Badili Mkao Uliokaa
Kila mtu aliumbiwa upekee wake, dunia inakuhitaji, vivyo hivyo ulivyo ndivyo unavyohitajika.
Sasa, wewe, unachohitajika kufanya ni kubadili mkao uliokaa.
Mtu hawezi kubadilika, ila mtu anaweza kubadili mazingira. Hapo mwanzo, zamani za wakoloni, wazungu walibadili mkao wakatafuta utofauti ili watambue njia. Kwani ukiwa na kichwa ukikosa mwili lazima utafute mwili uko wapi.
Ndugu yangu, unahitajika hivyo hivyo ulivyo, sasa, badili mkao ili utengeneze uwiano.
Upekee wako, wewe, ni zawadi yako wewe, na kwa wengine.
Usijilaumu kwa jinsi ulivyo bali mtukuze Mungu kwani utapokea neema zaidi ukiwa na shukrani.
Utumishi unakuja kwa mkao uliokaa, mtumishi unakuja kwa maneno, utumishi unakuja kwa matendo, utumishi unakuja kwa jinsi ulivyo na unavyovhukulia mambo.
Leo, ninakuambia maneno haya, wewe, uliye mtumishi. Sisemi utumishi wa kwenye majukwaa, nasema na mtumishi, kwa jinsi unavyochukulia mambo.
Nasema, nakuuliza, je! wewe hupendi mwenzio? Kama unampenda mwenzio basi wewe u mtumishi.
Na kama wewe u mtumishi, haijarishi upo katika hali gani? Wewe u mtumishi tu. Mtukuze Mungu kwaajili ya utumishi wako, ndio, mtukuze Mungu.
Maana aliyemzima katika mwili atasema, hakika, Mimi ni afadhali kuliko huyu na huyo asiye mzima atasema, tazama, Mimi ambaye si mzima nimemtia moyo aliye mzima, ndio, nimemweka mabegani kwangu na kumwinua juu ili apate unafuu katika maisha.
Unahitajika kwa jinsi ulivyo, ikiwa u mtumishi. Haijarishi upo katika hali gani? Utanena maneno ya faraja, utatenda vema na kulitukuza jina la Bwana.
Ee wewe, uliye kilema, nawe uliyekosa chakula, nawe uliyeumizwa moyo wako, tazama, nafasi, hii, hii ni zawadi yako. Mungu anakupenda sana na ndio maana una, hii, nafasi.
AMINA.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment