Ushawahi kukutana na mtu anasema hivi, MIMI SIJUI! Labda hata wewe ni mmoja wapo wa watu ambao hutumia neno hili.
Ukweli ni kwamba, hakuna mtu ambaye hajui duniani, hata mtoto ambaye anatoka kuzaliwa bado anajua kitu gani alichonacho ndani mwake na ndiomaana wakati wa uhitaji wa kula chakula atafumbua mdomo na kulia na kuashilia anajua kitu.
Zawadi ya peke ambayo Mungu ametupa ni pale tulipo, yaani pale ambapo tumesimama pana kila kitu, sasa kitu ambacho kinahitajika ni kukipa thamani kile ulichonacho kwanza, lazima ujiulize; Mimi sijui, nimejuaje kwamba mimi sijui? Kwa hiyo, umejua kwamba hujui kwa sababu unajua.
Kitu cha muhimu katika maisha, tukiona kwamba, tumejua kwamba, hajui, kujuwa kule tunakoelekea huwa tunarudi kule tunakojua ili kujua kule tunakoelekea kujua.
Popote ulipo una wewe na chochote unachokiendea kina wewe, thamini uwepo wako.
Asante.
Kitabu cha dunia mama ndicho hicho kipo kuchapwa, funua kinywa chako nao mdomo upokee na usindike kile ambacho unapaswa kusindika. Vaa utayari huo.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment