Maneno matatu ambayo yanapaawa kudumu katika maisha yako ni;
Haki
Huruma na
Imani.
Yesu alileta amri kuu ambayo ni ya upendo, upendo ndio haki na huruma. Haki na huruma vikifanya kazi kwa pamoja huzaa upendo. Mpendwa msomaji, kuwasaidia maskini, kuishi kwa kuamua kwa haki, kujali wengine, kuwaonea huruma waliofungwa na mengine yote yanayohusu upendo ndiyo yanayofaa.
Jifunze kutoka;
Mathayo 23:23
Walawi 1:9
Yohana 3:1-21.
Mungu anahitaji vitu viwili kwa watoto wake upendo na imani. Upendo ni kufanya matendo yanayofaa baada ya kukombolewa na Kristo. Maana ukimwamini Kristo utapata hekima ya Mungu nayo ndiyo itakufanya kuamua kwa haki.
Iamini injili ya maji na Roho, hili ndilo neno la Kristo kwetu na kwa ukamirifu huu ndio utapokea haki ya Mungu.
Watu wengi bado wanaudini, hupeleka sadaka nyingi kanisani, huimba kwaya kwa bidii, hijitaidi kwa matendo yao wakifikiri Mungu huangalia matendo, Mungu anataka uangalie neno lake linasema nini. Si kwa kutoa sadaka sana ndipo utaokolewa hapana, si kwa kuomba sana ndiko kutakupa wokovu, hapana, bali ni upendo na imani.
Na ili uelewe namna ambavyo upendo na imani vinavyofanya kazi naomba utafakari maneno haya mawili; Kati ya kusikia na kusikiliza ni kipi kinaanza na ni kipi cha muhimu zaidi. Kati ya kusikia na kusikiliza.
Kitabu tayari kwaajiri yako, ambacho nimekiandika nikigusia zaidi kuishi na ibada ya kweli. Kitabu hiki kinaitwa UKRISTO NA MAISHA, jipatie kitabu hichi haraka iwezekanavyo.
Nimeigusia kwa undani injili ya maji na Roho ambayo ndiyo hutupa wokovu mpaka leo.
Tuwasiliane ili ujipatie kitabu hiki ni bure kabisa. Kila mmoja anahitaji kufurahia maisha sasa kwenye kitabu hiki nimeonyesha funguo za ufalme wa Mungu. Karibu sana rafiki yangu ujipatie kitabu hiki bure kabisa, tumepewa injili bure na tutoe bure. Nitafurahi kama ukiifahamu injili ya maji na Roho kwa undani, asante sana.
Wewe ni zawadi yangu, daima tupo wote.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni sadikila65@gmail.com au 0687000768.
0 comments:
Post a Comment