JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, July 31, 2018

Injili Ya Maji Na Roho [SEHEMU YA PILI]

 Sadick Kilasi     July 31, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Habari rafiki?  Natumai unaendelea vizuri kabisa. Karibu katika sehemu ya pili ya injili ya maji na Roho ambapo najaribu kukuonyesha kwa undani kabisa kuhusu ubatizo wa Yesu aliobatizwa na Yohana Mbatizaji.

Natumai kwa sasa umeanza kuelewa kuhusu ubatizo, karibu tena ili tuendelee kuuchimbua kwa undani ubatizo huu na kufahamu siri kubwa ambayo ipo ndani yake, karibu sana.
                                                         Jipatie kitabu hiki.

Yohana alimbatiza Yesu ili kumtwisha dhambi za ulimwengu na hii ndio sababu ambayo ilimfanya Yohana awe anabatiza. Sababu kubwa ya Yohana kubatiza watu katika mto Yordani ilikuwa ni kumtambua Yesu ni yupi baada ya kumbatiza, ikisha kkupitia ubatizo huo amtwishe dhambi Yesu. Yeye aliyemtuma Yohana alimwambia kwamba utakaye mbatiza na Roho akimshukia basi huyo ndiye mwanakondoo ambaye atachukua dhambi ya ulimwengu.
Yohana 1:29-34, Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya Ulimwengu! Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Wala mimi sikumjua;  lakini kusudi adhihrishwe kwa Israeli ndiyomaana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. Tena Yohana alishuhudia akisema, nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.

Ilikuwa ni muhimu kwa Yesu kubatizwa na Yohana maana Yohana alikuwa kuhani wa mwisho wa wanadamu na Yesu kwa sababu alifanyika mwana kondoo ambaye ataichukua dhambi ya ulimwengu basi Yohana kama kuhani wa uzao wa Haruni na ni kuhani mkuu wa wanadamu alimtwisha dhambi Yesu kwa kumwekea mikono juu yake, dhambi zote Yesu alizibeba. Mfumo huu ndio ambao hata makuhani wa zamani waliutumia kuondoa dhambi za wana wa Israeli lakini kwa sababu zile zilikuwa dhabihu ubatizo haukukamilika na ndiomaana iliwalazimu kila baada ya mwaka mara moja walifanya tendo la kuondoa dhambi. Lakini Yesu alifanya mara hii moja na kwa wakati wote dhambi zote ziliondolewa kwa sasa hatuna dhambi kabisa. Utajiuliza mbona mimi nina dhambi wakati namwamini Yesu? Ndio, pasipo kuitambua vema injili hii ya maji na Roho huwezi kuokolewa hata kama unamwamini Yesu. Sio kumwamini Yesu pekee ndio kutakupa haki ya wewe kutokuwa na dhambi bali ni kuiamini injili yake ambayo yeye mwenyewe alisema, Yohana 3:5, Yesu akajibu, Amini, amini, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Wapaswa kumwamini Ysu na kuamini maneno yake ni muhimu muhimu zaidi kuitambua injili ya maji na Roho vizuri

Jambo la ubatizo wa Yesu lilitabiliwa na manabii na kupitia ubatizo wake hivi leo sisi sote tumepokea neema ambayo inatufanya kutokuwa na dhambi na kushiriki utukufu wa Mungu kwa kufanyika familia moja na Yesu. Mambo haya yote hufanyika kwa imani, tukiisha kuamini ndipo Yesu yeye anatubatiza kwa Roho Mtakatifu, wewe unapaswa kuamini tu, kwamba mimi sina dhambi, dhambi zangu zote zilitwishwa kwa Yesu miaka 2000 iliyopita na Yohana ambaye ndiye aliyemtwisha dhambi Yesu. Ubatizo huu ndio unatupa haki ya kusafishwa dhamiri zetu mioyo yetu haihukumiwi tena maana tumeiamini injili ya maji na Roho na Yesu ametubatiza Roho wake.

1Petro 3:21, Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi siku hizi; [siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu,] kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Ni katika imani si katika matendo, jibu la dhamiri safi mbele za Mungu, tunashiriki utukufu huu kwa imani si kwa matendo yetu hapana lazima utambue hili vema, ubatizo huu ndio unatufnya hatuna dhambi, tunashiriki mambo yote aliyoyafanya Yesu kwa imani na ndiomaana lazima uamini maji, damu na Roho, haya yote Yesu aliyapitia lakini mwanzo wake ulikuwa ni ubatizo ambao wengi kwa sasa wanaupuuzia, wengine hubatizwa baharini lakini nataka nikuambie hivi rafiki, tunashiriki kwa imani. Ikiwa utashiriki ubatizo wake kwa matendo basi wapaswa pia kuteswa msalabani maana huwezi kushiriki nusu na inapaswa ufufuliwe baada ya kufa kwa sababu mateso ya msalabani. Lazima utambue kitu kimoja, mpango wa Mungu ni nini? Mpango wa Mungu ni kumwamini mwanaye Yesu na yale aliyoyafanya basi si matendo yetu, si kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu. Lazima utambue kitu kimoja mwanadamu atatenda dhambi mpaka kufa na Mungu amesema ondoeni matendo yenu mbele zangu. Haleluya!

Unapaswa kuliamini neno la Mungu na kulitii, wengine nikiwahubiria injili hii husema, imani bila matendo imekufa, na mimi nakubari, lakini wapaswa kutambua hayo matendo unayaelekezea wapi, kama kweli unamwamini Mungu na unataka kufanya jambo la shukrani kwa matendo basi wasaidie wanae maana sisi sote ni wana wa Mungu, Yesu aliwafundisha hivi mafalisayo, Mathayo 23:23, Ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na binzari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani adili, na rehema na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Anaposema, adili na rehema anamaanisha haki na huruma yaani upendo. Mambo ya kufanya kwa haki na huruma tunapaswa kuwatendea watu vema, kama unampenda Mungu basi watendee watu mema na imani yako ipeleke kwa Mungu. Haleluya!

Kwa leo naommba tuishie hapa, wakati unaokuja tutaendelea kuuchimbua kwa undani ubatizo wa Yesu. Kwa hapa tulipofikia ikiwa utaiamini injili hii basi utaokolewa. Warumi 10:10, Kwa maana kwa moyo wa mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Basi, wewe unapaswa kuamini tu na kukiri kwa maombi  na maombi unayokiri yanapaswa kuwa kama mtu ambaye hajaokolewa Warumi 10:3, Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuthibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Kwa hiyo ni muhimu katika kulielewa hili nalo litakujenga, unapaswa kutambua kila hatua na kutambua nafasi yako.

                                         OMBI:
Omba hvi; Mimi ni mwenye dhambi na kwaajili ya dhambi zangu napaswa kwenda motoni lakini sasa namwamini Yesu ya kwamba amechukua dhambi zangu zote alipobatizwa na Yohana katika mto Yordani na mimi sina dhambi tena, namtwisha Yesu dhambi kwa kumwani ubatizo wake, kupitia Yohana kama kuhani wangu alimtwisha dhambi Yesu, akateswa msalabani kwa sababu ya dhambi zangu na kufufuliwa kutoka kwa wafu kwa uweza wa Roho Mtakatifu na sasa yu hai Yesu Kristo. Nakuomba Yesu unibatize kwa Roho Mtakatifu. AMINA.

Pia unaweza kumwomba Mungu akupe ishara baada ya kumpokea Roho Mtakatifu. Fanya maombi kila siku, maombi yako sasa yawe ya shukrani na siyo yaulalamishi na jikite sana katika kusoma neno la Mungu wakati wote.

Ukimpokea tafadhari naomba ushuhuda wako, ili unitie moyo na tuendelee kwa pamoja kuihubiri injili hii njema. Asante sana

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, July 29, 2018

Maneno Matatu Ambayo Yanapaswa Kudumu Katika Maisha Yako Yote.

 Sadick Kilasi     July 29, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Maneno matatu ambayo yanapaawa kudumu katika maisha yako ni;

Haki
Huruma na
Imani.

Yesu alileta amri kuu ambayo ni ya upendo, upendo ndio haki na huruma. Haki na huruma vikifanya kazi kwa pamoja huzaa upendo. Mpendwa msomaji, kuwasaidia maskini, kuishi kwa kuamua kwa haki, kujali wengine, kuwaonea huruma waliofungwa na mengine yote yanayohusu upendo ndiyo yanayofaa.

Jifunze kutoka;
Mathayo 23:23
Walawi 1:9
Yohana 3:1-21.

Mungu anahitaji vitu viwili kwa watoto wake upendo na imani. Upendo ni kufanya matendo yanayofaa baada ya kukombolewa na Kristo. Maana ukimwamini Kristo utapata hekima ya Mungu nayo ndiyo itakufanya kuamua kwa haki.

Iamini injili ya maji na Roho, hili ndilo neno la Kristo kwetu na kwa ukamirifu huu ndio utapokea haki ya Mungu.

Watu wengi bado wanaudini, hupeleka sadaka nyingi kanisani, huimba kwaya kwa bidii, hijitaidi kwa matendo yao wakifikiri  Mungu huangalia matendo, Mungu anataka uangalie neno lake linasema nini. Si kwa kutoa sadaka sana ndipo utaokolewa hapana, si kwa kuomba sana ndiko kutakupa wokovu, hapana, bali ni upendo na imani.

Na ili uelewe namna ambavyo upendo na imani vinavyofanya kazi naomba utafakari maneno haya mawili; Kati ya kusikia na kusikiliza ni kipi kinaanza na ni kipi cha muhimu zaidi. Kati ya kusikia na kusikiliza.

Kitabu tayari kwaajiri yako, ambacho nimekiandika nikigusia zaidi kuishi na ibada ya kweli. Kitabu hiki kinaitwa UKRISTO NA MAISHA, jipatie kitabu hichi haraka iwezekanavyo.


Nimeigusia kwa undani injili ya maji na Roho ambayo ndiyo hutupa wokovu mpaka leo.

Tuwasiliane ili ujipatie kitabu hiki ni bure kabisa. Kila mmoja anahitaji kufurahia maisha sasa kwenye kitabu hiki nimeonyesha funguo za ufalme wa Mungu. Karibu sana rafiki yangu ujipatie kitabu hiki bure kabisa, tumepewa injili bure na tutoe bure. Nitafurahi kama ukiifahamu injili ya maji na Roho kwa undani, asante sana.

Wewe ni zawadi yangu, daima tupo wote.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni sadikila65@gmail.com au 0687000768.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, July 22, 2018

Neno La Pekee Ambalo Hunijaza Furaha Wakati Wote

 Sadick Kilasi     July 22, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Neno ASANTE ni neno dogo ambalo limekuwa likitumika na kila mtu. Kwa muda mrefu sana wa maisha yangu nimekuwa nikitumia neno ASANTE kama neno la kawaida yaani kwa mazoea tu lakini kumbe neno ASANTE lina nguvu sana kwa anayetumia ikiwa utalitumia kwa shukrani halisi.

Kwa muda mrefu nilisema ASANTE kwa sababu nilitaka kumilidhisha yule ambaye amenifanyia kitu lakini kumbe neno hili linanijaza mimi mwenyewe furaha ya kutosha.

Yapo mengi ambayo yamekuwa yakitokea katika maisha, kutoelewana na watu, watu kutokuelewa unavojisikia, tinafikiri tofauti, tunawaza tofauti lakini ikiwa utaweza kuweka nafasi kwenye kila kitu na kujipa muda wa uvumilivu ukatumia neno ASANTE, kuwa na shukrani utakuwa na furaha tu katika maisha yako.

Nimegundua kwamba nikiwa na shukrani mambo huendelea kuwa mazuri tu hata kama tunapitia katika hali fulani ngumu ambayo si sawa.

Maisha yametawaliwa na mambo mengi maisha yanamengi yanayotukia, kila hali, sekunde, dakika, lisaa, siku mwezi, miaka kila wakati wote mambo yatukia kama muujiza.

Mambo yote haya yamejificha ambayo sisi kama binadamu hatuwezi kung'amua ni kitu gani kitatutukia baada ya sekunde moja ijayo. Yote haya anayejua ni Mwenyezi Mungu pekee yake.

Sema ASANTE kwa kila kitu, sema asante kwa Mungu ambaye kashikilia uhai wa maisha, sema asante kwa huyo ambaye upo naye maana Mungu anasema muwapo wawili watatu nami nitakuwa katikati yenu.

SOMA: Injili Ya Maji Na Roho.

Neno asante litakufanya uendelee kufurahia maisha japokuwa ni uchungu mwanzoni lakini Mungu hawezi kukuacha kupitia hali hiihii wakati wote. Maana utajishusha kwa watu ni jambo gumu lakini ni lazima ufie hali hii ya shukrani.

Sema asante kwa kila kitu harafu endelea kufanya unachofanya kwa upendo, amua maamuzi kwa upendo na siyo kwa Huruma maana waweza kupoteza wengine na kuharibu maisha ya wengine kwa huruma yako.

Asante sana,WEWE NI ZAWADI YANGU.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, July 15, 2018

Injili Ya Maji Na Roho.

 Sadick Kilasi     July 15, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Yesu alimwambia Nikodemo Mfalisayo mtu asipozaliwa katika maji na Roho hawezi kuingia ufalme wa mbinguni. Ni lazima mtu aitambue injili ya maji na Roho kisawasawa ndipo atakapoingia katika Ufalme wa Mungu.

Na huku ndiko kuzaliwa mara ya pili katika maji na Roho, injili ambayo Yesu mwenyewe alimhubiria Nikodemo ambaye alimwendea nyakati za usiku Yesu. Nikodemo alikuwa ni mwalimu wa mafalsayo lakini hakuitambua injili hii. Japokuwa alikuwa anawafundisha watu lakini alikuwa hailewi injili hii ambayo Yesu alimhubiria.

Katika nyakati hizi wapo wengi ambao hawanauhakika kwamba wameokolewa au la. Japo wengine hujiaminisha mwenyewe kufanya wanalojisikia mwenyewe na kusema wameokoka. Wengi kumwamini Yesu bila kutambua injili hii ambayo ni ya muhimu katika kila mmoja kutambua ndipo upate kuokolewa kisawa sawa kwa utambuzi sahihi. Wengi wanabahatisha hawana uhakika kwamba wameokolewa kweli au la. Hawana uhakika na wanachofanya kwa sababu wameaminishwa na watu ambao hawajawaambia ukweli haswa. Wengine huamini katika damu pekee, nusu ya injili, kitu ambacho huwezi kuokolewa kwa namna hiyo. Kwenye neno la Mungu hupaswi kuchagua unalotaka wewe na uliamini, kwa kweli huo ni upotokwaji mkubwa sana. Wengine huenda kubatizwa katika maji mengi na wengine katika maji machache. Yote haya hutukia katika kuutafuta Ufalme wa Mungu.

Kuzaliwa upya mara ya pili kumekuwa na changamoto nyingi sana. Wengine hufikiri labda ni pale ambapo unaacha kutenda mabaya na kutenda mema ndipo tayari utakuwa umezaliwa mara ya pili. Wengine hufikiri kwa kuwekewa mikono ndipo utapewa Roho Mtakatifu. Wengine hutoa sadaka kubwa na hufikiri kwamba ipo siku watazaliwa mara ya pili.

Kuzaliwa upya mara ya pili hakuhusishi mabadiliko ya kimwili bali katika kuliamini neno la Mungu kikamilifu. Yakupasa uiamini injili ya maji na Roho ndipo utaokolewa.

Unapokuwa umezaliwa upya unakuwaje?

Kwa kweli unakuwa huna dhambi tena, unakuwa umesafishwa moyo wako na kuwa mtu mpya.
Je utahisi dhambi tena?
Hapana, hutahisi dhambi tena.

Je mtu ambaye anaenda kanisani harafu anahisi ni mwenye dhambi ameokoka? Hapana, hajazaliwa upya.

Kitu gani ambacho unapaswa kufanya mtu ambaye hajaokoka?
Ni kuiamini injili ya Yesu, injili ya maji na Roho. Je hii hutegemea matendo ya mtu, hapana, haitegemei matendo ya mtu. Kwamba, ufanye mema ili uokolewe au ufanye jambo fulani ili uokolewe, hapana.  Inategemea imani yako katika injili ya Yesu ya maji na Roho.

Tunashiriki mambo aliyofanya Yesu kwa imani na kukili mambo aliyofanya.

MAJI.
Lazima uamini kwamba Yesu, alibatizwa na Yohana, Yohana yule ambaye Mungu aliahidi kumtuma kwamba atalijia hekalu lake ghafla ambaye atakuja kutangaza habari ya ukombozi. Malaki 3:1.
Unapoamini katika ubatizo wa Yesu unakuwa unamtwisha dhambi Yesu Kristo na wewe unabaki huna dhambi. Kwa hiyo Yohana alikuwa ni mtu wa muhimu sana, ndiye aliyekuwa kuhani wetu mkuu wa kibinadamu ambaye alimtwisha dhambi Yesu, Yesu alifanyika mwana kondoo ambaye anaichukua dhambi ya ulimwengu, ilikuwa ni lazima pawepo na kuhani ambaye angemtwisha dhambi Yesu, ambaye alikuja kama mwanakondoo wa kuchukua dhambi zetu.

Hii inamaana gani?
Tujifunze kutoka Agano la Kale, Ibada ya Upatanisho.
Walawi 16:7-10.
Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele ya Bwana mlangoni pa hema ya kukutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili, kura moja ni kwaajili ya Bwana na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwaajili ya Bwana na kumtoa awe sadaka ya dhambi. Bali yule mbuzi aliyeangukiwa kura kwaajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwaajili ya Azazeli.

Nini kilifuata baada ya kuwapata hao mbuzi wawili, mbuzi wa kwaajili ya Bwana na Mbuzi wa Azazeli?

Walawi 16:21.
Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote wa Wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.

Yesu alitwishwa dhambi na Yohana ambaye alimbatiza, Yohana Mbatizaji. Yohana alikuja kama kuhani wa kumtwisha dhambi Yesu na Yesu alikiwa kama mwanakondoo wa sadaka katika ubatizo yaani Azazeli. Kati ya wale wawili Yesu katika eneo la ubatizo alikiwa ni mbuzi wa Azazeli, ambaye alikiwa amewekewa mikono na Haruni na kutwisha dhambi zote za Bwana wa Israeli. Kwa hiyo Yesu alijitwisha dhambi zetu kupitia ubatizo wake alibatizwa na Yohana.

Yahana alidhibitisha hilo,
Mathayo 1:29. Aliposema, tazama mwanakondoo achukuaye dhambi ya Ulimwengu.

Ni vema ukamtwisha dhambi Yesu sasa kwa kuamini kwamba Yohana mbatizaji alimteisha dhambi Yesu, hii itakufanya wewe kuwa huna dhambi, dhambi zako hazitoki bila kuamini hivi, ni lazima uamini ubatizo wa Yesu kwamba Yohana alimbatiza katika mto Yordani na akamteisha dhambi zote za ulimwengu.

Kwa hiyo ukimtwisha Yesu dhambi unabaki wewe huna dhambi. Moyo wako unabaki hauna dhambi. Kwa imani na si matendo.

Nitaendelea kufafanua zaidi katika makala ijayo.  Kuna Maji, damu na Roho.

Maswali ni muhimu.
Asante.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, July 12, 2018

Kumpa Nafasi Mungu Atawale Kila Eneo La Maisha Yako.

 Sadick Kilasi     July 12, 2018     KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Kila binadamu ana tamaa yake, wengi tunataka kufikia katika nafasi fulani ambazo wenyewe tunapenda kuzifikia na ndipo tunafikiri tunapaswa kufika ili kutimiza tamaa zetu.

Ni vema kwenye kila ambalo unalifanya kumkabidhi Mungu kwa kiasi kikubwa cha tamaa yako ili akupe unachopaswa kukipata. Unajua nini, sisi huwa tunaangalia nje tu, hatuwezi kujua usahihi wa ndani zaidi juu ya jambo ambalo tunalitaka.

Hebu fikiria kama wewe unataka mwanamke mzuri mwenye umbile fulani, lakini nakumbia hivi Mungu anatambua hivo kwamba wewe unahitaji mwanamke wa namna hiyo. Yeye kutambua tamaa zetu na kila kitu ambacho tunakitaka, yeye ni mwanzo na mwisho, yeye hutambua kabla ya sisi kutambua. Sisi huwa tunaangalia tu tunachokiona na kufananisha na tulicho kiona, ni vema tukamwachia Mungu atawale kila eneo.

Je tufanye nini?
Maombi yetu yawe ya kumpa nafasi kubwa sana Mungu kuliko kutimiza wewe mwenyewe katika maombi yako. Mfano, kama unamwomba mwanamke mzuri, mrefu, ni bora ukamwomba hivi, ninaomba mwanamke anayenifaa. Yeye hutambua tamaa zetu, hutambua kila mawazo, fikira zetu hata kabla hatujawaza, yeye ni mchunguzi wetu wa ndani, yeye huchunguza mpaka ndani kabisa ya mioyo yetu na siku zote yeye ni Mungu wa upendo, humpa mtu anachoomba, kilicho kizuri na kinachofaa.

Jifunze kutoka,
Warumi.8:27.

Sasa ikiwa wewe utamwomba mimi nataka mwanamke mzuri na mrefu, hapo tayari umetimiza mwenyewe haki yako na ukitoka nje ya nyumba yako ukimwona mwanamke wa namna hiyo unasema huyu sasa ndiye niliyekuwa namtaka kumbe umejichagulia mwenyewe bila kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Kwa hiyo ni vema ukamkabizi Mungu hadi chaguo lake yeye ambaye huyajua yote ya ndani.

        MUHIMU
Umeokoka kwa injili ya maji na Roho?  Unapaswa kuokolewa kwa injili hii njema ya maji na Roho.

SOMA:Injili Ya Maji Na Roho Ambayo Ndiyo Kweli Yenyewe.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, July 10, 2018

Mungu Anakuona Kila Kitu Unachofanya.

 Sadick Kilasi     July 10, 2018     KUFURAHIA MAISHA, TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Nimekuwa nafanya mambo mengi sana kabla ya kwenda kulala, nafanya haya na yale.

Nimekuwa nawashuhudia watu kuhusu Injili ya Maji na Roho lakini watu wengine hupokea na kujifunza na wengi hawajali kabisa. Huwa nafikiria kwamba wakipuuza, inamaana watu hawapendi maisha ya furaha. Haya ni mawazo yangu na mtazamo wangu.

Mungu waajabu sana katika kutimiza jambo lake, yeye anasema maono yake huwa yanawakati wa kufaa, kama yanaonekana kuchelewa usubiri hayata  kawia.

Mimi hufikiri napaswa kufanya jambo na lilete matokeo hapo hapo lakini kumbe Mungu anawakati wa kufaa kutimiza jambo. Wakati mwingine yeye huwa tayari ameshatimiza lakini kwa sababu sisi binadamu hupenda muujiza yaani ahaaaaa, tayari.

Yesu alifundisha juu ya Ufalme wa mbinguni kwamba ni kama mbegu iliyopadwa, mpanzi hawezi kujua lolote lakini mbegu huendelea kuota na udongo ndio unajua, wewe huwezi kujua lakini wakati ukifika wa mavuno unavuna.

Jifunze kutoka,
Marko 4:26-29.

Ni vema kuendelea kufanya linalofaa kufanywa na majibu tumwachie yeye, kwa sababu yeye huona kila kitu tunachofanya.

Mungu anakuona unachofanya jinyenyekeze kwake kwa kuukubali upendo wake.

Itambue Injili ya Maji na Roho, kuishi maisha ya furaha.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Mambo Mawili Yanayolenga Ibada Ya Kweli.

 Sadick Kilasi     July 10, 2018     KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Ibada ya kweli imekuwa ni adimu sana toka kizazi cha babu mpaka sasa hivi wakati huu wa neema ya Kristo.

Kwa bahati mbaya wengi wa watu bado hawajaokolewa na neema hii ya Kristo. Inakuwa ngumu kwao kufanya ibada ya kweli kwa sababu hawana mahusiano yoyote na Mungu kwa sababu hawajapokea Roho Mtakatifu. Wengi wamejikuta wanafanya yasiyofaa kwa sababu bado hawajapokea upendo wa Mungu.

Kuna mambo mawili yanayolenga ibada ya kumpendeza Mungu.

1. Wasaidie wasiojiweza na walio katika vifungo. Ibada ya kweli ndo hii kuwasaidia wasio jiweza na maskini, hii ndio ibada ya kumpendeza Mungu. Watu wengi hufikiri kwamba kwa matendo yao wanaweza kumpendeza Mungu, kufanya maombi mengi mno lakini unabaki palepale kwamba hatuwezi kufanya kwa matendo yoyote juu ya Mungu. Ni vema tukawa tunawasaidia maskini na watu walio onewa, Mungu ataka tufanye mambo kama haya mbele zake. Matendo ya kuwasaidia wengine na wasio jiweza. Wengi wamekuwa kama wqfungwa wa dini maana hawaelewi wala kulitii neno la Mungu. Zamani Mungu aliwavumilia watu wake walipokuwa wanamwabudu yeye kupitia dhabahu lakini sasa ni wakati Mungu tuondoe matendo yetu mbele zake kwa sababu tunayofanya uovu mtupu.

Jifunze kutoka,
Matendo ya mitume mlango 7.
Isaya 1:10-17.
Matendo ya mitume 17:19-30.

SOMA:Injili Ya Maji Na Damu Ambayo Ni Kweli Yenyewe.
2. Kumtafakari yeye na kurudisha shukrani kwake. Hii ni ibada inayolenga ibada ya kweli. Lakini kwa hakika binadamu hawezi kufanya kisawa sawa ibada ya kweli. Yatupasa kutambua nafasi yetu ili tufanye ibada inayoelekea ibada ya kweli. Ni vema kutafakari neno la Mungu na kutafakari matendo yake ya ajabu na kurudisha shukrani kwake. Ibada ya shukrani ni ibada njema mbele za Mungu na utukufu ni wake.

Mpendwa rafiki, eneo hili la kufakari hii ni ibada ya mtu binafsi na ni eneo la muhimu sana kwa mhusika. Mungu aliondoa mambo yote sikukuu na matendo yote ili watu wajitambue wao ni akina nani. Alitaka watu wamtafakari yeye wakati wote na kwa matendo yao yenye mipaka, kwamba unasubiri wakati fulani ndipo ukafanye toba. Tunapaswa kutambua kitu kimoja matendo yanamipaka na sisi tunapaswa wakati wowote tuwe tayari mbele zake.

Kitabu kinatoka karibu nimejaribu keleza mambo haya kwa upana zaidi kwa sababu ni ngumu kuelewa kwa haraka haraka. Lakini ni vema ukawa mtu wa kulitafakari neno la Mungu kuliko kuwa mwana dini.

Mambo mengi katika kanisa la sasa si ya kweli na ndio maana niwambia watu ni vema kulitii neno la Mungu kuliko kuwatii watu, kwenda kanisani kwa sababu unaogopa watu watakuuliza kwanini hujaenda au Mungu atanionaje. Nataka nikwambie kitu kimoja rafiki kabla hujawaza kwenda kanisani yeye alijua kwamba hutokwenda kanisani. Yeye alilujua kabla wewe hujajijua, yeye alikutambua kabla wewe hujajitambua. Ishi ukiwa utambua hilo. Usimwekee Mungu mipaka, hana mipaka, anaona kila mahali. Huwezi kumfanyia Mungu lolote kwa matendo yako.

Ni lipi la muhimu sasa?
Je umepokea upendo wa Mungu? Kama bado jinyenyekeze mbele zake kwa kuutambua upendo wake ambayo aliuonyesha kupitia Mwanae Yesu Kristo kwa Injili aliyoleta ya Maji na Roho. Itambue injili hii ikisha uanze kufurahia maisha kwa kuwa ndani ya Mungu.

Ukawe na tafakari njema. Tafadhali, nitumie ujumbe kwa swali lolote kuhusu upendo wa Mungu na tafadhali maoni yako ni muhimu. Nimeamua kuwekeza muda mwingi katika kuhakikisha watu wanaponywa na kuihubiri injili njema.
 Kumbuka hiki, mimi ni zawadi yako, nitumie kisawasawa na wewe ni zawadi yangu nakuhitaji sana.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.  Karibu katika Group letu la SURA YA UKWELI.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, July 8, 2018

Injili Ya Maji Na Damu Ambayo Ni Kweli Yenyewe

 Sadick Kilasi     July 08, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Yesu alisema, mtu asipozaliwa katika maji na damu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu. Leo hii kumekuwa na injili tofauti tofauti ambazo huhubiriwa lakini injili ya kweli ambayo ndiyo kweli yenyewe imeshindwa kuhubiriwa.

Watu wengi bado hawajaponywa na kusafishwa dhambi zao. Neno ambalo ni kweli bado halijahubiriwa bado kwao. Wengi hawaimbui kabisa injili ambayo ndiyo kweli yenyewe. Inapaswa kila mmoja kumpokea Roho Mtakatifu aweke makazi ndani yako. Bila hivi huwezi kuokolewa na bila kweli ya injili ya maji na damu kuifahamu huwezi kuokoka. Mtu yeyote ambaye anamwamini Mungu, anapaswa kumwamini Yesu ni Kristo na yeyote atakaye mwamini Yesu huyo ataokoka lakini si kumwamini Yesu ni Kristo pekee ndipo utakapo okoka, hapana, lazima uamini  kwamba yeye alikuja katika maji na damu na Roho ndiye huwa anashuhudia kwamba mtu huyu sasa hana dhambi moyoni mwake. Roho Mtakatifu huweka makao kwa mtu ambaye hana dhambi kabisa. Roho Mtakatifu haweki makao mahala ambapo pana dhambi.

Swali, umeokoka katika injili hii?

Kama bado hijaokoka unapaswa kuokoka kupitia injili hii ambayo Yesu mwenyewe alimhubiria Nikodema aliyemwendea usiku.

Jifunze kutoka, Yohana mlango wa 3.

Unapaswa kuiamini injili hii sasa ili upate kuokolewa. Jinyenyekeze mbele za Mungu kwa mapenzi yake atakuokoa.

Wasiliana nami kwa swali lolote ili tuhabarishane mengi zaidi. Liamini Neno la Mungu. Pia kujifunza zaidi karibu kwenye group letu ambako huko unaweza kuuliza swali na kujibiwa kiurahisi. Pia unaweza kiniuliza private.

Natani nawe uipokee hii neema ambayo ni ya bure kabisa. Mungu kaupenda Ulimwengu tayari, wewe kubari upendo wake kwa kuikiri injili hii njema.

Furaha yangu mimi ni wewe kifurahia maisha, karibu sana.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, July 6, 2018

Mambo Mawili Ya Kuzingatia Wakati Wa Kufanya Chaguo.

 Sadick Kilasi     July 06, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Ni ukweli usio pingika ya kwamba kila siku huwa tunafanya machaguo fulani. Tumekuwa tukifanya machaguo kuanzia asubuhi mpaka jioni. Kwa kweli wakati kwetu imekuwa chaguo tu.

Wakati mwingine tumekuwa tunafanya chaguo bila sisi wenyewe kutambua kwamba tunafanya chaguo na ndio maana muda mwigi tumejikuta tunastukia maisha yetu.

Ni ukweli usipingika kwamba chaguo ulilofanya dakika chache zilizopita ndizo zimekufanya usome makala hii wakati huu. Na kwa jinsi ambavyo utafanya chaguo zuri wakati huu ndivyo utakavyopata majibu mazuri wakati ujao.

Na kama ukifanya machaguo mabaya wakati huu ndivyo matokeo yatakavyokuwa wakati ujao. Ni vema ukatumia hekima wakati unafanya chaguo ili likuletee faida wakati ujao.

Kuna mambo mawili ya kuzingatia wakati unafanya chaguo, wakati wa kufanya chaguo.

1. Chaguo liwe la kukujenga wewe mwenyewe. Ni wakati ambapo tunaamka asubuhi kutaka kufanya jambo fulani lakini asubuhi huwa kunakuwaga na usingizi mzuri ambao huwa unaleta changamoto kidogo, muda mwingine unaweza kuharibu siku yako kwa sababu ya usingizi wa asubuhi. Ni vema tujinyime burudani ya muda mfupi ili tufanye jambo la maana katika maisha na tuje tufurahi kwa muda mrefu zaidi katika maisha yetu. Yesu Kristo amekuwa mfano kwetu, aliacha makao yake huko ya kifalme na kuteseka katika dunia ili jina lake litukuke na ndilo jina liyashindalo majina yote. Binafsi wewe leo hii unaweza kufanya chaguo ambalo hutojuta katika maisha yako yote lakini pia unaweza kufanya chaguo ambalo linaweza kufanya majuto katika maisha yako yote. Ni vema ukawa na hekima na uamuzi ilio mwema katika kufanya machaguo yako binafsi. Je umempa Mungu maisha yako? Je umezaliwa upya katika injili ya maji na damu? Kama hujafanya hivo ni vema ukafanya chaguo lililo sahihi sasa.

Jifunze kotoka;
1Yohana 5:9.
Chaguo lililo sahihi ni lile linalokupa furaha katika maisha wakati wote na siyo burudani au starehe ya muda tu.

2. Chaguo lisiwe la kibinafsi. Unapofanya chaguo hakikisha kwamba huwaumizi wengine. Ni vema chaguo lako lile la kuwajenga wengine na sio kuwabomoa. Wakati mwingine huwa tunakuwepo kwenye chaguo la kuwambia watu ukweli au kuto wambia, tunashindwa kuwambia watu ukweli kwa sababu tunaogopa kuwaumiza. Lakini ngoja nikwambie ukweli ni vema ikamwambia mtu ukweli aumie kwa muda ikisha afurahie maisha yake muda mrefu. Usifanye machaguo ya kibinafsi, kama ni maswala ya imani ni vema ukamwacha mtu akawa na uhuru wake kuliko kuhukumu jambo na kivutia kwako. Kwa mfano kwenye maswala ya vyakula, kama wewe huli usihukumu anayekula, mpe nafasi mwenzako ajisikie huru kwenye mambo kama hayo.

Jifunze kutoka;
1Wakorintho 10:24.

SOMA:Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Hali Ya Mungu.


Maisha yanahitaji kitu kimoja ujitambue wewe na utambue nafasi ya wengine katika mahusiano. Ni vema ukatumia kanuni za kibiblia kuishi vema.

Kikubwa ni furaha katika maisha, mafanikio yatakuja.

Ukawe na tafakari njema.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Karibu katika Group letu la SURA YA UKWELI, ili uwe karibu nasi kujifunza zaidi.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, July 4, 2018

Sababu Moja Kwanini Unapaswa Kusoma Neno La Mungu Na Kujifunza.

 Sadick Kilasi     July 04, 2018     TAFAKARI YA ROHO, USHAURI     No comments   



Sababu yenyewe ni hii, MIMI NI KIVULI CHA MIMI. Je mimi niko wapi?

Ni eneo la kiroho ambalo kwa sasa limepuuzwa sana ambako wewe unajipata humo. Kiburi majivuno ndiyo sababu kubwa ambayo imesababisha watu mpaka leo kutouona umuhimu wa eneo hili nyeti la kiroho ambalo ni muhimu sana kwa kila mmoja.

Ilikuwa vema kila mmoja ajitambue katika maisha yake baada tu ya kuzaliwa na ndivyo tulivyozaliwa lakini tunaanza kupoteza uhalisi wetu kwa kuyaiga mambo ya dunia hii ambayo ni kivuli tu cha ukweli.

Eneo la kiroho ni eneo nyeti na la muhimu sana kwa kila mmoja, maneno matakatifu pekee ndiyo yanaweza kurudisha uhalisi wetu kwa sababu Neno la Mungu ndiyo ukweli yenyewe.

Ni muhimu kwa kila mmoja kwa nafasi hii muhimu kupokea Upendo wa Mungu kwa kusoma Neno lake ikisha ndipo tuanze kuyaishi maisha kwa misingi ya ukweli na uhalisi wa elimu ya Mungu.

Ukiishi kwa kusukuma maisha na kufikiri ya kwamba hayo ndiyo maisha yenyewe, basi maisha yako yatakosa ladha kuishi, utafika lakini ukiwa umechoka sana na kumbe maisha mazuri yalikuwepo na ukachagua uchaguzi mbovu mwenyewe kwa kibuli cha kukataa kujifunza.

Maisha ni kama maji ya mto yanayotiririka kutoka kwenye mlima kwenda kwenye mteremko kwa yule ambaye tayari anaukubali upendo na Neno la Mungu.

Kwa bahati mbaya eneo hili la kiroho limekosa ladha kwa sababu ya watu wa kiroho ambao wanahudhulia kwenye maeneo ya ibada kwa kutafuta tamaa zao wenyewe na kuharibu sifa ya Neno la Mungu. Wamefanya sehemu hii kuwa kama sehemu yakujipatia faida na kutatua matatizo ya kidunia kumbe eneo hili ni kwajili ya kujitambua na kuuona uhalisi wako na kuishi maisha yenye maana.

Kila hatua, kila sehemu, kila wakati unaposogea mahali, unasogea ukiwa unatambua ya kwamba wewe ni nani na unanafasi gani katika dunia hii na unapaswa kufanya nini.

Eneo la kujifunza, kwanza kutafakari maisha yako na mazingira yanayokuzunguka, pili kusoma Neno la Mungu na tatu kujifunza kutoka kwa wengine kwa kusoma vitabu vyao na kuwasikiliza wengine ni jambo la muhimu sana.

Ni vema ukajitambua, harafu unafanya ukiwa unajitambua unafanya nini.

Kwa bahati mbaya wengi wanamiliki kivuli cha ukweli harafu wanaamini huo ndio ukweli wenyewe na hawapo tayari kujishusha ili kujifunza.

Ukishika kitu kama hutoachia kamwe hutoshika chochote mpaka uachie ulichoshika.

Rafiki, tafuta uhalisi wako kwa kusoma Neno la Mungu harafu ishi maisha.

Kama bado hujapokea Upendo wa Mungu maana upendo tayari upo lakini wewe unapaswa kupokea Upendo wake tu. Zipo kanuni za kuupokea upendo wa Mungu, na kwa bahati mbaya Wakristo wengi kutokana na tabia za kiitikadi na ushabiki wameshindwa kupokea wokovu.

Naandika Kitabu ambacho nimeelezea kwa kina juu ya maisha ya Wakristo na kupokea  wokovu kutoka kwa Mungu. Huwezi kuishi sawasawa kama unaishi bila kutambua nafasi yako wewe ni nani.

Kaa mkao wa kula kwa ajili ya kitabu hichi naamini kitakusaidia.
Mungu awe nawe.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, July 3, 2018

Tafuta Mtu Huyu Popote Alipo.

 Sadick Kilasi     July 03, 2018     NJOZI, USHAURI     No comments   



Ni wachache na ni adimu kupatikana watu ambao wanatafuta ukweli na kuuishi ukweli.

Watu hawa wapo lakini kuwapata ni adimu sana. Ni vema kuwa mchunguzi katika kila eneo la maisha yako na usiache kujifunza kutoka kwao. Lakini pia usiache kuchunguza sana mienendo yao kwa sababu watu hubadilika na ukajikuta unafikishwa usiko kujua.

Neno la Mungu linasemaje?
Yeremia 5:1, Pigeni mbio huku na huku, katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yupo mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji.
Waebrania 13:7, Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.

Neno la Mungu limeweka wazi mambo yote, mambo yote yapo waziwazi, shida kubwa ni kwamba ushabiki umekuwa mwingi mno kiasi kwamba wanaofunzwa hawatambui kwamba wanachokichukua ni ukweli au la.

Kwa hiyo rafiki yangu tafuta watu ambao unahusiana nao ambao wanatafuta ukweli na kuuishi ukweli huo lakini pia usiishie hapo chunguza sana ndipo uwape nafasi katika maisha yako, kila siku kuwa mtu wa kujifunza zaidi ya hayo usiwe shabiki hata siku moja bali kuwa mwanafunzi. Hili ni jambo huwa nawambia kila siku, ukiwa shabiki hutokuja kujifunza lolote kwenye maisha yako kwa sababu huto kuwa makini bali utakuwa unashabikia na mambo ya ovyo.

Watu wengine wanazungumza ukweli lakini wanakuja kuuharibu ukweli kwa tamaa zao wenyewe ili kuvutiwa na watu wengi zaidi, ukweli hauwezi kuwa sanaa hata siku moja.

Tafuta mtu huyu, wapo, ikisha kuwa mwanafunzi siku zote za maisha yako.
Kuwa na wasiwasi kidogo na kila mtu. Kidogo tu, kuwa mtu wa kujihoji ili ili uumiliki ukweli ule.

Ukawe na tafakari njema.
Karibu katika group letu la SURA YA UKWELI.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, July 2, 2018

Mimea Midogo Chini Ya Kivuli Cha Mti Mkubwa.

 Sadick Kilasi     July 02, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   



Ukiitazama mimea ambayo ipo chini ya kivuli cha mimea mikubwa mara nyingi huonekana kana kwamba inaukijani fulani. Mimea mara nyingi hupatikana kwenye mito, chini ya madaraja, chini ya miti mikubwa na sehemu nyingine yenye kivuli.

Ukiitazama kwa umakini mimea ambayo hupatikana kwenye vivuli wakati wote huwa ni ya kijani kibichi kabisa lakini huwa inahuzunisha.
Mimea hii ina woga mkubwa sana na ndiomaana inakuwa chini ya kivuli na huwa inaogopa jua kali la saa sita. Inahuzuni wakati wote, kwanza haiwezi kukua kwa sababu ipo chini ya kivuli na kamwe haiwezi kuona chakula kizuli cha mwanga wa jua kwa sababu woga wa jua la saa sita. Hunyonywa na miti mikubwa kwa sababu kwa kupewa tu kivuli tu kidogo, na mti mkubwa hufaidi chakula chote cha jua.

Mti mkubwa huendelea kukua taratibu licha ya kupigwa na jua la saa sita. Hupitia hali zote ngumu za maisha yake kwa kupigwa na mawe ya mvua, dhoruba ya upepo, ndege kutua juu yake lakini mti mkubwa mwisho hushia kuwa mti mkubwa licha ya kupitia magumu.
Mimea mdogo licha ya kuishi kwenye kivuli na kuwa wa kijani wakati wote hushia kufa mapema na kutokukua kabisa na hata siku moja hauwezi kutoa matunda yoyote.

Mpendwa msomaji, wewe ni mimea midogo au mti mkubwa?

Mungu alitupa maisha ya Uhuru kwa kila mmoja, kila mmoja anapaswa kuwa kiuongozi wa maisha yake, kila mmoja ni ufalme mkubwa sana.

Ni lazima uwe wewe mti mkubwa, usijifiche kwenye kivuli cha mti mkubwa, wewe ni mkubwa peke yako ni lazima ujitambue wewe ni nani katika maisha, ongoza sehemu yako katika maisha yako. Mungu anakupenda sana wewe kama wewe. Wewe ni kama tofari ambalo limeshikwa mkoni na fundi kwa ajili ya kujenga. Wewe ni wa kipekee katika maisha yako japo unafanana na wengine lakini wewe ni wa kipekee.

Kama ni neno la Mungu soma wewe mwenyewe, utafunuliwa wewe kama wewe. Kama mafanikio mkubwa usikubali kuwa chini ya kivuli bali wewe uwe kivuli kwa wengine.

Inashangaza kuona waumini wa makanisani, wazazi kwa watoto wao wakati wote wanataka kuwa mimea midogo tu siku zote.

Usikubali rafiki yangu, Neno la Mungu linasema kwamba ijue kweli nayo kweli itakuweka huru lakini Mimi nakuambia hakuna ukweli wa kuambiwa, na kamwe huwezi kuambiwa ukweli harafu ikisha ukweli huo ukuweke huru.
Jiunganishe na ukweli na ndipo ukweli utakuweka huru.

Jifunze kutoka: Isaya 28:9-11. Usikubali rafiki yangu, dunia inaendeshwa kwa mitazamo na hisia. Usimiliki mitazamo wala usiishi kwa hisia wakati wote.

Ukawe na wakati bora na kutafakari kwema.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home
View mobile version

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ▼  July (12)
      • Injili Ya Maji Na Roho [SEHEMU YA PILI]
      • Maneno Matatu Ambayo Yanapaswa Kudumu Katika Maish...
      • Neno La Pekee Ambalo Hunijaza Furaha Wakati Wote
      • Injili Ya Maji Na Roho.
      • Kumpa Nafasi Mungu Atawale Kila Eneo La Maisha Yako.
      • Mungu Anakuona Kila Kitu Unachofanya.
      • Mambo Mawili Yanayolenga Ibada Ya Kweli.
      • Injili Ya Maji Na Damu Ambayo Ni Kweli Yenyewe
      • Mambo Mawili Ya Kuzingatia Wakati Wa Kufanya Chaguo.
      • Sababu Moja Kwanini Unapaswa Kusoma Neno La Mungu...
      • Tafuta Mtu Huyu Popote Alipo.
      • Mimea Midogo Chini Ya Kivuli Cha Mti Mkubwa.
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates