa na matumaini yenye nguvu.
Kwa sabubu tumedhamiria kufanya kitu na tumekusudia kufikia lengo tukijiweka chini ya neema ya Mungu tunategemea tutafikia viwango vikubwa vya kuijua asili na kueletea maana kwenye mawazo na Ubongo wa mwanadamu.

Tuliahidi kwamba mwaka 2019 kwa kadili ambavyo Mungu atajalia utakuwa mwaka wa falsafa, ambayo ambapo ni kuchunguza na kuleta kitu kipya ambacho kinaleta mantiki na kueleweka.

Falsafa ya kilimo na ufugaji, na jinsi ya kutumia mfumo wa kilimo na ufugaji ili kuyaondoa mawazo mabovu ambayo yanakugandamiza na kukuchelewesha kuwa na fikira chana ni falsafa ambayo ni bora zaidi, na namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuelewa hili.

Watu wengi sana wanateswa na fikira ambazo hawazitaki, ni fikira ambazo kwao ni mzigo lakini jinsi ya kutua hizi fikira mgandamizo linakuwa ni jambo gumu kwa kwani kwa kadili ambavyo wanajitaidi kujiachilia kutoka kwenye fikira hizo mgandamizo ndivyo wanajikuta katika hali mbaya zaidi. Na hapo ndipo utawakuta watu hawa wanajiingiza kwenye pombe, wengine wanaumia tu na kuvumilia na kusubili mawazo hayo yaondoke yenyewe. Wengine hali hii ikiendelea wanakata tamaa kabisa na kushuka kabisa kihisia na kukosa hamasa ya kuishi maisha yenye maana na furaha.

Ili kujiondoa katika hili tunapaswa kutumia dhana ya ukulima na ufugaji, na ili kuielewa vizuri unapaswa kuelewa nini maana ya ukulima na nini maana ya ufugaji. Kutokana na sisi wenyewe kutokufanya lolote ardhi yetu yaani Ubongo hujilima na kusababisha miiba kumea na kusababisha sisi kufuga mawazo ambayo sisi wenyewe hatuyahitaji.

Dhana hii ni ngumu kidogo kuifanyia kazi ijapokuwa ni rahisi kuelewa. Ila hakuna jambo ambalo haliwezekani kama ukijiweka chini ya haki ya Mungu, kwani Mungu ni mweza wa kila jambo.

Kwa wale ambao wangependa kujifunza dhana hii ambayo ni highest level thinking, (najisifu mbele za Mungu), hakikisha unakuja inbox, tutajifunza pole pole na kufikia viwango vikubwa zaidi na zaidi kwani hakuna lisiliwezekana chini ya uwepo wa Mungu, na tutatumia neno la Mungu  ili iwe rahisi kwa kila mmoja kuelewa na kujifunza zaidi.

Karibu sana, na asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Kila Tendo Ni Kujisaidia

 Sadick Kilasi     February 15, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Ili Kuwa Mzima.
Kila tendo ambalo unalifanya kwa siku ni kujisaidia. Chochote ambacho umekifanya siku hii ya leo umejisaidia sasa lazima utambue kuwa kila taka mwili ambayo inatoka ndani ya mtu huwa inabeba nguvu fulani. Zamani wakati nachunga kila nikijisaidia polini nilikuwa naangalia kile nilichojisaidia, natafakuri. Sasa nikiona kwamba nilichojisaidia hakina tatizo nafurahi lakini nikiona kuna tatizo furaha inanitoka. Mpendwa, jifunze kuitafakuri siku kupitia yale uliyojisaidia siku nzima. Hapo utakuwa unaipa thamani siku na siku inayofuata utajirisha vitu vizuri ili ujisaidie vitu vizuri. Na hii ni moja ya zile kanuni tano za kuishi maisha ya furaha.
πŸ•΄πŸšΆπŸƒ✊
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, February 14, 2019

Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji 2

 Sadick Kilasi     February 14, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji, Mkulima Lazima Auharibu Ufugaji Ambao Hauna Uzalishaji.

Karibu tena katika mwendelezo wa uchunguzi wetu wa Falsafa ya kilimo na Ufugaji. Katika mwendelezo huu wa kutumia Falsafa hii wengi tutatoka katika vifungo fulani vya mazoea endapo tu tutachukua hatua.

Ukichunguza katika historia utagundua kwamba Ufugaji ulianza kabla ya kilimo. Ufugaji ni ile hali ya kufanya kitu Na kinakuwepo tayari. Kuna Ufugaji ambao hauna tija kabisa ambao mara husababisha majanga katika ardhi kwa sababu unakuwa hauna maana na hauleti mabadiliko yoyote. Sasa ili Ufugaji uwe  na tija lazima mkulima ahusike hapo. (Kidogo hapo huwezi kunielewa lakini utanielewa huko mbele kwanini ili mfugaji awe na ufugaji wenye tija lazima mkulima ahusike).

Wakati namhoji fundi kushona nguo, alinambia kwamba yeye lazima aharibu kitambaa ambacho kimefugwa ili kutengeneza nguo mpya. Yeye ananunua kitambaa ambacho kipo tu na kimefugwa, sasa ili atengeneze nguo ambayo anataka lazima aharibu na kukatakata kile kitambaa. Wakati huo kwenye kilimo lazima uiharibu ardhi ambayo na haina kazi, inawezekana ilikuwa ni msitu mnene lazima ukatekate miti na kuugeuza udongo ambao upo ugeukie chini na ardhi iwe katika hali ya ukiwa na utupu ndipo iruhusu mazao mapya kumeya. Na hapa ndipo tunakutana na Falsafa ya finger thinking✊.  Kila kitu ambacho kipo nje kipo ndani ya ubongo na mwili wako.

Katika maisha inawezekana kuna kitu kinakutesa kwa muda mrefu, katika maisha inawezekana Ubongo wako umejifunga katika hali fulani, inawezekana upo katika uraibu wa hali fulani, zana pekee ambayo utaitumia ni ukulima na kuanza ufugaji mpya ambao wewe mwenyewe unakuwa unajipangia si kama ufugaji ule wa kimasai ambao wewe unafuga mang'ombe mengi kiasi kwamba hujui kwanini unafuga na unafuga kwa sababu wewe ni mfugaji.

Kilimo ndicho kilicholeta  kutafakari japo ufugaji ndio ulikuwa wa kwanza kuwepo, kilimo ndicho kilicho ruhusu ufikiri wa kimaendeleo, kwani usipokuwa mhuharibifu huwezi kufanya jambo lolote jipya. Wakati Yesu alipopokea Roho mtakatifu ilibidi apelekwe jangwani na huko jangwani tunajua jinsi hali ya jangwani ilivyo, huko ndiko tunajitambua tukuwa tunapitia majaribu mazito mazito. Katika maisha ili uwe na ufikiri wenye maana lazima uende kwanza jangwani yaani hali ya ukiwa na utupu. Tengeneza hali ya ukiwa na utupu ndani ya ubongo wako, wakati unatengeneza hali hii ndipo unamruhusu Mungu kupitisha ujumbe kwenye fikira zako. Wengi tumeweka tamaa za vitu ambavyo tunavihitaji na ndio maana hatuwezi kuzifanya fikira zetu kuwa pevu. Katika maisha watu wengi tunashindwa kujivisha ile hali ya ukiwa na utupu kwani hali hii ndio inaruhusu zao jipya kumea na ndilo zao ambalo Mungu anakuwa amepanda kwani kila mzao wa kwanza ni wakifu kwa Mungu lakini kutokana na tamaa zetu tunajikuta tunapandikiza vitu ambavyo havina maana yaani sanamu na huku ndiko kuabudu miungu mingine.

Hatuwezi kujivisha rangi ya samawi yaani buluu kama upepo wa dunia hii utatuendesha. Mara nyingi sana tunatolewa katika upekee kwa sababu ya kutokulinda uwepo wetu na tunachukuliwa na kawaida ya dunia hii, kwahiyo jifunze kutunza uwepo wako na uhalisi wako.

Kwa leo tuishie hapa. Asante na Mungu akubariki.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, February 13, 2019

Link Yako

 Sadick Kilasi     February 13, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Ili Kuwa Mzima.
Tatizo si kuwahimili wengine, tatizo ni kujihimili mwenyewe. Tatizo si kuwasamehe wengine tatizo ni kujisamehe mwenyewe. Tatizo si kuwapenda wengine tatizo ni kujipenda mwenyewe. Unajifanyia nini wewe mwenyewe? Kichwa chako kipo tayari kujaza nini? Unajua nini? Kama mtu akija kubonyeza kompyuta yako, zile link zinazokuja ili zikuingize ndani zaidi zinategemea wewe namna ambavyo huwa unaingiza ndani yake. Usishangazwe kuumizwa na wengine kwani hiyo ni link ambayo wewe mwenyewe uliiandaa.
Chunguza mwelekeo wa fikira zako wakati wote.
πŸ•΄πŸšΆπŸƒ✊
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, February 12, 2019

Jinsi Ya Kutoka Katika Msongo Wa Mawazo Kwa Kutumia Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji.

 Sadick Kilasi     February 12, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Jinsi Ya Kutoka Katika Msongo Wa Mawazo Kwa Kwa Kutumia Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji.

Ninamshukuru Mungu ambaye ameniwezesha kupata wakati mzuri wa kuchunguza mazingira mbalimbali na kuniwezesha kupata dhana mbalimbali ambazo zitanisaidia na kuwasaidia wengine katika kufikia lengo la kila mmoja la kuishi maisha yenye maana na furaha. Ninamshukuru Mungu ambaye anahusika katika kila jambo ili kuhakikisha tunafikia lengo hilo la kuchunguza na kupata maana halisi kwa kutumia misingi ya neno la Mungu na mazingira ambayo tunaishi.

Maisha yetu yamekuwa kama bahati hivi, hisia zetu zimekuwa zinapanda na kushuka, mawazo yamekuwa yanakuja na kuondoka, kitu ambacho kimesababisha sisi kukosa furaha na kushindwa kuwa na matumaini yenye nguvu.
Kwa sabubu tumedhamiria kufanya kitu na tumekusudia kufikia lengo tukijiweka chini ya neema ya Mungu tunategemea tutafikia viwango vikubwa vya kuijua asili na kueletea maana kwenye mawazo na Ubongo wa mwanadamu.

Tuliahidi kwamba mwaka 2019 kwa kadili ambavyo Mungu atajalia utakuwa mwaka wa falsafa, ambayo ambapo ni kuchunguza na kuleta kitu kipya ambacho kinaleta mantiki na kueleweka.

Falsafa ya kilimo na ufugaji, na jinsi ya kutumia mfumo wa kilimo na ufugaji ili kuyaondoa mawazo mabovu ambayo yanakugandamiza na kukuchelewesha kuwa na fikira chana ni falsafa ambayo ni bora zaidi, na namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuelewa hili.

Watu wengi sana wanateswa na fikira ambazo hawazitaki, ni fikira ambazo kwao ni mzigo lakini jinsi ya kutua hizi fikira mgandamizo linakuwa ni jambo gumu kwa kwani kwa kadili ambavyo wanajitaidi kujiachilia kutoka kwenye fikira hizo mgandamizo ndivyo wanajikuta katika hali mbaya zaidi. Na hapo ndipo utawakuta watu hawa wanajiingiza kwenye pombe, wengine wanaumia tu na kuvumilia na kusubili mawazo hayo yaondoke yenyewe. Wengine hali hii ikiendelea wanakata tamaa kabisa na kushuka kabisa kihisia na kukosa hamasa ya kuishi maisha yenye maana na furaha.

Ili kujiondoa katika hili tunapaswa kutumia dhana ya ukulima na ufugaji, na ili kuielewa vizuri unapaswa kuelewa nini maana ya ukulima na nini maana ya ufugaji. Kutokana na sisi wenyewe kutokufanya lolote ardhi yetu yaani Ubongo hujilima na kusababisha miiba kumea na kusababisha sisi kufuga mawazo ambayo sisi wenyewe hatuyahitaji.

Dhana hii ni ngumu kidogo kuifanyia kazi ijapokuwa ni rahisi kuelewa. Ila hakuna jambo ambalo haliwezekani kama ukijiweka chini ya haki ya Mungu, kwani Mungu ni mweza wa kila jambo.

Kwa wale ambao wangependa kujifunza dhana hii ambayo ni highest level thinking, (najisifu mbele za Mungu), hakikisha unakuja inbox, tutajifunza pole pole na kufikia viwango vikubwa zaidi na zaidi kwani hakuna lisiliwezekana chini ya uwepo wa Mungu, na tutatumia neno la Mungu  ili iwe rahisi kwa kila mmoja kuelewa na kujifunza zaidi.

Karibu sana, na asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, February 9, 2019

Tumia Vizuri.

 Sadick Kilasi     February 09, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Ili Kuwa Mzima.
Wakati mmoja tulikuwa tunajifunza somo la ubunifu. Ikawa imeingia maada ya neti, jinsi ambavyo tunapokea misaada ya neti na jinsi watanzania wavyotumia neti hizo. Lengo la watoa misaada ni kujikinga na ugonjwa wa maleria lakini ikaonekana kwamba wabunifu wanaweza kutumia neti kuvua samaki na wengine uswahilini huku tunatumia kama madodoki. Lengo la watoa misaada halitimii kwa sababu ya matumizi ovyo ya wapokea misaada japo nao ni ubunifu.

Mpendwa, ninachotaka kukuonyesha hapa ni nini? Kumekuwa na watu ambao wanawatumia hovyo watu kutimiza tamaa zao. Kumekuwa na watu ambao wanatumia neno la Mungu hovyo ili kutimiza tamaa zao. Hatuutafuti ukweli ila tunatumia kama tunavyotaka sisi. Wewe uliyepewa hicho ulichopewa tumia vizuri kuwajenga wengine. Usiwe na tamaa, timiza kile ulichotumwa. Tunatumia vitu, tunawatumikia watu. Hatujaja ulimwenguni kukusanya vitu bali tumekuja kutimiza kwa kila mmoja sehemu yake. Usiwe na tamaa, tambua kusudi la kila kitu.
πŸ•΄πŸšΆπŸƒ✊
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, February 3, 2019

Tano Ambazo Zitakujaza Furaha, Visababishi Vya Furaha.

 Sadick Kilasi     February 03, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Ijapokuwa mti una mengi chini yake lakini maua ndio kila kitu. Maua huja huupendezesha mti nankufuta ubaya sura ya mti kama ilivyo furaha. Tunafanya mengi lakini ili tuishi na kuleta matokeo tunapaswa kuwa na furaha kwani ndani ya ua ndipo tunda hujitokeza kwahiyo furaha huzarisha matunda makamirifu na bora zaidi.Binafsi wakati nachunguza hili kupitia falsafa ya kula chakula, nimekutana na hatua tano ambazo zinampa mtu furaha. 1. Harufu, hii ni kama habari njema, 2. Mchakato ama utamu, ambao humu umezungumzia kama kipooza maumivu, kwa mfano mtu anapokula pilipili licha ya kuwa ni kali lakini bado anakula. 3. Tatu ni kushiba, hii inamfanya mtu kulidhika na kuwa katika hali ya usawa ndani ya tumbo lake. 4. Kupunguza ama kufanya excretion, hii hufanyika pale ambapo mtu anajaribu kuondoa makosa kwenye kile ambacho ameshiba na 5. Ni kutafakuri kile ambacho tayari umekifanya. Mfano kama umemsaidia mtu hii inakufanya kujisikia furaha pia.
Hizi ni tano ambazo nimejaribu kuchunguza kwa kutumia falsafa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Usisahau kujiweka chini ya haki ya Mungu.
πŸ•΄πŸšΆπŸƒ✊
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ▼  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ▼  February (11)
      • Kutekeleza Na Kutafakuri Ulichotekeleza.
      • Jivishe Reflector Yako.
      • Falsafa Ya Ufungaji Wa Mbuzi Na Uhuru.
      • Mitazamo Ni Kama Oksijeni Ambayo Watu Hawaijui.
      • Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji
      • Kila Tendo Ni Kujisaidia
      • Falsafa Ya Kilimo Na Ufugaji 2
      • Link Yako
      • Jinsi Ya Kutoka Katika Msongo Wa Mawazo Kwa Kutumi...
      • Tumia Vizuri.
      • Tano Ambazo Zitakujaza Furaha, Visababishi Vya Fur...
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates