JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, October 31, 2017

Mjasiriamali mdogo fanya mambo haya ili biashara yako ikue vizuri

 Sadick Kilasi     October 31, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu msomaji wa Jiko l ushauri. Mwenyezi Mungu mwema katujalia siku hii hii mpya na sisi kwa pamoja mimi na wewe msomaji wangu hatuna budi kusema asante Mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii mpya tunaomba utuongoze katika siku hii na kwenye shughuli zetu za kutafuta mafanikio tunaomba utujalie tufanikiwe.

Karibu tena mpendwa wangu msomaji ujifunze kwenye makala hii yenye kichwa kisemacho [Mjasiliamali mdogo atafanikiwa kwa kufanya mambo haya kwenye biashara yake]. Makala hii inawalenga wajasiriamali wadogo lakini hata wakubwa wanaweza kujifunza maana elimu haina mwisho.

Kwanza mpende mteja wako. Unatakiwa kumpenda mteja wako kuriko hata biashara yako. Mteja lazima ajisikie kuwa na furaha wakati anahudumiwa na wewe, wakati ananunua kutoka kwako dhamani unayompa lazima iwekubwa kuliko hata bidhaa yako au huduma unayo muuzia. Mteja wako ndiye anaye simamisha biashara yako bila yeye wewehuna biashara. Kwa kuonesha unamjari mda mwingine unaweza kumpigia simu na kumweleza kuhusu huduma unayotoa labda imepanda bei au kushuka, unamweleza kabla hajaja dukani kwako. Hivyo utaonyesha ya kwamba unamjali na yeye atakuamini wewe.

Uza bidhaa zenye ubora mzuri. Hakuna mtu anayependa kitu kibaya na ambacho hakina ubora. Kama mteja akinunua kwako ambato haina ubora kwa kutokujua harafu ikaenda ikamharibia usitegemee ya kwamba huyo mteja atarudia kwako tena. Mfano; Wewe unauza matifari ambayo si bora na mteja akaja kwako kununua wakati huo yeye hana utaalamu wowote kuhusu matofari na wewe ukamwuzia , mteja wako akapakia kwa uslama tu kwenye gari na wakati wa kushusha akakuta yamekatika sana na kuvunikavunjika, akauliza mtaalamu kwanini matofari yangu yamekatika sana akaambiwa matoafari haya si mazuri na hayana ubora. Usitegemee mteja huyo ya kwamba atarudi kwako, wewe ndo umemfukuza kwa bidhaa yako.

Jihadhari sana na mikopo. Lazima uwe na tahadhari juu ya mikopo. Neno mkopo kwako kiwe kitu cha mshangao lazima ujiulize swali kwanini namkopesha au kwanini nakopa. ukipata majibu fanya maamuzi. Kumbuka usimkopeshe mtu bila sababu hata kama unamjua vipi pia kopa wakati wateja wanapokuwa wengi kuliko bidhaa zako.

Ijali sana biashara yako. Kuwa na nidhamu na biashara yako katika nyanza zote. Fungua biashara yako kwa mda maalumu na kufunga kwa mda husika , usafi ni muhimu sana katika mazingira ya biashara yako. Jifunze mengi juu ya biashara yako.

Kutokana na mabadiriko ya mazingira, uchumi na teknolojia ipo sababu ya kujifunza mara kwa mara juu ya biashara yako. Mambo mengi yanaibuliwa kila kukicha kwahiyo huna budi kujifunza kila siku.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 068700076 au kwa barua pepe sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, October 30, 2017

Tengeneza tabia hizi ili ufanikiwe kimaisha.

 Sadick Kilasi     October 30, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena ambayo ni siku mpya, hatuna budi kusema asante kwaajili ya siku hii ya leo. Mpendwa wangu msomaji tuseme asante Mungu kwa kutujalia siku hii mpya, tunaomba utuongoze wakati wote na katika safari yetu ya kutafuta mahitaji yetu muhimu endelea kutujalia katika kutafuta mafanikio.

Nina furaha kukukaribisha tena mpendwa wangu kwenye makala hii ambayo yenye kichwa, [tengeneza tabia hizi ili ufanikiwe kimaisha]. Makala hii ya leo inamlenga kila mtu si mzee wala si kijana si mama wala si baba, hii ni ya kila mtu maana mafanikio ni ya kila mtu.

Maana halisi ya mafanikio ni pale mtu anapokuwa na uhitaji wa jambo furani au kitu fulani ukawa unatafuta ikisha ukakipata basi tayari umefanikiwa. Mafanikio tunayoyazungumzia leo ni mafanikio ya kimaisha. Na hizi ni tabia ambazo unapaswa kuzitengeneza ikisha ukaziishi ili ufanikiwe.

Tabia ya kwanza ambayo unatakiwa kuwa nayo ni kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu katika mafanikio yako. Kama unahitaji mafanikio basi yakupasa umwombe Mungu. Unaweza kuomba kama hivi 'ehe Mwenyezi Mungu naomba unijalie mafanikio nataka kufanikiwa' Na yeye alisha tuambia ya kwamba ombeni nanyi mtapewa. Mwombe Mungu bila kuchoka wala kukata tamaa.

Tabia ya pili ambayo unatakiwa kuwa nayo ni kuamini ya kwamba utafanikiwa. Lazima ujenge imani ya kwamba ipo siku moja utafanikiwa, ila jenga imani huku ukiwa unaendelea kufanya jambo lako ambalo unataka kufanikiwa, usijenge imani na jambo ambalo wewe mwenyewe binafsi hulifanyi utashindwa kupata kile unachokitaka.

Tabia ya tatu ambayo unatakiwa kuwa nayo ni kujitenga na watu wavivu. Unatakiwa kujitenga na watu wavivu maana hawa watakupotezea mda wako tu na kukurudisha nyuma kwenye harakati zako za maisha. Mara nyingi watu hawa huwa na tabia za kuomba tu na kukaa vijiweni kupiga stori na kufanya mambo yasiyo ya msingi. Kaa mbali na watu hawa ila uwapende usiwaonyeshe jeuri yoyote ile usiwachukie.

Tabia ya tatu ni kuepukana na watu wanao kukatisha tamaa. Hawa ni watu wale ambao huwa hawapendi kitu ambacho wewe unakifanya. Watu hawa kaa nao mbali kabisa ila wapende usiwachukie. Kama wakikujia na kukukwambia ya kwamba jambo hili wewe huliwezi wambie kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu lazima nifanikishe, usiwe na maneno nao mengi sana wajibu kwa ufupi.

Tabia ya tano ambayo unatakiwa kutengeneza ni kujifunza kila siku. Lazima uwe na tabia ya kujifunza kila siku, unaweza kujifunza wakati ambao umesafiri, jitaidi kujifunza kwa mambo mapya ambayo unayaona yataweza kukusaidia kupata wazo jipya la biashara, jifunze kwa kusoma vitabu, makala za magazeti, internet, redio na njia nyingine nyingi.

Hizi ni tabia chache kati ya nyingi ambazo unapaswa kuwa nazo ili ufanikiwe kimaisha. Katika makala zijazo nitakupikia hapahapa jikoni kwenye jiko la JIKO LA USHAURI. Mpendwa wangu nakusihii uziishi tabia hizo sio kuzijua tu haitoshi.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI.
Mawasiliano ni 0687000768 barua pepe sadikila65@gmail.com.
Asante.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ▼  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ▼  October (2)
      • Mjasiriamali mdogo fanya mambo haya ili biashara y...
      • Tengeneza tabia hizi ili ufanikiwe kimaisha.
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates