JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Sunday, December 17, 2017

Maeneo manne ya kuimarisha ili kuweza kupata mafanikio makubwa

 Sadick Kilasi     December 17, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu tunakutana tena hapa JIKO LA USHAURI ili kuweza kujifunza yale mazuri ambayo mimi rafiki yako nimekupikia hapa na kukuletea wewe uyale maana maarifa ndicho chakula cha ubongo. Rafiki yangu hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutujalia siku hii ya leo ambayo ni siku bora sana kwetu kuliko siku zote maana maisha ni sasa yaliyopita ni kumbukumbu na ya mbele ni ya kufikirika. Kwahiyo rafiki yangu siku  ya leo ni ya muhimu sana maana kesho maandlizi yake ni leo na leo maandalizi yake yalikuwa jana. Rafiki yangu jinsi unavojiona leo ni kwasababu ya jana kwahiyo itengeneze leo kuwa siku bora ili kesho yako kuwa bora zaidi.


Rafiki yangu kuna maeneo manne ambayo unatakiwa kuyaimarisha ili kuweza  kuwa bora katika maisha yako na kuweza kupata mafanikio makubwa. Maeneo yote manne yanatakiwa kuwa bora sana na ni muhimu bila kuacha hata eneo moja na hapo ndipo utakuwa bora mafanikio yatakuwa ni yako. Maeneo hayo ni kama yafuatavyo;

Eneo la kwanza ambalo unatakiwa kuwa bora ni eneo la kiroho. Eneo la kiroho ni eneo ambalo ni la muhimu sana, hapa tunazungumzia imani yako lazima uwe na imani na Mungu kwa dini yoyote bila misingi na falsafa za kidini huwezi kufanikiwa na hata kama ukifanikiwa utakuwa bado hujapa mafanikio ya kweli. Ukiishi na kuimarika katika falsafa za kidini utakuwa mtu mwenye amani na furaha na utakuwa na imani na Mungu ambaye yeye ndiye aliye tuumba sisi.

Eneo la pili ambalo unatakiwa kuwa bora ni eneo la kiakili. Rafiki eneo hili ni la muhimu sana, ni eneo ambalo kila siku uwe unaimarika ubongo wako unahitaji kupata chakula chake kila siku. Kama bado hujaanza kuurisha ubongo wako chakula basi anza leo jifunze kwa bidii sana. Kuna wengine huwa wanasema mimi nishasoma shuleni siwezi kusoma tena, elimu haina mipaka na elimu ya shuleni ni kipande kidogo sana kwenye maisha elimu kubwa ipo mitaani anza leo soma vitabu, kuwa makini na watu unao kutana nao wasikilize kwa umakini ulio makinika, tembelea mitandao kama huu wa JIKO LA USHAURI na mitandao mingine, soma vitabu vya dini na zama hizi za taarifa kujifunza ni rahisi sana ukiwa na simu janja tayari utakuwa bora.

Eneo la tatu ambalo unatakiwa kuawa bora ni eneo la kiafya. Mwili wako ndio nyumba yako, ukishindwa kuwa na afya bora maeneo yote utaferi. Hakikisha unawekeza kwenye afya yko kwa kufanya mazoezi, kula kwa afya, fanya tahajudi au kusali na usafi kwa ujumla.

Eneo la nne na la mwisho ni eneo la kimahusiano. Watu ambao unahusiana nao hakikisha unauza kwao. hakikisha unauza kipawa chako, unauza tabasamu, unauza tabia zako na hayo maeneo yote hapo juu hakikisha watu wanajifunza kutoka kwako. Huwezi kubadirisha watu kwa maneno bali kwa matendo yako. Ukiuza kwa matendo lazima utafanikiwa kazana kujenga mahusiano mazuri na watu wanao kuzunguka kwa matendo yako.

Kwa kumalizia ntasema hivi , dunia inakuhitaji sana rafiki yangu, hivyo ulivyo umekamirika unachohitaji ni kujiendeleza tu na kujitambua, rafiki yangu Mungu alituumba kila mtu kwa nafasi yake aangaze na kama wewe huwa unaangalia nyota za juu ndio sisi tulivo simama katika nafasi yako toa ulicho nacho acha kuiga kutoka kwa wengine, kuna mwanafalsafa mmoja alishawahi kusema siku hizi watu hawafungwi na mapepo ila wanafungwa na watu wanaowazunguka, watu watano wanao kuzunguka ndio wastani wa maisha yako. Hatua ya kuchukua sasa hakikisha unakuwa bora kwenye maeneo hayo yote manne lazima utapata mafanikio ya kweli.

Endele kutembelea blogu hii ya jiko la ushauri ili kujifunza zaidi pia jiunge na mtandao huu ili kupata makala mpya kila itakapo toka.

Maisha ni KUWA+KUFANYA=KUPATA
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ▼  2017 (58)
    • ▼  December (16)
      • Kitu gani kipo nyuma ya hili? Kitu gani kitafuata ...
      • Maeneo matatu ambayo unatakiwa kuwa makini kama un...
      • Mambo niliyojifunza kutoka kwenye kitabu cha ONGEA...
      • Hii ndio maana halisi ya kupotea
      • Mbinu bora ya kuwa na afya bora ni hii hapa
      • Haya ndiyo maumivu ambayo tunajitengenezea wenyewe
      • Jinsi ya kujenga mahusiano bora na watu wako wa k...
      • Maeneo manne ya kuimarisha ili kuweza kupata mafan...
      • Huyu ndiye mtu ambaye unatakiwa kuwa naye makini k...
      • Haya ndiyo mambo ambayo wewe unatakiwa uyaache yap...
      • Huyu ndiye mtu pekee ambaye wewe unatakiwa kumjua ...
      • Hivi ndivyo unavyotakiwa kufanya wakati unapo taka...
      • Hii ndio falsafa ambayo kila mtu inatakiwa kuiishi.
      • Hivi ndivyo ambavyo tunavyotakiwa kutazama juu ya...
      • Huyu ndiye mtu pekee ambaye wakati wote wewe unata...
      • Nyeusi na nyeupe si rangi
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates