JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, September 26, 2017

Hofu kubwa ulionayo inasababishwa na mambo haya

 Sadick Kilasi     September 26, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni ukweli usio pingika hofu ni kitu ambacho kinawasumbua watu wengi kwa kiasi kikubwa. Hofu ikikutawala inakufanya ushindwe kufanya jambo lako kwa usahihi lakini inaweza ikakufanya ufanye jambo lako kwa umakini mkubwa.

Wakati hofu inajitokeza kwa kawaida huwa kuna jambo ambalo linatakiwa kukamirishwa na ukisha kamirisha jambo hilo basi tayari hofu yote itakutoka. Mara nyingi vitu ambavyo huna uhakika navyo huwa vinasababisha hofu.

Unapotaka kufanya jambo ambalo ni sahihi basi hapo hofu hujitokeza na kukupinga na kukuonyesha kwamba lile jambo si sahihi.

Hofu huongezeka pale mtu unapotaka kujua ukweli, yenyewe husimama na kukufanya kuwa na wasiwasi na matokeo ya jambo hilo litakua kweli au uongo?

Unapotaka maisha ambaayo ni ya kweli ndani yako basi hofu hujitokeza. Unapotaka kujua kilicho chako basi hofu hujengeka, wakati unapotaka kujua kipaji chako basi hofu inajitokeza na kuona kwamba huwezi.

Niliwahi kusoma mahala moja paliandikwa huwezi kuikimbia hofu, njia pekee yni kuishinda kwa kufanya. Kwahiyo rafiki yangu njia pekee ya kuishinda hofu ni kufanya jambo linalokupa hofu.

Endelea kutembelea mtandao huu wa JIKO LA USHAURI ili kujifunza zaidi na kuyafikia mafanikio makubwa.

Kupata blogu tuwasiliane kwa 068700768 tuma ujumbe whatsap nitakujibu.
Wako Sadick Kilasi.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, September 25, 2017

Namna ya kuweka template kwenye blogu yako

 Sadick Kilasi     September 25, 2017     BIASHARA, USHAURI     No comments   

Uhali gani mpendwa msomaji wa blogu yetu ya JIKO LA USHAURI? Natumai umuzima na unaendelea vizuri. Hongera kwako kwa siku nyingine ya leo na nakuarika leo katika mafunzo ya leo ya jinsi ya kuupload template kwenye blogu yako.

Template ni nini hasa? Template ni mwonekano wa blogu na mpangilio wa makala katika blogu yako.

Kwa kawaida blogu za blogger huwa zinakuwa na template za bure na zinazouzwa. Wakati unafungua blogu yako huwa kunakuwaga na template ambazo huwa zipo hapohapo ambazo hazihitaji kudownloudiwa wala kununuliwa. Template hizi huwa zinakuwaga hazina mwonekano mzuri sana.

Kama wewe upo makini na biashara yako lazima utahitaji template ambazo ni nzuri na zenye mwonekano mzuri unao vutia.

hizi ndizo hatua kwa hatua namana ya kuweka template kwenye blogu ya blogger kama hii ya jikolaushauri.bogspot.com. Nifatilie hatua kwa hatua ili uwe na uwezo wa kuweka template kwenye blogu yako.

1.Kwanza fungua browser yako kisha search xml template

2.Kisha baada ya hapo anza kutafuta zilizoandikwa free blo template.

3.Kisha baada ya hapo tafuta na uichague template unayotaka kisha ichague.

4.Mara baada ya hapo bonyeza mahala palipoandikwa [view demo] ili kuichulia

5. Kama umelidhishwa na teplate hiyo basi bonyeza mahali palipoandikwa download

6. Mara baada ya hapo hifadhi faili la hilo

7.Mara baada y a hapo kungua hilo faili

8.Ikifunguka faili tafuta faili lililo na mwisho huu  [xml]

9.Ikisha likopy na liweke kwenye desktop

10.Ikisha baada ya hapo log in kwenye blogu yako na fungua dashboard ya blogu yako.

11.Baada ya hapo shuka mpaka chini palipoandikwa theme na ufungue

12.Kisha uchague kitufe cha BACKUP/RESTORE kipo juu kabisa

13.Baada ya hapo itakuja window yenye option tatu unachotakiwa kufanya ni kubonyeza mandishi yaliyoandikwa CHOOOSE FILE

14.Baada ya hapo itakuja window ya kuchagua mafile kinachotakiwa kufanya ni kuchagua location sahihi na uchague file lilile la xml

15.Baada ya hapo upload file lako ns kisha savechange.

Kwa mchakato huo basi tayari utakua umesha badili templte yako kwenye blogu yako. Kama unataka kuangalia mabadiliko yako bonyeza sehemu iliyoandikwa VIEW MY BLOGili kuona.

Mpendwa msomaji blogu ni kitu cha muhimu sana hasa kwa kipindi hichi cha mapinduzi ya internet.
Kama wewe unafanya biashara yoyote ili na hauna blogu sawa sawa na kufungia biashara yako chumbani kwako.

 Kupata blogu tuwasiliane kwa 068700768 tuma ujumbe whatsap nitakujibu.
Wako Sadick Kilasi
sadikila65@gmail.com

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, September 24, 2017

Mbona yote hayo ni ubatili mtupu

 Sadick Kilasi     September 24, 2017     BIASHARA, MAHUSIANO, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili mtupu, mtu ana faida gani ya kazi yake anayoifanya chini ya jua? Kizazi huenda kizazi huja ; nayo dunia hudumu  daima. Jua lachomoza, na jua lashuka na kufanya haraka mahala pa mawio yake.

Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazini; hugeuka daima katika mwendo wake na upepo huyarudia mazunguko yake. Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai, huko iendako mito ndiko irudiko tena.

Mambo yote yamejaa uchovu usionekana, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.

Mambo yote unayotaka kukimbizananayo hayo yote ni ubatili mtupu, kila toleo la simu likitoka wewe unataka kununua ubatili mtupi, kila fashion ya nguo ikitaka kutoka unaitaka ubatili mtupu, kila toleo la gari likitoka unalitaka ubatili mtupu, ubatili mtupu, ubatili mtupu.

Kwanini dunia inakupelekapeka peleka huku na kule kijana mwenzangu, mambo yote yamejaa uchovu mtupu, tamaa ya mwili inakupeleka wapi? Yote hayo ni ubatili mtupu.

Yaliyo kuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo hakuna tena chini ya jua. Je? kuna jambo lolote ambalo watu husema juu yake, tazama hili ni jambo jipya chini ya jua? Limesha kuwako tangu zamani za kale zilizo kuwa kabla yetu sisi.

Kijana mwenzangu kwanini unakimbizana na upepo vyote hivi vipya vilikuwapo, vipo na vitakuwepo. Jiwekee misingi katika maisha yako wacha kukimbizana na mambo ya dunia hii.
         Kutoka MUHUBIRI 1 kwenye kitabu cha Biblia.

Endelea kutembelea blogu hii JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, September 23, 2017

Jiulize maswali haya manne yatakupa majibu ya maisha yako yote.

 Sadick Kilasi     September 23, 2017     BIASHARA, UJASIRIAMALI     No comments   

Mara nyingi sana watu wamekua wanajiuliza namna gani nitayafikia mafanikio makubwa katika maisha. Maswali mengi sana wamekua wanajiuliza ili kujua vipawa vyao na mengine mengi lakini hakuna majibu wanayo pata.

Kama wewe unataka mafanikio yapo maswali kwanza lazima ujiulize ambayo ni ya muhimu sana na yatakupa majibu yote kuhusu maisha yako. Haya maswali utajiuliza kila siku ya kuweka misingi na malengo yako ambayo yatakupa majibu yote.

Kwenye maisha yako ushawahi kujiuliza wewe ni nani? Lazima ujiulize wewe ni nani na hapo ndipo utakapo pata majibu. Majibu utakayopata ndiyo yatakayokupa namna ya kuweka misingi na malengo yako katika safari yako ya maisha.

Swali la pili jiulize nimetoka wapi? Swali hili litakupa majibu wewe upo katika nafasi gani katika maisha na katika jamii inayokuzunguka majibu yafanyie kazi.

Jiulize swali la tatu uko wapi? Lazima ujiulize uko wapi katika safari yako ya maisha umefikia wapi na unapaswa kufanya nini ili kufikia ndoto zako.

Swali la tatu jiulize wewe unaelekea wapi? hili swali litakupa majibu ya mwelekeo wako. Kuna usemi unasema kamahujui unakoelekea lazima utapotea tu, kwahiyo tambua dira yako unako kuelekeza uelekee uelekeo huo.

Maswali haya manne ni muhimu kujiuliza kila siku yatakupa majibu yote lazima ujiwekee kanuni yakujiuluza kila siku na hapo ndipo utakapo jenga misingi yako ya mafanikio kwa kila sehemu ya maisha yako.

Endelea kujifunza kupitia blogu yetu ya JIKO LA USHAURI, blogu ambayo inakupa misingi ya mafanikio katika maisha. Ili kupata blogu tuwasiliane kwa 068700768 nitumie ujumbe nitakujibu.
Wako Sadick Kilasi.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, September 22, 2017

Hii ndio misingi minne ya mafanikio, ukitumia misingi hii lazima utafanikiwa.

 Sadick Kilasi     September 22, 2017     BIASHARA, KUPATA BLOGU, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ipo misingi minne ya kufuata na kuifanya ili ufanikiwe, nje na hapo lazima utafeli na hutofikia kilele cha mafanikio  katika safari yako ya mafanikio. Karibu tuangalie misingi hii ya mafanikio moja baada ya nyingine japo leo sipendi kuongea sana.

Msingi wa kwanza lazima ufanye kazi kwa bidii. Ndio lazima uwekeze nguvu kazi kwa kiasi kikubwa, hapa lazima ufanye kazi yako vizuri na yenye ubora mzuri, jali mda wako vizuri bila kupoteza hata sekunde moja.

Waheshimu watu. Lazima uwahemu watu wa kila rika wakubwa na wadogo ili wawe wanavutiwa na wewe. Ukiwaheshimu watu lazima watakupa nafasi ya kufanikiwa na watakuamini katika biashara yako au ajira yako, washimu mabosi wako au wateja wako.

Matumizi mazuri ya kipato. Lazima uwe na matumizi ya kipato chako, lazima uwe na mpango mzuri wa kukigawa kipato chako.

Mwombe mwenyezi Mungu ili azidi kukupa mafanikio. Usisahau kumwomba mwenyezi Mungu kwa kila jambo unalofanya, ukimtanguliza Mwenyezi Mungu lazima utafanikiwa kwa jambo lolote lile unalofanya.

Hizo ndizo kanuni kuu za mafanikio, misingi hii ukiitanguliza kwenye safari yako lazima utafanikiwa. Tii kanuni za mafanikio lazima utafanikiwa.

Patablogu yako sasa iliutengeneze kipato kupitia blogu, tuma ujumbe whatsap 068700768. Ongeza dhamani yako na kipato chako sasa.
Wako Sadick Kilasi.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, September 21, 2017

Kwanini unaacha ushahidi wako unapotea bila sababu? Weka ushahidi wako hapa hauta potea kamwe.

 Sadick Kilasi     September 21, 2017     BIASHARA, KUPATA BLOGU, NJOZI, PATA BLOGU, USHAURI     No comments   

Katika vipindi ambavyo watu wanaandika sana basi zama hizi za mapinduzi ya internet watu wanaandika sana. Kuwepo kwa mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, whatsap, tango, istagram na mingineyo imesababisha na kuwapa ulahisi wa kuandika na kupost video na picha mbalimbali.

Lakini uandishi wa kwenye mitandao ya kijamii umekuwa hauna mfumo mzuri wa kuhifadhi maandishi, mtu anaweza kuandika leo halafu kesho asijue aliandika nini kutokana na uandishi usio na mpangilio. Watu wamekua wakishindwa kutengeneza jukwaa vizuri kwenye mitandao ya kijamii kutokana na mwingiliano wa watu wengi.

Sasa rafiki yangu ushahidi unao acha unapotea bure, weka ushahidi wako mahala salama. Yaani hayo maandishi mazuri unayoandika kwaajiri ya marafiki zako yanapotea bure baadae utaonekana kama hujawahi kuandika, na marafiki zako pia hawakujui nyumbani kwako wapeleke kwako hapo kwenye mitandao ya kijamii ni sehemu tuu ya kupigia sog tu [kijiwe], sasa wapeleke kwako wapajue.

Kivipi? kuwa na BLOGU, ambako kutakuwa ndo nyumbani kwako harafu kijiweni kwenye mitandao ya kijamii. Miliki blogu yako kama hii ambayo utatumia kuandika na kufanya maandishi yako kuwa salama na yenye mpangilio mzuri. Blogu hiyo itakuwa ni yako ambayo utakua unaandika kila siku na kuwaarika marafiki wakutembelee kwako kwenye blogu yako.

Faida za blogu;
1.Unapata wateja kiurahisi kutokana na shughuli unayofanya.
2.Utatangaza biashara yako kwa bei nafuu
3.Utawaliwaza watembeleaji wa blogu yako wakati fulani wakiwa hawana mambo ya kufanya watatembelea na kujifunza kwenye blogu yako.
4.Blandi yako ni rahisi kukumbukwa na watembeleaji wako tofauti na kwenye mitandao ya kijamii.

Hizo ni moja ya sababu chache kati ya nyingi kwanini wewe uwe na blogu yako. Acha alama mahali sahihi  na blogu ndo mahali sahihi pa kuandika wewe rafiki yangu.

Kupata blogu tuwasiliane kwa kutuma ujumbe whatsapp 068700768 au piga 0659639168.
Wako Sadick Kilasi.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, September 20, 2017

Fanya mambo haya manne ili hujenga mahusiano bora na watu wanao kuzunguka ili kufikia mafanikio

 Sadick Kilasi     September 20, 2017     BIASHARA, MAHUSIANO, NJOZI, USHAURI     No comments   

U hali gani mpendwa rafiki msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, katika makala,hii ya leo ambayo mimi rafiki yako nimeona nikushirikishe swala zima la mahusiano kati ya wewe rafiki yangu na jamii inayokuzunguka. Naomba tusafiri kwa pamoja ili tujifunze makala hii ya leo na tuweze kufikia mafanikio makubwa.

Mara nyingi kumekuwa na watu wengi ambao hujisikia upweke na kuona kama wananyanyapaliwa na wengine, watu hawa huwa wanajitenga kabisa na wengine na wengine hujaribu kutengeneza mahusiano na watu wao wa karibu lakini huona kama bado watu hao hawaoneshi ushirikiano mzuri kwake.

Lakini wakati mwingine yaweza ikawa watu wanakutenga kwa sababu fulani ambazo wewe mwenyewe unaonesha na kuzifanya na ndiomana wanajaribu kujitenga na wewe, lakini rafiki yangu kama wewe  unataka kutengeneza mahusiano mazuri na watu wako wa karibu, ndugu pamoja na marafiki ili upendwe fanya mambo haya manne yatakusaidia kujenga mahusiano mazuri.

1.Tengeneza mahusiano mazuri na watu. hakikisha unatengeneza mahusiano mazuri na watu wote bila kujari ni ndugu yako ama rafiki yako au mtu yeyote wa karibu tengeneza mahusiano kwa kuwafanyia mambo mazuri na hakikisha huwakeli.

2.Wanapo ongea watu sikiliza kwa makini kwa lengo la kutaka kuelewa sio kubishana. Mtu mbishi sikuzote hapendwi kwa ubishi huleta mashindano yasiyo na maana. Wasikilize watu wanapo ongea ili kuongeza maarifa na sio kuongea sana.

3.Wasaidie wengine kufanya kazi wakati ambao wameelemewa na wanahitaji msaada. Ndio wasaidie watu mizigo yao hiyo itakusaidia kujenga mahusiano mazuri zaidi baada ya wewe kuonyesha kwamba unawajari wao.

4.Yajue majina ya watu wako wa karibu na uwaite kwa majina yao. Unapokuwa unawaita kwa majina yao wao wanakuwa wanajisikia vizuri na kuona kwamba kumbe unawafahamu na kuwajari.

Watu wanao kuzunguka ni ngazi yako ya kuyafikia mafanikio makubwa kwahiyo hakikisha unajenga mahusiano mazuri na watu wako wa karibu ili kuyafikia mafanikio. Mahusiano ni moja kati ya mafanikio katika maisha, ukifaulu hapa basi tayari umeyafikia mafanikio ya mahusiano.

Karibu na uendelee kujifunza kupitia blogu hii ili kujifunza zaidi. Kupata blogu tuma ujumbe whatsap 068700768 au 0659639168 jipatie blogu yako sasa.
Wako Sadick Kilasi.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, September 19, 2017

Kama huna mtaji hii ndio biashara nzuri ya kufanya [biashara ya mtandao]

 Sadick Kilasi     September 19, 2017     UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ipo mifumo mingi sana ya biashara, lakini watu wengi wanautambua mfumo mmoja ambao ni wa uchuuzi. Kwenye mfumo wa uchuuzi mtu ananunua kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu zaidi ili apate faida. Biashara hii ni ya kawaida, kila mmmoja anatambua. Mfumo huu umeanza kutumika toka enzi na enze za mababu zetu wa kale.

Lakini dunia inabadirika, sasa hivi kuna mifumo mingi ya biashara. Biashara ya mtandao [NETWORK MARKETING] ni mfumo wa biashara ambao ulianza miaka mingi kidogo huko lakini kwa nchi zetu mfumo huu wa biashara haujulikani sana na haujashamiri kwa kiasi kikubwa.

Kuwepo kwa biashara hii ya network marketing yaani biashara ya mtandao wengi huzani hii ni biashara ya mtandao wa simu na wengine huwa na mitazamo tofauti na kusema biashara ya mafreemason na ndio maana nimeamua niandike makala hii ili kukupa maana halisi ya biashara ya mtandao.

Biashara ya mtandao ni biashara ambayo inatumia mfumo wa bidhaa kutoka kiwandani na kwenda kumlenga mteja moja kwa moja kwa kupitia stoo tu ambako bidhaa huhifadhiwa. Inaitwa biashara ya mtandao kwa sababu mteja anaponunua bidhaa ili kutatua matatizo yake anaambiwa awaambie na wengine wanunue ile bidhaa na atalipwa kamisheni yake kutokana na kununua ile bidhaa na watu aliowaarika wanunue ile bidhaa, ila atafanya hivo endapo atafurahishwa na huduma yao na bidhaa ilivyomsaidia.

Biashara hii ni nzuri sana kwa wale ambao hawana uwezo wa kuanza biashara kwa mtaji na pango la biashara. Mara nyingi kiingilio cha kujiunga huwa kinatofautiana kampuni na kampuni zingine huwa inakuwa bure au kiasi kidogo sana.

Biashara hii ni nzuri sana maana unaingiza kipato masaa 24 na huhitaji kulipia pango wala mtaji wa biashara lakini pia uzuri wake ni kufanya kazi mda mdogo na kipato chake ni endelevu kisicho na kikomo, kikubwa ni kuwaambia watu jinsi bidhaa ulio tumia ilivyokusaidia ili nao watatue changamoto zao zinazofanana na yako.

Lakini pamoja na uzuri wa biashara hii kuna changamoto zake ambazo huwa ni uchaguzi wa kampuni, ipi ina kamisheni nzuri na pia kumekuwepo na makampuni ya kitapeli ambayo yanajificha chini ya biashara hii ya mtandao ili kutapeli watu. Kuna namna ya kujua ipi ni kampuni sahihi na ipi ya kitapeli.

Rafiki yangu kama wewe upo kwenye biashara hii na unataka kukuza biashara yako tuwasiliane au kama unataka kuanza biashara hii tuwasiliane pia.

Kama umefurahishwa na makala hii unaweza kutoa maoni yako hapo chini pia unaweza kujinga nasi kwa email. Endeleamkutembelea JIKO LA USHAURI kuhusu biashara hii na mambo mengine mazuri kwaajili yako rafiki.

Pata blogu yako sasa 0659639168 tuma ujumbe wasapu natakujibu.
Wako rafiki Sadick Kilasi
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, September 14, 2017

Hawa ndio maadui wakubwa sana wa mafanikio katika safari ya maisha.

 Sadick Kilasi     September 14, 2017     BIASHARA, UJASIRIAMALI     No comments   

Mafanikio ni haki ya kila mmoja, kila mmoja anatakiwa kufanikiwa katika jambi lolote analofanya, hakuna mtu hufanya jambo na kutegemea kushindwa, watu wote hufanya jambo lolote tukitegemea ushindi la sivyo hakuna sababu za kufanya jambo hilo.

Matokeo ya kushindwa siku zote ni mabaya sana, na maana nimeona nikuoneshe maadui hawa  katika safari ya kutimiza lengo katka mafanikio ya maisha.

Moja ni kutokuweka malengo. Maisha bila malengo ni sawasawa na gari isiyo na dereva ni lazima itapata ajari tu, kwahiyo kujipanga na kuweka malengo ni swala la muhimu sana katika safari ya mafanikio.

Mbili ni matumizi mabaya ya fedha. Huna bajeti na unatumia tu pesa bila ya tahadhari ni lazima utafeli tu.

Tatu ni marafiki au makundi yasiyo na malengo. Watu wetu wa karibu ni watu ambao huwa wnayaadhiri maisha yetu kwa upande mkubwa na mara nyingi hawa ndio walio fanya uwe ulivyo sasa, watu wetu wa karibu kama wazazi na marafiki ndio wafanya uwe hivo ulivo sasa na ndio maana maana kuna msemo unasema "pesa hufuata mkondo wake" kwahiyo kama utachagua marafiki wenye fikra hasi lazima utashindwa tu.

Nne ni matumizi mabaya ya rasilimali muda. Muda ndio rasilimali pekee ambayo binadamu tumepewa sawa, matajiri na maskini wote tuna masaa 24 kwa siku kwa hiyo matajiri ni watu ambao walitumia vema mda wao na maskini ni watu ambao walitumia vibaya rasilimali hii.

Maadui hawa ni wabaya sana kwenye safari ya mafanikio, kutokujipanga ni adui mkubwa sana katika safari ya mafanikio.
Endelea kujifunza kupitia mtandao huu pia unaweza kujiunga nami kwa kujaza fomu hiyo hapo ili kupata makala na kujenga uhusiano wa karibu na kujifunza zaidi.
Unaweza kutoa maoni pia kuhusu blog hii.
Wako  Sadick Kilasi

Subscribe to our mailing list



Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, September 11, 2017

Hii ndio kanuni moja kuu ya mafanikio ni ;

 Sadick Kilasi     September 11, 2017     BIASHARA, UJASIRIAMALI     No comments   

Kuweka mipango, mikakati yako vizuri leo ili kesho yako iwe ya mafanikio makubwa na tabasamu.Tumia uwezo wako wote ulio nao mpaka kufanikiwa. Ili usiyumie njia ya mkato ya kung'ang'aniza kuvunja yai ili utoe kifaranga, nenda kwa taratibu na UTAFANIKIWA. Usivunje kanuni. Sadick kilasi
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, September 9, 2017

Chanzo cha kufanikiwa ni kujipanga

 Sadick Kilasi     September 09, 2017     BIASHARA, NJOZI     No comments   

Kuufia ulimwengu wa mafanikio sio lelemama, mhusika lazima ajipange. Barabara ya kupitia iwe imeandaliwa, injini ambayo ni kichwa iwe imefanyiwa uchunguzi stahiki, kila nati imefungwa sawasawa na miguu yako imewekewa nguvu na imani kwamba inawezekana, mabawa yako yana uthubutu wa kutosha kuruka, malengo, fursa, muda na akiba vimepimwa nakuhakikiwa kwamba safari haita ishia njiani, kiwiliwili chote kimepata joto la njozi ya mafanikio na vifaa vya uokozi wakati wahatari. Mwanzo wa kufanikiwa ni kujipanga.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ▼  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ▼  September (11)
      • Hofu kubwa ulionayo inasababishwa na mambo haya
      • Namna ya kuweka template kwenye blogu yako
      • Mbona yote hayo ni ubatili mtupu
      • Jiulize maswali haya manne yatakupa majibu ya mais...
      • Hii ndio misingi minne ya mafanikio, ukitumia misi...
      • Kwanini unaacha ushahidi wako unapotea bila sababu...
      • Fanya mambo haya manne ili hujenga mahusiano bora ...
      • Kama huna mtaji hii ndio biashara nzuri ya kufanya...
      • Hawa ndio maadui wakubwa sana wa mafanikio katika ...
      • Hii ndio kanuni moja kuu ya mafanikio ni ;
      • Chanzo cha kufanikiwa ni kujipanga
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates