Ukweli ni kwamba, kila kitu ambacho huwa tunafanya huwa tunafanya kwaajili yetu. Kinachokifanya nafanya kwa sababu yangu mimi binafsi na hata na wewe kila unachofanya unafanya kwa sababu yako wewe binafsi. Licha ya kwamba tunaweza tukaona kwamba tunawafanyia wengine lakini bado kile ambacho tunafanya huwa kinarudi kwetu na kutuadhiri kwa namna tofauti na jinsi ambavyo tulikuwa mwanzo.
Kuna mambo mengi sana ambayo tumekuwa tunafanya katika maisha. Moja ya mambo hayo ni yale ambayo tumekuwa tunafanya na kuona tunafanya ili kujijijenga wenyewe ili afya zetu ziwe bora. Katika zama hizi mambo haya yamekuwa yakihamasishwa sana ili kuhahakikisha kwamba afya zetu zinakuwa bora.
Kufanya mazoezi, kula chakula bora, kupumzika, kuwa katika hali ya usafi ni mambo ambayo tumekuwa tunayapa kipaumbele sana katika maisha yetu lakini kuna jambo muhimu sana ambalo tumekuwa tunalisahau.
Jambo hilo ni HALI MHEMUKO au MAWIMBI YETU. Hili ni jambo ambalo limesahaulika kabisa katika maisha yetu japokuwa hili ndilo lilipaswa kuwa kipaumbele kwa sababu hili linayaendesha yote. Mawimbi yetu ni hali ambayo ipo ndani mwetu ndiyo huwa inatunza uzima wetu. Hali hii hutokana na jinsi ambavyo unatafsi mambo ambayo unakutana nayo kwa jinsi mitazamo yako ilivyo. Mtazamo ni muhimu sana katika maisha ili tuwe na uzima. Lakini pia namna ambavyo tunawachukulia wengine bado tinajiweka katika hatari ya kuwa na uzima ama kupoteza uzima, jinsi ambavyo unachukulia chakula, jinsi ambavyo unachukulia maisha unayoishi yaani mazingira yako pia husababisha uzima. Unaweza kujiuliza kwanini Yesu alitembea juu ya maji? Lakini yote hii ni ndani ya hali mtazamo na namna ambavyo unachukulia hatari zinazokuzunguka zinaweza kukupa uzima. Unaweza kujiuliza kwanini Mama yule alishika pindo ya Yesu mpaka Yesu akahisi nguvu zake zimemtoka, yote hii ni hali mtazamo.
Kumbuka kitu kimoja neno la Mungu ndilo uzima kwa hiyo neno la Mungu linakuja kutubadilisha mitazamo yetu endapo tu tutakuwa hatusomi kishabiki na tunamruhusu Roho Mtakatifu atufunze mwenyewe. Kumbuka hapo mwanzo tumesema kwamba kila kitu tunachofanya tunajifanyia wenyewe, kwa hiyo hata neno unaposoma unasoma kwaajili yako mwenyewe harafu excretion ikisha fanyika yale mabaki ndio unawapa wengine nao wafaidike.
Uzima ni kitu cha muhimu sana katika maisha, na ndilo jambo limetufanya tupitie hapa duniani. Na lengo la neno la Mungu ni sisi tupate uzima, Kumbuka katika kitabu cha mithali imeandikwa, linda sana moyo wako maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima.
Hili jambo ni la muhimu sana katika maisha yetu ili kuwa wazima. Na ili kuwa mzima lazima uwe tayari kutii neno na kulichambua kisawasawa bila ushabiki ndani yake wa kusoma ili kuonekana kwa wengine ama kusoma bila kulitii, na kuwa tayari kubadilika. imeandikwa katika Isaya, ibada ya kweli ambayo Mungu anataka ni mtu ambaye akisikia neno lake roho yake inapondeka na kitetemeka maana vitu vyote ndivyo Mungu kaumba.
Katika kitabu cha Dunia Mama nimelichambua hili kwa uzuri, ni kitabu ambacho kitabadili mtazamo wako kwa hiyo usipange kukosa.
Kitabu kipo jikoni kwa wale wa soft copy zitaanza kupatikana mapema zaidi, kikubwa ni kuwasiliana tu.
Usikose kupata kitabu hichi ili urudi katika mti ule wa UZIMA uliopatikana katika Edeni.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment