Biashara ndani ya ajira ni kitabu ambacho ni mahususi kwa waajiriwa ambao wanapata changamoto kubwa jinsi ya kujikwamua kutoka kwenye ajira na kuingia kwenye biashara. Kitabu hiki kinaonyesha namna ya kuzikwepa changamoto hizi, na mwandishi ameonyesha njia za kukabiriana na changamoto hizi.
Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi mashuhuri na mhamasishaji MAKIRITA AMAN ambaye yeye anaishi kusudi la maisha yake ambalo ni kuwasaidia watu kuwa na maisha bora kupitia kazi wanazofanya. Mimi binafsi napenda kazi zake na nipo tayari kununua kutoka kwake. Karibu tuangalie mambo niliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki;
1.Kutokana na mapinduzi ya teknologia na kuwepo kwa mitandao ya internet, ajira zimekuwa hazina uhakikana ni chache. Hii imetikana na sehemu ambayo walikuwa wanakaa watu watano sasa hivi anakaa mtu mmoja.
2.Chanzo kimoja cha kipato ni utumwa. Kwasababu huna uhuru wa kuchagua mambo kwa sababu wewe ni mwajiriwa na nilazima uingie kwenye madeni kupitia mikopo.
3.Biashara inahitaji mda kukua.
Kwa wale ambao wanatoka kwenye ajira moja kwa moja wanapata changamoto kubwa sana kwa sababu mipango sio matumizi. Unapokuwa umeweka mipango yako kunachangamoto ambazo wewe hukutegemea kuzikuta unakutananazo.
Na kwa wale ambao wanasubiri mpaka kustaafu nao pia hii inakuwa changamoto pia kwa sababu umri nao unazidi kwenda, na watu hawa huwa wakipata mafao yao huwekeza yote kwenye biashara na kuaanza kuitegemea biashara wakati bado ikiwa changa. Kutokana na changamoto hizi ni bora kuanza biashara huku ukiwa ndani ya ajira ili upambane kwa uhuru na kukuza biashara yako vizuri na kwa mda sahihi.
4.Lazima ukubali kupoteza.
-kubali kupoteza mda wakupumuzika
-kubari kupoteza muda wakijamii
-kubali kupoteza starehe na burudani.
Kufanya biashara ukiwa ndani ya ajira lazima ukubali kuacha mambo ambayo unayapenda sana na hayana maana.
5.Sio kila biashara unaweza kufanya ukiwa bado kwenye biashara, bali kuna kuna biashara furani unaweza kuzifanya na kufikia mafanikio makubwa, biashara kama;
-kipaji ulichonacho,
-utaalamu na uzowefu wako,
-biashara za kawaida,
-biashara za mtandao na
-kilimo cha biashara.
Ni hatari sana kuchoma meli moto ili usipate nafasi ya kurudi nyuma, hii ni kutokana na kutotabirika kwa uchumi ni bora kupambana ukiwa ndani ya hiyo hiyo meli. Usiache ajira nakuingia kwenye biashara ni hatari sana.
Haya ni mambo machache kati ya mengi niliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki. Nakusihi rafiki yangu tafuta kitabu hiki kisome hata kama wewe huja ajiriwa kitakusaidia.
Endelea kutembelea mtandao wetu wa JIKO LA USHAURI.
jikolaushauri.blogspot.com
sadikila65@gmail.com
0659639168
Sadick Kilasi.
0 comments:
Post a Comment