Nimekuwa nafanya mambo mengi sana kabla ya kwenda kulala, nafanya haya na yale.
Nimekuwa nawashuhudia watu kuhusu Injili ya Maji na Roho lakini watu wengine hupokea na kujifunza na wengi hawajali kabisa. Huwa nafikiria kwamba wakipuuza, inamaana watu hawapendi maisha ya furaha. Haya ni mawazo yangu na mtazamo wangu.
Mungu waajabu sana katika kutimiza jambo lake, yeye anasema maono yake huwa yanawakati wa kufaa, kama yanaonekana kuchelewa usubiri hayata kawia.
Mimi hufikiri napaswa kufanya jambo na lilete matokeo hapo hapo lakini kumbe Mungu anawakati wa kufaa kutimiza jambo. Wakati mwingine yeye huwa tayari ameshatimiza lakini kwa sababu sisi binadamu hupenda muujiza yaani ahaaaaa, tayari.
Yesu alifundisha juu ya Ufalme wa mbinguni kwamba ni kama mbegu iliyopadwa, mpanzi hawezi kujua lolote lakini mbegu huendelea kuota na udongo ndio unajua, wewe huwezi kujua lakini wakati ukifika wa mavuno unavuna.
Jifunze kutoka,
Marko 4:26-29.
Ni vema kuendelea kufanya linalofaa kufanywa na majibu tumwachie yeye, kwa sababu yeye huona kila kitu tunachofanya.
Mungu anakuona unachofanya jinyenyekeze kwake kwa kuukubali upendo wake.
Itambue Injili ya Maji na Roho, kuishi maisha ya furaha.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment