JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Sunday, January 20, 2019

Jinsi Ya Kukipa Thamani Cha Karibu Yako.

 Sadick Kilasi     January 20, 2019     No comments   

Jinsi Ya Kukipa Thamani Kile Kitu Cha Karibu Yako.

Ukweli ni kwamba kwa kadili ambavyo kitu kinakuwa karibu ndivyo kinakosa thamani. Kwa kadili ambavyo kitu kinapatikana kwa urahisi ndivyo thamani yake huwa inashuka haraka sana.

Hii ni kanuni ya asili wala si mtu husababisha hivyo. Lakini pia kuna kanuni ya mvutano, kwa kadili ambavyo kitu kinakuwa mbali ndivyo ambavyo huwa kinahitajika. Hii ni kanuni ya Mungu na si mwanadamu ameanzisha. Mungu kaanzisha na dunia huitunza kanuni hii.


Mwanzo 1:6, Mungu akasema, Na liwe anga kati kati ya Maji, likayatenge maji na Maji.

Ukweli ni kwamba kila kitu ambacho kinaonekana kwa macho asili yake ni maji kwani dunia ilianza katika maji, ikiwa ndani ya maji.
Wakati Mungu anafanya kutenga maji na maji alikuwa anatengeneza thamani ya kitu ili utupu wa katikati uruhusu mjongeo yaani kuhitajiana.

Sasa lengo langu si kuzungumzia swala la utupu ijapo nalenga hapo hapo, lengo langu ni kuzungumzia swala la kuvipa thamani vile vitu ambavyo tayari upo jilani kabisa, yawezekana huduma unayotoa, ama mahusiano na mtu wako wa karibu, ama pia vitu ambavyo umenunua.


Kuna wakati huwa inafika kipindi huduma uliyonayo huwa tunazichukulia kawaida na kuona si huduma ambanzo tunapaswa kuwa nazo na viwango tulivyonavyo, labda unawe kufikiri kuhitaji zaidi ya kile ulichonacho. Lakini pia, kuna wakati wale watu wetu wa karibu huwa tunawachukulia poa tu ukilinganisha na mwanzoni namna ambavyo tulikuwa tunawahitaji. Labda kama ni mchumba wakati wa mwanzo kabla ya kuwa ndani ya ndoa mambo yalikuwa safi lakini sasa mambo hayaeleweki kabisa. Lakini pia unaweza ukawa umenunua kitu ambacho ulikuwa unahitaji sana na ulikipenda lakini kwa sasa unaona kana kwamba hakifai na unahitaji kununua kingine, na hii husababisha kujaza vitu ambavyo havina maana ndani mwako.

Kanuni ambayo tunaizungumzia hapa ni kanuni ya ulevi wa mambo, yaani kutokushiba mambo.

Nakumbuka wakati ambao nipo darasa la tano, nilikuwa nimehama kutoka shule moja kwenda shule nyingine, sasa nilipofika katika shule hiyo, wanafunzi walikuwa wananishangaa sana jinsi ninavyoandika, wanafunzi walikuwa wanasema naandika mwandiko mzuri sana mpaka darasa nzima walikuwa wanakujaa kujaa kwangu ili kuangalia namna ambavyo naandika, wengine walikuwa wanaomba niwaandikie, wewe unajua tabia za utoto. Sasa mimi binafsi nilikuwa naona si kitu cha ajabu lakini pia nilikuwa natamania wanafunzi fulani wa mule mule darasani namna ambavyo wanaandika.

Kitu ambacho kilikuja kutokea baadae wanafunzi wakawa wananichukulia kawaida japo wengine walikuwa wananiiga na mimi pia nilikuwa nawaiga wengine. Nikajikuta napoteza kabisa ile asii ya mwandiko mwangu. Na mpaka leo sina mwandiko wa aina moja.

Sasa kidogo hapa nataka tujifunze kitu, kuna mambo mawili ambayo unapaswa kuyaelewa hapa.
1.Si kwamba mimi nilikuwa na mwandiko mzuri ila nikuwa tofauti na wengine namna ambavyo wamezoea.
2.Kitu cha pili ulevi yaani kutokudhamini kile ambacho Mungu amekupa ni kitu kibaya sana.

Sasa katika maisha hakuna kitu cha muhimu kama kuthamini asili yako. Unajua watu wengi tumeitwa lakini wengi tunapoteza wito wetu kwa sababu ya tamaa zetu. Katika neno imeandikwa usifuate namna ya dunia hii. Lakini pia Paulo alipokuwa anamfunza Timotheo alimwambia kumbuka sana asili yako ulikotokea, usiwe mlevi wa dunia hii na kupoteza hazina yako. Mapito yako ni lugha yako halisi kabisa kwani Mungu alikufundisha kwa kukupa maumivu na unatambua kwa sababu umepitia.

Tumekuja kuwasilisha itofauti duniani ili utambue wito wako angalia umetoka wapi, ulivokuwa unaitwa ulikuwa katika hali gani, asili, hakuna kitu cha muhimu kama kukumbuka ulikotoka na hii itasababisha kujua unakokwenda. Paulo anasema, tumikeni namna ambavyo mmeitwa.

Tumesema kwamba mara nyingi tulivyonavyo huwa vinapoteza thamini,  yaani kama nguo inavyochafuka, sasa kitu cha muhimu katika maisha ni kukumbuka mapito uliyo pita na kuona kwamba hustahili kile ambacho umepewa. Huwa hatuthamini vile tulivyonavyo navyo mpaka pale ambavyo tunahisi kuvipoteza. Wewe kama unafanyaga maziezi unaijua kanuni hii. Maumivu yanapojitokeza sasa hapo ndipo huwa tunapaangalia sana pale panapouma.

Sasa ili uishi maisha yenye maana na halisi ona kwamba hustahili. Mtu wako wa karibu ni zawadi yako kubwa sana,  hatustahili kuwa nao, vitu ambavyo unavyo hustahili kuwa navyo, huduma uliyonayo ona kwamba hustahili. Kwanini wewe upewe na mwingine anyimwe? Mwambie Mungu asante kwa kila kitu. Hii itakufanya kufua nguo zako na kuebdelea mbele. Chochote ulichonacho kama huta booresha kitaliwa na kutu na kuisha kabisa.

Asante kwa wewe ambaye unasoma makala zangu maana unanifanya natua mzigo wa ujumbe wangu. Imeandikwa katika Waebrania, vyombo vya madhabahu tunayoihudumia hatuna ruhusa ya kula vitu vyake tunatoa nje na kuipa dunia.

Wewe endelea kuwa mvumilivu kwenye kitabu chetu ambacho kinatoka kW kadili Mungu ambavyo akipangilia, mambo yatakuwa sawa.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaishauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Mimi Sijui!

 Sadick Kilasi     January 20, 2019     No comments   

Mimi Sijui!

Ushawahi kukutana na mtu anasema hivi, MIMI SIJUI! Labda hata wewe ni mmoja wapo wa watu ambao hutumia neno hili.

Ukweli ni kwamba, hakuna mtu ambaye hajui duniani, hata mtoto ambaye anatoka kuzaliwa bado anajua kitu gani alichonacho ndani mwake na ndiomaana wakati wa uhitaji wa kula chakula atafumbua mdomo na kulia na kuashilia anajua kitu.

Zawadi ya peke ambayo Mungu ametupa ni pale tulipo, yaani pale ambapo tumesimama pana kila kitu, sasa kitu ambacho kinahitajika ni kukipa thamani kile ulichonacho kwanza, lazima ujiulize; Mimi sijui, nimejuaje kwamba mimi sijui? Kwa hiyo, umejua kwamba hujui kwa sababu unajua.

Kitu cha muhimu katika maisha, tukiona kwamba, tumejua kwamba, hajui, kujuwa kule tunakoelekea huwa tunarudi kule tunakojua  ili kujua kule tunakoelekea kujua.

Popote ulipo una wewe na chochote unachokiendea kina wewe, thamini uwepo wako.
Asante.

Kitabu cha dunia mama ndicho hicho kipo kuchapwa, funua kinywa chako nao mdomo upokee na usindike kile ambacho unapaswa kusindika. Vaa utayari huo.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, January 12, 2019

Kitu Hiki Kimesahaurika Licha Ya Mengine Kuwepo.

 Sadick Kilasi     January 12, 2019     No comments   

Kitu Hiki Kimesahaulika Katika Maisha Licha Ya Mengine Kuwepo.

Ukweli ni kwamba, kila kitu ambacho huwa tunafanya huwa tunafanya kwaajili yetu. Kinachokifanya nafanya kwa sababu yangu mimi binafsi na hata na wewe kila unachofanya unafanya kwa sababu yako wewe binafsi. Licha ya kwamba tunaweza tukaona kwamba tunawafanyia wengine lakini bado kile ambacho tunafanya huwa kinarudi kwetu na kutuadhiri kwa namna tofauti na jinsi ambavyo tulikuwa mwanzo.

Kuna mambo mengi sana ambayo tumekuwa tunafanya katika maisha. Moja ya mambo hayo ni yale ambayo tumekuwa tunafanya na kuona tunafanya ili kujijijenga wenyewe ili afya zetu ziwe bora. Katika zama hizi mambo haya yamekuwa yakihamasishwa sana ili kuhahakikisha kwamba afya zetu zinakuwa bora.
Kufanya mazoezi, kula chakula bora, kupumzika, kuwa katika hali ya usafi ni mambo ambayo tumekuwa tunayapa kipaumbele sana katika maisha yetu lakini kuna jambo muhimu sana ambalo tumekuwa tunalisahau.

Jambo hilo ni HALI MHEMUKO au MAWIMBI YETU. Hili ni jambo ambalo limesahaulika kabisa katika maisha yetu japokuwa hili ndilo lilipaswa kuwa kipaumbele kwa sababu hili linayaendesha yote. Mawimbi yetu ni hali ambayo ipo ndani mwetu ndiyo huwa inatunza uzima wetu. Hali hii hutokana na jinsi ambavyo unatafsi mambo ambayo unakutana nayo kwa jinsi mitazamo yako ilivyo. Mtazamo ni muhimu sana katika maisha ili tuwe na uzima. Lakini pia namna ambavyo tunawachukulia wengine bado tinajiweka katika hatari ya kuwa na uzima ama kupoteza uzima, jinsi ambavyo unachukulia chakula, jinsi ambavyo unachukulia maisha unayoishi yaani mazingira yako pia husababisha uzima. Unaweza kujiuliza kwanini Yesu alitembea juu ya maji? Lakini yote hii ni ndani ya hali mtazamo na namna ambavyo unachukulia hatari zinazokuzunguka zinaweza kukupa uzima. Unaweza kujiuliza kwanini Mama yule alishika pindo ya Yesu mpaka Yesu akahisi nguvu zake zimemtoka, yote hii ni hali mtazamo.

Kumbuka kitu kimoja neno la Mungu ndilo uzima kwa hiyo neno la Mungu linakuja kutubadilisha mitazamo yetu endapo tu tutakuwa hatusomi kishabiki na tunamruhusu Roho Mtakatifu atufunze mwenyewe. Kumbuka hapo mwanzo tumesema kwamba kila kitu tunachofanya tunajifanyia wenyewe, kwa hiyo hata neno unaposoma unasoma kwaajili yako mwenyewe harafu excretion ikisha fanyika yale mabaki ndio unawapa wengine nao wafaidike.

Uzima ni kitu cha muhimu sana katika maisha, na ndilo jambo limetufanya tupitie hapa duniani. Na lengo la neno la Mungu ni sisi tupate uzima, Kumbuka katika kitabu cha mithali imeandikwa, linda sana moyo wako maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima.

Hili jambo ni la muhimu sana katika maisha yetu ili kuwa wazima. Na ili kuwa mzima lazima uwe tayari kutii neno na kulichambua kisawasawa bila ushabiki ndani yake wa kusoma ili kuonekana kwa wengine ama kusoma bila kulitii, na kuwa tayari kubadilika. imeandikwa katika Isaya, ibada ya kweli ambayo Mungu anataka ni mtu ambaye akisikia neno lake roho yake inapondeka na kitetemeka maana vitu vyote ndivyo Mungu kaumba.

Katika kitabu cha Dunia Mama nimelichambua hili kwa uzuri, ni kitabu ambacho kitabadili mtazamo wako kwa hiyo usipange kukosa.
Kitabu kipo jikoni kwa wale wa soft copy zitaanza kupatikana mapema zaidi, kikubwa ni kuwasiliana tu.

Usikose kupata kitabu hichi ili urudi katika mti ule wa UZIMA uliopatikana katika Edeni.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, January 3, 2019

Unachokifanya Kitaleta Matokeo

 Sadick Kilasi     January 03, 2019     No comments   



Ushujaa hauji mara moja tu bali unategemea ni kitu gani na maamuzi gani ambayo ulikuwa unafanya hapo nyuma.

Wakati ambao ulikuwa unafanya huku giza nene lilikuwa limefunika kile kitu ambacho unakifanya. Wakati ambao unajisukuma na kufurukuta huku giza likiwa linakugandamiza kwa nguvu sana.

Pale ambapo utaanza kuchomoza juu kama mbegu ambayo imelishinda giza ambalo lilikuwa limeifunika mbegu chini na hapo ndipo utaitwa shujaa. Sio lazima watu wakuite shujaa lakini pale matokeo ya kile ambacho unakifanya yanaonekana huo ni ushujaa na ni ushindi.

Inawezekana kwa sasa unafanya jambo harafu huoni matokeo giza nene limefunika kile ambacho unakifanya, endelea kufanya maana kwa kadili ambavyo unafanya ndivyo unalisukumilia mbali giza ambalo lipo.

Inawezekana kuna mtu wako wa karibu unataka abadilishe tabia fulani ambayo ni mbaya lakini huoni dalili ambayo inaonyesha kwamba atabadilika, giza nene limemtawala na linazuia nuru yako isionekane kwa kiasi kikubwa, endelea kufanya kile ambacho unapaswa kufanya kwani hiyo ni tabia yako ambayo polepole itabomoa na kusukuma mbali kabisa giza hilo.

Ilibidi Mungu atumie mapigo kumi ili kuondoa giza la Farao na kuonyesha ukuu wake. Ilikuwa ni ngumu kwa wana wa Israeli kumkubali Mungu na kuona kama kweli atawatoa katika nchi ya Misri.

Inawezekana wewe ni mtume ama Mwalimu ambaye ungependa kuona matokeo kwa wale ambao unawahubiria ujumbe lakini matokeo hayajipenyezi kwa juu pale, juu ya ardhi, endelea kusukuma, ipi siku giza litakimbia lenyewe.

Endelea kufanya kwa sababu unapaswa kufanya, fanya kwa sababu ni jukumu lako kufanya, mambo mengine mwachie Mungu, endelea kuonyesha matunda ya kile ambacho umetumwa kufanya, wakati wako upo.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, January 1, 2019

Falsafa Ya Asili Na Jinsi Ya Kuishi Maisha Yenye Maana.

 Sadick Kilasi     January 01, 2019     No comments   

Falsafa Ya Asili Na Jinsi Ya Kuishi Maisha Yenye Maana.

 Falsafa ni nini? Ni jaribio la kutaka kuelewa  ulimwengu kwa kutumia hoja zinazoeleweka. Ni muhimu sana kuyaelewa mazingira ambayo tunaishi ili kuwa na utambuzi nayo. Kwani dunia hii imeumbwa na Mwenyezi Mungu na alitunga kanuni zake ambazo ndizo zitaendesha Ulimwengu. Kuishi maisha yenye maana ni kuelewa ulimwengu na formula zake.

Matawi ya Falsafa.
Yapo matawi manne ya Falsafa kulingana na vipengele vyake.

1. Elimu ya kutafakari mazingira kwa kutumia dhana mbalimbali zenye mfululizo mfanano.  Hapa tuangalia formula mbalimbali za mental modal.

2. Elimu ya kutenda mema. Watu wengi tumekuwa tunashindwa kuishi maisha ambayo yanaeleweka si kwa sababu hatuwezi ila ni kwa sababu hatutambui Elimu juu ya maadili. Hata kama tunatambua bado tunakuwa hatujui kwani Elimu ya kutenda mema inakuwa haijajaa ndani mwetu kwahiyo ubaya unakuwa unanguvu kubwa kuliko wema. Kwa hiyo kwa kujifunza elimu hii tutapunguza ubinafsi na kijaribu kuishi maadili ya kufaa.

3. Elimu ya kutaka kuitambua asili kwa undani. Tunaishi katika Ulimwengu ambao ni asili, asili ambayo hubadilika, kwa kujifunza hili tutapata kuelewa uhalisia wa jambo uko wapi badala ya kupambana na asili ambayo hubadilika.

4. Elimu ya utambuzi wa mipaka. Kuna vitu vingine ambavyo hatuna ufahamu navyo kwani hatuvijui kwa sababu vipo nje ya sisi, kwa hiyo tunatumia utambuzi kiasi chetu kinaishia wapi.

Falsafa Asili
Tunatumia mazingira ambayo ni asili ili kuuelewa Ulimwengu.  Neno la Mungu ndio msingi ambao natumai kupima hoja kwani kila kitu ambacho kipo duniani Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba, utukufu ni wake. Kwa neno la Mungu ndilo litakalofanya tuipe tiki hoja yetu. Hakuna ambacho kipo, ambacho hakipo kwenye neno la Mungu.

Karibu katika kuishi na kuelewa maisha. Mwaka 2018 tuliutazama mti kwa kiasi kikubwa lakini tulielewa kwa kiasi na bado tunapaswa kuelewa zaidi na zaidi. Kwa hiyo mwaka huu tutaendeleza tulipoishia.

Lengo letu ni sisi kuishi maisha yenye maana na kurudisha utukufu kwa Mungu muumba wetu. Kwa kiasi tunafanya pale ambapo tuishia ili hata wajukuu wetu waendeleze tulilolianza.

Mimi ni mwanafunzi wa dunia mama ambayo Baba yetu na Mungu wetu ametuweka ili tuishi humu. Fungamanisho letu ni kufurahia maisha na kuacha zawadi kwa watoto wetu.

Mithali 6:20, Mwanangu, shika maagizo ya Baba yako wala usisahau sheria ya Mama yako.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ▼  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ▼  January (5)
      • Jinsi Ya Kukipa Thamani Cha Karibu Yako.
      • Mimi Sijui!
      • Kitu Hiki Kimesahaurika Licha Ya Mengine Kuwepo.
      • Unachokifanya Kitaleta Matokeo
      • Falsafa Ya Asili Na Jinsi Ya Kuishi Maisha Yenye M...
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates