JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Sunday, January 20, 2019

Jinsi Ya Kukipa Thamani Cha Karibu Yako.

 Sadick Kilasi     January 20, 2019     No comments   

Jinsi Ya Kukipa Thamani Kile Kitu Cha Karibu Yako.

Ukweli ni kwamba kwa kadili ambavyo kitu kinakuwa karibu ndivyo kinakosa thamani. Kwa kadili ambavyo kitu kinapatikana kwa urahisi ndivyo thamani yake huwa inashuka haraka sana.

Hii ni kanuni ya asili wala si mtu husababisha hivyo. Lakini pia kuna kanuni ya mvutano, kwa kadili ambavyo kitu kinakuwa mbali ndivyo ambavyo huwa kinahitajika. Hii ni kanuni ya Mungu na si mwanadamu ameanzisha. Mungu kaanzisha na dunia huitunza kanuni hii.


Mwanzo 1:6, Mungu akasema, Na liwe anga kati kati ya Maji, likayatenge maji na Maji.

Ukweli ni kwamba kila kitu ambacho kinaonekana kwa macho asili yake ni maji kwani dunia ilianza katika maji, ikiwa ndani ya maji.
Wakati Mungu anafanya kutenga maji na maji alikuwa anatengeneza thamani ya kitu ili utupu wa katikati uruhusu mjongeo yaani kuhitajiana.

Sasa lengo langu si kuzungumzia swala la utupu ijapo nalenga hapo hapo, lengo langu ni kuzungumzia swala la kuvipa thamani vile vitu ambavyo tayari upo jilani kabisa, yawezekana huduma unayotoa, ama mahusiano na mtu wako wa karibu, ama pia vitu ambavyo umenunua.


Kuna wakati huwa inafika kipindi huduma uliyonayo huwa tunazichukulia kawaida na kuona si huduma ambanzo tunapaswa kuwa nazo na viwango tulivyonavyo, labda unawe kufikiri kuhitaji zaidi ya kile ulichonacho. Lakini pia, kuna wakati wale watu wetu wa karibu huwa tunawachukulia poa tu ukilinganisha na mwanzoni namna ambavyo tulikuwa tunawahitaji. Labda kama ni mchumba wakati wa mwanzo kabla ya kuwa ndani ya ndoa mambo yalikuwa safi lakini sasa mambo hayaeleweki kabisa. Lakini pia unaweza ukawa umenunua kitu ambacho ulikuwa unahitaji sana na ulikipenda lakini kwa sasa unaona kana kwamba hakifai na unahitaji kununua kingine, na hii husababisha kujaza vitu ambavyo havina maana ndani mwako.

Kanuni ambayo tunaizungumzia hapa ni kanuni ya ulevi wa mambo, yaani kutokushiba mambo.

Nakumbuka wakati ambao nipo darasa la tano, nilikuwa nimehama kutoka shule moja kwenda shule nyingine, sasa nilipofika katika shule hiyo, wanafunzi walikuwa wananishangaa sana jinsi ninavyoandika, wanafunzi walikuwa wanasema naandika mwandiko mzuri sana mpaka darasa nzima walikuwa wanakujaa kujaa kwangu ili kuangalia namna ambavyo naandika, wengine walikuwa wanaomba niwaandikie, wewe unajua tabia za utoto. Sasa mimi binafsi nilikuwa naona si kitu cha ajabu lakini pia nilikuwa natamania wanafunzi fulani wa mule mule darasani namna ambavyo wanaandika.

Kitu ambacho kilikuja kutokea baadae wanafunzi wakawa wananichukulia kawaida japo wengine walikuwa wananiiga na mimi pia nilikuwa nawaiga wengine. Nikajikuta napoteza kabisa ile asii ya mwandiko mwangu. Na mpaka leo sina mwandiko wa aina moja.

Sasa kidogo hapa nataka tujifunze kitu, kuna mambo mawili ambayo unapaswa kuyaelewa hapa.
1.Si kwamba mimi nilikuwa na mwandiko mzuri ila nikuwa tofauti na wengine namna ambavyo wamezoea.
2.Kitu cha pili ulevi yaani kutokudhamini kile ambacho Mungu amekupa ni kitu kibaya sana.

Sasa katika maisha hakuna kitu cha muhimu kama kuthamini asili yako. Unajua watu wengi tumeitwa lakini wengi tunapoteza wito wetu kwa sababu ya tamaa zetu. Katika neno imeandikwa usifuate namna ya dunia hii. Lakini pia Paulo alipokuwa anamfunza Timotheo alimwambia kumbuka sana asili yako ulikotokea, usiwe mlevi wa dunia hii na kupoteza hazina yako. Mapito yako ni lugha yako halisi kabisa kwani Mungu alikufundisha kwa kukupa maumivu na unatambua kwa sababu umepitia.

Tumekuja kuwasilisha itofauti duniani ili utambue wito wako angalia umetoka wapi, ulivokuwa unaitwa ulikuwa katika hali gani, asili, hakuna kitu cha muhimu kama kukumbuka ulikotoka na hii itasababisha kujua unakokwenda. Paulo anasema, tumikeni namna ambavyo mmeitwa.

Tumesema kwamba mara nyingi tulivyonavyo huwa vinapoteza thamini,  yaani kama nguo inavyochafuka, sasa kitu cha muhimu katika maisha ni kukumbuka mapito uliyo pita na kuona kwamba hustahili kile ambacho umepewa. Huwa hatuthamini vile tulivyonavyo navyo mpaka pale ambavyo tunahisi kuvipoteza. Wewe kama unafanyaga maziezi unaijua kanuni hii. Maumivu yanapojitokeza sasa hapo ndipo huwa tunapaangalia sana pale panapouma.

Sasa ili uishi maisha yenye maana na halisi ona kwamba hustahili. Mtu wako wa karibu ni zawadi yako kubwa sana,  hatustahili kuwa nao, vitu ambavyo unavyo hustahili kuwa navyo, huduma uliyonayo ona kwamba hustahili. Kwanini wewe upewe na mwingine anyimwe? Mwambie Mungu asante kwa kila kitu. Hii itakufanya kufua nguo zako na kuebdelea mbele. Chochote ulichonacho kama huta booresha kitaliwa na kutu na kuisha kabisa.

Asante kwa wewe ambaye unasoma makala zangu maana unanifanya natua mzigo wa ujumbe wangu. Imeandikwa katika Waebrania, vyombo vya madhabahu tunayoihudumia hatuna ruhusa ya kula vitu vyake tunatoa nje na kuipa dunia.

Wewe endelea kuwa mvumilivu kwenye kitabu chetu ambacho kinatoka kW kadili Mungu ambavyo akipangilia, mambo yatakuwa sawa.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaishauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ▼  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ▼  January (5)
      • Jinsi Ya Kukipa Thamani Cha Karibu Yako.
      • Mimi Sijui!
      • Kitu Hiki Kimesahaurika Licha Ya Mengine Kuwepo.
      • Unachokifanya Kitaleta Matokeo
      • Falsafa Ya Asili Na Jinsi Ya Kuishi Maisha Yenye M...
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates