Mpendwa msomaji, leo ningependa nikushirikishe kumbukumbu zangu kwa Babu yangu ambaye tayari ameshafariki miaka mingi na bado najifunza mengi kutoka kwake kutokana na kumbukumbu zangu kwake. Natumai nawe utajifunza kitu hapa. Karibu.
Namkumbuka Babu yangu, namkumbuka jinsi ambavyo alivyokuwa wa tofauti na watu wengine. Babu yangu alikuwa anaitwa Halani Kilasi, tayari Babu yangu alishafariki, amefariki miaka 17 iliyopita. Babu alikuwa ni mtu wa tofauti sana. Watu walikuwa wanamwita Babu yangu maskini. Walimbatiza jina hilo kama jina la ukweli na alipewa jina hilo kwa sababu alikuwa haoni. Babu yangu alikuwa ni kipofu. Watu walikuwa wanamwita Babu maskini lakini si kwamba Babu yangu alikuwa tufauti sana na watu wa kijijini pale hapana, walimwita maskini kwa sababu yeye alikuwa haoni. Kwa kweli anayejua uskini wa mtu kiukwelikweli ni Mungu maana yeye haangalii mambo ya mali. Mimi huwa naamini kwamba Babu yangu alikuwa mtu tajiri sana hata kama alikuwa haoni na wala hakuwa na mali lakini kwa jinsi ambavyo anaishi, aliishi maisha mazuri, maana utajiri wa mali ni kama kiungo cha mkono au kidole tu ndani mwili. Kumbukumbu La Torati 8:18, Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako. Kwahiyo mpendwa wangu rafiki, utajiri si mbaya, hapa tuelewane vizuri. Utajiri ni kama kiungo cha mwili labda kidole au mkono kwahiyo si kwamba mtu akikosa kidole au mkono hawezi kuwa na uhai. Kwahiyo Babu yangu alikuwa ni maskini wa mali na viungo lakini aliishi kama tajiri, namkumbuka sana Babu yamgu.
Namkumbuka sana Babu yangu, Babu yangu alikuwa haoni lakini Babu yangu alikuwa ni mtu mwenye imani na matumaini. Babu yangu licha ya kuwa alikuwa haoni lakini Babu yangu alikuwa mkulima mzuri sana. Babu yangu alikuwa anapenda kufanya kazi sana yeye mwenyewe. Babu aliwashangaza watu kijijini kwa sababu alikuwa analima wakati haoni. Alikuwa sio mtu wa kukata tamaa haraka, Babu alikuwa anamaarifa sana, aliandaa mianzi mirefu akawa analima kilimo cha matuta, alikuwa anautandika mwaanzi chini ikisha anafuatisha mwanzi huo katika kulima kwake. Tuta lilikuwa linapita kwenye mwanzi, yeye kazi yake ilikuwa ni kuukanyaga mwazi na kufuatisha kwenye mguu. Babu alikuwa anapendelea kilimo cha viazi vitamu. Alikuwa pia anapanda miti. Binafsi mimi nafunza mengi sana kutoka kwa Babu yangu. Babu yangu alikuwa sio mtu wa kulalamika bali yeye alikuwa ni mtu kuhamasisha. Babu alikuwa sio mtu wa kusema mimi ni kipofu, hapana, alikuwa mtu ngangali. Kama Babu angelalamika kwa kukosa macho, basi nahakika Babu ni mtu ambaye angekuwa anaabudu sanamu kwa kulalamika kwake, maana maneno ya Mungu yanasema hivi; Luka 12:34, Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako. Labda Babu angelifikiria kwamba macho yake yalikuwa ni ya muhimu kuliko mwili wake basi hazina yake ingekuwa imekufa, lakini Babu hakufikiri hivo Babu alikuwa ni mtu wa matumaini. Matumaini ya Babu ilikuwa ni uhai maana aliendelea kufanya shughuli za kawaida kama mtu ambaye anaona.
Namkumbuka sana Babu yangu, Babu ambaye alikuwa anajua kuzungumza kingereza ambacho alifuzwa na wazungu alipokuwa kijana. Ilikuwa inashangaza Bibi yangu yaani mke waka alikuwa hajui hata kiswahili lakini Babu yangu alikuwa anajua vema kiswahili na kingereza. Lakini kwa kingereza sina uhakika kwamba alikuwa anajua vizuri maana shule aliyesoma yeye ni shule za ngumbalo tu na alipata bahati ya kufanya kazi na wazungu kabla ya wakati macho yake hayajapofuka. Namkumbuka sana Babu, Babu yangu alikuwa mbishi sana lakini nilikuwa nampenda sana kwa sababu alikuwa anapenda sana kuniuliza maswali ya kingereza. Kwa kweli Babu alikuwa nafurahia sana kuuliza watu maswali ya kingereza maana yeye alikuwa hampati mtu wa kuzungumza naye kimgereza, sasa wajukuu, nyakati za jioni, utasikia meza kwa kingereza inaitwaje? sahani kwa kingereza inaitwaje? Binafsi nilikuwa nafurahia sana maswali yake, kipindi hicho nilikuwa darasa la pili tu, nilikuwa sijui vizuri, akiniambia naenda kutambishia watu, Kwa kweli, ninahisi Babu yangu yupo japo alikufa miaka 17 iliyopita. Nawakumbuka sana Bibi na Babu, walikuwa wanabishana sana, Babu yangu licha ya kuwa ni kipofu lakini alikuwa hataki kushindwa. Bibi alikuwa hajui hata kuongea kiswahili, yaani kiswahili chake kukielewa bora usikilize kingereza. Lakini Babu yangu alikuwa anajua kuongea kiswahili na kingereza na alikuwa akipata fursa ya kuonana na mtu anayejua lugha hizo alikuwa anapenda sana kuongea naye. Ndipo huwa nakumbuka mstari mmoja kwenye; Waebrania 13:10-15, Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kura vitu vyake. Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi. Kwa ajili ya Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi tukichukua shutumu lake. Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twatafuta ule ujao. Basi kwa njia yake yeye, tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. Basi hapa nawaza mimi mwenyewe, labda Babu yangu alikuwa anawapenda sana watu ambao wapo tayari kuzungumza naye kingereza na kujisemea moyoni mwake, Mungu asante kwa kuniletea mjukuu wangu ambaye kidogo anajua kingereza. Basi hapa tumejifunza swala la upendo. Ukiwa nacho unamhitaji asiye nacho. Anayepanda na anayekuza wote ni sawa. 1Wakorintho 13:1, Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao.
Namkumbuka sana Bibi na Babu yangu, Bibi yangu alikuwa anapenda sana kuimba nyimbo za kilugha za kanisani. Basi kila nikienda kuwatembelea nilikuwa najisikia vibaya wakati wa kwenda kulala maana wao wakuwa wanalala mapema sana, chakula cha jioni kilikuwa kinaliwa saa 12 jioni na kulala saa moja. Jua linapozama nasisi tulikuwa tunaenda kulala, mimi nilikuwa sipendi alikini milikuwa nafarijiwa na nyimbo za Bibi na Babu, nyimbo za kilugha, nakumbuka sana. Bibi yangu alikuwa anaanzisha na Babu yeye ni kuitikia, walikuwa wanapendana sana, nyakati zote mambo yalikuwa shwari. Walishirikiana kwa pamoja kuimba, Babu alimsapoti Bibi kwenye kipawa chake cha kuimba. Neno la Mungu linasema; 1Wakorintho 11:11, Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana. Basi utofauti wa sauti zao ulileta ladha kwelikweli na ubora wa nyimbo, walikuwa vuzuri sana. Nilijikuta nalala na wao wakiendeleza songi zao.
Nawakumbuka wazungu ambao waliwahi kuja kumtembelea Babu yangu, maana walisikia habari kwamba kuna kipofu jina lake maskini ni mkulima na hushika jembe mwenyewe. Walipo kuja walisema huyusio maskini. Kwa sababu anashughulika kwa sehemu yake huyu si maskini, nakumbuka sana. Babu alikuwa kipofu lakini alikuwa mtu wa tofauti sana. Babu yangu ni shujaa wangu. Namkumbuka siku moja alinambia niende kulinda shamba kware wasifukue mbegu za mahindi yanayoota mimi nikaenda kucheza, akamtumia jamaa moja ambaye alikuwa jilani anishike ili aniadhibu, akanishika, yeye Babu alinishika mkono aanza kunifinya. Babu yangu alikuwa mtu wa matumani alifanya kitu ambacho anapaswa kufanya, hakuwa mtu wa kulalamika kama wana Waisraeli walivolalamika kule jangwani na kugongwa na nyoka, alikuwa na matumaini. Kutoka 17:3, Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? Babu hajawahi kulalamika kwa sababu ya macho yake aliishi tu kama mtu wa kawaida, hakusema Mungu! macho yangu ya zamani yako wapi? sijawahi kumsikia, aliishi tu kama mtu wa kawaida. Babu yangu ni shujaa wangu.
Mpendwa msomaji, nimempa sifa nyingi Babu yangu, nimesema hajawahi kulalamika lakini mimi sijui maana mimi nimezaliwa nikimkuta Babu yangu ni kipofu kwahiyo, sijui mengine, naye alikuwa binadamu kama sisi ana udhaifu wake lakini mimi nachukua mazuri yake tu, ona wema usine ubaya. Mwanzo 1:4, Mungu akaiona nuru, yakuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Namkumbuka sana Babu yangu, BABU YANGU NI SHUJAA WANGU.
Asante sana kwa kushiriki kumbukumbu zangu, hayo ni machache tu ambayo nimekushirikisha yapo mengi Babu yangu aliyafanya. Natumai umejifunza kitu. Mistari ya Biblia ambayo nimetumia basi nataka ujifunze kitu juu ya hilo. usisahau kujipatia kitabu cha bure cha UKRISTO NA MAISHA. NItumie ujumbe whatsapp au email nikutumie kitabu.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment