JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, July 9, 2019

Hii Ndio Siri Ya Rhodesia Ya Kaskazini Na Kusini Kibiblia.

 Sadick Kilasi     July 09, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Hii Ndio Siri Ya Rhodesia Ya Kaskazini Na Kusini Kibiblia.

Mtu aliyekuwa mwanzirishi wa Rhodesia ya kaskazini na kusini aliitwa John Rhodes.

Katika biblia mtu aliyeunganisha Agano la kale na jipya ni Yohana.

Rhodes ya kusini mfano wake ni agano la kale, yaani hiyo Zimbabwe na Rhodesia ya kaskazini mfano wake ni agano  jipya yaani hiyo Zambia.

Rhodes ya kusini ni hifadhi ya vitu vya kale, mfano wake Torati iliyoasili ya mwili.

Rhodes ya kaskazini mfano wake ni vitabu vya injili ya Yesu Kristo, naam, hiyo Zambia. Hii ndio mfano wa Kichwa cha Kristo Yesu yeye aliyekichwa cha kanisa.

Hii inamaana gani? Inamaana kuwa Torati ni mwili na injili ya Yesu ni kichwa. Je! Shingo ni nani? Shingo ni Yohana yeye aliyekatwa kichwa baada ya Yesu kuanza kufanya kazi yeye ndiye shingo kiunganishi cha Torati na injili ya Yesu Kristo.

Basi, Yohana mfano wake pia John Rhodes, hawa wote ni viunganishi vya maajabu haya.

Hamkusoma habari ya David Livingston? (Jiwe linaloishi) yeye aligundua habari ya kiunganishi hichi. Hamjaelewa habari ya mto Zambezi? Hamtafakari habari ya jina la mtu huyu David Livingston? Naam, jiwe walilolikataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la pembeni.

Hekima umejificha chini ya ardhi, inaonekana juu ya ardhi.

Mungu mwenye nguvu amefanya kitu cha ajabu, amefanya maajabu katika uumbaji wake, amefanya maajabu katika mwenendo wa watu, amefanya maajabu katika maisha yetu.

Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, July 8, 2019

Rhodes Ya Kaskazini Na Kusini Na Siri Yake

 Sadick Kilasi     July 08, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Rhodes Ya Kaskazini Na Kusini Yaani Zambia Na Zimbabwe Na Nini Maana Yake.

Ukizungumza Rhodes ya kusini na kaskazini, utakuwa unazungumzia matuo ya Wingereza wakati wa mkoloni.

Na ukizungumzia Wingereza, wakati wa mkoloni Afrika Mashariki tayari unagusia utendaji wa kiinjili ambao Mungu aliufanya kwa hekima nyingi kwa kufanya kama hazina katika nchi zote za Afrika Mashariki.

Lakini pia huwezi kuzungumzia Rhodes hizi  bila kutaja Zambia ambayo ilikuwa ni Rhodes ya kaskazini na Zimbabwe ambayo ilikuwa Rdodes ya kusini.

Lakini pia huwezi kuzungumzia Rhodes hizi bila kumtaja mwanzirishi wake ambaye anaitwa Cecil John Rhodes.

Lakini pia ni vema sana kuyajua maporomoko ya Victoria katika habari ya mambo haya.

Mungu mwenye nguvu hufanya hekima zake kwa hekima nyingi lakini pia humtumia mtu kama chombo cha kufichua hekima hizo. Kilichofungwa na Mungu, Mungu atafanya kwa wakati na makusudi yake.

Lakini ili uichambue vema Rhodes ya kaskazini na ya kusini inakubidi utumie njia, kwa sababu hata utendaji kazi wa nchi hizi mbili ni utendaji wa injili na injili ni njia ambayo ipo wazi.

Unapozungumzia Rhodes hizi unazungumzia utendaji wa kurutubisha ardhi ambayo imekosa rutuba. Lakini nisingependa kuchambua sana juu ya rutuba na kinyesi kwa sababu hayo nimeyaeleza sana katika sehemu za uchambuzi katika nchi husika, hapa najumuisha utendaji wa kiujumla.

Basi tutatumia mstari mmoja kufafanua haya yote, naam, tutatumia mstari kutoka katika kitabu cha Yohana.

Yohana 13:13, Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vyema, maana ndivyo nilivyo.

Tazama, Rhodes ya kaskazini ni Mwalimu, na, Rhodes ya kusini ni bwana, kwa mifano yake. Lakini Na, ni kama maporomoko ya Victoria.

Basi, mambo haya hunenwa kwa mifanano. Rhodes ni kinyesi kwa ujumla. Hapa kinyesi kinafanya kazi moja kwa moja baada ya mtu kujisaidia. Sehemu hiyo mimea ya karibu itastawi vema kwa kupata kitu kipya na nguvu ya harufu yake.

Rhodes ya kaskazini ni Mwalimu katika utendaji wa injili ya moja kwa moja kwa mkao. Huu ni mkao wa utayari ambao unajiendesha kiroho. Kwa hiyo, unakuwa unamwadhili mtu bila yeye mwenyewe kujijua ama akajijua baada ya ishara kutokea kwake. Lakini wewe unakuwa unajua kinachoendelea. Lakini hata wewe unakuwa unaendeshwa si kwa uwezo wako wewe bali Mungu mwenyewe maana wewe ni kitume uliyetumwa. Lakini sisemi kwamba unakuwa huelewi kabisa, bali nasema kwamba mambo yote unakuwa unafanya kama mtumwa wa Mungu kama Yesu alivyokuwa anafanya kwa kukaa na watu ambao Mafarisayo walikuwa hawakai nao.


Haya, Hapa mfano wake ni maporomoko ya Victoria, hiyo, NA.  Hapa ni jinsi ya kuchukuliana na wengine kimchakato. Kwa sababu neno Victoria tulisema kuwa maana yake ni shibana ama shinda. Kuchukuliana kwa umoja katika utofauti. Na, ni kiunganishi cha utofauti. Kwa hiyo, huu nao ni Ualimu ambao mtu anaelewa kuwa mimi najiona kupitia wengine, kwa hiyo anakuwa tayari kuchukuliana akijua kuwa sisi ni watoto wadogo tunaohitaji msaada.

Wakati huu kile kinyesi chetu kinakuwa kinavunjikavunjika na kushuka chini ya ardhi lakini mchakato unapokuwa unaendelea kuna baadhi ya mimea itapokea rutuba. Mfano wake ni, mtoto anapokuwa anachapwa fimbo ni kiwango kidogo kinachoweza kumsaidia kukumbuka na kuacha tabia fulani kwa sababu ya woga wa kimchakato.

Na, ni Ualimu mdogo na hufanya kazi kwa umakini sana.


Basi, Bwana ni umiliki wa mambo mengi. Hapa Waalimu wanaenda kujihifadhi chini kabisa. Rhodes ya kusini, ama nchi ya Zimbabwe katika formula yetu ya utendaji.
Nchi ya Zimbabwe ni nchi inayisifika kwa madini, lakini pia ni nchi ambayo imeendeshwa kidicteta kwa muda mrefu, yote haya ni kwa sababu ya habari ya tabia na asili ambazo Mungu mwenye hekima alifanya ili yapate kutimia na kutimiza lengo.

Sasa hapa sisi Waafrika Mashariki ndio watunzaji wa mambo ya kale, ndio, sisi tunatunza kihistoria kwa desturi zetu.

Hapa ndipo ambapo mfano wake ni Ubongo wako wa nyuma unavyohifadhi mambo yote ambayo umepitia katika maisha. Hapa tunazungumzia asili na mambo ya kale. Kristo Yesu ndiye Bwana wa yote, yeye ndiye wa milele.

Basi, mfano wake hayo ni maandishi haya unayosoma, yanauwezekano wa kujihifadhi muda mrefu na mtu wa baadae kabisa akasoma. Vipo vitu vingi ambavyo mtu anaweza kujifunza kutoka katika asili na hata katika mwili wake akapata maana ya maneno mbakimbali kupitia viungo vya mwili wake.

Neno la Mungu ni mwili wa Kristo, tunalisoma hilo.  Mwili wetu sisi ni hekalu la Kristo, basi, mwili wetu si wetu bali ni wa Kristo. Basi, kwa sababu hii, Kristo ndiye Bwana wa yote katika yote Amina.

Basi  ndugu zangu nimegusia mambo matatu muhimu, naam, manne, katika yote.

Rhodes ya kaskazini, maporomoko ya Victoria, Rhodes ya kusini, yote hutufunza.

Basi, mambo haya ni muhimu sana kuyaelewa,  Mungu mwenyewe ndiye amefanya, kwani kwa haya Yesu aliinesha  mfano kwa kuwambia wanafunzi wake wawape chakula watu elfu tano.

Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.t
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, July 7, 2019

Hii Ndio Hofu Ya Kweli.

 Sadick Kilasi     July 07, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Hii Ndio Maana Ya Hofu.

Hakuna kitu ambacho kinatisha kama hofu, hofu inatisha sana.

Mara nyingi huwa tunafikiri kuwa hofu ni ile hali ya kuogopa kufanya kitu, lakini ukweli ni kwamba ile sio hofu halisi, ile ni ishara ndogo ya hofu ambayo inamtaka mtu kuwa makini.

Wakati mtu hataki kufanya kitu kwa sababu woga, woga huleta tabia ambayo humkaa mtu ndani yake asitake kufanya mambo kwa sababu ya hofu ya umakini.

Ipo hofu ya kweli ambayo ilimfanya Mtumishi wa Mungu Daudi awe anamlilia Mungu, ipo hofu ya kweli ambayo iliwafanya wanafunzi wa Yesu wapige kelele walipokuwa wanavuka bahari na Yesu alikuwa amelala, naam, hii ni hofu ya kifo.

Hofu hii  inakuua ukikosa uelewa, kwa lugha ya kikwetu tunasema (Idzumile Manga) naam, katika kitabu cha Tumaini Jema, ambacho kinaeleza juu ya hazina ya Afrika Mashariki nimeeleza kwa Undani juu ya Idzumile Manga yaani amepata mstuko wa imani. Hofu ya Torati. Mambo haya nimeandika juu ya Madagascar ambayo ni kama mapafu, naam, mapafu ambayo ndiyo imani yenyewe.

Kwa hiyo, usiogipe kufanya mambo makubwa kwa sababu ya hofu ya umakini, hii ni hofu tu ya upendo. Hofu hii kubwa inaletwa na nguvu za kiimani, haiwezi kuwepo tu.

Jipende, fanya mambo makubwa ishi maisha yako kwa matumaini, usiogope hofu ya umakini. Hofu ya kifo inamjia mtu kwa sababu maalamu na neema ya Kristo Yesu ndio mkombozi juu ya hofu hii.

Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, July 6, 2019

Talanta Yako

 Sadick Kilasi     July 06, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Hivi Ndivyo Ambavyo Unaweza Kujua Vipawa Vyako Na Kufanyia Kazi Mapema Sana.

Wakati nikiwa mdogo sana, nikiwa darasa la pili, nilikuwa napenda sana kuvaa saa mkononi mwangu. Naam, kipindi hicho saa zilikuwa zinauzwa elfu moja tu, saa ya kimulimuli.

Lakini nilikuwa na tatizo moja, saa ilikuwa haidumu mkononi mwangu kwa sababu nilikuwa napenda kuifungua ndani na kuitengeneza tena. Niliharibu saa nyingi lakini kuna nyingine ambazo nilikuwa nafanikiwa kuirudishia kama ilivyokuwa mwanzo.

Huu ulikuwa ni mchezo wangu, kuharibu na kutengeneza. Nilikuwa sijui ni kitu gani ambacho kilikuwa kinanisukuma kufanya hivi, wala nilikuwa sijiulizi kwanini nafanya hivyo, Mimi nilikuwa nafanya kwa kadili ninavyosukumwa kutoka ndani. Utoto nao ulikuwa unachangia kufanya vitu kama hivyo.

Sasa, leo hii wakati nimekuwa ndio naelewa kwanini nilikuwa naharibu saa na kutengeneza tena.

Mimi ni mtafiti, mtu ambaye naharibu kilichopo na kutengeneza tena kwa jinsi inavyotakiwa, naam, nafumbua fumbo lilifichwa na kufanya vile inavyotakiwa.

Talanta au kipawa ni zawadi ambayo mtu anapewa na kuwekewa katika nafsi yake ili ipate kumsaidia na kuwasaidia wengine. Kwani Mungu anaweka zawadi hii ndani yetu, na tunazaliwa nayo. Kila mtu anapewa sawasawa na makusudi yake yeye Mungu.

Mathayo 25:14, Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.

Lakini kwa sababu ya maisha ya mazoea katika jamii zetu talanta hizi hupotea bure kabisa zisifanye kazi kabisa. Wengi sana tunachukuliwa na talanta za watu na wengine hatutumii chochote.

Kila mtu anatalanta yake, na talanta ya mtu hujionyesha anapokuwa mdogo, kwa sababu katika kipindi hichi Mungu ndiye huwa anamwongoza mtoto kwa kiasi kikubwa.

Kuna wakati mtoto anakuwa anafanya vitu ambavyo vinakuwa kwa mzazi wakati mwingine havileti maana kama mimi kuharibu saa. Mimi niliyekuwa mharibifu wa thamani na natengeneza thamani nyingine.

Ukisoma katika neno la Mungu utagundua kwamba Yesu alimponya mtoto ambaye alikuwa na pepo la kuangusha, na kumpeleka huku na huko tangu utoto. Marko 9.

Sasa, talanta ni kitu ambacho kila mmoja anapaswa kutia juhudi kutumia kwa sababu talanta sio ya kwako wewe peke yako bali ni kwaajili ya kuwahudumia wengine.

Kitu chochote kilicho ndani mwetu, hicho si cha kwetu kwa sababu hicho tunapaswa kutoa nje, cha kwetu ni kile ambacho tunakihitaji kwa sababu hicho tunakiingiza ndani mwetu.

Talanta yoyote inahitaji kuboreshwa na mwenye talanta kwa kutia juhudi sana, kwa sababu kila mwenye talanta atadaiwa ni namna gani ametumia. Mwanadamu hamiliki chochote tumeazimwa kwa muda Mungu atachukua kwa wakati wake.

Mathayo 25:19, Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.

Hapa duniani watu wanahitaji faraja tofauti tofauti  kutoka kwenye utofauti.

Ni muhimu sana kuthamini kile ambacho umepewa na Mungu uwape watu.

Na ili uthamini talanta hiyo unapaswa kuwa na shukrani na uvumilivu. Nitakupa Falsafa moja ambayo huwa tunaishi kila siku hasa vijana tunapenda sana.

Shukrani ni uwezo wa kuthamini chenga, sasa sijui ni chenga ya mchele ama chenga ya mpira, yote na yote unaweza kujifunza. Chenga ni uwezo wa kuendesha vitu vidogo vidogo, naam, chenga chenga na kuthamini kwa unyenyekevu mkubwa.

Umakini unahitajika katika sehemu hii kwa sababu ni sehemu ambayo wengine wataona ni upuuzi tu mwanzoni unapoanza kufanya lakini kwa sababu mpanzi huenda akipanda kwa machozi na kuvuna kwa furaha, wewe unatambua hili.

Kitu cha pili kinachohitajika ni pasi, naam, sijui unavyosha nguo ama unapiga pasi ya mpira lakini hapa ninazungumzia kuboresha kile kidogo ulichopokea. Kama ni chenga za ubwabwa basi hakikisha unaweka viungo ili viboreshe mchezo wako.

Mathayo 25:16, Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.

Mwisho unafunga goli lako, unafikia kusudi na malengo yako. Hapa ndipo utawambia waliokukatisha tamaa kuwa, chenga ikiboreshwa inakuwa pasi na pasi huleta goli.

Kwa hiyo, kila mmoja lazima azingatie hatua hizi tatu, naam, hizi ni njia ambazo tunazifanya kila siku katika maisha yetu.

Kuna wakati mwingine unaweza ukawa hujasoma lakini unaweza kusoma mchezo unaendelea na ukapata majibu.

Ukihakikisha macho yako yanasoma na kulia hakuna kitu ambacho kinashindikana, ndio, malengo na kuchukua hatua ni muhimu sana.

Kama unatalanta na unaitumia vema basi Kristo atakupa zaidi ya talanta yako. Usichezee talanta yako.

Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768  au sadikila65@gmail.com.

Kitabu cha Mormoni ambacho ni ushuhuda wa Yesu Kristo nakigawa hakikisha unatuma ujumbe kama unahitaji. Asante.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Hivi Ndivyo Wewe Unaweza Kutafsiri Neno La Mungu.

 Sadick Kilasi     July 06, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Hivi Ndivyo Wewe Unaweza Kutafsiri Neno La Mungu.

Mungu kwa upendo wake ametupa Roho Mtakatifu kwa njia ya Kristo Yesu awe msaidizi wetu katika yale ambayo tunayafanya.

Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu katika yale ambayo tunayafanya yanayomtukuza Kristo Yesu.

Lakini pia katika hayo hayo tunayoyafanya kuna sehemu kubwa ambayo sisi kama sisi tunapaswa kuhusika na kuwekeza nguvu zetu na Roho Mtakatifu anahusika zaidi kwenye hayo hayo kwa pamoja.

Kwa hiyo, kuna uwekezaji fulani ambao mtu anapaswa kufanya  naye Kristo Yesu kupitia Roho Mtakatifu atamsaidia mtu huyo kuhakikisha anafikia kusudi.

Marko 8:22, Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? Akatazama juu, akasema,  Naona watu kama miti, inakwenda. Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote wazi wazi. Akampeleka nyumbani kwake akamwambia hata kijijini usiingie.

Kwa hiyo, hapa tunaona kuwa kuna sehemu ambayo kipofu ikimbidi ahusike kwa kutazama sana ili apate kuona wazi wazi. Ingawa Yesu alikuwa anamsaidia lakini hata yeye kipofu alijitaidi kuhusika katika kutenda na kuona uhalisi wa mambo.

Sasa, Leo,  katika injili ya Kristo Yesu, nitakupa njia ya kufasiri neno la Mungu, ambayo ni njia ya injili yenyewe ya Maji na Roho.

Zaburi 1:1, Heri mtu yule asiyekwenda  Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Mtu, asiyekwenda, asiyesimama wala kuketi; kwa mchakato huu kila neno hufasiliwa.

Kwa hiyo, njia hii ndio njia ambayo kila neno hufasiliwa. Tunasoma vitabu vingi sana lakini maneno yote ya kwenye vitabu tunayosoma huhifadhiwa  kwa njia hii.

Katika neno la Mungu, neno la Mungu limeandikwa kwa njia, tofauti na vitabu vingine vya kawaida.

Hiyo ndiyo siri ya kufasiri neno, naam, hiyo njia ndio njia kutafsiri neno. Mara nyingi hiki huwa ni kipawa ambacho mtu anawekewa ndani yake ili kuwasaidia wengine.

Kwa njia hii kila neno ambalo utasoma na kusikia utatambua ni sehemu gani ambayo unapaswa kulihifadhi neno hilo.

Baadae maneno hayo huvunjwavunjwa ili yatumike sawasawa na inavyopaswa. Na Roho Mtakatifu ndiye humsaidia mtu katika kunena hayo.

Kwa hiyo, chukua hatua leo ya kuongeza talanta hii nawe utaona wazi wazi.

Mungu akubariki, hiyo ni zawadi yako. Amina.

Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, July 5, 2019

Falsafa Za Asili (Songa Ugali).

 Sadick Kilasi     July 05, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Falsafa Za Asili, Songa Ugali.

Wanasayansi wanaamini kwamba mmea hauwezi kujitengenezea chakula kama hamna mwanga wa jua, Maji na Caborndioxide.

Mimi naamini katika Falsafa Za Asili kuwa siwezi kula ugali kama Maji na Unga na mwiko usiposonga. Lakini naamini zaidi ya mwiko kuwa mwiko hauwezi kujiendesha wenyewe kama hamna mtu anayeendesha.

 Kwa hiyo tangu sasa elewini habari za mambo haya nyinyi mlio wanasayansi kuwa jua linaendeshwa halijiendeshi lenyewe, maana jua ndio mwiko ambao unasonga chakula cha mmea.

Sayansi bora ni ile sayansi ambayo inapatanisha watu na Mungu na si kujiinua yenyewe. Je! Mwiko ujisifu wenyewe?

Aliyetumwa si zaidi ya aliyemtuma, naam, mwenye kutuma ni mkuu zaidi ya aliyetumwa.

Kwa hiyo, Falsafa Za Asili ni zawadi yetu sisi Waafrika, maana hizo ndizo tunazoishi. Tunamshuru Mungu kwaajili ya asili hii, naam, mwenye maarifa hula vya Babaye.

Sayansi ni yetu kwani inatuendeleza zaidi ya viwango hivi tulivyonavyo kwa utukufu wa Mungu. Ukikosa shukrani kila kitu kilichopo ni mzigo.

Tukithamini asili tutapata sayansi ili kurusha vitu vya asili angani.

Umpe Mungu utukufu kwa kila kitu kwa shukrani na unyenyekevu nawe utapokea zaidi ya hivi. Mafanikio yako yapo katika shukrani.

Nasema tena, sayansi bora ni ile ambayo inamtukuza Mungu kwa kazi zake, ikijua kuwa mwiko hauwezi kujizungusha wenyewe.


Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Huu Ndio Mji Tulivu Uliojificha.

 Sadick Kilasi     July 05, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Huu Ndio Mji Tulivu Uliojificha.

Ushawahi kutaka kuishi maisha ya utulivu katika maisha yako? Au ushawahi kuutafuta utulivu katika maisha yako? Ndio, naamini utanataka sana utulivu wa maisha, maana kila unachohangaikia sasa ni kutafuta utulivu.

Utulivu huleta imani na imani huleta amani ya moyo na Amani huzaa tabasamu. Sasa, imani ya kweli hutoka katika neno la Kristo Yesu ili uwe Mwenye kujiamini.

Kama umekuwa ukihangaika sana kutafuta mji tulivu basi leo nakutangazia mji tulivu uko wapi. Mji tulivu ni mji ambao umejificha sana na mji huo umejificha ndani mwako.

Na ili ujengeke katika mji tulivu huo unapaswa kuwa na matumaini, matumaini katika neno la kweli na upekee.

Huwezi kuwa mtulivu kama hujachagua, na huwezi kuchagua kama huna imani, na huwezi kuwa na imani kama huna utambuzi sahihi wa chanzo cha imani yako.

Katika maisha lazima uwe mtu wa kuchagua vema ili ujiamini, kwani kujiamini ni kujilinda dhidi ya, na kuchagua njia sahihi.

Njia sahihi ya maisha ni kuishi ukweli uliopo ndani mwako. Ukiishi ukweli uliopo ndani mwako basi utawasilisha matokeo ya mji tulivu.

Kama unataka kujiamini basi usifanye yale yaliyo ya kawaida ambayo dunia inafanya. Lazima ujiami dhidi ya mambo na uishi upekee wako ulio mji tulivu wako ulioko ndani mwako.

Ukitaka kuishi sana mambo ya dunia utaendeshwa nayo. Mji tulivu unakuhitaji wewe uingie huko na uishi huko.

Usijikose wewe ishi wewe mwenyewe kama wewe.

Anza sasa na uishi wewe na uingie katika mji tulivu wako ukatulie huko huku ukiwa na uhakika wa matumaini yako.

Kuwa na matumaini katika neno la Kristo Yesu ili kuwa na hakika ili upate kutulia. Anza sasa kuishi maisha ya upekee wako kwa shukrani na kutaka sana kujua kile kilichopo ndani mwako.

Jipatie softcopy ya kitabu cha Dunia Mama, upate kujisomea polepole kwa upole wa moyo na matumaini na kujijenga katika upekee wako maana katika kitabu hichi nimeeleza kwa upana juu ya upekee.

Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Kaa Sehemu Yako.

 Sadick Kilasi     July 05, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Yapo mambo mengi sana ambayo Mungu angetamani ufanye kwa utukufu wake yeye; Ijapokuwa unakata tamaa na kuona kana kwamba wewe si sehemu ya watu ambao waneweza kufanya mambo yanayoleta heshima.

Inawezekana sana wewe kufanya mambo makubwa pale ambapo wewe unaanza kuishi na kufanya mambo yale ambayo Mungu anataka ufanye. Na kama utafanya yale ambayo Mungu anataka ufanye basi tambua kuwa umechagua njia sahihi kabisa na ni upekee wako ambao mwingine hawezi kufanya kwa sababu kila mmoja katika dunia Mungu alimleta kwa kusudi la kutimiza sehemu ambayo Mungu alitaka atimize.

Zawadi pekee ambayo Mungu amekupa ni upekee wako wewe. Na jambo unalopaswa kufanya kuishi wewe kama mtu uliyetumwa na Mungu. Kila mmoja amekuja kutimiza sehemu yake, kwa hiyo ni muhimu sana kabla ya kuona mambo mengi ya dunia ona kwanza mengi ambayo unaweza kuwapa watu wa dunia.

Kila mmoja ana sehemu ambayo anapaswa kutimiza sehemu ya upekee wake. Kwa hiyo, katika maisha ni muhimu kujijalia wewe mwenyewe na kujilinda na yale yanayokuzunguka ili utimize sehemu yako ya pekee.

Jilinde na uishi maisha sahihi ili uwe zawadi kwa watu wa dunia hii, maana Adamu alipomwona Hawa alisema, naam, huyu ndiye mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama zangu.

Hatuwezi kutengeneza uwiano kama mioyo yetu kila mmoja anataka, tunataka kitu kimoja. Tunaweza kutengeneza uwiano, kama tutaishi kwa kutimiza kusudi la Mungu.

Kila mmoja ni zawadi ya mtu mwingine. Kwa hiyo penda sana kujiona kuliko kuona sana.

Jipatie Soft copy ya kitabu cha Dunia Mama kwa bei nafuu kabisa ujisomee kwenye simu yako polepole kwa upole. Katika kitabu hichi nineeleza juu ya upekee kwa upana sana.

Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ▼  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ▼  July (8)
      • Hii Ndio Siri Ya Rhodesia Ya Kaskazini Na Kusini K...
      • Rhodes Ya Kaskazini Na Kusini Na Siri Yake
      • Hii Ndio Hofu Ya Kweli.
      • Talanta Yako
      • Hivi Ndivyo Wewe Unaweza Kutafsiri Neno La Mungu.
      • Falsafa Za Asili (Songa Ugali).
      • Huu Ndio Mji Tulivu Uliojificha.
      • Kaa Sehemu Yako.
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates