JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Monday, May 28, 2018

Ukiufikia Ukweli Unakuwa Umebakiza Kitu Hiki.

 Sadick Kilasi     May 28, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, TAFAKARI YA ROHO     No comments   




Kuufikia ukweli kwenye hii dunia sio kwamba umemaliza kila kitu. Kuifikia ukweli utakuwa umebakiza mambo haya ambayo ni;

HAKI. Ukiufikia ukweli lazima utambue kwamba hapa nilipo ni haki yangu, huu ndo ukweli wenyewe. Unapaswa kutunza sana ulichonacho bila kuyimbushwa na chochote. Haki inakupa ujasiri wa kumiliki ukweli bila kuyumbishwa na chochote.

Utayari wa kuchukua hatua. Moja kati siri kubwa ambayo watu wengi hawaijui ni kwamba ukweli ni maisha. Wakati wote lazima uwe kwenye mwendo ili uweze kumiliki haki yako. Usiseme nataka kitu fulani harafu hupo kwenye mwendo utaumia.

SOMA:Kutembea Ni Moja Ya Kujifunza.

Vitu hivi vyote vitatu vinaongozwa na imani. Imani ndo nguvu yenyewe inatupa uhakika wa kuendelea kusonga mbele wakati wa magumu. Imani ndo nguvu ya tumaini letu. Hata kama kuna mambo magumu kiasi gani tuna imani kuwa tutayafikia tusiyoyaona kwa sababu tunauhakika wa mambo hayo. Ukweli, haki na utayari vinaongozwa na imani.

Mtu yeyote ambaye ameufikia ukweli harafu hana vitu hivi hawezi kudumu katika ukweli. Ukweli ni matendo, ukweli ni maisha. Badala ya kusema nataka kitu fulani jifunze kuwa kwenye mwendo.

Ukawe na siku bora ukitafakari hili.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail. com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, May 27, 2018

Kutembea Ni Moja Ya Kujifunza.

 Sadick Kilasi     May 27, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   



Mtu ambaye amekaa na kutulia si sawa na mtu ambaye anatembea.

Moja kati siri kubwa ambayo watu hawaifahamu ni kwamba mtu anayetembea si rahisi kupatwa na msongo wa mawazo.

Watu wengi waliofanikiwa ni watu ambao wanachukua hatua. Watu ambao wapo katika hali ya kutembea, kukwea hawana woga wowote.

Mtu ambaye anapigana vita huwa anawoga mdogo kuliko yule ambaye bado hajaingia vitani.

Kwahiyo katika maisha moja ya jambo ambolo mtu anapaswa kufanya ni kuendelea kufanya jambo.

Kufanya jambo si sawa na kutokufanya jambo.

Ukawe na siku bora ukitafakari juu ya hilo.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot. com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, May 23, 2018

Hakuna Matatizo Duniani, Tatizo Ni.....

 Sadick Kilasi     May 23, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   


Inawezekana ikawa ni jambo la kushangaza sana kwako lakini, lakini huu ndo ukweli wenyewe, hakuna matatizo duniani.

Unaweza kusema mbona mimi ninapitia katika hali fulani ngumu, lakini je huo ndo ukweli wenyewe? Fikiria kidogo mwenyewe, je hakuna watu wanaoishi maisha kama hayo au chini ya hayo?

Watu wanapitia katika hali ngumu zaidi ya unayopitia wewe lakini wanaishi wakiwa na furaha.

Tatizo lako si tatizo lako, tatizo lako ni mtazamo wako.

SOMA:Ufikiri Ambao Unaufikiri Ambao Sio Wewe Ambaye Unaufikiri.

Kuna kitu kidogo ambacho watu wote huwa tunapitia na tunaweza kujifunza kupitia hapo, fikiria wakati ambapo huwa tunapata furaha na wakati ambapo tunakuwa katika hali ya udhaifu, kwa kweli ni mtazamo wako.

Wakati unapitia hali yoyote ambayo ni tatizo kwako jiulize maswali haya, kwanini hali hii? Je ni sahihi kuwa katika hali hii? Usijijibu kibinafsi kwamba hili ni tatizo kwangu. Kujionea huruma mwenyewe ni tatizo.

Ukawe na siku bora rafiki yangu ukitafakari hii.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Ukiufikia Ukweli Ni Gereza Huru.

 Sadick Kilasi     May 23, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   




Mtu yeyote ambaye anautafuta ukweli, harafu akaufikia basi kaingia katika kifungo cha milele.

Kifungo cha ukweli ni cha utulivu. Mtu akiufikia ukweli siku zote maisha yake si ya kutangatanga.

Kuufikia ukweli ni gereza huru ambalo huwezi kwenda popote. Mtu akiufikia ukweli hawezi kutoka katika gereza hilo labda awe mtu wa kuasi, muasi wa ukweli.

Watu ambao hawajaufikia ukweli siku zote hawatulii kwa sababu wanamashaka na walicho nacho.

Tafuta kweli nayo kweli itakuweka huru.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, May 21, 2018

Kwanini Watu Wanahasira?

 Sadick Kilasi     May 21, 2018     MAHUSIANO     No comments   



Je mtu unapokuwa unahasira na mwingine unakuwa umekosa haki yake? Au umeshindwa kulinda haki yake?

Je si kila mtu ni ufalme mwingine? Kwanini wewe unataka kutawala kwa mabavu utawala mwingine?

Je huwezi kufikiria kwamba kila mtu anatafuta uhuru wake mwenyewe kwanini wewe unataka kuingilia uhuru wa mwingine?

Je si tupo tofauti sisi, kwanini unataka niwe kama wewe katika kila kitu?

Je si kila mtu anataka kuwa mshindi sasa kwanini wewe pekee yako unataka wewe?

Upendo ndo jibu la mambo yote.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, May 19, 2018

Usiweke Sheria Kwa Kila Mtu.

 Sadick Kilasi     May 19, 2018     MAHUSIANO     No comments   



Sheria ni taratibu ambazo zimewekwa baada ya watu kushindwa kuishi kwa nidhamu yao binabsi.

Sheria inamipaka katika kufanya jambo lolote lile, sheria haina usawa.

Maisha yoyote ambayo hayana usawa ni vigumu sana maisha hayo kuwa na furaha kwa sababu ya mipaka ambayo sheria imeiweka.

Watu wanapenda sana kuwa na kiongozi japokuwa hawapendi kuongozwa. Kuongozwa na mtu ni kuwa chini ya sheria ambayo mara nyingi watu wameshindwa kuishi chini ya sheria.

Watu hawepindi kuongozwa kabisa japokuwa wanapenda kuwa na kiongozi. Watu wanapenda kuwa na kiongozi ili mambo yanapokwenda vibaya wamjue mtu wa kumtupia lawama. Si kwamba watu wanapenda kuwa na kiongozi awaongoze raha sha! Wanapenda kuwa na kiongozi ili atupiwe lawama.

Unapomwambia mtu fulani fanya hivi na hivi ni sawa na kuwa sheria kwake haijarishi jambo unalomwambia ni zuri au la kwake sheria ni tatizo na ndiomaana kuishi na mtu na kumwambia usifanye hiki na hiki huwezi kubadilisha mtu, labda aige kutoka kwako au apate pigo ambalo litakuwa funzo kwake.

Kila mtu anapenda kuwa katika hali kujiachia mwenyewe kuwa huru, haya ndiyo maisha ambayo watu wanataka, kuwa huru kwa kila jambo.

Unapokuwa unahusiana na mtu harafu mwisho kukawa na migogoro  wewe ni kama sheria kwake, unapizuia mtu asifanye jambo mtu analotaka kufanya ni sawa na kuwa sheria kwake na wewe ni chanzo cha migogoro.

Usiwawekee watu mipaka. Kocha Makirita anasema,  njia nzuri ya kumbadirisha mtu ni wewe kubadilika. Badilika wewe na kisha wao wataona tunda kutoka kwako.

Ukawe na siku bora.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, May 18, 2018

Ufikiri Ambao Wewe Unafikiri Ambao Sio Wewe Ambaye Umefikiri.

 Sadick Kilasi     May 18, 2018     NJOZI     No comments   

Si kila jambo ambalo unalifikiri ni wewe ambaye unafikiri. Mambo mengi unayafanya na mwisho unaishia kujilaumu mwenyewe kwa sababu si wewe ambaye umefanya.

Maamuzi yoyote yale ambayo utafanya ukiwa na hasira, hayo sio maamuzi yako ni ya hisia zako.

Maamuzi yoyote utakayo fanya ukiwa na furaha sana hayo siyo yako ni hisia zako.

Maamuzi yoyote utakayofanya ukiwa na huzuni sana hayo si yako ni ya hali yako.

Kwa ujumla maamuzi yoyote ambayo utayafanya ukiwa katika hali fulani hayo si yako ni ya hali yako.

Maamuzi sahihi ni yale ambayo unayafanya ukiwa wewe mwenyewe umekamilika, uko katika hali ya usawa.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, May 17, 2018

Mbegu Haioti Mpaka Ife.

 Sadick Kilasi     May 17, 2018     NJOZI     No comments   

Ni rahisi sana kulalamika wakati ambapo unapitia magumu lakini ninakwambia ukweli huu mbegu haioti mpaka ife.

Inawezekana unaumwa sana na huoni matumaini kabisa lakini mimi nakuambia mbegu haioti mpaka ife.

Je ni wakati gani wewe unapitia? Wakati mzuri au wakati mgumu?

Rafiki yangu inawezekana unataka kuwa tofauti zaidi ya mwanzo, basi vema, lakini jambo moja ambalo unatakiwa kutambua ni kwamba lazima ulifie hilo badiliko.

Ukipanda mbegu harafu ikabaki kama ilivo kamwe haiwezi kuota. Ukiyaendea mabadiliko kwa jinsi ulivyo huwezi kubadilisha chochote, lazima uyafie mabadiliko.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, May 14, 2018

Usijichoshe Na Wakati, Wakati Hutoa Majibu.

 Sadick Kilasi     May 14, 2018     No comments   

Wakati siku zote ndio hutoa majibu ya matarajio yako. Ikiwa umeweka nguvu kazi kidogo basi hata jibu litakuwa sawasawa na kipimo cha mtazamo wako.

Wakati mwingine mambo huwa magumu lakini kwetu sisi tunaangalia matarajio yetu na ndoto zetu. Wakati mgumu huna haja ya kujichosha na wakati uliopo.

SOMA:https://jikolaushauri.blogspot.com/2018/05/jifunze-kwa-wenye-hekima-ishi-na-wajinga.html?m=1

Wakati wote ni sawa kwetu. Msimu wa mvua na kiangazi ni wakati wetu. Hakuna mtu awezaye kubadili wakati.

Wakati hutoa majibu ya mambo yote haijarishi umepata jibu la aina gani wakati huongea na kufichua kilicho jificha.

Ukawe na wakati bora.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, May 11, 2018

Namna Ambavyo Unajipoteza Mwenyewe Wakati Wa Changamoto.

 Sadick Kilasi     May 11, 2018     NJOZI     No comments   

Changamoto ni kitu ambacho kinajitokeza kwenye maisha wakati wote. Changamoto ni kama kifundo cha muwa na utamu wake.

Kifundo cha muwa ni kidogo ukilinganisha na sehemu ambayo ni tamu. Hivi ndivyo changamoto na raha kwenye maisha zilivyo kama muwa.

SOMA:Kufikiria Kwa Shukrani.

Usipoangalia kipande kile cha muwa ambayo ni ngumu inaweza kugeuza kabisa muwa wote kuwa fundo na ukashindwa kufurahia radha na utamu wa muwa.

Siku zote unapo kula muwa huku ukifikiria jino lako huwezi kuufurahia muwa na utamu wake.

Angalia ushindi usiangalie matatizo, popote utapita kwa sababu ushindi ni mkubwa kuliko changamoto.

Ukawe na siku bora ukitangaza ushindi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, May 10, 2018

Kufikiri Kisheria Ni Mwanzo Wa Ujinga.

 Sadick Kilasi     May 10, 2018     NJOZI     No comments   

Kufikiri kwa kukalili wakati wote ni mwanzo wa ujinga. Kufikiri kwa kujishikiza na kuamini kwamba unatambua jambo ni mwanzo wa ujinga.

Ujinga ni pale mtu unapokosa taarifa sahihi juu ya jambo fulani na wewe ukaamini kwamba wewe unaelewa kila kitu. Kuwa na taarifa nusunusu ni ujinga.

Kufikiri kisheria ni pale mwenyewe unapojiwekea mipaka katika kifikiri. Ukiambiwa jambo na mtu harafu ukalichukua jinsi lilivo na kuchukulia kwamba hiyo ni taarifa sahihi huko ni kufikiri kisheria, kujiwekea mipaka kwa kukalili.

Zamani Musa aliwaongoza wana wa Israeli Kisheria, walikuwa hawatambui nini wanafanya lakini waliendelea kusonga mbele kwa kujikokota hivohivo huku wakiwa hawatambui wanachokifanya.

Ndiomaana ilikuwa rahisi kulalamika kwa sababu walikuwa wanafanya kwa kujisukuma tu. Musa ndo alikuwa anatambua anachokifanya.

Wakati tulionao wa imani na utambuzi. Tunatafuta ukweli ikisha ukweli nao unatuweka huru. Kwa kweli hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutupa uhuru mkubwa zaidi wa kufikiri.

Kufikiri kwa usawa kunaleta amani na furaha. Kwa hiyo lazima tufikiri vema na tuupate ukweli nao ukweli utupe uhuru.

Ukawe na siku bora sana ukiwa unatumia ubongo vema kabisa ili kupata ukweli wa kweli.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, May 8, 2018

Jifunze Kwa Wenye Hekima Ishi Na Wajinga.

 Sadick Kilasi     May 08, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, NJOZI     No comments   

Ingekuwa watu wanaishi katika hali moja sijui dunia ingekuwaje? Kama watu wote wangekuwa na hekima sijui watu wangeishije.

Watu wote wangekuwa ni wenye mafanikio, mambo yangekuwa tofauti sana. Mafanikio yangekuwa hayana maana kabisa kama watu wote wengekuwa sawa.

Utofauti wetu ndo zawadi yetu na ndo ubora wetu.

Lakini pamoja na yote haya kila mtu anakazana kusonga mbele kwa pale. Hakuna mtu ambaye anataka kubaki pale alipo, walio fanikiwa wanaongeza mafanikio yao na wachache wa mafanikio nao wanakazana kupata wanachotaka.

Kwa sababu wote tunakazana kutoka kwenye utupu kwenda kwenye utele basi ni vema tukajifunza hekima za waliofanikiwa na kuishi maisha yetu na tukatoka kwenye utupu mpaka kufikia mafanikio.

Tunategemeana mafanikio yapo kwa watu maskini. Lazima ujifunze kutoka kwa watu waliofanikiwa na uishi na maskini ili nawe ufanikiwe.

Ukawe na siku bora rafiki yangu.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Usiogope Kuanza Katika Hali Ya Utupu.

 Sadick Kilasi     May 08, 2018     NJOZI     No comments   

Kitu chochote ambacho unakiona kwa macho yako basi hicho kitu kilianza katika hali ya utupu.

Nyumba unayoiona ni nzuri basi mwanzo wake kulikuwa hakuna nyumba ndiomana ikajengwa nyumba. Miti ilikuwa haipo ndiomaana ikamea, milima nayo ilimea kwa sababu ya utupu.

Palipo jaa hapahitaji kujazwa ila panahitaji kupunguzwa, mti hauwezi kuota kwenye mti. Furahia kwa sababu upo tupu maana utajazwa.

SOMA:Kama Huna Kitu Cha Kufanya Unapaswa Kufanya Kitu Kwa Sababu Kipo Kitu Cha Kufanya.

Hivi ndivyo mambo yote yalivyo, hata dunia yenyewe ilianza katika hali ya upweke na utupu. Ukisoma kitabu cha Mwanzo 1 katika Biblia kinaelezea vizuri namna dunia ilivyoanza.

Kwenye maisha ya kawaida mambo yote ndivyo yanavoanza, hali ya utupu kwenda utele, kutoka kutofanikiwa kwenda kufanikiwa, kutoka mtu mbaya kwenda mtu mzuri.

Kikubwa kuwa na tumaini la jambo zuri likutokee katika maisha. Mungu anatupenda sana, tatizo kubwa tumekosa shukrani na tumaini la kweli kwake.

Popote pale ulipo anza kufikiria kusongonga mbele, kikubwa kuwa na matumaini na weka tumaini katika Mungu.

Chochote chenye utupu kinahitaji ujazo.

Ukawe na siku bora kabisa.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, May 7, 2018

Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha WAAMBIE Nawapenda, Kilicho Andikwa Na Joyce Meyer.

 Sadick Kilasi     May 07, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Upendo upendo upendo ni jambo ambalo linazungumzwa kila mahala na ni jambo zuri sana. Maisha yenyewe ni mahusiano na ili mahusiano yawe yenye tija basi ni vema upendo ukahusika.

Joyce Meyer ametufunulia juu ya upendo wa Mungu kwetu. Ametuonyesha ni namna gani Mungu anavotupenda kutoka kwenye maandiko yake matakatifu kwenye kitabu cha Biblia.

Karibu tujifunze kwa pamoja ninapoenda kukushirikisha mambo niliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki.

1. Watu wanahitaji ufunuo wa kibinfsi wa upendo wa Mungu kwao. Watu wengi wanaishi kwa kutokutambua ya kwamba Mungu anawapenda au hawapendi, wanamashaka na maisha yao. Kwa hiyo wanahitaji ufunuo wa upendo wa Mungu kwao ili wautambue vema upendo wa Mungu.

2. Hatuhitaji ufahamu wa kimawazo kuhusu upendo wa Mungu. Kwa kweli hatuhitaji ufahamu wa mawazo yetu juu ya upendo wa Mungu, kwa akili zetu ni ngumu kujitambua upendo wa Mungu mpaka tufunuliwe upendo huo.

3. Ni Roho Mtakatifu pekee ambaye anaweza kutufunulia upendo wa Mungu mioyoni mwetu. Ukifunuliwa utauona upendo wa Mungu wazi wazi.

4.Kukubali kwamba Yesu alitumwa ulimwenguni kwa upendo wa Mungu si jambo gumu lakini kukubali kwamba Yesu alitumwa kwa ajili yako pekee ungalikuwa unaishi duniani ni jambo gumu. Pamoja na kwamba Mwana wa Mungu alitolewa kwa sababu Mungu aliupenda ulimwengu lakini bado Mungu anakupeda wewe binafsi, amekufunulia upendo huo kupitia Roho Mtakatifu ukiwa peke yako.

SOMA:Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu cha Mbwana Wetu aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu (II)

5. Kama ungalikuwa peke yako hapa ulimwenguni yaani duniani Yesu bado angalikufa kwa ajili yako. Kwa sababu Mungu hataki hata mtu mmoja apotee.

6. Mungu anatupenda ajabu na upendo wake ni wa milele. (Teremos 31:3).

7. Wakati mwingine tunajinenea maneno yenye mwelekeo chanya, maneno ya ushindi lakini adui yetu mkubwa ambaye ni mwelekeo hasi huja haraka na kutushitaki na kusema kwamba wewe ni mtu dhaifu.

8. Kila mmoja wetu ni mtu binafsi aliyeumbwa kipekee na Mungu. Mungu anatupenda kwa upekee huu wa utofauti wetu wa kila mtu. Ndio maana ni vibaya kujilinganisha na mwingine.

8. Tunavipawa vya ajabu ndani mwetu, ambavyo Mungu kaweka ndani mwetu. Vipawa hivi vitutegemea sisi kuishi tukiwa na mtazamo chanya na tukiruhusu Mungu atupende.

9. Hatuwezi kitambua nini hasa upendo wa Mungu ulivyo kwa sababu tumepewa kila kitu kwa ajili yetu, jua, mvua, hewa, wadudu na mengine yote ni kwa ajili yako wewe.

10. Huwezi kumfanya Mungu akome kukupenda. Wengi wetu hufikiri tunamchosha Mungu, ukweli ni kwamba upendo wake ni wa milele kwetu. Tunafanya maovu tunapojikwaa, tunafikiri kwamba Mungu ameacha kutupenda. Upendo wake si tendo analolifanya bali ni kile alichofanya. Yote yapo tayari.

11. Mwanzo wa kuanza kufurahia maisha ni katika upendo na hapa ndipo utapata uponyaji wa kila kitu. Utaanza kupiga hatua katika maisha yako haijarishi utajifunza nini.  (1Yohana 4:18).

12. Kufikiri kwamba wewe ni mkosaji mbele za Mungu na Mungu hakupendi unajiumiza mwenyewe. Huwezi kumtumikia Mungu kwa matendo yako.

13.Huwa tunapokea kutoka kwa Mungu kupitia imani, kwa imani, lakini hata imani inafanya kazi kupitia upendo wa Mungu.

14. Upendo wa Mungu hutiwezesha kuishi bila hofu, na jambo zuri kwetu ni kutimiza hatima yetu.

15. Ni rahisi kuamini kwamba Mungu hutupenda bora tusitende kosa. Shida ni kwamba watu wengi hawajipendi na hii hufanya wajihisi kwamba huenda hata Mungu hawapendi sana.

16. Utajawa na huzuni tele katika maisha yako kama ukishi kwa kujilinganisha na wengine. Ukiwa pamoja na Mungu si lazima ufanye vyema au mema ya kutosha, kwa hiyo huna haja ya kutazama wengine, kwamba mbona wengine wanafanya hivi, wewe ni wa kipekee.

17. Kulingana na kile tunachojua Mungu anatalajia hicho kutoka kwetu mwisho anatibadilisha kutoka utukufu hadi utukufu ili tumfanane.

18.  Tujipe viwango vikubwa katika maisha yetu kwa sababu hivyo ndivyo Mungu anavyowaza juu yetu, tusijione ni wachache katika macho yetu au wadogo lazima tujiongeze.

19. Usimwambie Mungu matatizo yako, alikupenda tangu ukiwa na dhambi kwa hiyo wewe huna haja ya kumwambia matatizo yako.

20. Kila mtu ajiwazavyo ndivyo alivyo. Kama ukijiweka kwenye picha ya mtu mbaya basi ndivyo ulivyo. Hili ni tatizo la kutojipenda mwenyewe. Lazima ujitazame kwa mazuri kwa kila kitu

21. Tunahitaji imani na ujasiri ili kuwa huru.

22. Ni wakati ambao unajipa kichapo mwenyewe kupitia adui yetu shetani lakini Yesu alilipa uovu wote ambao unakusumbua kwa hiyo upo huru.

23. Hisia za hatia au mtazamo hasi na adhabu tinazojipatia hutukandamiza chini kiasi ambacho hawezi kuwa huru kabisa. Sio rahisi kuondoka kwa hali hii ya mgandamizo lakini polepole huku ukitambua kwamba Kristo alikufa kwa ajili yako kwa sababu ya udhaifu huu mwisho utakuwa huru.

24. Ukikosa Upendo wa Mungu pale ambapo utaanza kujihukumu mwenyewe, kutegemea haki yako mwenyewe. Tunaweza kujifunza kwa watoto, watoto hawana msongo wa mawazo na wakati ambao hujihisi hawapo huru basi huwalilia na kutua mzigo huo kwa mzazi. Kwa hiyo nasi hivyo hivyo lazima tumpe mzigo Mungu kwa sababu yeye ndiye Baba yetu, mambo yote atayamaliza.

25. Kuna tundu lililo wazi ndani mwetu kwa kila mmoja wetu. Upweke ambao Mungu peke yake awezaye kuuziba kwa hiyo ni vema ukamruhusu Mungu akupende. Upweke huo hauwezi kutoka bila yeye kuujaza.

26. Wakati au muda ni zawadi ya ajabu kutoka kwa Mungu lazima tutambue nini kipaumbele chetu katika wakati.  Shughuli zetu kwa wakati na Neno la Mungu lazima tulipe kipaumbele.

27. Upendo wa Mungu huleta uzima, amini, furaha na msisimuko wa kuishi.

Haya ni machache kati ya mengi ambayo nimejifunza kutoka kwenye kitabu hichi. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwenye kitabu hiki. Usikose kusoma mwenyewe.

Kitabu hiki ni softi copy na audio copy. Kitabu napenda nawe ukisome. Nitumie ujumbe wasapu kwa 0687000768 ama kwenye email sadikila65@gmail.com nitakutimia bure kabisa. Andika ujumbe wa neno KITABU N, ili upate zawadi yako.

Ukawe na kufikiri kwema.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, May 5, 2018

Kufikiria Kwa Shukrani.

 Sadick Kilasi     May 05, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Inaweza ikawa ni jambo gumu sana kumpenda mtu usiye kupenda.

Ni jambo gumu sana kumpenda mtu ambaye anakutendea maovu. Watu wengi hufikiri juu ya hili, kivipi huyu ananiharibia halafu ndo nimpende?

Watu wengi hufikiri kwamba, nitampenda adui yangu kwa sababu nimeambiwa nimpende. Lakini hiyo au mawazo ya namna hiyo hayawezi kudumu kwa muda mrefu kwa sababu igizo haidumu muda mrefu.

SOMA:Kama Wewe Hujawahi Kuona Hata Kisogo Chako, Yanini Yote Hayo.

Usimpende adui yako eti kwa sababu vitabu vya dini vinasema nimpende adui yangu, hapana, lazima ufikiri kwanini? Kwa kweli Mungu pekee aliyetupenda bila sababu lakini mwanadamu hapana.

Mpendwa msomaji, ni moyo wa shukrani ambao utakufanya umpende adui yako na si vinginevyo. Ukianza kuwaza na kufikiri hili hakika utambua haswa upendo wa Mungu uko wapi? Utambua kwanini unapaswa kuwa na upendo na watu.

Hakuna mkimbiaji anayekimbia  akawa anajifukuza mwenyewe na kusema mimi nina mbio sana.

Ukawe na siku bora rafiki yangu.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Je Ni Muhimu?

 Sadick Kilasi     May 05, 2018     No comments   

Wakati fulani unaweza kufanya maamuzi ambayo wewe mwenyewe hujategemea kabisa kufanya. Maamuzi yoyote ambayo unaweza kuyachua bila kufikiria ni hatari kwenye maisha yako.

Ushawahi kukutana na muuza kiatu njiani au ukapita njiani ukaona kiatu kuzuri ukakinunua bila hata wala hukutegemea kununua?

Mara nyingi mtu akinunua tayari, anajifariji mwenyewe atakwambia kwa sababu nimekipenda, lakini sio kweli huo ni utumwa wa vitu, sio kila unachokipenda lazima ukinunue, kuwa mvumilivu.

Nunua kitu kinachohitajika sio kitu ambacho unafikiri umekipenda. Ukiwa na mapenzi sana na vitu utakusanya makolokolo mengi sana  mpaka utachoka mwenyewe baadaye utaona hayana muhimu na utaishia kutupa tu.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.co.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, May 3, 2018

Mtu Mzima Chezea Akili Kama Watoto. Bado Hujajuaa.........

 Sadick Kilasi     May 03, 2018     NJOZI     No comments   

Watoto wadogo mara nyingi sana huonekana kama hawajui kitu lakini wanajua kitu. Japokuwa huonekana hawajui kitu lakini wanatambua mama yuko wapi na ziwa la kunyonya likowapi.

Mfumo wa watoto wa kuelewa mambo ni kukalili.  Wanatumia zaidi ubongo uliojificha kuelezea mambo japokuwa wanakuwa hawana mambo mengi sana ambayo wameyaficha nyuma ya ubongo wao.

Japo kuwa wanatumia zaidi akili hii iliyojificha lakini kunawakati wanashangaza kidogo hasa wakiwa wadogo miaka mitatu mpaka sita hivi, wanamaswali magumu sana, sasa hapa ndipo wanajaribu kutumia akili isiyo fikika.

SOMA:Hiki Hapa Ndo Chanzo Kikuu Cha Msongo Wa Mawazo.

Labda Mpendwa msomaji nikufafanulie kidogo juu ya aina za akili kwa mjibu wa wanathiolojia na kwa uchunguzi wangu mwenyewe. Kuna akili za aina tatu, akili ya ubunifu, akili iliyojificha na akili isiyofikika.

Watoto wanapokuwa wanauliza maswali wanakuwa wanatumia akili isiyofikika na unapowapa jibu, wanaweka jibu hilo kwenye akili iliyojificha.

Watoto wanapokuwa wanaliza haya maswali wanakuwa wanachezea akili yao japokuwa wengi tunajua watoto wanapenda kuchea vitu pia.

Watoto wanapenda kujua kila kitu kwa sababu ubongo wao unaruhusu kufanya hivo. Watoto hawatumii zaidi ubongo wa ubunifu kwa sababu bado akili yao iliyojificha haijakusanya mambo mengi ambayo yatafanyika kama mawazo. Akili zetu zinafanya kazi kama mawingu, sasa mawingu ya mbele, yanayotembea tembea ndiyo akili ya ubunifu au mawazo.

Watu wazima wanatumia zaidi akili  hii ya ubunifu na akili iliyojificha lakini hawapendi zaidi kutumia akili isiyofikika ambayo ukitumia mara zote unakuwa na furaha.

Kutumia akili isiyofikika ni pale ambapo unakuwa na usawa na ndiomaana unapotumia akili hii unakuwa na furaha. Akili hii inataka wakati wote uwe mjinga yaani uwe tayari kufundishika.

Akili hii itakupa Haki,  amani na furaha. Ni vema zaidi watu wazima tutumie akili hii tuwe tayari kufundishika kama watoto na mwisho akili nyingine zitakuwa zinajiendesha zenyewe bila shuruti ya mawazo hasa kwenye akili ya ubunifu na akili iliyojificha.

Ni vema kuchezea akili, kujiuliza maswali kama, kwanini, imekuajekuaje, hapa utakuwa umetambua haki yako ni kutafuta sababu na ukipata sababu utapata amani ni mwisho ni furaha kwa sababu umepata ukweli. Kweli humweka mtu huru.

Chezea akili kama mtoto kwa akili isiyo fikika, usishikilie jambo kwa kuaminishwa na mtu utakosa haki ya kumiliki jambo.

Ukawe na siku bora katika kuchezea akili.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 068700768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Kama Huna Cha Kufanya Kuna Kitu Unapaswa Kufanya Kwa Sababu Kipo Cha Kufanya.

 Sadick Kilasi     May 03, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Ukiwakuta vijana wamekaa vijiweni wanapiga stori ukiwauliza vipi mbona mumekaa muda huu wa kazi? watakwambia hatuna cha kufanya.

Ni kweli hawana cha kufanya kwa sababu hawajaona cha kufanya lakini kipo cha kufanya. Watu wengi huwa wanafikiri chochote unachofanya unapaswa kulipwa hela, lakini hiyo si  kweli.

Kama huna chochote kile cha kufanya yaani hujasimama kwa chochote tafuta kitu cha kufanya ambacho kitakusimamisha.

SOMA:Kipi Kinakusukuma Kukua?

Biblia inasema wewe ni hai kwa macho ya watu lakini umekufa. Inakwambia tafuta jambo lililo salia, jambo jema,  tena inakwambia uwe mwenye kukesha katika hilo jema ulilolichagua kufanya. Ufunuo 3:1-3 kasome ujifunze.

Tafuta kitu ambacho unaweza kusimama nacho kikakupa jina lako wewe ili mladi kiwe msaada kwa wengine.

Sio lazima jambo hilo likupe pesa, hapana, lazima ujijenge wewe mwenyewe kwanza.

Ni vema kutumia falsafa ya mti ili kukua vema.

Ukawe na siku bora rafiki yangu.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, May 2, 2018

Tunapojongea Kusogea, Kusogea Na Kusogea.

 Sadick Kilasi     May 02, 2018     NJOZI     No comments   

Inaweza ikawa ni maajabu mtu kumaliza kusoma kitabu cha kurasa mianne kwa wiki mbili kwa mtu mwingine lakini kwa mwingine hilo sio jambo la ajabu ni muda aliojipa.

Mambo ndo yapo hivo kwa kila eneo la maisha yetu. Ukitaka kwenda safari ya maili nyingi unaanza kwa hatua moja moja mwisho unafika unakotaka kufika bila kujali imekuajekuaje.

Maisha yapo hivo, lakini kuna hatari kubwa kwa sasa ambayo imeingia ya teknolojia. Mambo yamerahisishwa katika kila eneo la maisha, kwenye mawasiliano badala kuandika barua sasa tunatuma maseji au kupiga simu, usafiri ni ndege au gari.

Yote haya yamekuwa ni maisha mazuri kwa kila mtu lakini kunachangamoto kubwa ambayo ni kwamba watu wanafikiri wanaweza kurahizisha kila kitu, kitu ambacho hakiwezekani kabisa.

Maendeleo yameleta uvivu mkubwa sana hasa kwa wale wanao pokea, kwa watoaji kwao si tatizo kwa sababu mpaka wameleta jambo jipya inamaana tayari wamelipa gharama.

SOMA:Dunia Inatufundisha Kutegemea.

Kila eneo la maisha watu wanataka mambo yaende kwa haraka kabisa kitu ambacho hakiwezekani. Siku hizi kila mtu ukimwambia aandike barua atakwambia ni kitu ambacho hakiwezekani, kutembea vituo viwili, vitatu kwake anakwambia ni kitu kigumu na haiwezekani. Yote hii ni kuzoea tu maisha.

Kila eneo la maisha kwa sasa watu wanataka kwenda kwa haraka. Mpaka chakula kwa sasa watu wananunua madukani.

Tunapokea maendeleo kwa namna tofauti inavyopaswa kupokea maendeleo. Tunafanya vitu ambavyo vinatusahaurisha hata sisi ni akina nani. Maisha yanahitaji usawa kwa kila eneo, unapozidisha kwenye jambo moja tambua kuna kingine unapoteza na ipo siku lazima utalipa gharama.

Usikimbie sana ukamsahau anayekukimbiza.

Ukawe na siku njema.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ▼  May (19)
      • Ukiufikia Ukweli Unakuwa Umebakiza Kitu Hiki.
      • Kutembea Ni Moja Ya Kujifunza.
      • Hakuna Matatizo Duniani, Tatizo Ni.....
      • Ukiufikia Ukweli Ni Gereza Huru.
      • Kwanini Watu Wanahasira?
      • Usiweke Sheria Kwa Kila Mtu.
      • Ufikiri Ambao Wewe Unafikiri Ambao Sio Wewe Ambaye...
      • Mbegu Haioti Mpaka Ife.
      • Usijichoshe Na Wakati, Wakati Hutoa Majibu.
      • Namna Ambavyo Unajipoteza Mwenyewe Wakati Wa Chang...
      • Kufikiri Kisheria Ni Mwanzo Wa Ujinga.
      • Jifunze Kwa Wenye Hekima Ishi Na Wajinga.
      • Usiogope Kuanza Katika Hali Ya Utupu.
      • Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha WAAMB...
      • Kufikiria Kwa Shukrani.
      • Je Ni Muhimu?
      • Mtu Mzima Chezea Akili Kama Watoto. Bado Hujajuaa....
      • Kama Huna Cha Kufanya Kuna Kitu Unapaswa Kufanya K...
      • Tunapojongea Kusogea, Kusogea Na Kusogea.
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates