JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Wednesday, February 28, 2018

Zawadi Ya Pekee Ambayo Leo Hii Unapaswa Kujizawadia.

 Sadick Kilasi     February 28, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI,  natumai umeamka salama kabisa. Hongera kwa ushindi huo mkubwa wa kuamka salama ambao Mwenyezi Mungu kakushindia.  Hatuna budi kumshukuru yeye aliye tuamsha salama, maana wapo wengi tu ambao waliitamani na kuiwekea siku hii malengo lakini hawaja amka, mimi na wewe tumeaka, kwa upendo na neema zake Mwenyezi Mungu.

Mpendwa msomaji,  kuna zawadi pekee ambayo unaweza kujizawadia mwenyewe bila gharama yoyote ile. Zawadi ambayo imekuwa ikitafutwa kwa gharama kubwa sana hapa dunia, lakini leo ipo mikononi mwako, wewe ni kutoa amri tu.

Unajua ni zawadi gani hiyo?  Ni "FURAHA", ndiyo furaha, ndiyo zawadi yako pekee ambayo unayo na unatakiwa kujizawadia mwenyewe, tamka kwa sauti,  Leo nina furaha, Leo nina furaha, Leo nina furaha, basi siku yako itatawaliwa na furaha sana, usiseme nitakuwa, hapana sema ninafuraha, hata kama huna, kila kitu unavuta mwenyewe kwa maneno yako.

Mpendwa msomaji, ukawe na siku ya furaha sana leo hii na kupata ushindi mkubwa wa siku ya leo. Jizawadie zawadi hii ambayo ipo ndani yako mwenyewe.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. Maoni yako muhimu rafiki yangu.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, February 27, 2018

Chachu Za Maisha Na Mafanikio.

 Sadick Kilasi     February 27, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama kabisa,  vema kabisa kwa kuamka salama. Hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuamka salama, ni upendo wake tu sisi tumeona siku hii mpya, wengi walipanga kuiona siku hii na kuweka malengo yao lakini wameshindwa kuamka.

Ukisoma kitabu cha Biblia, kitabu cha Mathayo 16 mstari wa 6, Yesu alikuwa akiwakumbusha wanafunzi wake na kuwafundisha wanafunzi wake, aliwambia, 'Yesu aliwaambia, angalieni,  jilindeni na chachu za mafarisayo na masadukayo'.

Katika zama hizi na kizazi hiki chachu za mafarisayo ni mitengo ambayo imekuwa mingi sana. Yesu alikuwa anawakumbusha ya kwamba wasiwe watu ambao wamekosa msimamo,  watu wenye tamaa, watu wa kukata tamaa mapema, na udanganyifu. Ni mstari mdogo lakini umebeba mambo mengi sana.

Mpendwa msomaji,  zama hizi tumezungukwa na fursa nyingi sana za biashara, lakini kwa njia hiyo hiyo watu wenye tamaa na fedha wanatumia mianya hiyo hiyo kutuibia, wanakuja na neno hilo hilo ya kwamba ni fursa mpya ya biashara kumbe ni matapeli, mpendwa wangu msomaji hizo ndizo chachu za masadukayo na mafarisayo lazima tujilinde sana tusije tukaingia kwenye mtego wao.

Mpendwa msomaji, kama huwezi kufurahia maisha  pale ulipo sasa jilinde sana hizo ni chachu za tamaa, chachu za mafarisayo. Katika maisha tunapitia katika viwango mbalimbali kwahiyo lazima ufurahie maisha katika kiwango ulicho nacho sasa, kuwa na shukrani, usisubiri sana furaha mpaka upate kitu fulani, hiyo siyo furaha ya ukweli na huto kuja kufurahia maisha. Jilinde rafiki yangu na chachu hii ya tamaa.

Mpendwa msomaji, chachu za changamoto za maisha zimekuwa zikifanya watu wafanye maamuzi mabaya sana katika maisha yao. Watu wanao jinyonga ni kushindwa kuelewa vizuri. Ukiangalia mstari wa mbele kwenye Mathayo hiyo utakuja kugundua ya kwamba wanafunzi walisahau mikate, Yesu akawaambia inamaana mmesahau mara hii watu elfu tano walikula mikate mitano tu. Wanafunzi walijilaumu wao kwa wao baada ya kusahau mikate. Popote unapopitia lazima ujifunze kumwamini Mungu, angalia nyuma mambo mangapi kakupitisha magumu, acha kujinyonga na kusahau ulikotoka, utapita hapo pagumu.

Mpendwa msomaji, jilinde jilinde na chachu za mafarisayo na masadukayo, tamaa, ubinafsi, woga,  ukatili, zote hizo ni chachu mbaya kwenye maisha, tafadhari rafiki yangu jilinde sana, chachu ni nyingi kuliko mkate.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. OMBI: Nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwagikie wengi zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, February 26, 2018

Dunia Imejaa Maswali, Kwanini Dunia Imejaa Maswali? Jibu Hili Hapa.

 Sadick Kilasi     February 26, 2018     USHAURI     No comments   

Moja kati ya sifa kubwa ya dunia ni kwamba, dunia imejaa maswali mengi sana. Dunia imejaa maswali lakini majibu yapo kwako. Unaweza kujiuliza kivipi dunia imejaa maswali? Lakini ndo ukweli ulivyo dunia imejaa maswali.

Mpendwa msomaji,  changamoto zote unazopitia ni maswali kwako lazima uyajibu. Dunia inakuuliza na inataka uijibu maswali hayo.

Magonjwa yanayotokea duniani ni maswali ambayo wanadamu wanatakiwa kuyajibu, wakati wowote jiandae namna ya kuyajibu. Majibu yanayotakiwa ni tiba ya magonjwa.

Uonapo popote pale panaupungufu wa kitu tambua ya kwamba hilo ni swali kwako,  unatakiwa kilijibu. Dunia imejaa maswali mengi sana na majibu yote yapo kwa mwanadamu, maana yeye alipewa uwezo mkubwa wa akili na kutawala kila kitu cha dunia.

Kwanini dunia imejaa Maswali?  Dunia imejaa maswali inataka kila mmoja aweze kuwajibika katika nafasi yake. Dunia inauliza na kutaka kujibiwa.

Maswali yanakuwa mengi ya dunia hii kwa sababu watu wengi hawawajibiki katika nafasi zao, maswali yanakuwa mengi wakujibu wanakuwa wachache.

Mpendwa msomaji, dunia inakuhitaji na kukutegemea sana wewe, lazima uwajibike katika nafasi yako, tabia ya kuwategemea watu wengine na kujiona wewe hufai ni kuwaumiza wengi, maana watu wanategemea vipawa ulivyo navyo, elimu uliyo nayo, uzowefu ulio nao, lazima uijibu dunia kwa uwezo wako.  Watu wanategemea kutoka kwako, sio wewe kuwa tegemezi kila siku.

Dunia inauliza maswali mengi sana, sasa wewe kwanini unaishia kwenye maisha ya wengine, utawezaje kuijibu dunia? Mpendwa msomaji,  kuna tabia zama hizi watu kuishia kwenye maisha ya wengine, kuigana mambo, unakuta huyu anafanya kama huyu yaani utofauti unakuwa haupo kabisa. Ukiiga vipawa vya mwingine unawezaje kuijibu dunia kwa nafasi yako wakati hufanyii kazi vipawa vyako? Unaiga vipawa vya wengine?  Mpendwa msomaji, ishi maisha yako halisi, usiishie kwenye maisha ya wengine, dunia inakuhitaji kama wewe ulivyo sio kopi ya mwingine. Lazima uijibu na kuionesha dunia kwamba wewe unaweza kuijibu kwa usahihi, ulizaliwa ili uje udhihirishe vipawa na uwezo wako na ndio maana ulipozaliwa watu walifurahi, lazima uoneshe na uijibu dunia.

Mpendwa msomaji, umezaliwa kuijibu dunia, umezaliwa kusababisha mambo, umezaliwa kuwa tegemezi kwa watu, umezaliwa kuwajibu wengine matatizo yao sio kuwa tegemezi au kuiga maisha ya wengine na kufungana, badirika.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. Maoni yako muhimu.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, February 25, 2018

Maisha Yanahitaji Kitu Hiki Ili Yawe Maisha Yenye Mafanikio.

 Sadick Kilasi     February 25, 2018     NJOZI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama kabisa,  kama umeamka salama hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii ya leo.

Karibu katika makala ya leo ili tupate kujifunza kwa pamoja.

Ukizungumzia mafanikio katika maisha kila mtu anatamani sana kufanikiwa katika maisha. Neno mafanikio ndilo neno linalotajwa mara nyingi zaidi katika midomo ya watu. Kila mtu anazungumziai mafanikio, kufanikiwa katika maisha.

Ili upate kufanikiwa unahitaji kuwa katika mwendo. Kila mtu ana njozi zake ambazo anatamania kuzifikia, watu wananjozi tofauti tofauti ambazo wanatamania kuzifikia. Lakini ili kufikia njozi zetu lazima tunahitaji mwendo.

Maisha ya mwanadamu katika kizifikia njozi zake ni kama mto unaotiririsha maji yake kutoka kwenye mwinuko kuelekea kwenye bonde. Maisha yanahitaji kutiririka ili yawe maisha ya mafanikio.

Mara nyingi maji yanayotiririka kwenye mto wenye mawe mengi huwa ni matamu sana, na yanavutia zaidi tofauti na maji ambayo yanatiririka yatakavyo bila vikwazo huwa sio mazuri kwa kunywa na hayavutii zaidi kwenye kunywa. Maisha nayo yapo hivo hivo, ukikutana na vikwazo vingi na ladha ya maisha inapokuwa nzuri na mafanikio yanaonekana. Maji yaliyosimama hayafai kwa kunywa na maisha yaliyoganda sio maisha lazima yatiririke.

Maji mwisho wake kwenye bahari au ziwa lakini maisha mwisho wake kwenye njozi zetu za mafanikio. Maisha yanahitaji kutiririka ili yasonge mbele, kila siku lazima kifanyike kitu cha tofauti na usonge mbele. Ukiona huna changamoto basi wewe hufai kuishi na maisha yako hayana ladha.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii ya jikolaushauri.blogspot.com.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, February 24, 2018

Nguvu Za Mwanadamu Ni Ujana, Maisha Ya Kuzingatia Ni Utoto, Vipaumbele Uzeeni, Maisha Ndani Ya Siku Moja.

 Sadick Kilasi     February 24, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Mwanadamu ni kiumbe anayezaliwa, anazaliwa akiwa hana nguvu kabisa za mwili. Mwili huanza kupokea nguvu polepole na baadae huwa na nguvu kubwa sana ambapo hiki ni kipindi cha ujana. Kutoka ujana wa nguvu nyingi huanza kupoteza nguvu zake pole pole na baadae huisha kabisa nguvu zake.

Maisha ya mtu mfumo wake umekaa kama siku moja tu, siku huanza na mwanga hafifu na baadae huongezeka na kuwa Mkali sana, kuanzia saa saba kuendelea nuru huanza kupoteza makali yake na baadae huisha kabisa.

Kipimo cha maisha yote ya mtu, kipo ndani ya siku moja, wakati wa utoto ambapo mtu anakuwa anaishi maisha halisi, kama jua linapochomoza huanza kwa kuvutia sana. Baadae mtu anakomaa na kuzongwa na mengi ya dunia, ambapo hiki ni kipindi cha ujana. Kipindi hiki cha ujana, ni kama jua kali sana linaloangaza kwa nguvu na kupoteza uzuri wake. Japokuwa ujana ndio kipindi cha nguvu nyingi lakini ndio kipindi ambacho mtu anazongwa na kila kitu cha dunia hii. Wakati wa ujana pamoja na kuwa na nguvu nyingi lakini ndio wakati haswa wa kutengeneza maisha ya mtu. Ndio fursa pekee ambapo mtu anaipata, fahari ya ujana ni nguvu zake mwenyewe.

Maisha huanza kupoteza nguvu za mwili pole pole na baadae kuufikia uzee. Ni kama jua linapoelekea mawiyo, huanza kuvutia pole pole na kupungua na baadae kupotea kabisa. Watu huanza kupoteza nguvu pole pole na baadae huisha kabisa. Maisha ya uzee huvutia sana, maisha ya uzee huwa na hekima midomoni mwao na kuishi maisha halisi. Fahari za wazee ni hekima zao.

Maisha yote ya mtu yapo kwenye kipimo cha siku moja tu, tunaishi maisha marefu ya siku nyingi lakini siku moja ndio kipimo chako cha maisha yako yote. Mpendwa msomaji, siku inapoisha huwa unafanya nini? Je hukutambua hicho ndicho kipimo chako cha maisha yote? Anza kuipa siku yako vipaumbele, ishi maisha ya uzee kwenye ujana. Wazee hufanya jambo ambalo linaleta maana kwao na huwa hawana mambo mengi sana. Mpendwa msomaji, fursa ya ujana nguvu, tukiweka vipaumbele kwenye kufanya mambo yetu kama wazee basi sisi tutafanya kwa ubora zaidi. Kijana, ishi kama mtoto, watoto wana sifa moja kubwa sana ambayo ni kuishi maisha. Kila wanapofanya jambo hufanya kwa uzingativu mkubwa.

Mpendwa msomaji, maisha yako yote yapo ndani ya siku moja, sasa ni muhimu kufanya hivi, kutumia sifa zote tatu za maisha yote ya mtu kwenye siku moja.
$#Kwanza kwenye utoto ni uzingatifu.
$#Pili, ujana ni nguvu na
$#Tatu uzee,  ni vipaumbele.

Maisha ni wakati, ni kipindi kifupi ambacho tumepewa hapa duniani ili tusababishe jambo ambalo litakuwa misingi kwa vizazi vijavyo. Kuwa mzingativu kwa kila jambo unalofanya,  fanya kwa bidii yaani tumia nguvu zako vizuri na weka vipaumbele, usisubili uzee.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii, pia nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu mzuri. Maoni yako ni muhimu sana.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, February 23, 2018

Kutaka Taka Sana Mwisho Utakuwa Takataka.

 Sadick Kilasi     February 23, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Kutaka taka sana mwisho utakuwa takataka, hii ni kauli mbaya lakini pia haieleweki vizuri. Hii ni ambayo nimeitumia kukupa ujumbe wewe rafiki yangu msomaji.

Katika maisha kuna mambo mengi sana yanatokea, tunafanya mambo mengi na kutimiza ndoto zetu. Maisha yetu yamejaa changamoto nyingi sana zinazofanya maisha yaendelee kusonga mbele.

Tumekuwa tunandoto kubwa sana katika maisha yetu, lakini pia hata kama huna ndoto kuna kitu lazima unataka kitokee kwenye maisha yako. Sasa hivi kila mtu ukimwuliza, mwingine atakwambia mimi nataka pesa, mwingine atakwambia mimi nataka kuoa au kuolewa, mwingine furaha na vinginevyo.

Chochote unachotaka ndugu sio mbaya lakini unatakaje?  Kuna wakati unaweza ukawa unataka kupata kitu kizuri tu unachokipenda na ukapata lakini ukizidisha tu kinakuwa madhara kwako. Kucheka ni kuzuri lakini kukizidi ni kelo, furaha ni nzuri lakini ikizidi inakosa radha, pesa ni nzuri lakini ikizidi inakuwa haina maana.

Jana nilikuwa sehemu nakula, nimezoea kula sana hapo, mama mmoja akaniuliza mbona umenuna, ukweli ni kwamba nilikuwa sijanuna, nikamjibu, nimenuna kwa sababu kunakucheka. Nilimjibu jibu hili bila mimi mwenyewe kujielewa, lakini baadae ikanifanya nijiulize sana, hivi jibu hili ni sahihi? Nilijiuliza uliza sana, nilijipa jibu moja kwamba huwezi kwenda tu bila kurudi nyuma, yaani maisha yako yote ukawa mwendaji mbele tu ni kitu ambacho hakiwezekani.

Mpendwa msomaji, kila anayeongezewa lazima ajue kupunguziwa, dunia inataka kitu peke kinachoitwa 'USAWA'  ndipo maisha yatakuwa mazuri kwako. Jambo zuri lolote lile linakuja na ubaya, ubaya,  uzuri. Huwezi kuishi na uzuri tu bila ubaya, lazima kuwe na hali zote mbili, utafuta uzuri lakini ubaya utakunyemelea.7

Mpendwa msomaji chochote unachofanya na unakitaka angalia usije kuwa taka taka, kwahiyo kama utaka furaha lazima unune kidogo tu, sio mbaya ndio utajua furaha ipoje, ukienda kumbuka kurudi ndio uzuri wa safari, ukijumrisha kumbuka kutoa, maisha yapo hivo.

Chochote unachofanya angalia usiwe mtumwa wa kitu hicho, usizidishe kutaka sana.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, February 22, 2018

Siraha Mbili Ambazo Unapaswa Kutumia Ili Kujenga Mahusiano Bora Na Wengine.

 Sadick Kilasi     February 22, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama kabisa. Hongera kwa ushindi huu mzuri wa kuamka salama, ambao Mwenyezi Mungu kakushindia. Hatuna budi mimi na wewe msomaji wangu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ushindi huu. Kulala na kuamka ni ushindi mkubwa sana, wapo ambao waliweka mipango mizuri kwa ajiri ya leo lakini washindwa kuamka.

Ni ukweli usiopingika kabisa maisha ni mahusiano, huwezi kuishi vema kama usipokuwa na mahusiano na mtu yeyote. Tunaishi tukiwa tunahusiana na watu mbalimbali, ambao tunawajua na wengine hatuwajui lakini yote haya ni mahusiano. Kuna mahusiano ya aina mbalimbali, mahusiano ya ndoa, mahusiano ya ndugu, mahusiano ya marafiki na mahusiano ya mwingiliano wa watu mbalimbali ambao hatuwajui.

Tunahusiana na watu kwa sababu mbalimbali, lakini ukweli ni kwamba wakati huohuo wa mahusiano ndipo na migogoro na matatizo na mafarakano huanza. Tukiwa tunakutana, kila mtu anawasirisha tabia na haiba yake, kwa mwingine. Ukweli ni kwamba kila mmoja amelelewa tofauti na mwingine lakini pia na haiba ni tofauti kabisa na mwingine. Watu wawili wanapokutana lazima wawe tofauti kabisa kutokana na tabia na haiba zao. Hata mapacha tu hawezi kufanya vitu vinavofanana.

Tofauti na migogoro huanzia hapa kwenye uwasirishaji wa tabia na haiba. Mtu anapowasirisha tabia yake mwingine anaona kero kwake na haifai kutokana na maadili yake.  Lakini yote hii inategemea utambuzi na uelewa wa mtu juu ya hilo jambo aliloambiwa. Mafarakano yanaanza pale tunaposhindwa kuelewana watu wawili au makundi mawili.

Kuna siraha mbili ambazo wewe msomaji wangu unapaswa kutumia wakati wa migogoro inapotokea na ukajenga mahusiano bora kabisa na wengine. Migongano haina budi kutokea lazima itokee.

1. Wachukulie watu wote wanamapungufu. Hii ni siraha bora sana, utakapo wachukulia watu wote wanamapungufu kwako haita kuwa shida unapokutana na mtu mkashindwa kuelewana. Ukweli ni kwamba kila mmoja anamapungufu yake na udhaifu wake. Utakapochukulia kila binadamu anamapungufu haitakuwa tatizo sana kwako kwa sababu utakuwa umejiandaa kisaikolojia.

2. Chukulia ya kwamba hakuna mtu mbaya duniani, ila kuna mabaya duniani. Hii nayo ni siraha nzuri sana katika maisha. Ukweli ni kwamba hakuna mtu mbaya duniani lakini kuna mabaya duniani. Tulizaliwa tukiwa wazuri tu lakini yote haya tumeyakuta huku huku duniani kwahiyo sisi siyo wabaya ila kuna mabaya. Jambo muhimu unapoishi fuata njia njema tu,  achana na mabaya, mabaya yapo na yataendelea kuwepo. Unapokutana na mtu kafanya makosa wewe unapaswa kuichukia ile hali iliyotokea pale na wewe utakuwa huna mgogoro na mtu yeyote na utaishi vema.

Siraha mbili hizi zinatosha kwako wewe rafiki yangu kuishi vema na watu na itapunguza kwako wewe mafarakano na wengine.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. OMBI: Nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu uwafikie wengi zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com, maoni ni muhimu.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, February 21, 2018

Hii Ndio Sababu Kubwa Ya Mahusiano Mengi Kuvunjika.

 Sadick Kilasi     February 21, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI,  natumai umeamka salama kabisa, hongera kwa ushindi huo ambao Mwenyezi Mungu kakushindia kwa kukuamsha salama. Hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hilo na kwa upendo wake kwa ujumla.

Karibu katika makala haya ya leo ili uweze kujinza nami jambo ambalo mimi rafiki yako nimeingia jikoni ili nilipike tule kwa pamoja. Karibu sana tujifunze kwa pamoja.

Katika mahusiano ni rahisi sana kumwambia mwingine hafai, ni rahisi sana kuona mapungufu ya wengine, ni rahisi sana kuona ya kwamba huyu mtu sio mtu sahihi wa kuhusiana nami. Haijarishi ni mahusiano ya aina gani lakini wengi tukiona mambo fulani fulani hayapo huwa tunakata tamaa kabisa na kusema ya kwamba mimi siwezi kabisa kuishi na huyu mtu.

Je ishawahi kujiuliza kwanini mahusiano mengi yanavunjika? Najua unatambua vizuri kabisa ya kwamba ni nini kinasababisha. Haijarishi ni mahusiano ya aina gani, lakini mahusiano mengi, au yote yanavinjika kwa sababu ya maslahi. Wengi wanao vunja mahusiano ni kwa sababu ya matakwa yao binafsi.

Mtu anaweza kukuelezea sababu nyingi sana za kuvunja mahusiano, lakini sababu kubwa ni kutafuta matakwa yake binafsi.  Yawe mahusiano ya ndoa au mahusiano mengine ya kawaida.

Utakuta mtu anajielezea vizuri sana, ohoo mimi siwezi kuishi na huyu mtu kwa sababu huyu mtu anapenda sana hela, siwezi kuishi na huyu mtu kwa sababu alinidanganya, siwezi kuishi na huyu mtu kwa sababu anatoka nje ya ndoa. Sasa unaona, sababu zote hizi ni nzuri lakini, zote ni za kibinafsi. Mtu anavunja mahusiano na mtu kwa sababu zake binafsi, kwa sababu hataki yeye kuumizwa na jambo lolote.

Mahusiano ni kitu cha ajabu sana, ubinafsi ukizidi waweza kujikuta hata wewe mwenyewe ukajivunja. Unaposhindwa kuhusiana na watu wa nje inamaana ya kwamba huwezi kujiongoza ndani mwako, utawatenga wengine mwisho utajitenga na wewe mwenyewe. Mwalimu Nyerere alishawahi kusema ya kwamba, dhambi ya kuwatenga watu, haiwezi kukuacha salama. Ni  kweli kabisa, ukianza kumkana mwenzako mwisho utajikana hata wewe mwenyewe. Na sababu nyingi za kujinyonga ni sababu kama hizihizi.

Mahusiano ni kitu kipana na ni muhimu sana katika maisha yetu, lazima tukazane kujenga mahusiano mazuri na wengine. Jambo la muhimu la kuzingatia ni kuweka mipaka yako katika mahusiano yako. Kama inavotamburika zama hizi hata mahusiano yamekuwa changamoto, muda umekuwa ni mchache sana kwahiyo lazima utambue ni wakati gani unapaswa kuwa na watu fulani na wa aina gani.

Jambo la muhimu hapa mpendwa msomaji, siku zote wewe usiwe chanzo cha mahusiano kuvunjika yaani bora kuachwa kuliko kuacha, kikubwa ni kujitaidi na kuje. Jitaidi sana isije dhambi ya kumtenga mtu ikakuadhibu. Waweza kujitadhimi mwenyewe wale wote ambao waliacha makaenda kuolewa kwingine mpaka leo wanatangatanga na wanaona kila mtu hafai. Hii yote ni kwa sababu ya ubinafsi na kutafuta vitu na matakwa yao.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, February 20, 2018

Sifa Ya Barua Ambayo Itakuwa Msaada Kwa Vizazi Vijavyo.

 Sadick Kilasi     February 20, 2018     MAHUSIANO     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai umeamka salama. Ni siku nyingine tena ambayo tumejaliwa kuiona ambayo ni siku mpya, hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii mpya ni ushindi mkubwa kwetu.

Mpendwa msomaji, karibu katika makala ya leo tujifunze kwa pamoja, makala ambayo mimi nimekuandalia. Makala yenye kichwa kinachosema, barua ambayo itakuwa msaada kwa vizazi vijavyo.

Kwanza kabisa mpendwa msomaji, naomba tukubaliane kabisa ya kwamba mtu yeyote yule kwenye hii dunia ni barua, ni ambayo inatakiwa kusomwa na watu, Kutokana na maisha unayoishi utasomeka vizuri au vibaya au utakua barua iliyo potea.

Kwa kizazi chetu hiki haswa ndo imedhihirika kabisa ya kwamba mtu ni barua. Tumezaliwa kuwasirisha uwezo wetu na vipawa vyetu. Kwa bahati mbaya tumekuwa tukifungana sisi kwa sisi, yaani kumekuwa na tabia ya mtu mmoja kuwasirisha tabia ya mtu mwingine. Je tutasomeka vizuri na vizazi vijavyo?

Hizi ndizo sifa bora za barua ambayo itasomeka vizuri na vizazi vijavyo.

Ukitambua ya kwamba wewe ni barua ya vizazi vijavyo lazima uishi maisha ya ukweli. Jambo lolote inalofanya hakikisha ni la ukweli la sivyo hakikisha linaeleweka kwenye jamii. Sifa ya ukweli ni kwamba hudumu daima lakini uongo una mwisho na haufiki mbali unapotea. Ukweli ni nuru katika giza, na nuru imeishinda giza, kuwa  na chagua maisha kuiishi kweli.

Tengeneza misingi bora katika maisha. Ili barua yako isiweze kupotea lazima iwe na misingi bora katika maisha yako. Tumekuwa tunawasoma watu waliopita leo wa vizazi vya zamani misingi mizuri waliyo itengeneza ndo imefanya mpaka sasa wanasomeka vizuri.

Lazima uwe mtu wa kujali wengine. Ukikosa sifa hii huwezi kusomeka kabisa na vizazi vijavyo, lazima iwe na mchango kwa wengine sio wewe kutegemea kutoka kwao.  Mtu atakumbukwa kwa mchango alioutoa kwa wengine, mfano wetu hai hapa Tanzania ni Mwalimu Nyerere anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuleta amani ya Tanzania.

Lazima uwe mtu wa kutatua matatizo ya wengine. Ipo mifano mingi  sana tunaiona ya watu ambao wametatua matatizo. Mfano: Madaraja yenye majina ya watu, shule zenye majina ya watu, majengo makubwa, yote hii ni namna ya kutatua tatizo la sehemu fulani.

Hizi ndizo sifa za barua ambayo itasomeka vizuri na vizazi vijavyo. Je wewe umechagua nini? Kutosomeka kabisa, kufa na kupotea au kusomeka vibaya kama mtu mbaya. Mpendwa msomaji, kila mtu ni barua, kipindi tunazaliwa watu walifurahi sana wakijua sisi ni msaada kwao, lazima tuendeleze hilo na kuwa msaada kwenye jamii. Ondoa ubinafsi na kuiangalia jamii inayokuzunguka, inahitaji nuru yako. Dunia inazidi kujaa giza kwasababu sisi tunafungana wenyewe kwa wenyewe, mtu mmoja anaishi maisha ya mwingine, anaiga kila kitu, pengo lako hakuna mtu wa kuziba, rudi kwenye nafasi yako uangaze.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawsiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, February 19, 2018

Kama unapitia changamoto nzito katika maisha yako, basi waweza kujishangaza mwenyewe sasa hivi.

 Sadick Kilasi     February 19, 2018     TAFAKARI YA ROHO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, hongera kwa kuamka salama na kuiona siku hii mpya. Ni ushindi mkubwa sana katika maisha yako na kwangu pia katika siku hii. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kuiona siku hii ya leo.

Karibu tena katika makala ya leo ambayo nimekuandalia msomaji wangu ili wote kwa pamoja tupate kujifunza niliyokuandalia.

Mpendwa msomaji,  inawezekana unapitia katika hali ngumu sana katika maisha lakini leo nataka nikwambie kitu kimoja, waweza kujishangaza mwenyewe, ndio waweza kujishangaza mwenyewe na magumu yako hayo uliyo nayo.

Jishangaze mwenyewe kwa kugeuza changamoto zako kuwa fursa, najua inawezekana ukifanya hivyo na utajishangaza sana kwa kuona nilikuwa wapi kipindi chote na sikufanya hivi.

Inawezekana umetengwa na wapendwa wako unao wapenda, waweza kujishangaza mwenyewe kwa kuwasamehe bure kabisa na kutua huo mzigo wa mawazo,  tena sema kwa sauti kuu nawapenda nyinyi nyote mlio nitenga na ambao hamjanitenga, tamka upendo kwa sauti kubwa.

Inawezekana unamzigo wa mawazo kichwani mwako lakini leo hii waweza kujishangaza mwenyewe kwa kufikiri tofauti kabisa juu ya mawazo yako hasi unaweza kufikiri chanya sasa, kama kuna kitu au tabia inakusumbua kwa muda mrefu, sasa dhibiti mawazo yako kwa kukataa hicho kinachokusumbua, tamka kwa sauti mara mia hivi kwa siku, sitaki, sitaki, sitaki... Basi utajishangaza mwenyewe.

Mpendwa msomaji,  kitu gani hicho kinachokutesa, au ni jambo lipi linalokutesa, kwa taarifa yako hakuna mtu anayeweza kukutesa wewe au kukuonea wewe, wewe mwenyewe unaweza kujitesa, sasa kwanini unajitesa, sasa leo waweza kujishangaza mwenyewe, igeuze na ithibiti kabisa dhamiri yako, angalia kwa jicho lingine kwa chochote kile ambacho ni mzigo kwako, vua kabisa hilo gamba la maumivu, jishangaze mwenyewe.

Mpendwa msomaji, jishangaze mwenyewe, usisubiri kushangazwa nje na wewe, jishangaze, jishangaze, jishangaze.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI: Washirikishe wengine ujumbe huu ili watoke kwenye vifungo vya mda mrefu na mizigo ambayo wameibeba.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, February 18, 2018

Hakuna mazuri yanayokuja bila mabaya.

 Sadick Kilasi     February 18, 2018     USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, hongera kwa siku hii mpya uliyo iona, na hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye katujalia kuiona siku hii ya leo.

Mpendwa msomaji, karibu katika makala hii ya leo ili tupate kujifunza kwa pamoja mimi na wewe msomaji wangu.

Moja kati ya sifa kubwa ya dunia hii ni kwamba kila kitu kimeumbwa pande mbili, dunia imewekwa katika mfumo wa kuchagua, chochote unachohitaji kipo katika machajiguzi hii ndio asili ya dunia yetu tunayoishi.

Wakati wote binadamu tumekuwa tukikazana kuyaangalia mazuri yako wapi, haswa hiki ndo kitu ambacho tunakihitaji, lakini kwa dunia ilivo lazima upate maumivu kwanza, lazima kwanza mabaya, usiyo yapenda yakutokee harafu yale mazuri yaje.

Mpendwa msomaji, ndivyo jinsi dunia ilivyo sio wewe unayosababisha au mimi au mtu fulani kakuloga, hapana, hii ni asili ya dunia. Tutajivunia matunda tunayoyachuma sasa lakini kwa mda mrefu tumekuwa wavumilivu wa hali ngumu tukitumainia tunachotaka, na sasa tunafurahi tumepata tunachotaka baada ya maumivu mda mrefu.

Mpendwa msomaji, kitu gani unakiona kwa mwenzio ni kizuri na unakitamani, Juan tayari alipata maumivu, kitu gani unakitaka kwenye hii dunia?  Basi lazima ujiandae kwa maumivu makali, ili upate unachotaka, na ukiona unaanza kwa kutokupokea maumivu hayo basi yakupasa utazame kwa umakini, yaweza kuwa umepotea au kuna maumivu yanakuja mbele yako, ambayo yameandaliwa kwa ajili yako. Hii ndio asili ya dunia, sio mimi, hapana.

Mpendwa msomaji, mabaya unayopitia yamewekwa na dunia hii kwa sababu ya kukuonyesha wewe, unachokitaka ni cha thamani kiasi gani, kama maumivu yake ni madogo basi na mazuri nayo ni madogo, unapata jinsi ulivyo pokea. Maumivu yanakuonesha thamani ya kile kitu, maumivu yanakupa tumaini, maumivu yanakujenga kuwa mtu wa uvumilivu. Mpendwa msomaji lazima ujifunze hilo.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI: Naomba unisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi. Maoni yako pia ni ya muhimu.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, February 17, 2018

Hiki ndicho kitu adimu kupatikana zama hizi.

 Sadick Kilasi     February 17, 2018     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa JIKO LA USHAURI? Natumai unaendelea vizuri na upo salama kabisa. Karibu tena katika makala ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja.

Katika zama za zamani watu waliishi, kwa kuaminiana sana, watu walifanya mambo kwa uaminifu mkubwa, japokuwa uongo ulikuwepo lakini haukuwa umekithiri sana. Ni kweli kwamba maisha yao yalikuwa ya kumaanisha kuliko sasa hivi maisha yamekosa ladha yenyewe.

Zama hizi, zama za kizazi chetu, zama za intaneti na taarifa, ukweli ni kitu adimu. Kila kitu ambacho mtu amekuwa akifanya ni uongo mtupu. Mambo yamekuwa tofauti kabisa, ukweli umekuwa adimu sana na ni gharama kuupata.

Mwenye ukweli na taarifa sahihi zama hizi ndiye amekuwa akifanikiwa kimaisha. Wengi sana ambao hawana taarifa sahihi wamekuwa wakipata shida na kuishi maisha ya kuigiza tu.

Mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu ambayo watu wanafanyia uongo mkubwa, mtu anapiga picha yupo sehemu fulani nzuri na anaonekana anamaisha mazuri lakini huo ni uongo, kama tunavojua uongo ni mwendelezo ukiongopa mara moja inakulazimu uendelee kuongopa kila siku, uongo unambana anatakiwa kila anapotaka kipiga picha ajiweke vizuri aonekane anamaisha mazuri, kitu ambacho kwake ni usumbufu mkubwa na kutafuta gharama zisizo na maana.

Mpendwa msomaji,  ukweli umekuwa kitu adimu sana, kila anafanya analojisikia yeye kufanya na kuababisha maumivu kwa wengine, biashara za utapeli zimekuwa nyingi, watu wamekosa kuishi maisha halisi sasa wanaishia maisha ya wengine, maarifa sahihi nayo yamekuwa adimu sana maana kila mtu anafanya analojisikia yeye kufanya. Mpendwa msomaji,  kweli imekuwa kitu adimu sana kupatikana.

Mpendwa msomaji,  tafuta kweli nayo kweli itakuweka, unaweza kujiuliza sasa nitafutie wapi, lakini cha muhimu anza wewe kuwa mkweli, nawe utauona ukweli na uongo kwa sababu wewe unaishi kweli, soma vitabu vya dini vitakusaidia.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Ombi: nisaidie kuwashieikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, February 16, 2018

Chochote unachopitia kinapita.

 Sadick Kilasi     February 16, 2018     USHAURI     No comments   

Inawezekana kwa sasa unapitia hali ngumu sana, habari nzuri  sana kwako ambayo itakusaidia kwa kusoma makala hii na utakuwa tofauti.

Katika maisha kila mtu anapitia hali mbalimbali,  kuna wakati mgumu sana kwako na wakati ambao ni rahisi sana kwako. Hivi ni vipindi tofauti tofauti ambavyo kila mtu huwa anapitia.

Mpendwa msomaji,  inawezekana kwa sasa unapitia wakati mgumu sana lakini leo nakutangazia huo ni wakati wa mapito, unapitia mapito ambayo yanapita, kwahiyo lazima utambue dunia ndivyo ilivyo kwamba lazima upitie hilo na hiyo ndiyo ladha yenyewe ya maisha. Kuna wakati utafika utapitia mazuri mpaka wewe mwenyewe utashangaa, kikubwa ni kutafuta njia ya kutokea ili kisiwe kipindi kirefu kwako.

Mpendwa msomaji, inawezekana kwa sasa unapitia wakati ambao ni mzuri sana, lakini naomba nikukumbushe ya kwamba, jua tu ndo linaangaza lakini dunia yote imejaa giza nene. Lazima utambue ya kwamba tunatawaliwa na changamoto zaidi kuliko furaha, lazima ujirinde na furaha isije ikawa burudani kwako.

Mpendwa msomaji, jambo lolote lile unalopitia ni darasa kwako na ni maandalizi ya baadae. Changamoto zipo na zitaendelea kuwepo.

Jambo la muhimu hapa kutambua hapa kama unapitia wakati mgumu tambua ya kwamba ni mapito na lazima upitie na kama unapitia wakati mzuri pia nayo hayo ni mapito tu lazima upitie, maisha ndivyo yatakavyokuwa siku zote na hiyo ndo ladha ya maisha.


Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.co.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Hili ndilo darasa tosha kwa kila mmoja katika maisha.

 Sadick Kilasi     February 16, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Msiba, kifo ni darasa zuri sana katika maisha ya mwombolezaji, mfiwa.

Mwombolezaji anaweza kutambua dhamani muda ambao anao na jinsi ya kuutumia vizuri.

Mwombolezaji anatambua dhamani ya wengine kupitia ya yule ambae tayari amemwondoka.

Mwombolezaji atambua ya kudhamini na kutenga mambo ya muhimu na kuyapa dhamani kubwa.

Mpendwa msomaji, kulia na kulalamika sio mbaya katika msiba lakini funzo la maisha ni jambo la muhimu zaidi. Msiba iwe ni fundisho kwa sisi tunaobaki.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, February 14, 2018

Jambo moja ambalo unapaswa kulifikiria kila siku

 Sadick Kilasi     February 14, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Unaweza kujiuliza kwanini Mungu alituumba tukiwa na sura za tofauti na mwingine yaani hatufanani?

Binafsi nafikiri ya kwamba Mungu alifanya hivi ili kuweza kuweka ubora wa kutosha katika mahusiano, ingekuwa watu wote wanafanana ubora usinge kuwepo kwasababu watu wote wa dunia hii wanamapungufu, mtu mwingine wa kuziba pengo la mwingine asingekuwepo.


Tumezaliwa duniani kuwezesha kitu ambacho mwingine hawezi kufanya hivo. Tunakamirisha pasipo kamirika, ili kufanya ubora uonekane, na hili ndilo jambo ambalo unatakiwa kulifikiria kila siku.

Imekuwa kawaida kwa watu kutofurahia mahala walipo na kufikiri kuna sehemu zaidi wangepaswa kuwepo, ni kweli inawezekana kabisa mahali ulipo sio penyewe, ukitambua hivo unapaswa kuchukua hatua haraka kugeuka na kupaendea mahala unapotaka wewe na unahisi patakupa furaha.

Mungu alipo tuumba kwa sura tofauti ilitaka, kila mmoja asababishe kadili ya uwepo na uwezo wake. Na hii ndiyo sababu pekee ya kuzaliwa, utafuta huku na huko lakini sehemu zote hizo ni funzo tu la maisha, kusababisha kwa wengine ndo maisha ya kweli.

Waweza ukawa na mali nyingi na utajiri mkubwa lakini zisikusaidie kwa lolote maana utakufa na utaacha mali hizo. Wenye mafanikio ya ukweli wanatambua ya kuwa wamebarikiwa kuwa baraka kwa wengine. Maisha ni mahusiano, ukifeli hapo maisha yatakuwa magumu sana.

Mpendwa msomaji, jambo la muhimu hapa ambalo unapaswa kutambua ni kwamba wewe ni muhimu sana kwa wengine na ndiomaana hakuna mtu unayefanana naye, utapaswa kutambua umezaliwa kusababisha kwa wengine,  ondoa ubinafsi, kwa nafasi au wakati au hali yoyote ile uliyo nayo unaweza kufanya lolote lile la kumgusa mwingine kutokana na utofauti wako na huyo, usijishushe na kuona ya kwamba hufai hapana, lazima utambue ya kwamba unaweza kumfanya mwingine ajihisi na anafuraha, waweza hata kutabasamu tu, naye atatabasamu kwaajiri ya tabasamu lako.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Maoni yako ni muhimu sana pia washirikishe wengine ujumbe huu.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, February 12, 2018

Nimekusamehe, lakini sitakusahau.....Mzani.

 Sadick Kilasi     February 12, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Ni wakati ambao mtu huwa amekuwa amefanyiwa kosa, anakuwa na machungu mengi moyoni mwake, anakuwa na mzigo mkubwa sana wa machungu. Anapohisi ya kwamba hana pa kuupeleka mzigo huo wa maumivu ya ndani kwa ndani anaamua kuweka mzigo huo kwenye mzani na kuupima, anagundua ni kosa kubwa sana alilofanyiwa, anamaumivu makali sana ya kukosewa, hatua anayochukua ni kumgawia nusu ya mzigo huo yule aliyemkosea kwa kusema, nimekusamehe lakini sito kusahau. 

Mpendwa msomaji, ni kiasi gani umekosewa na mwingine mpaka unafikia hatua hiyo ya kusema, nimekusamehe lakini sito kusahau, kwanini unamgawia maumivu mtu mwingine kama kweli umemsamehe? Je unafikiri hata ukimwambia hivo na yeye ataumia kama wewe unavyoumia?

Je huo mzani ulio uweka unafikiri nani atakula hasara zaidi?  Inawezekana kabisa hujawahi kujiuliza au kuambiwa kwanini unapaswa kumsamehe mtu au nini maana ya msamaha, lakini leo nataka nikwambie kwanini utatakiwa kusamehe mtu.

Mpendwa msomaji, kila kitu tunachofanya hapa duniani ni kwaajili yetu wenyewe yaani kwaajili yako, unatakiwa kumsamehe mtu ili wewe uachilie mzigo ulioubeba wewe, kwani yeye haelewi mzigo ulionao wewe, mpendwa msomaji, hata ukiongea kwa uchungu kiasi gani aliyekukosea hayupo kama wewe, na mzigo wako hauelewi. Mpendwa msomaji, unaposema, nimekusamehe lakini sito kusahau ni kuendelea kujiumiza mwenyewe na aliyekukosea hatambui hilo.

Kila mtu anapokosewa, huwa tunachukua uzito tofauti wa lile kosa, na ndiomaana wengine wanajinyonga,  mwingine atanuna sana, mwingine hata nuna kabisa.  Mpendwa msomaji, chizi akikosea hutonuna, basi hata mtu mwenye akili timamu mchukulie hivohivo, sio kila mtu anachukulia uzito huo uliochukulia wewe, wengi ni machizi japo wanaonekana ni wazima, na usipo samehe utakuwa kama yeye, kusamehe ni kuonyesha tofauti kati yako na yeye.


Samehe, samehe, samehe, Acha kuweka kwenye mizani unapokosewa, achilia kila kitu kwa faida yako mwenyewe.

Kuna kitabu ambacho kimeandikwa na Mwandishi Deo Kessy, kitabu hicho kinaitwa Kwanini msamaha, ni kitabu kizuri sana na kitakufunza mengi juu ya msamaha, inawezekana umeumizwa sana, lakini mimi nakwambia tafuta kitabu hiki kitakusaidia sana, Wasiliana nae kwa namba hii 0717101505.  Wapende wengine kwa kuwasamehe ili uwe mtu kamili na sio kichaa.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, February 10, 2018

Hatima ya maisha ya kila mtu inategemea kitu hiki

 Sadick Kilasi     February 10, 2018     USHAURI     No comments   

Habari za leo mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAIRI, hongera rafiki yangu kwa kuamka salama. Hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuamsha salama na kuiona siku hii nzuri ambayo mimi na wewe tumeiona.

Katika hatua uliopo sasa hivi inategemea hatma ya maamuzi uliyo chukua huko nyuma. Maisha ya kila mtu yanategemea chaguo utakalofanya. Maamuzi ni misingi ya maisha ya mtu, maamuzi ndiyo yanayoonesha asili yako.

Mpendwa msomaji, kila kitu kipo juu yako, maamuzi unayochukua kila siku ndiyo yamepelekea ulipo sasa hivi. Kwa maamuzi madogo madogo unayochukua au makubwa yote yamekuweka hapo ulipo.

Kama kila kitu kinategemea maamuzi yaani chaguo, sasa wakati unafanya maamizi inakupasa uwe makini sana, maamuzi ndiyo hatma ya maisha yako, kuwa makini sana juu ya maisha yako, chochote kile unacho amua na kuchagua kiwe kinaleta maana kwako na mengine, jambo liwe linaeleweka.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogpot.com
Mawasiliano ni 0687000768.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, February 8, 2018

Hili ndilo kosa kubwa ambalo wengi tumekuwa tunalifa katika kazi zetu.

 Sadick Kilasi     February 08, 2018     USHAURI     No comments   

Tumekuwa tukifanya kazi kwa bidii sana lakini lipo kosa moja ambalo wengi tumekuwa tukilifanya, na kosa lenyewe ni kutokujikagua kazi zetu wenyewe.

Kutokukagua kazi yako, huwezi kutambua wapi upo vizuri na wapi kunamakosa, unapokuwa unajikagua mwenyewe inakuwa ni vizuri na utaondoa makosa madogo madogo ambayo baadae yanakuwa na madhara makubwa kwenye kazi yako.

Kabla mwingine hajaipipitia kazi yako hakikisha wewe mwenye kazi unaipitia vizuri na unanufaika na kulidhia wewe mwenyewe. Kukagua kazi yako ni moja ya eneo ambalo linakujenga katika hali ya kujiamini, hapo utakuwa na uhakika wa kazi yako.

Ukaguzi wa kazi huwa haujalishi wewe ni mtu wa mwisho kwa kukagua au la, muhimu ni kukagua kazi yako ili inapoenda kwa mwingine iwe na ubora.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. Pia usiache kutoa maoni yako au kunitumia ujumbe kwenye mawasiliano yangu.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Hii ndiyo hali ambayo inawatesa watu wengi sana zama hizi.

 Sadick Kilasi     February 08, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Moja kati ya sababu kubwa ya migogoro ya watu ni uthibiti wa mawazo. Uthibiti wa mawazo ndio kazi kubwa ambayo wengi wamefeli na kupelekea migogoro kwenye maisha yao.

Changamoto za maisha zinaanzia kwenye uthibiti wa mawazo yako, kwa utakavyo thibiti basi ndivyo utakavyo pokea matokeo yale. Hili limekuwa ni tatizo kwa wengi, kwasababu wetu ni wavivu kufikiria zaidi.

Uthibiti wa mawazo ni vile wewe unavyopokea taarifa na kuifikiria kwa namna gani. Waweza kuipokea taarifa ambayo huipendi sasa kama huna uwezo wa kuthibiti, utaendelea kuchukia mwisho utajiumiza mwenyewe.

Unapokuwa kuwa kwenye changamoto lazima utambue wewe ndiye mhusika wa jambo hilo, usitafute majibu nje au wa kusingizia, hapana, lazima uyageuze mawazo mabuvu kuwa chanya.

Mawazo yanapokujia lazima uwe tayari kuyathibiti, kumbuka kila kitu kina pande mbili kwahiyo wewe chagua kufikiri chanya, taarifa yoyote inapoingia kichwani mwako ipokee kama ilivyo ikisha igeuze kuwa chanya, haijarishi ipoje wewe igeuze kuwa chanya.

Inapoigeuza taarifa hasi kuwa chanya, hapo unakuwa mtu wa shukrani na utaendelea mbele.

Mpendwa msomaji hatujaja duniani kuumia bali tupo duniani kufurahia maisha, changamoto zote unazoziona ni machaguo yako mwenyewe uumie au la, kwani hayupo anayetaka maumivu, ama la chagua maumivu.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, February 7, 2018

Mienendo miwili unayotakiwa kuishi nayo ili kupata furaha ya kweli.

 Sadick Kilasi     February 07, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Furaha ndio hali ambayo imekuwa inatafutwa kwa gharama kubwa sana na watu. Watu wamekuwa wakikazana kufanya mambo mengi ili mradi wapate furaha.

Kwa bahati mbaya wengi wamekuwa wakitafuta furaha lakini wameshindwa kutambua aina gani ya furaha wanayo itafuta. Wengi wamekua wakifikia pale wanapokuwa wanataka kufika wanapata furaha lakini furaha haidumu, mwisho wanagundua kuna kitu hawajakamirisha.

Watu wengi wamekuwa wakikazana kukusanya vitu wakifikiri watapata furaha lakini imekuwa tofauti kabisa hawapati furaha wanayoitaka. Kwa bahati mbaya furaha huwezi kuikusanya ama kununua kama kitu. Ukweli ni kwamba hata uwe na pesa kiasi gani huwezi kuinunua furaha.

Upendo na ukweli ndio hali pekee ambazo zinaweza kukupa wewe furaha ya kweli. Wengi wamekuwa wakitafuta furaha kwenye vitu.

Mpedwa msomaji, upendo ndio hali pekee ambayo inaitawala dunia, lazima uanze kutambua wajibu wako kwa wengine, huwezi kuwapenda wengine kama wewe ni mbinafsi, huwezi kupenda wengine kama wewe unaajali sana vitu. Lazima utambue kwamba wewe umezaliwa kuwajali wengine. 

Kwenye swala la ukweli wengi saizi hatuna ukweli kabisa, wengi tumekuwa tunawaongopea wengine tukijua ya kwamba tunawapenda. Unaweza ukaona ya kwamba unampenda mtu kwa kumuonea huruma lakini ukweli huo sio upendo wa kweli. Sehemu ambayo mtu anatakiwa mtu kuambiwa ndiyo, mwambie ndiyo, wakati ambao unatakiwa kuambiwa hapana basi na iwe hivo. Unapomwongopea mwingine kumbuka ukweli haukimbii na utakuja kudhihirika siku moja. Ukiongopa unahitaji kusimamia uongo wako usitoke nje lakini ukweli unaisha hapohapo.

Mpendwa msomaji, upendo na ukweli ndio siraha pekee ya furaha na mafanikio unayotaka utapata.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com 
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, February 6, 2018

Je hivi ndivyo ilivyo?

 Sadick Kilasi     February 06, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Wakati mwingine huwa tunapitia katika hali ngumu sana, haya ni mawazo na akili zetu ambazo zinatuambia hivi. Lakini tuna nafasi ya kujiuliza, je ni kweli nipo katika wakati mgumu?

Unaweza usinielewe nini namaanisha, ila yapaswa kujiuliza mwenyewe. Fikiria ya kwamba mwanzo ulikuwa na pesa za kujikimu mwenyewe au na familia lakini ukatumia pesa tofauti na matumizi yako ya kawaida na ukawa huna pesa, Je hapo utakuwa katika hali ngumu au mwenyewe umeamua kufanya hivo.

Ulimwamini mtu, ukajenga imani kubwa juu yake ukategemea msaada juu yake, akashindwa kukusaidia kama ulivyotegemea, unaona hafai, kakukosea, ni mchoyo, hutomsamehe, je ndivo ilivyo?

Jiulize swali hili unapokutana na migogoro mbalimbali lakini jiulize swali hili wakati wa raha na  burudani. Hofu kubwa tuliyo nayo kizazi hiki ni kuchukulia mambo kwa ukubwa mkubwa, tunazidi viwango vya kawaida. Mpendwa msomaji chochote unachokiangalia chini ya jua, kiangalie kwa ukawaida. Mtukuze Mungu na umutegemee yeye.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, February 4, 2018

Njia ya kudhibiti mawazo yako.

 Sadick Kilasi     February 04, 2018     TAFAKARI YA ROHO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama na umeinza siku yako  mpya ya wiki mpya ya mwezi mpya ukiwa na hamasa kubwa sana ya kufikia malengo yako ya mwaka huu mpya.

Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuamsha salama.

Karibu katika makala yetu ya leo ili tujifunze kwa pamoja yale ambayo mimi rafiki yako nimekuandalia. Karibu tutafakari na kukifunza kwa pamoja.

Kuna wakati unaweza ukawa upo makini sana unaposikiliza au kutazama au kusoma kitu lakini kuna hali huwa inatokea ghafla na kuharibu usikivu wako. Ni hali tu ambayo inatokea, na kwa halo hii unapoteza vitu muhimu sana, hasa kutokana na jambo lenyewe unalolifatilia.

Hali hii huwa inatokea sana unapokuwa makini sana, sio kwamba haitokei usipo kuwa makini, hapana, usipokuwa makini huwezi kutambua ya kwamba wewe umepoteza usikivu makini kwa sababu hupo makini.

Mara nyingi huwa tunachukilia kawaida, huwa hatujali ya kwamba hii hali kwanini inatokea tunaona ya kwamba ni jambo dogo sana hili. Mpendwa msomaji,  binafsi huwa nasema mambo madogo madogo ni hatari kuliko jambo ambalo unaliona kubwa na shida kubwa. Mambo madogo ndiyo mizizi ya hilo unaloliona kubwa.

Kupoteza usikivu kutakuletea madhara makubwa baadae bila ya wewe mwenyewe kujijua. Unaweza ukawa ulikuwa kwenye kikao lakini ghafla ukapoteza usikivu sehemu ndogo ya maelekezo ya muhimu, ukaona kwako si tatizo lakini umepoteza kitu cha muhimu sana na itashindwa kutekeleza jambo vizuri.

Mpendwa msomaji, changamoto kubwa tulio nayo zama hizi za taarifa na mambo mengi ya mitandao ya kijamii ni usikivu makini ulio makinika. Huwezi kukwepa hilo kwa kusema mitandao ya kijamii isiwepo hapana, ila ni wewe tu kuwa makini sana na kila jambo.

Kuna njia ambayo unaweza kutumia kupunguza hii hali kwanza tambua unalo tatizo hilo, ikisha kuwa makini wakati wote yaani jitawale mwenyewe, unaweza ukawa makini sana ukapotelea kwenye umakini huohuo. Shetani ana akili sana huwa anatumia nafasi hiyo hiyo uliyo nayo kukupoteza.

Lakini pía kuwa na tabia ya kutahajudi hii, nayo itakusaidia kuwa na umakini ulio makinika. Fanya tahajudi kila siku.

Makala hii katika maneno matatu ya kuishi nayo yaani KUWA, FANYA na POKEA, makala hii inataka KUWA,  husika mwenyewe.

Endelelea kutembelea blogu hii kukifunza zaidi. Maoni yako ni ya muhimu sana pia nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu uwafikie wengi zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com, tuma ujumbe nitakujibu.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, February 3, 2018

Penye wema pana ubaya, penye ubaya pana wema pia.

 Sadick Kilasi     February 03, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Kuna wakati unaweza ukawa umefanya jambo kwa ubora sana, na ukahisi umefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hakuna tena ubaya wa jambo hilo. Lakini pia unaweza ukawa unatazama mafanikio ya mtu fulani, ukajisemea mwenyewe, na ukasema, huyu mtu amefanikiwa sana, maisha yake ni mazuri sana.

Lakini wakati mwingine unaweza ukawa unapitia wakati mgumu, na ukaona hamna kabisa njia ya kutokea, unaona kote kumefungwa giza tupu hamna njia. Je kweli njia inakuwaga haipo?

Mpendwa msomaji, ukisoma Biblia, mwanzo 1, mstari wa nne, maneno yanasema, Mungu akaiona Nuru ya kuwa ni njema, ikaitenga nuru na giza.

Mpendwa msomaji, giza lipo mahali pale palipo kosa nuru, ubaya upo mahali palipo kosa wema, na hata kama wema ukijaa bado chembechembe za ubaya zipo. Wakati wote lazima utambue ya kuwa, unapopata Mafanikio makubwa lazima pia uwe makini sana na kushindwa kwasababu hivi vyote vinaenda kwa pamoja.

Unapo pitia magumu lazima utambue kuna wema, lazima uangalie tu, ya kuwa uafadhari wangu uko wapi hapa penye magumu. Usilaumu sana unaposhindwa, tazama na uone ni wapi pa kupitia wewe.

Mpendwa msomaji, dunia nzima imejaa giza, jua linapopita basi giza linafifia, lakini bado linakuwepo,  jua linapopotea ndivyo na giza linapoongezeka. Rafiki yangu, jiandae kwa yote hayo, unapokuwa na wema tambua kuna ubaya, unapokuwa na ubaya tambua kuna wema.

Endelea kukifunza kupitia blogu hii. Pia nisaidie kisambaza ujumbe huu uwafikie wengi zaidi, maoni yako ni ya muhimu sana rafiki yangu.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, February 2, 2018

Kwanini makosa?

 Sadick Kilasi     February 02, 2018     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, MAWASILIANO, NJOZI, USHAURI     No comments   


Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, Karibu katika makala ya leo tupate kujifunza kwa pamoja.

Mara nyingi mtu akikosea huwa anaonekana kana kwamba hafai na thamani yake hupungua ghafla kwa sababu ya kosa alilofanya, kiwango cha thamani yake hushuka kwa sababu ya kosa la mara moja tu. Kosa moja linauwezo wa kufuta mazuri yote mengi ambayo mhusika aliyafanya huko nyuma. Watu, hasa wenye matazamo hasi huchukulia ya kwamba kile ni kiwango cha mwisho kabisa ambacho mhusika amefikia na hata mazuri ya nyuma aliyofanya huchukuliwa kwa kiwango cha chini zaidi ukiringanisha na kosa alilofanya.

Lakini hilo linaweza likawa sio tatizo kubwa sana kwako wewe mhusika au kwa upande mwingine likawa tatizo kubwa sana kwako wewe.  Linaweza likawa sio tatizo kwako wewe kutokana na mtazamo wako juu ya kosa ulilolifanya, mtazamo ndio utakao kufanya wewe kuendelea kusonga mbele na unachukuliaje maneno ya wengine kwako. Unaweza ukawa ndio mwisho wa safari yako.

Je ushawahi kujiuliza kwanini watu tunakosea? Au kwanini makosa yanatokea? Inawezekana jambo unalolifanya unalitambua na kulielewa vizuri lakini bado makosa ukajikuta unafanya makosa. Kwenye kuelewa kuna kuaminishwa na kuelewa vibaya, sasa haya ni makosa ya kuelewa. Wakati mwingine unaweza ukawa ni uzembe ambao unapelekea kufanya makosa lakini hiyo sio sababu kwanini makosa yanatokea.

Hizi ndizo sababubu kwanini makosa yanatokea katika shughuri zetu za kila siku.

1.Ni kipimo cha imani yako. Tunaposema kipimo cha imani hatumaanishi imani ya dini, sivyo ni maarifa, taarifa na uelewa sahihi juu ya jambo unalofanya. Kwahiyo kosa linapokuja linakuja kukupima je wewe unauelewa kiasi gani juu ya jambo unalofanya? Wengine wanaweza wakakwambia wewe ni mzembe lakini ikawa sivyo, kumbe huna uelewa sahihi juu ya jambo hilo. Kwahiyo wewe mhusika unapokuja kugundua ya kwamba kumbe huna taarifa sahihi na uelewa mzuri, unachopaswa ni kuongeza imani yako tu au maarifa.


2.Kosa pia linakupima kuwa wewe mhusika unamtazamo gani juu ya jambo unalofanya. Inawezekana ukawa unafanya jambo hilo kwa ubora lakini bado hujaweka utayari wako pale, yaani unafanya jambo kwa kujilazimisha lazima makosa yatatokea. Kosa linapima viwango vya utayari wako kufanya jambo hilo.

3. Kosa linakupa hatua ya ziada mbele. Ndio kosa linakukumbusha ya kwamba unatakiwa kusonga mbele zaidi ya hapo ulipo, linakukumbusha ya kwamba kuna zaidi ya hapo ulipo.


4.Lakini kosa pia linakukumbusha ya kwamba wewe bado ni binadamu tu. Binadamu anamapungufu yake hilo lazima utambe, kwahiyo inawezekana wewe unajiaminisha ya kwamba wewe huwezi kukosea lakini kosa linakukumbusha kwamba binadamu anamapungufu yake. Usije ukajiinua sana ukasahau kwamba kunamakosa.

Sababu hizi zote zinakupa maandalizi juu ya matokeo mabaya utakayo yapata wakti unafanya jambo. Wewe utakapo kuwa uanfanya jambo, matokeo yakija tofauti na wewe ulivyo fikiria basi kwako wewe halitakuwa tatizo kubwa kwa sababu unatambua na utatumia fursa hiyo kusonga mbele.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. OMBI; Nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbu huu ili uwafikie wengi zaidi. Maoni yako ni ya muhimu sana mpendwa msomaji.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, February 1, 2018

Acha kusubiri ukamirifu, walio kamirika wapo makaburini.

 Sadick Kilasi     February 01, 2018     UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Inawezekana wewe ni mtu ambaye ni moja kati ya watu wanaotamani kufanya jambo fuluni lakini sasa kuna mambo fulani fulani yanakutatiza.

Inawezekana ukawa ni mtu mwenye kipaji fulani lakini unashindwa kufanya na kuonyesha kipaji chako kwa sababu ya kujiona wewe hujakamirika peke yako unahitaji wanagrupu au mdhamini atakaye kufikisha mahali fulani unapotaka wewe kufika.

Lakini pia inawezekana wewe ni moja kati ya watu ambao wanatakiwa kutimiza jambo fulani lakini unaona bado wewe hujakamirika bado. Unaweza ukawa unatakiwa kutoa fungu la kumi lakini bado unaona kwamba kipato chako ni kidogo sana kwahiyo huwezi kutoa mpaka ufikishe kiasi fulani.

Mpendwa ndugu msomaji, kama bado unasubili kukamirika au kukamirisha vitu au wakati fulani unachelewa bure,  huwezi kukamirika, walio kamirika wanapatokana makabulini. Kama bado wewe ni mzima wa afya, basi yakupasa uchukue hatua sasa hivi.

Moja kati ya sifa ya ukamirifu, hapa duniani, hapana ukamirifu, chochote utakacho fanya hapa duniani ukimaliza unahitaji kuboresha zaidi na zaidi la sivyo unarudi nyuma zaidi.

Jambo ambalo naweza kukushauri sasa hivi chukua hatua, anza kufanya, kadili utakavyo kuwa unafanya ndivyo utakavyo kuwa unajiboresha zaidi na zaidi ila usitegemee ukamirifu.

Endelea kutembelea blogu hii ili kukifunza zaidi. OMBI LANGU, nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi. Maoni yako yanakuhusu.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home
View mobile version

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ▼  February (25)
      • Zawadi Ya Pekee Ambayo Leo Hii Unapaswa Kujizawa...
      • Chachu Za Maisha Na Mafanikio.
      • Dunia Imejaa Maswali, Kwanini Dunia Imejaa Maswal...
      • Maisha Yanahitaji Kitu Hiki Ili Yawe Maisha Yenye ...
      • Nguvu Za Mwanadamu Ni Ujana, Maisha Ya Kuzingatia...
      • Kutaka Taka Sana Mwisho Utakuwa Takataka.
      • Siraha Mbili Ambazo Unapaswa Kutumia Ili Kujenga M...
      • Hii Ndio Sababu Kubwa Ya Mahusiano Mengi Kuvunjika.
      • Sifa Ya Barua Ambayo Itakuwa Msaada Kwa Vizazi Vi...
      • Kama unapitia changamoto nzito katika maisha yako,...
      • Hakuna mazuri yanayokuja bila mabaya.
      • Hiki ndicho kitu adimu kupatikana zama hizi.
      • Chochote unachopitia kinapita.
      • Hili ndilo darasa tosha kwa kila mmoja katika maisha.
      • Jambo moja ambalo unapaswa kulifikiria kila siku
      • Nimekusamehe, lakini sitakusahau.....Mzani.
      • Hatima ya maisha ya kila mtu inategemea kitu hiki
      • Hili ndilo kosa kubwa ambalo wengi tumekuwa tunali...
      • Hii ndiyo hali ambayo inawatesa watu wengi sana za...
      • Mienendo miwili unayotakiwa kuishi nayo ili kupata...
      • Je hivi ndivyo ilivyo?
      • Njia ya kudhibiti mawazo yako.
      • Penye wema pana ubaya, penye ubaya pana wema pia.
      • Kwanini makosa?
      • Acha kusubiri ukamirifu, walio kamirika wapo makab...
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates