JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Thursday, August 30, 2018

Nguvu Mbili Ambazo Hutawala Katika Ulimwengu Huu.

 Sadick Kilasi     August 30, 2018     KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Katika dunia hii ambayo tunaishi kuna nguvu kuu mbili ambazo watu hurusu ziwatawale katika maisha yao.  Yaani kama una hii basi nyingine utakuwa huna. Lazima mojawapo uwenayo. Nguvu hizi huwatawala kila mmoja katika maisha. Nguvu zenyewe ni;
-FURAHA NA
-WOGA.

Nguvu hizi humtawala kila mmoja kutokana na mazingira ambayo mhusika anayaishi na namna alivyochagua mwenyewe kuishi. Furaha ni nguvu ambayo inamwelekeo chanya. Furaha ni mwanga katika maisha ya mtu lakini Woga ni nguvu yenye mwelekeo hasi katika maisha. Woga ni giza nene katika maisha ya mtu.

Nguvu zote hizi mbili nimekwambia hapo juu humtawala mtu kutokana na maisha yake anavyoyaendesha. Watu wengi wamejikuta katika hali tofauti tofauti kutokana na maisha yao. Wengi tumejikuta tunafanya machaguo bila kutambua kwamba kwa sasa tunafanya machaguo ya kuleta woga au furaha katika maisha yetu. Maana yeyote ambaye amechagua maisha ya kuishi katika maisha ya kiasi hamna woga ndani yake.

Tunapitia katika hali hizi zote ili mradi tu tujifunze kuishi maisha yenye maana lakini bahati mbaya wengi huwa hatutambui nyakati na wakati maalumu kwa sababu tumekosa uwepo ndani mwetu. Mungu hutumia nyakati hizi tofauti ili tutambue utofauti wa mambo katika maisha ili tuishi kwa shukrani.


Kumbukumbu la Torati 8:1-11, Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika na kutenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki. Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana Mungu wako alikuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone nja, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini. Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo. Nawe uzishike amri za Bwana, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha. Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemichemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima, nchi ya ngano na shairi, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali; nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba. Nawe utakula ushibe, utamshukuru Bwana, Mungu wako kwa nchi nzuri aliyokupa. Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, ninazokuamuru leo.

Woga hautoki kwa Mungu, bali woga ni zao la hofu, na hofu ni tahadhari ya kuwa makini. Katika nyakati hizi zote ambazo Mungu ametumbia, mtu haishi kwa mkate tu, bali na kwa neno la Mungu, kuna wakati ambapo utajikuta katika jangwa, nchi ya ukame, nchi ambayo mambo ni magumu kwa macho ya uanadamu yaani tafsiri ya mwanadamu. Lakini wakati huu sio wakati wa kuishi kwa woga, bali unapaswa kuwa na hofu na Mungu, weka tumaini kwake, tambua kabisa ninaishi kwa neno lake. Neno lolote ambalo Mungu analituma kwako ili ulipitie unapaswa kupia, tambua kabisa anayeshuka huwa anapanda. Katika kifungu hicho Mungu anataka tuyaelewe mazingira ili baadae tuje kuishi kwa furaha.

Unapokuwa umejiingiza katika maisha ya kulaumu kila wakati tambua kwamba umejiingiz katika maisha ya woga, na woga ukikutawala umekufa, kumbuka wana Waisraeli walipokuwa wanamnung'unikia Musa kule jangwani, walishia kufa tu, Mungu aliwatuma nyoka wenye sumu, wakawagonga wakafa. Kwahiyo weka tumaini lako kwa Mungu na hutapungukiwa na lolote wala mguu, wala mavazi yako hayatachaka. Kila wakati huwa unapita, Mungu amekuandalia yaliyo mema.

Ishi kwa upendo katika wakati huu mgumu na upendo ndio huleta amani na furaha, upendo hauhesabu muda, upendo huvumilia yote,upendo hutoka kwa Mungu maana kwake ndimo yanayotoka ya upendo yaliyo mazuri bali ubinafsi huleta hofu na hofu inakupeleka kwenye woga na woga ni nguvu ya shetani sasa.

Furaha mwanzo wake upendo ni kuwafikiria wengine na kuwatendea kwa kuzingatia kiasi, na kiasi huleta amani na amani huleta furaha na furaha ni nguvu yenye mwelekeo chanya kwa wahusika.

Woga mwanzo wake ubinafsi, ubinafsi usio na kiasi na ubinafsi usio na kiasi huleta hofu isiyo na tumaini na hofu isiyo na tumaini kwa Mungu itakutupa kwenye woga na woga ni gereza la shetani la mateso.

Mpendwa mosomaji, rafiki yangu, Ndugu katika Bwana Mungu, maisha ambayo hayana shukrani ni maisha ambayo ni ya kizungumkuti ni maisha ya kupelekwa huku na huko, maisha ambayo hayazingatii kiasi  yanakosa uwepo. Mtumaini Mungu wakati wote na uishi katika nguvu zake.

Leo ni ninazawadi ya vitabu viwili kwako, kitabu ambacho nimekiandika mimi mwenyewe cha UKRISTO NA MAISHA na kitabu kilichoandikwa na JOYCE MEYER cha NISAIDIE NAOGOPA.  Hakikisha unajipatia vitabu hivi ambavyo vitakusaidia kulingana utayari wako wa kutaka kujua  Mungu anataka nini katika maisha yetu. Kwenye kitabu changu nimeeleza kwa undani juu ya Injili ya Maji na Roho ambayo ndiyo ufunguo katika Ufalme wa Mungu na kitabu cha nisaidie naogopa, mwandishi ameeleza namna ya kukabiliana na hofu, emeleza kwa undani zaidi. Hakikisha unajipatia vitabu hivi bure kabisa, nitumie ujumbe kwa namba 0687000768 au sadikila65@gmail.com. Nitumie ujumbe nami nikutumie kitabu.

Asante kwa kusoma makala hii, Mungu akubariki, mimi ni zawadi yako na wewe ni zawadi yangu mimi, Mungu amenizawadia wewe.
asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
 



Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, August 20, 2018

Kama Unayo Leo.

 Sadick Kilasi     August 20, 2018     No comments   




Habari Ndugu? Natumai unaendelea salama, Mungu anakupigania. Hongera kwa siku hii ya leo, leo ni siku yako ya kipekee kwako.


Kama una leo basi tambua kwamba unauwezo wa kubadilisha kabisa sura ya maisha yako hapo mbeleni.


Kama una leo basi unafursa ya kufanya makubwa ya kuweza kuchukua hatua kubwa ambazo zinaweza kubadili historia ya maisha yako kabisa.

Je wewe ni mfungwa kwa jambo fulani lakini bado unamatumaini?

Basi Batimayo kipofu alikuwa mfungwa kwaajili ya upofu wake lakini alikuwa na matumaini na aliitumia vizuri leo yake akaponywa.


Mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka mingi na kuhangaika kwa muda mrefu lakini siku moja alimwona Yesu, akajisemea moyoni mwake nikigusa tu pindo la vazi lake nitapona. Basi mwanamke alikuwa ni mfungwa mwenye matumaini na siku moja fursa ilipojitokeza ilibadili maisha yake kabisa, alitumia leo yake vizuri.


Paulo aliyekuwa mwuwaji, alikuwa anaangamiza kanisa, leo yake moja tu ilibadili maisha yake leo hii Paulo ndiye aliyefanya kazi kubwa sana ya kutangaza injili mahali pote duniani. Ni kwasababu ya leo yake moja ilibadili kila kitu katika maisha yake.


Jifunze kutoka;
Matendo 9:1-10.

Je wewe ni mfungwa wa shughuli nyingi? Unayo leo, itumie leo vizuri, chagua mambo yanayofaa na utimize kwa ukubwa na uadilifu zaidi. Unayo leo, leo ndiyo siku yako ambayo unauhakika nayo, pale ulipo ndipo ulipo,

Fanya kwa wakati,
Kwa kuwa una wakati,
Utafika wakati,
Hutakuwa na wakati,
Wa kufanya kwa wakati.

Ndugu wawili Martha na Maliamu, walipata fursa ya kutembelewa na Yesu, Maliamu alitumia vizuri fursa na kuchagua kinachofaa akawa anasikiliza neno la uzima la Yesu lakini ndugu yake alikuwa anajishughulisha na mambo mengi huku akinung'unika kwamba kwanini ndugu yake hamsaidii! Yesu akamwbia unajihangaisha na mengi yasiyofaa, chagua linalofaa.

Jifunze kutoka;
Luka 10:38-42.


Unayo leo, kama ukiamini na kutii neno basi ni lazima maisha yako yabadilike. Leo moja tu ilibadili maisha ya Ibrahimu, kutoka kutokuwa na mtoto mpaka kuwa na watoto.


Leo yake moja iliharibu maisha ya Kaini kwa kumwua ndugu yake Abeli, kwa sababu ya wivu.

Leo yake moja tu ilibadili, siku ile ambayo Hawa alikula tunda la mti wa matunda ya mema na mabaya iliharibu maisha yake na kusababisha dhambi kuingia katika ulimwengu mzima.

Unaye "LEO" leo ndiyo siku yako, weka nanga yako kwa Mungu juu ya matumaini yako. Haijarishi unaubaya kiasi gani umezunguka maisha yako. Nataka nikuambie kitu, kama unaona ubaya mwingi umezunguka maisha yako basi upo uzuri mwingi pia ambao ukiuruhusu utazunguka maisha yako.


Kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na watu wengi wakafa kwa sababu ya dhambi basi hivyo hivyo kwa mtu mmoja yaani Kristo watu wengi wanaokolewa kupitia yeye. Ona wema kwenye kila kitu.

Unayo leo, leo unaiendeaje?
Je leo utatumia kama siku ya kukujenga zaidi katika maisha yako?
Je leo utafanya maamuzi ya kuharibu maisha yako?
Ama leo itakuwa ni siku yako ya kama kawaida?

Unayo leo, leo ndiyo siku yako. Siku moja tu huandika historia mpya ya maisha ya MTU, haijarishi ilichokifanya kinaleta picha gani katika jamii, maamuzi utakayochukua ndiyo yatakayoandikwa katika historia.


Leo, leo mimi nakupa kitabu bure kanisa kama unataka kununua ni sawa nami nitakushukuru kwa shukrani yoyote ile ambayo utanipa ili mradi uhitaji kitabu. Kitabu cha UKRISTO NA MAISHA, kitabu ambacho kinaweza kubadili leo yako na kuelekea katika hatua nyingine.

Leo, leo ni ya kwako.
Wewe ni zawadi Yangu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Tuma ujumbe.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, August 14, 2018

Katika Shamba La Mabomu

 Sadick Kilasi     August 14, 2018     PATA BLOGU, TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Fikiri kana kwamba upo kwenye shamba la mabomu na unahitaji kutoka katika hatari hiyo ya mauti.

Ni ukweli usiopingika, tumaini la maisha yako litakuwa na thamani kubwa sana kwa sababu  kiwango cha uhakika wa maisha yako kitakuwa ni mdogo sana. Chochote ambacho ni adimu kupatikana huwa kikuwaga na thamani kubwa sana.

Kwa wakati kama huu wa kwenye shamba la mabomu, imani kwa Mungu itakuwa ni kubwa sana. Wakati kama huu wengi huwa tunamtegemea Mungu kwa kiasi kikubwa na huwezi kujitegemea mwenyewe. Maombi yatakuwa ni ya imani na kweli na hapa ndipo mtu anaweza kukuta anamwabudu Mungu katika roho na kweli kwa sababu ya mazingira ambayo yupo kwa wakati huo. Hivi ndivyo binadamu tulivyo hukumbuka wakati tunahisi na kuona kwa macho yetu kwamba huu ni wakati wa hatari.

Lakini pia katika mazingira hayo maamuzi ambayo mtu atakua anachukua ni maamuzi yenye tahadhari ili kulinda kile ambacho yeye anaona ni kidogo ambacho amebaki nacho.

Katika shamba la mabomu, upo katikati, ukijiona unajiona wewe tu na mabomu na unahitaji kujinasua kutoka hapo, hapo ndipo mambo hayo matatu hufanywa kwa ufasaha na uzingativu mkubwa sana.

Mpendwa msomaji, inawezekana huwa unafanya hivi ukiwa na shida, vizuri maana unapaswa kweli kumtegemea Mungu  katika hali kama hii lakini nikuambie kitu hivyo si sawa, kumtemea Mungu wakati wa shida pekee hivyo si sawa. Huwezi kumtegemea Mungu kwa matukio.

Katika maisha tunapaswa kumtegemea Mungu wakati wote, usimwabudu Mungu kwa mambo ya nje ya mwili yenye mipaka ni lazima tumwabudu Mungu katika roho.

Kama tunamwabudu Mungu katika matendo ya kusubiri mipaka, yaani mpaka jambo fulani litokee basi tutakuwa wanafiki kwani kama mtu huyu yupo katika shamba la mabomu, anachothamini pale ni Mungu ama uhai wake? Si Mungu ni bora kuliko uhai wake? Maana yeye ndiye mwenye uhai wake, anaweza kuamua kuchukua wakati wote, wakati ambao upo katika shamba la mabomu au la, upo katika hali nzuri kabisa. Yesu alisema, atakaye kuokoa uhai wake naye ataupoteza na atakayepoteza uhai wake kwaajili yangu naye yatakuwa na uhai, je maneno haya si kweli?

Unajua mara nyingi sisi hatuoni kabisa na ndiomaana tumekosa shukrani na hata kama tukitoa shukrani ni ya kinafiki kwa sababu, Mungu katupigania uhai wetu kabla hatujafika kwenye shamba la mabomu, hatujashukuru, lakini mpaka pale ambapo tutashuhudia kwa macho yetu wenyewe.

Tunasahau kwamba jambo ambalo mwanadamu huthamini ni uchomvu mtupu kwani jambo lolote ambalo ni dhaifu ndilo lenye nguvu na lenye nguvu ndilo dhaifu. Na tukubaliane hapa, je! Sehemu za siri si ndizo sehemu za aibu? Je! si ndizo sehemu ambazo tunazipa thamani kubwa? Nakuuliza swali sasa, je! kitu kichovu unaweza kulipia gharama kubwa?

Mpendwa msomaji, huu ndio wakati wa kubadilika, tumwabudu Mungu katika roho na kweli, Neno linasema kesheni msilale maana kwenu hakuna giza na kulala tena. Kabisa linapaswa kubadilika sasa, ondoa mipaka kwa Mungu, Mungu ni mkamirifu. Tena linasema jifungeni dirii ya haki viunoni mwenu.

Katika maamuzi sasa, maamuzi unayofanya siku zote yawe ni upendo tu, hakikisha kila jambo unalichunguza, je! linakujenga wewe binafsi? Je! Haliwaumizi watu wengine? Wakati unafanya maamuzi juu ya watu wengine jipime mwenyewe, vipi kama ingekuwa ndo mimi hapo, ukiisha pata jibu basi ndivyo unavopaswa kumfanyia mwingine.

Mpendwa msomaji, tunaishi ndani ya wakati, tupo ndani ya shamba la mabomu wakati wote ila hatuoni tu, kwahiyo hakikisha kanuni unazotumia ukiwa ndani ya shamba la mabomu unatumia wakati wote, sio mpaka uipime hatari kwa macho yako harafu uanze kufanya maamuzi mazuri, hapana, Kila wakati ni sahihi kufanya jambo sahihi.

Hakikisha imani kwa Mungu ni wakati wote, maombi yawe mengi na rahisi. Sasa simaanishi yale maombi ya udini yale, maombi yako yawe kama mtu anayekimbia mbio ndefu yaani wakati wote, ukiwa pekee yako unaomba kwa sauti kidogo, ukiona kuna watu maombi yako ni ya ndani yaani ili mradi wakati wote uwe unashugulika, neno la Mungu lidumu daima, shukrani itawale katika maisha yako. Usiwe mtu wa kulalamika sana. Fanya kwa ubora zaidi, kwa kadili ya mazingira yako.

Asante sana, Mungu akuongoze katika hatua za maisha yako.

Kitabu cha MAISHA NA UKRISTO ni kwaajili yako, kitabu hiki ni bure kabisa. Hakikisha tunawasiliana ili nikutimie kitabu hiki. Kitabu ambacho nimeandika zaidi juu ya kushiriki utukufu wa Mungu na funguo za ufalme wa Mungu. Jipatie kitabu hiki.
 Juu ya kitabu hiki, watu wengi vitu vya bure huwa hawathamini kama nilivoeleza hapo juu, chochote ambacho kinapatikana bure huwa kinashushwa thamani lakini nataka nikwambie rafiki yangu, nimeandika kitabu hiki na kukitoa bure nikiwa ninamaana kwamba kila mmoja ambaye atakutana na ujumbe huu apate kitabu haijarishi yupo katika mazingira gani? Wengine wana pesa wengine hawana lakini katika maisha wote ni sawa na wote tunahitaji uponyaji na kufurahia maisha. Ni vema kufanya maamuzi yaliyo sahihi ukitambua kwamba wakati wote upo katika shamba la mabomu. Lengo ni kila mmoja apate kwahiyo kama ni pesa unatoa kwa kadili ya shukrani yako, yoyote ile sawa. Kila mtu anapaswa kushiriki utukufu wa Mungu.

Wewe ni zawadi yangu, hakikisha unajipatia kitabu hiki. Nitumie ujumbe whatsap au kwenye email ili nikutumie kitabu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.





Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, August 9, 2018

Namkumbuka Babu Yangu Babu Yangu Ni Shujaa Wangu.

 Sadick Kilasi     August 09, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   

Habari za wakati huu rafiki? Binafsi namshukuru Mungu kwa kunipigania wakati wote. Maana yeye huniingiza katika siku mpya kila siku na kuacha kumbukumbu zangu ili nijisome kwenye mapito yangu. Mambo yote hutukia kwa siku, na si tu bali kwa lisaa na si kwa lisaa bali dakika na si dakika na si dakika tu bali sekunde  na si sekunde tu bali hali yaani pale nilipo. Wakati huu wote mimi binafsi siwezi kujitambua matukio ambayo yanaweza kutukia ila mimi naweza kujiona tu kwamba mimi nipo. Yeye hutambua kilakitu juu yangu matukio yote, yaliyopita, yaliyopo na yatakayotukia. Mimi nipo tu yeye hunipigania. Ufunuo wa Yohana:3-7, Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. Basi nami namshukuru Mungu maana yeye ndiye anayenipigania.





Mpendwa msomaji, leo ningependa nikushirikishe kumbukumbu zangu kwa Babu yangu ambaye tayari ameshafariki miaka mingi na bado najifunza mengi kutoka kwake kutokana na kumbukumbu zangu kwake. Natumai nawe utajifunza kitu hapa. Karibu.


Namkumbuka Babu yangu, namkumbuka jinsi ambavyo alivyokuwa wa tofauti na watu wengine. Babu yangu alikuwa anaitwa Halani Kilasi, tayari Babu yangu alishafariki, amefariki miaka 17 iliyopita. Babu alikuwa ni mtu wa tofauti sana. Watu walikuwa wanamwita Babu yangu maskini. Walimbatiza jina hilo kama jina la ukweli na alipewa jina hilo kwa sababu alikuwa haoni. Babu yangu alikuwa ni kipofu. Watu walikuwa wanamwita Babu maskini lakini si kwamba Babu yangu alikuwa tufauti sana na watu wa kijijini pale hapana, walimwita maskini kwa sababu yeye alikuwa haoni. Kwa kweli anayejua uskini wa mtu kiukwelikweli ni Mungu maana yeye haangalii mambo ya mali. Mimi huwa naamini kwamba Babu yangu alikuwa mtu tajiri sana hata kama alikuwa haoni na wala hakuwa na mali lakini kwa jinsi ambavyo anaishi, aliishi maisha mazuri, maana utajiri wa mali ni kama kiungo cha mkono au kidole tu ndani mwili. Kumbukumbu La Torati 8:18, Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako. Kwahiyo mpendwa wangu rafiki, utajiri si mbaya, hapa tuelewane vizuri. Utajiri ni kama kiungo cha mwili labda kidole au mkono kwahiyo si kwamba mtu akikosa kidole au mkono hawezi kuwa na uhai. Kwahiyo Babu yangu alikuwa ni maskini wa mali na viungo lakini aliishi kama tajiri, namkumbuka sana Babu yamgu.


Namkumbuka sana Babu yangu, Babu yangu alikuwa haoni lakini Babu yangu alikuwa ni mtu mwenye imani na matumaini. Babu yangu licha ya kuwa alikuwa haoni lakini Babu yangu alikuwa mkulima mzuri sana. Babu yangu alikuwa anapenda kufanya kazi sana yeye mwenyewe. Babu aliwashangaza watu kijijini kwa sababu alikuwa analima wakati haoni. Alikuwa sio mtu wa kukata tamaa haraka, Babu alikuwa anamaarifa sana, aliandaa mianzi mirefu akawa analima kilimo cha matuta, alikuwa anautandika mwaanzi chini ikisha anafuatisha mwanzi huo katika kulima kwake. Tuta lilikuwa linapita kwenye mwanzi, yeye kazi yake ilikuwa ni kuukanyaga mwazi na kufuatisha kwenye mguu. Babu alikuwa anapendelea kilimo cha viazi vitamu. Alikuwa pia anapanda miti. Binafsi mimi nafunza mengi sana kutoka kwa Babu yangu. Babu yangu alikuwa sio mtu wa kulalamika bali yeye alikuwa ni mtu kuhamasisha. Babu alikuwa sio mtu wa kusema mimi ni kipofu, hapana, alikuwa mtu ngangali. Kama Babu angelalamika kwa kukosa macho, basi nahakika Babu ni mtu ambaye angekuwa anaabudu sanamu kwa kulalamika kwake, maana maneno ya Mungu yanasema hivi; Luka 12:34, Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako. Labda Babu angelifikiria kwamba macho yake yalikuwa ni ya muhimu kuliko mwili wake basi hazina yake ingekuwa imekufa, lakini Babu hakufikiri hivo Babu alikuwa ni mtu wa matumaini. Matumaini ya Babu ilikuwa ni uhai maana aliendelea kufanya shughuli za kawaida kama mtu ambaye anaona. 


Namkumbuka sana Babu yangu, Babu ambaye alikuwa anajua kuzungumza kingereza ambacho alifuzwa na wazungu alipokuwa kijana. Ilikuwa inashangaza Bibi yangu yaani mke waka alikuwa hajui hata kiswahili lakini Babu yangu alikuwa anajua vema kiswahili na kingereza. Lakini kwa kingereza sina uhakika kwamba alikuwa anajua vizuri maana shule aliyesoma yeye ni shule za ngumbalo tu na alipata bahati ya kufanya kazi na wazungu kabla ya wakati macho yake hayajapofuka. Namkumbuka sana Babu, Babu yangu alikuwa mbishi sana lakini nilikuwa nampenda sana kwa sababu alikuwa anapenda sana kuniuliza maswali ya kingereza. Kwa kweli Babu alikuwa nafurahia sana kuuliza watu maswali ya kingereza maana yeye alikuwa hampati mtu wa kuzungumza naye kimgereza, sasa wajukuu, nyakati za jioni, utasikia meza kwa kingereza inaitwaje? sahani kwa kingereza inaitwaje? Binafsi nilikuwa nafurahia sana maswali yake, kipindi hicho nilikuwa darasa la pili tu, nilikuwa sijui vizuri, akiniambia naenda kutambishia watu, Kwa kweli, ninahisi Babu yangu yupo japo alikufa miaka 17 iliyopita. Nawakumbuka sana Bibi na Babu, walikuwa wanabishana sana, Babu yangu licha ya kuwa ni kipofu lakini alikuwa hataki kushindwa. Bibi alikuwa hajui hata kuongea kiswahili, yaani kiswahili chake kukielewa bora usikilize kingereza. Lakini Babu yangu alikuwa anajua kuongea kiswahili na kingereza na alikuwa akipata fursa ya kuonana na mtu anayejua lugha hizo alikuwa anapenda sana kuongea naye. Ndipo huwa nakumbuka mstari mmoja kwenye; Waebrania 13:10-15, Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kura vitu vyake. Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi. Kwa ajili ya Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi tukichukua shutumu lake. Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twatafuta ule ujao. Basi kwa njia yake yeye, tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. Basi hapa nawaza mimi mwenyewe, labda Babu yangu alikuwa anawapenda sana watu ambao wapo tayari kuzungumza naye kingereza na kujisemea moyoni mwake, Mungu asante kwa kuniletea mjukuu wangu ambaye kidogo anajua kingereza. Basi hapa tumejifunza swala la upendo. Ukiwa nacho unamhitaji asiye nacho. Anayepanda na anayekuza wote ni sawa.  1Wakorintho 13:1, Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao.


Namkumbuka sana Bibi na Babu yangu, Bibi yangu alikuwa anapenda sana kuimba nyimbo za kilugha za kanisani. Basi kila nikienda kuwatembelea nilikuwa najisikia vibaya wakati wa kwenda kulala maana wao wakuwa wanalala mapema sana, chakula cha jioni kilikuwa kinaliwa saa 12 jioni na kulala saa moja. Jua linapozama nasisi tulikuwa tunaenda kulala, mimi nilikuwa sipendi alikini milikuwa nafarijiwa na nyimbo za Bibi na Babu, nyimbo za kilugha, nakumbuka sana. Bibi yangu alikuwa anaanzisha na Babu yeye ni kuitikia, walikuwa wanapendana sana, nyakati zote mambo yalikuwa shwari. Walishirikiana kwa pamoja kuimba, Babu alimsapoti Bibi kwenye kipawa chake cha kuimba. Neno la Mungu linasema; 1Wakorintho 11:11, Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana. Basi utofauti wa sauti zao ulileta ladha kwelikweli na ubora wa nyimbo, walikuwa vuzuri sana. Nilijikuta nalala na wao wakiendeleza songi zao.


Nawakumbuka wazungu ambao waliwahi kuja kumtembelea Babu yangu, maana walisikia habari kwamba kuna kipofu jina lake maskini ni mkulima na hushika jembe mwenyewe. Walipo kuja walisema huyusio maskini. Kwa sababu anashughulika kwa sehemu yake huyu si maskini, nakumbuka sana. Babu alikuwa kipofu lakini alikuwa mtu wa tofauti sana. Babu yangu ni shujaa wangu. Namkumbuka siku moja alinambia niende kulinda shamba kware wasifukue mbegu za mahindi yanayoota mimi nikaenda kucheza, akamtumia jamaa moja ambaye alikuwa jilani anishike ili aniadhibu, akanishika, yeye Babu alinishika mkono aanza kunifinya. Babu yangu alikuwa mtu wa matumani alifanya kitu ambacho anapaswa kufanya, hakuwa mtu wa kulalamika kama wana Waisraeli walivolalamika kule jangwani na kugongwa na nyoka, alikuwa na matumaini. Kutoka 17:3, Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? Babu hajawahi kulalamika kwa sababu ya macho yake aliishi tu kama mtu wa kawaida, hakusema Mungu! macho yangu ya zamani yako wapi? sijawahi kumsikia, aliishi tu kama mtu wa kawaida. Babu yangu ni shujaa wangu.


Mpendwa msomaji, nimempa sifa nyingi Babu yangu, nimesema hajawahi kulalamika lakini mimi sijui maana mimi nimezaliwa nikimkuta Babu yangu ni kipofu kwahiyo, sijui mengine, naye alikuwa  binadamu kama sisi ana udhaifu wake lakini mimi nachukua mazuri yake tu, ona wema usine ubaya. Mwanzo 1:4, Mungu akaiona nuru, yakuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Namkumbuka sana Babu yangu, BABU YANGU NI SHUJAA WANGU.


Asante sana kwa kushiriki kumbukumbu zangu, hayo ni machache tu ambayo nimekushirikisha yapo mengi Babu yangu aliyafanya. Natumai umejifunza kitu. Mistari ya Biblia ambayo nimetumia basi nataka ujifunze kitu juu ya hilo.  usisahau kujipatia  kitabu cha bure cha UKRISTO NA MAISHA. NItumie ujumbe whatsapp au email nikutumie kitabu.


Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, August 8, 2018

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

 Sadick Kilasi     August 08, 2018     NJOZI     No comments   



Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni upendo.

Mambo haya matatu yanapaswa kudumu katika maisha ya mtu yeyote ambaye anapumua. Ukikosa tumaini huna unakokwenda. Ndoto au tumaini ndiyo picha ambayo kila mtu huwa anajijengea katika fikra zake kwamba lazima ipo siku atafika anakotaka kufika.

Imani ndio siraha ya misukosuko. Wote ambao wanamwamini Mungu hutumia nguvu za Mungu katika changamoto zao za maisha. Mungu anataka kila mtu ambaye anamwamini atumie vizuri nguvu zake katika safari ya maisha. Tukitambua haki yetu katika Mungu, basi imani yetu inakuwa na nguvu kubwa sana kwa sababu yeye Mungu hutupigania tu nasi kazi yetu ni kuamini.

Upendo ndio mapito yetu ya kila siku, upendo ni maamuzi yetu tunayofanya kwetu sisi wenyewe na kwa wengine pia. Upendo unasimama katika maamuzi madogomadogo ambayo tunayachukua wakati tunaelekea kwenye tumaini letu.

Mpendwa msomaji, kila mtu anatumaini lakini wapo watu ambao walipambania haki yao na kulifikia tumaini lao, japokuwa mambo yalikuwa magumu. Na ili imani ifanye kazi lazima mambo yawe magumu. Maana imani inafanyakazi penye ugumu.

Katika Biblia yupo mtu anaitwa Bartimayo. Mtu huyu alikuwa kipofu na ni ombaomba lakini bado alikuwa na tumaini.

Jifunze kutoka;
Marko 10:46-52.

Mtu huyu hakupoteza haki yake ya kutaka kupona, licha ya kuwa ombaomba lakini tumaini lake kuu lilikuwa ni kuona.  Wakati Yesu alipokuwa akipita aliuliza kunanini? Watu wakamwambia Yesu anapita hapa; Ndipo Bartimayo aliona fursa na kupaza sauti akitaka kuponywa. Watu walimzuia lakini yeye alikuwa king'ang'anizi, aling'ang'ania tumaini lake, yeye alichokuwa anataka ni kuona licha ya watu kumzua alitambua kwamba wenda wakati huu ukipita sitoona tena labda tumaini langu litapotea. Ndipo alipojitoa kwa nguvu, akatupa vazi lake huko, nakupaza sauti naomba uniponye Mwana wa Daudi, ndipo Yesu akamwambia unataka nikufanyie nini? Bartimayo hakusita kuonyesha haja yake, nataka kuona tena, basi akaponywa.

Mpendwa rafiki, unaweza kusema kwamba labda Bartimayo aliponywa kwa sababu Yesu alikuwa anapita mahali pale lakini nataka nikwambie, Bartimayo alikuwa na ndoto za kuona tena na ndiomaana hakusita kuonyesha anachotaka, kwa sababu ni ombaomba labda kama angekuwa hana tumaini angeomba hata pesa. Tumaini la Bartimayo ni kuona na aliona.

Zakayo mtu mfupi, tumaini lake ni kumwona Yesu. Alifanya kila jitihada mpaka kumwona kwa kupanda juu ya mti. Yesu akamwambia leo nitakuja nyumbani kwako. Alipata na ziada, aliomwona vizuri zaidi.

Jifunze kutoka;
Luka 19:1-10.

SOMA:ONA WEMA KWENYE KILA JAMBO.

Mpendwa rafiki, yawezekana unatumaini sasa weka tumaini lao katika imani kwa Mungu, ishi kwa upendo, hakuna jambo linalomshinda yeye.

Kama bado huna tumaini lolote unapaswa kuwa na tumaini, maana wewe utakuwa mtu ambaye unatembea huku umekufa. Tumaini ndio uhai wa MTU, tumaini ndilo linafanya unajongea. Je, ushawahi kuona maji ambayo hayatembei yanafaa kwa lolote? Huwa yanakuwa yameoza na hayafai kitu. Maji yenye ladha ni yale ambayo hutiririka na mwisho wake ni baharini. Yakifika baharini hayafai kitu.

Kama unatumaini la kuishi maisha ya furaha ndani ya uwepo wa Mungu, kipo kitabu kwaajili yako. Kitabu hiki ni bure kabisa, nitumie ujumbe nikutumie kitabu hiki. Mpoke Bwana Yesu kuwa kiongozi wa maisha yako. Tumaini lenye nguvu.  Jipatie kitabu hichi, UKRISTO NA MAISHA. Nitumie ujumbe nikutumie kitabu bure kabisa.

KUWA NA TUMAINI, tumaini ndiyo uhai wa mtu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, August 7, 2018

Ona Wema Kwenye Kila Jambo.

 Sadick Kilasi     August 07, 2018     KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO     No comments   



Ona wema kwenye kila jambo. Upendo ni kuona wema kwenye kila jambo. Uvumilivu ni kuona wema kwenye kila jambo. Shukrani ni kuona wema kwenye kila jambo.

Haijarishi upo katika hali gani, Ona wema kwenye kila jambo. Haijarishi umeumizwa kiasi gani, Ona wema kwenye kila jambo.

Mwanzo wa hekima ni kuona wema kwenye kila jambo. Uumbaji wa dunia ulianza pale ambapo Mungu aliona wema katika giza. Ona wema kwenye kila jambo.

Furaha ya kweli ni kuona wema kwenye kila jambo.Watu waliofanikiwa waliona wema kwenye kila jambo.

Mpendwa msomaji, kwanini uumizwe na mapito yako. Kwanini uwe mtu wa kukosa furaha? Kwanini furaha yako itegemee vitu? Chagua wema usichague wema na ubaya.

Hawa aliacha mti wa matunda ya uzima akachagua mti wa mema na mabaya. Lakini wewe umelijua hilo, sasa chagua wema kwenye kila jambo haijarishi zuri au baya.

Mwanadamu alipoteza utu na wema  akaanza kuzingatia mema na mabaya lakini Mungu kaleta ukombozi wa kurudi katika mti ule wa matunda mema.

Jifunze kutoka:
Mwanzo 1:1-4...

SOMA:JE! UNATAKA KUWA BINGWA WA KUWASAMEHE WATU?

Yeyote yule anaweza kurudisha furaha yake ya kuona wema kwenye kila jambo.

Nimeandika KITABU CHA MAISHA NA UKRISTO. Kwenye kitabu hiki nimeweka waziwazi funguo za (Ufalme wa Mungu), Hekima Ya Mungu na kitabu hiki bei yake ni kuanzia bure hadi kitu chochote ambacho unaweza kutoa hata kama shukrani kwangu mimi inanitosha. Kikubwa ni wewe kukisoma kitabu hiki. Jipatie kitabu hiki sasa kwa kuwaailiana nami.

Ona wema kwenye kila jambo.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot. com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, August 3, 2018

Je Unataka Kuwa Bingwa Wa Kuwasamehe Watu?

 Sadick Kilasi     August 03, 2018     KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO     No comments   



Swali langu kwako wewe rafiki yangu na ndugu yangu, je unampango wa kuwa bingwa wa kuwa mtu wa kusamehe watu?

Ikiwa una mpango huu basi leo naomba nikuongezee mbinu ya kuwa na maisha ya msamaha kwa kila unalolipitia, haijarishi unapitia katika hali gani? Haijarishi nani kakuumiza? Haijarishi umejiumiza kiasi gani? Utasamehe.

Na mbinu yenyewe ni kusamehe kabla ya kukosewa. Ndio, unapaswa kusamehe kabla ya kukosewa.

Mtu ambaye hutoa msamaha wa ukweli ni yule ambaye hutoa msamaha kabla ya kukosewa. Ikiwa hujasamehe kabla ya kukosewa hivi utakuwa umesamehe kweli?

SOMA:Injili Ya Maji Na Roho (SEHEMU YA PILI).


Kwa yeyote ambaye anamwamini Mungu na anasoma neno la Mungu nadhani unatambua kwamba, Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae ili kila mtu amwaminiye apate kuokolewa. Ni wazi na ni kweli kwamba miaka 2000 iliyopita hakuna mtu ambaye alikuwa amezaliwa tayari, tulisamehewa kabla hatujazaliwa, leo hii, kama umezaliwa upya nadhani unaamini thamani ya msamaha ambao Mungu alitusamehe kabla hata hatujazaliwa japo watu wanaoishi kwa tabia za itikadi kali za kidini huwaambia watu waombe toba, kumbe ni swala la kupokea msamaha ambao Mungu tayari ambao alisha umwaga kwetu, msamaha wa ukweli.

Hivi ndiyo ambavyo tunapaswa kuishi, samehe kabla ya kukosewa, tambua kwamba binadamu anamapungufu, kila mtu anamzigo ambao ameubeba, tunatumia lugha ambayo si uhalia wa mambo tunayofanya, tunaishi kwenye vivuli vya ukweli, ukweli ambao si ukweli halisi, kila mtu anamatatizo au mabaya yaliyolala, uwepo wako unaamsha yaliyolala. Samehe kabla ya kukosewa, tambua haya yote watu tunaishi nayo.

Kama mpango wako ni kuanza kufurahia maisha, anza kumwaga misama, kusamehe mwenyewe, jielewe kabisa kwamba wewe hujakamilika. Samehe kabla ya kukosewa.

Wewe ambaye upo kama tai, mwenye majivuno hutaki kusamehe jiandae kwa maumivu. Maana mtu ambaye huenda tu, hana utofauti na aliyesimama. Msafiri lazima atoke na kurudi. Samehe ili usamehewe. Anaye Samehe amejisamehe. Asiyesamehe hajajisamehe mwenyewe.

Je wewe huishi katika msingi wa msamaha yaani umeokolewa kwa injili ya maji na Roho? Msingi wetu wa kusamehe ni pale tuliposamehewa, hekima ya Mungu, Kristo Yesu, ndiyo tunayoishi maana hakuna anayeweza kusamehe kama hujawahi kusamehewa ila kwetu ni Mungu mwenyewe.

Rafiki yangu, kwa yeyote inamhusu kama hujazaliwa upya na kupokea hekima ya Mungu basi unapaswa kuipokea. Hapa sizungumzii dini ila kuishi maisha yenye maana yaliyojaa furaha na hekima ya Mungu maana Ukristo sio dini kama wengi wanavyodhani bali ni maisha. Ila watu wamefanya Ukristo kuwa dini. Wewe rafiki unapaswa kufurahia maisha na ndiomaana nimeandika kitabu cha MAISHA NA UKRISTO, jipatie kitabu hiki bure kabisa. Nitumie ujumbe nikutumie kitabu hichi kwenye simu yako.

Samehe kabla ya kukosewa.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ▼  August (7)
      • Nguvu Mbili Ambazo Hutawala Katika Ulimwengu Huu.
      • Kama Unayo Leo.
      • Katika Shamba La Mabomu
      • Namkumbuka Babu Yangu Babu Yangu Ni Shujaa Wangu.
      • Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.
      • Ona Wema Kwenye Kila Jambo.
      • Je Unataka Kuwa Bingwa Wa Kuwasamehe Watu?
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates