Yesu alisema, mtu asipozaliwa katika maji na damu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu. Leo hii kumekuwa na injili tofauti tofauti ambazo huhubiriwa lakini injili ya kweli ambayo ndiyo kweli yenyewe imeshindwa kuhubiriwa.
Watu wengi bado hawajaponywa na kusafishwa dhambi zao. Neno ambalo ni kweli bado halijahubiriwa bado kwao. Wengi hawaimbui kabisa injili ambayo ndiyo kweli yenyewe. Inapaswa kila mmoja kumpokea Roho Mtakatifu aweke makazi ndani yako. Bila hivi huwezi kuokolewa na bila kweli ya injili ya maji na damu kuifahamu huwezi kuokoka. Mtu yeyote ambaye anamwamini Mungu, anapaswa kumwamini Yesu ni Kristo na yeyote atakaye mwamini Yesu huyo ataokoka lakini si kumwamini Yesu ni Kristo pekee ndipo utakapo okoka, hapana, lazima uamini kwamba yeye alikuja katika maji na damu na Roho ndiye huwa anashuhudia kwamba mtu huyu sasa hana dhambi moyoni mwake. Roho Mtakatifu huweka makao kwa mtu ambaye hana dhambi kabisa. Roho Mtakatifu haweki makao mahala ambapo pana dhambi.
Swali, umeokoka katika injili hii?
Kama bado hijaokoka unapaswa kuokoka kupitia injili hii ambayo Yesu mwenyewe alimhubiria Nikodema aliyemwendea usiku.
Jifunze kutoka, Yohana mlango wa 3.
Unapaswa kuiamini injili hii sasa ili upate kuokolewa. Jinyenyekeze mbele za Mungu kwa mapenzi yake atakuokoa.
Wasiliana nami kwa swali lolote ili tuhabarishane mengi zaidi. Liamini Neno la Mungu. Pia kujifunza zaidi karibu kwenye group letu ambako huko unaweza kuuliza swali na kujibiwa kiurahisi. Pia unaweza kiniuliza private.
Natani nawe uipokee hii neema ambayo ni ya bure kabisa. Mungu kaupenda Ulimwengu tayari, wewe kubari upendo wake kwa kuikiri injili hii njema.
Furaha yangu mimi ni wewe kifurahia maisha, karibu sana.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment