JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Saturday, July 6, 2019

Talanta Yako

 Sadick Kilasi     July 06, 2019     No comments   

Sadick Kilasi:
Hivi Ndivyo Ambavyo Unaweza Kujua Vipawa Vyako Na Kufanyia Kazi Mapema Sana.

Wakati nikiwa mdogo sana, nikiwa darasa la pili, nilikuwa napenda sana kuvaa saa mkononi mwangu. Naam, kipindi hicho saa zilikuwa zinauzwa elfu moja tu, saa ya kimulimuli.

Lakini nilikuwa na tatizo moja, saa ilikuwa haidumu mkononi mwangu kwa sababu nilikuwa napenda kuifungua ndani na kuitengeneza tena. Niliharibu saa nyingi lakini kuna nyingine ambazo nilikuwa nafanikiwa kuirudishia kama ilivyokuwa mwanzo.

Huu ulikuwa ni mchezo wangu, kuharibu na kutengeneza. Nilikuwa sijui ni kitu gani ambacho kilikuwa kinanisukuma kufanya hivi, wala nilikuwa sijiulizi kwanini nafanya hivyo, Mimi nilikuwa nafanya kwa kadili ninavyosukumwa kutoka ndani. Utoto nao ulikuwa unachangia kufanya vitu kama hivyo.

Sasa, leo hii wakati nimekuwa ndio naelewa kwanini nilikuwa naharibu saa na kutengeneza tena.

Mimi ni mtafiti, mtu ambaye naharibu kilichopo na kutengeneza tena kwa jinsi inavyotakiwa, naam, nafumbua fumbo lilifichwa na kufanya vile inavyotakiwa.

Talanta au kipawa ni zawadi ambayo mtu anapewa na kuwekewa katika nafsi yake ili ipate kumsaidia na kuwasaidia wengine. Kwani Mungu anaweka zawadi hii ndani yetu, na tunazaliwa nayo. Kila mtu anapewa sawasawa na makusudi yake yeye Mungu.

Mathayo 25:14, Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.

Lakini kwa sababu ya maisha ya mazoea katika jamii zetu talanta hizi hupotea bure kabisa zisifanye kazi kabisa. Wengi sana tunachukuliwa na talanta za watu na wengine hatutumii chochote.

Kila mtu anatalanta yake, na talanta ya mtu hujionyesha anapokuwa mdogo, kwa sababu katika kipindi hichi Mungu ndiye huwa anamwongoza mtoto kwa kiasi kikubwa.

Kuna wakati mtoto anakuwa anafanya vitu ambavyo vinakuwa kwa mzazi wakati mwingine havileti maana kama mimi kuharibu saa. Mimi niliyekuwa mharibifu wa thamani na natengeneza thamani nyingine.

Ukisoma katika neno la Mungu utagundua kwamba Yesu alimponya mtoto ambaye alikuwa na pepo la kuangusha, na kumpeleka huku na huko tangu utoto. Marko 9.

Sasa, talanta ni kitu ambacho kila mmoja anapaswa kutia juhudi kutumia kwa sababu talanta sio ya kwako wewe peke yako bali ni kwaajili ya kuwahudumia wengine.

Kitu chochote kilicho ndani mwetu, hicho si cha kwetu kwa sababu hicho tunapaswa kutoa nje, cha kwetu ni kile ambacho tunakihitaji kwa sababu hicho tunakiingiza ndani mwetu.

Talanta yoyote inahitaji kuboreshwa na mwenye talanta kwa kutia juhudi sana, kwa sababu kila mwenye talanta atadaiwa ni namna gani ametumia. Mwanadamu hamiliki chochote tumeazimwa kwa muda Mungu atachukua kwa wakati wake.

Mathayo 25:19, Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.

Hapa duniani watu wanahitaji faraja tofauti tofauti  kutoka kwenye utofauti.

Ni muhimu sana kuthamini kile ambacho umepewa na Mungu uwape watu.

Na ili uthamini talanta hiyo unapaswa kuwa na shukrani na uvumilivu. Nitakupa Falsafa moja ambayo huwa tunaishi kila siku hasa vijana tunapenda sana.

Shukrani ni uwezo wa kuthamini chenga, sasa sijui ni chenga ya mchele ama chenga ya mpira, yote na yote unaweza kujifunza. Chenga ni uwezo wa kuendesha vitu vidogo vidogo, naam, chenga chenga na kuthamini kwa unyenyekevu mkubwa.

Umakini unahitajika katika sehemu hii kwa sababu ni sehemu ambayo wengine wataona ni upuuzi tu mwanzoni unapoanza kufanya lakini kwa sababu mpanzi huenda akipanda kwa machozi na kuvuna kwa furaha, wewe unatambua hili.

Kitu cha pili kinachohitajika ni pasi, naam, sijui unavyosha nguo ama unapiga pasi ya mpira lakini hapa ninazungumzia kuboresha kile kidogo ulichopokea. Kama ni chenga za ubwabwa basi hakikisha unaweka viungo ili viboreshe mchezo wako.

Mathayo 25:16, Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.

Mwisho unafunga goli lako, unafikia kusudi na malengo yako. Hapa ndipo utawambia waliokukatisha tamaa kuwa, chenga ikiboreshwa inakuwa pasi na pasi huleta goli.

Kwa hiyo, kila mmoja lazima azingatie hatua hizi tatu, naam, hizi ni njia ambazo tunazifanya kila siku katika maisha yetu.

Kuna wakati mwingine unaweza ukawa hujasoma lakini unaweza kusoma mchezo unaendelea na ukapata majibu.

Ukihakikisha macho yako yanasoma na kulia hakuna kitu ambacho kinashindikana, ndio, malengo na kuchukua hatua ni muhimu sana.

Kama unatalanta na unaitumia vema basi Kristo atakupa zaidi ya talanta yako. Usichezee talanta yako.

Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768  au sadikila65@gmail.com.

Kitabu cha Mormoni ambacho ni ushuhuda wa Yesu Kristo nakigawa hakikisha unatuma ujumbe kama unahitaji. Asante.
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ▼  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ▼  July (8)
      • Hii Ndio Siri Ya Rhodesia Ya Kaskazini Na Kusini K...
      • Rhodes Ya Kaskazini Na Kusini Na Siri Yake
      • Hii Ndio Hofu Ya Kweli.
      • Talanta Yako
      • Hivi Ndivyo Wewe Unaweza Kutafsiri Neno La Mungu.
      • Falsafa Za Asili (Songa Ugali).
      • Huu Ndio Mji Tulivu Uliojificha.
      • Kaa Sehemu Yako.
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates