Mara nyingi kumekuwa na watu wengi ambao hujisikia upweke na kuona kama wananyanyapaliwa na wengine, watu hawa huwa wanajitenga kabisa na wengine na wengine hujaribu kutengeneza mahusiano na watu wao wa karibu lakini huona kama bado watu hao hawaoneshi ushirikiano mzuri kwake.
Lakini wakati mwingine yaweza ikawa watu wanakutenga kwa sababu fulani ambazo wewe mwenyewe unaonesha na kuzifanya na ndiomana wanajaribu kujitenga na wewe, lakini rafiki yangu kama wewe unataka kutengeneza mahusiano mazuri na watu wako wa karibu, ndugu pamoja na marafiki ili upendwe fanya mambo haya manne yatakusaidia kujenga mahusiano mazuri.
1.Tengeneza mahusiano mazuri na watu. hakikisha unatengeneza mahusiano mazuri na watu wote bila kujari ni ndugu yako ama rafiki yako au mtu yeyote wa karibu tengeneza mahusiano kwa kuwafanyia mambo mazuri na hakikisha huwakeli.
2.Wanapo ongea watu sikiliza kwa makini kwa lengo la kutaka kuelewa sio kubishana. Mtu mbishi sikuzote hapendwi kwa ubishi huleta mashindano yasiyo na maana. Wasikilize watu wanapo ongea ili kuongeza maarifa na sio kuongea sana.
3.Wasaidie wengine kufanya kazi wakati ambao wameelemewa na wanahitaji msaada. Ndio wasaidie watu mizigo yao hiyo itakusaidia kujenga mahusiano mazuri zaidi baada ya wewe kuonyesha kwamba unawajari wao.
4.Yajue majina ya watu wako wa karibu na uwaite kwa majina yao. Unapokuwa unawaita kwa majina yao wao wanakuwa wanajisikia vizuri na kuona kwamba kumbe unawafahamu na kuwajari.
Watu wanao kuzunguka ni ngazi yako ya kuyafikia mafanikio makubwa kwahiyo hakikisha unajenga mahusiano mazuri na watu wako wa karibu ili kuyafikia mafanikio. Mahusiano ni moja kati ya mafanikio katika maisha, ukifaulu hapa basi tayari umeyafikia mafanikio ya mahusiano.
Karibu na uendelee kujifunza kupitia blogu hii ili kujifunza zaidi. Kupata blogu tuma ujumbe whatsap 068700768 au 0659639168 jipatie blogu yako sasa.
Wako Sadick Kilasi.
0 comments:
Post a Comment